This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, February 28, 2013

MTOTO WA MWENYEKITI WA KIJIJI TANANGOZI IRINGA AJINYONGA KATIKA OFISI YA KIJIJI

  Katika hali ya kusikitisha  mtoto wa  mwenyekiti wa serikali ya  kijiji cha Tanangozi katika wilaya ya  Iringa vijijini  Doto Kikoti ameamua kujinyonga katika ofisi ya kijiji  hicho inayoongozwa na babake mzazi kama njia ya kupinga kuwekwa kizuizini katika ofisi hiyo. Tukio hilo  limetokea  usiku  wa kuamkia leo  baada ya kijana  huyo kutuhumiwa  kufanya  vurugu...

HEADLINES ZA HABARI ZA MICHEZO DUNIANI.

RAFAEL BENITEZ VS JOHN TERRY  Nahodha wa Chelsea John Terry na kocha wa muda wa club hiyo Rafael Benitez wameripotiwa kuwa kwenye mzozo mkubwa kufuatia ugomvi ulioibuka kwenye kiwanja cha mazoezi cha club hiyo Cobham London.Wawili hao walionekana kugombana baada ya Benitez kuitisha mkutano mdogo kabla ya mazoezi ya asubuhi ambao alizungumzia mechi yao ya jumapili waliyochapwa 2-0 na Man City. LUIS NANI – Mchezaji winga wa Manchester...

Wednesday, February 27, 2013

KOCHA WA AZAM FC APIGWA ADHABU

Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall (pichani) amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.   Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni ...

WAFANYA BIASHARA WAVUNA MAHELA VODACOM

 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingw(kulia) akiongea na Mshindi kwenye simu ya mezani wakati wa Droo  ya  kuwapata washindi wa shilingi Milioni 5 na Milioni moja  katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.wanaoshuhudia kushoto kulia ni Matina...

msd yawalipua wanaolinda wabadhirifu

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi. Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya...

BODI YA UTALII YASAINI MKATABA NA WAANDAAJI WA ONESHO LA UTALII LA INDABA AFRIKA KUSINI, KUANZISHA ONESHO LA SWAHILI TOURISM FAIR NCHINI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga katikati wa tatu kutoka kulia, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki kushoto na Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd wakisaini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha onesha la Utalii litakalojulikana kwa jina la Swahili Tourism Fair kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, ambalo kwa mara ya kwanza...

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku Waziri wa Ulinzi na...

Monday, February 25, 2013

MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR

Maalim Seif apinga mauaji ya Padri asema si ya kigaidi       Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amepinga kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi kuwa mauaji ya viongozi wa dini Zanzibar ni ugaidi na kusema kuwa wanaofanya hivyo ni watu wenye nia ya kuvunja umoja wa Wazanzibari. Baada ya mauaji ya Padre Evarist Mushi,...

NI WAREMBO MISS UTALII

HAPA NI WAREMBO TU .... LAKELAND AFRICA WADHAMINI UTALII WA NDANI , MISS UTALII TANZANIA 2012/13     Washiriki wa Miss Utalii tanzania wakiwa katika moja ya Makaburi ya zamani Kaole Bagamoyo. Mshiriki wa Miss Utalii Tanzania Pamoja na washiriki wengine wakikata utepe kwa ajili ya uzinduzi wa safari ya Kitalii Bagamoyo. Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa katika moja ya Kaburi maarufu la Wapendanao. Read...
MIWA YA MTIBWA YAMLEWESHA SIMBA  Timu ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo jioni katika Uwanja wa Taifa. Bao la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja. Bao hilo limedumu hadi...
ANGETILE :TUTAKAA KUJADIRI NINI TUFANYE KUZINGATIA FIFA INATAKA NINI ? Katibu mkuu wa tff angetile osiah amaesema tff itakutana ili kujadiri maamuzi ya serikali kuifuta kwani wao wanaendesha mpira kikatiba kwani wao wanaongoza mpira unaongozwa na fifa, caf ,cecafa,  na sio serikali na katiba tff inasema kuwa inatakiwa kufuata maagizo ya kutoka  fifa amesema wao watakaa chini na kulitazama na nini wataamua ...

Matokeo ya kidato cha Nne: Wakuu wa shule wadai ilitungwa kwa mfumo tofauti

MATOKEO mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yamezidi kuibua mapya, baada ya wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini kusema mitihani ilitungwa kwa mfumo tofauti na uliozoeleka miaka yote, huku tume iliyounndwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ikipondwa na baadhi ya watu.Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema kwamba maswali waliyoulizwa watahiniwa yalikuwa ya kujieleza tofauti...

jk atua uganda kumzika baba yake rais museveni

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ...

Man United yaelekea kushinda ligi kuu

Man United yaelekea kushinda ligi kuu Ligi kuu ya soka nchini England, imeendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbali mbali. Huko Loftous Road, Manchester United imeebuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya QPR, huku mshambuliaji Ryan Giggs akifunga bao la pili na kufikisha mabao 999 toka aanze kucheza soka la ushindani na kuifanya timu yake ya Manchester United, kuongeza tofauti ya point 15 na mabingwa...

Man City yailemea Chelsea

Wachezaji wa Manchester City Mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City wameandikisha ushindi mkubwa dhidi ya mabingwa wa ulaya Chelsea na hivyo kufufua matumaini yao ya kuhifadhi kombe hilo kwa mwaka wa pili, licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka wa vinara wa ligi hiyo kwa sasa Manchester United. Mechi hiyo iliyokuwa na mashambulizi na kila aina ya vivutio baina ya timu hizo zinazomilikiwa na matajiri wawili tofauti,imemalizika...

Saturday, February 23, 2013

FIFA WAJA KUFATILIA SOKA

OFISA Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi amewasili leo kwa ajili ya kufuatilia shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu.  Mamelodi, ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa shughuli za maendeleo nchini Tanzania tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, pia amekuja kumtambulisha msaidizi wake, Patrick Onyango aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibun...

hali ni tete drc;un

  Na Mwandishi Maalum Hali katika eneo la Mashariki ya Kongo inaelezwa kwamba ni tete na ya hatari kiasi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuibuka mgogoro mkubwa yoyote.Onyo hilo limetolewa siku ya Ijumaa na Bw. Roger Meece ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa Bw. Roger Meece amelitoa toa onyo hilo, wakati Katibu...

ZACO TECHNOLOGY

inatoa offer kwa wateja wake ambao wanataka kufanyiwa kazi za editing  kama vile matangazo ya mabango website movie  photo graphics kua wanatoa offer bomba kabisa kwa wateja wao tunapunguzo kubwa sana kwa yoyote yule atakaefanya kazi nasi zaidi ya moja...

SMART BOY

 zaidi fika mataa Karibu Smart Boy kwa mahitaji yako yote ya nguo za kisasa na zakijanja unakaribishwa kwa mawasilianowa uhuru karibu na daraja la wamasai kuna suti za kila aina mashart vibody vya kina dada watoto wadogo pia tuna punguzo la aslimia 90% kwa yule atakae nunua nguo zaidi ya moja...