Leo nataka kuzungumzia tabia ya baadhi ya watu kutumia fedha
wanazozipata kwa fujo kana kwamba wameambiwa kuwa kesho wanakufa. Hakuna
asiyefahamu umuhimu wa pesa, na kutokana na hilo, wengi wamekuwa
wakipambana usiku na mchana kuhakikisha wanazipata.
Cha ajabu sasa, wapo ambao wanatumia nguvu na akili zao kuzitafuta
fedha hizo lakini mwishowe wanazimwaga kwa matumizi yasiyo na mbele wala
nyuma.
Utakubaliana na mimi kwamba wapo watu ambao leo hii
wanashinda wakibeba zege, kuzibua mitaro, kubeba mizigo na kazi nyingine
nzito lakini jioni wanapopata ujira hukimbilia baa na kuzitumbua kwa
staili ya lete kama tulivyo.
Ninachokizungumza kipo huko mtaani, watu…
Leo
nataka kuzungumzia tabia ya baadhi ya watu kutumia fedha wanazozipata
kwa fujo kana kwamba wameambiwa kuwa kesho wanakufa. Hakuna asiyefahamu
umuhimu wa pesa, na kutokana na hilo, wengi wamekuwa wakipambana usiku
na mchana kuhakikisha wanazipata.
Cha
ajabu sasa, wapo ambao wanatumia nguvu na akili zao kuzitafuta fedha
hizo lakini mwishowe wanazimwaga kwa matumizi yasiyo na mbele wala
nyuma.
Utakubaliana na mimi kwamba wapo watu ambao leo hii wanashinda
wakibeba zege, kuzibua mitaro, kubeba mizigo na kazi nyingine nzito
lakini jioni wanapopata ujira hukimbilia baa na kuzitumbua kwa staili ya
lete kama tulivyo.
Ninachokizungumza kipo huko mtaani, watu
wanatumia pesa kama vile wana uhakika wa kuendelea kuzipata kila siku.
Ndiyo maana nadiriki kusema kwamba kutumia pesa ovyo ni sawa kabisa na
kujiandalia ufukara wa baadaye.
Wapo watu wengi tu ambao kwa sasa ni
mafukara wa kutupwa lakini utakapojaribu kuangalia historia yao huko
nyuma utagundua walikuwa na pesa nyingi ila walikuwa wakizutumia kana
kwamba wanamkomoa mtu lakini leo wanaishi maisha ya kuungaunga, hawana
mwelekeo.
Sikatai kwamba matumizi ya mtu yanatokana na kipato chake
na ndiyo maana mtu anayepokea mshahara wa shilingi milioni moja kwa
mwezi hawezi kuwa na matumizi sawa na mtu anayepokea laki moja lakini
je, kuwa na kipato kikubwa ndiyo kukufanye utumie fedha zako ovyo eti
kwa sababu tu una uhakika wa kupata nyingine mwezi ujao?
Jamani
tukumbuke kwamba, maisha ni kupanda na kushuka. Leo hii unafanya kazi
katika kampuni ama shirika fulani lakini uwezekano wa kuwepo katika
shirika hilo kwa kipindi chote cha maisha yako ni mdogo. Unaweza
kuachishwa kazi wakati wowote.
Sasa kama ulikuwa unatumia ovyo pesa
uliyokuwa unaipata, unatarajia nini kama siyo kuingia kwenye ufukara
ambao kwa kiasi fulani ungeweza kupunguza ukali wake kama ungekuwa
makini katika matumizi ya pesa zako?
Utumiaji ovyo wa pesa ni
kuzitumia bila mpangalio tena wakati mwingine katika mambo ambayo si ya
msingi lakini tutambue kwamba, ufujaji wa pesa hauko katika anasa tu
kama vile ulevi, kuhonga na mambo mengine kama hayo, bali pia katika
mambo ambayo hata yakikosekana hayawezi kuleta athari.
Tafiti
mbalimbali zimeonesha kwamba, wengi ambao hutumia pesa ovyo ni athari za
malezi waliyoyapata kutoka kwa wazazi wao tangu utotoni. Mzazi ndiye
anayeweza kumfundisha mtoto wake kutokuwa na nidhamu katika pesa.