![]() |
Mbunge Ezekiel Wenje. |
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Wednesday, July 31, 2013
MBUNGE WENJE ATUHUMIWA KWA UTAPELI MWINGINE WA HARAMBEE NAYE MBUNGE LAMECK AMTAKA ASHINDANE NAYE KWA VITENDO NA SIYO MATUSI JUKWAANI
MIKUTANO WA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA NA WANANCHI WA MTAA WA MALIMBE WATOA SULUHISHO KWA KERO ZAO
![]() |
Sehemu ya wananchi wa mtaa wa Malimbe kusanyikoni. |
![]() |
Afisa Ardhi Idara ya Urasimishaji Makazi holela jijila Mwanza Bw. Maduhu Kazi Ilanga, akijibu hoja motomoto za wananchi zilizowasilishwa. |
![]() |
Mhasibu wa Wananchi Mwalimu mstaafu Mzee Mahola aliwasilisha |
![]() |
Akinamama. |
![]() |
Mwananchi akitoa hoja ya ukarabati wa barabara ya Malimbe - Saut - Mnangani hadi Mkolani Centre ili kupitika kiurahisi. |
![]() |
Mwananchi huyu alimuomba Mstahiki Meya kuwasiliana na SUMATRA na kuwabana baadhi ya wamiliki wa vyombo vya Usafiri wanaokatiza ruti huku magari yao yakiwa yamesajiliwa kuihudumia njia yote. |
![]() |
Mwalimu Crecency Njogopa aliwakilisha akina mama kwa kulizungumzia suala la uhaba wa maji. |
![]() |
Mhandisi wa barabara wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Bw. Malulu akijibu hoja na maswali yaliyojitokeza kwenye mkutano wa wananchi waishio mtaa wa Malimbe. |
![]() |
Mstahiki Meya akitoa majibu na ufafanuzi kwa yaliyowasilishwa. |
![]() |
Kumalizika kwa mkutano eneo la mtaa wa Malimbe. |
![]() |
Wananchi wakimpongeza Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza mara baada ya mkutano kumalizika huku akitoa majibu mazuri yakitaalamu kupitia safu ya wataalamu alioongozana nao. |
![]() |
Akina mama nao hawakuwa nyuma kutoa pongezi ambapo ndani yake waliahidi kutoa ushirikiano kwake na wataalamu hao wakati wa utekelezaji. |
KUFUATIA kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya nje ya nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga polisi Julai 29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Idd Azzan alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Posta jijini Dar na kukutana na Kamanda wa Kanda Maalumu, Kamishna, Suleiman Kova.
“Kikubwa Azzan amemwambia Kova kwamba anataka jeshi la polisi limchunguze na kisha liwaambie wananchi kama yeye…
KUFUATIA kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya nje ya nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga polisi Julai 29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Idd Azzan alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Posta jijini Dar na kukutana na Kamanda wa Kanda Maalumu, Kamishna, Suleiman Kova.
“Kikubwa Azzan amemwambia Kova kwamba anataka jeshi la polisi limchunguze na kisha liwaambie wananchi kama yeye anahusika na biashara hiyo au la,” kimesema chanzo chetu.
Baada ya kupata habari hizo, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Azzan ambaye alikiri kufika polisi na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Hivi karibuni Mbunge huyo alitajwa katika habari zilizosambazwa mtandaoni kwamba anahusika na biashara hiyo baada ya mfungwa mmoja wa gereza moja nchini Hong Kong kumtaja kwamba ndiye anayewatuma vijana nje ya nchi kupeleka madawa ya kulevya.
Hata hivyo, Mbunge huyo amekanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa hausiki kwa njia moja ama nyingine na kutaka mfungwa huyo atajwe jina lake kamili, namba yake ya ufungwa na hata ndugu zake waliopo hapa nchini ili ukweli ujulikane.
Barua zilizosambazwa mtandaoni ambapo jina la Mhe. Idd Azzan lilitajwa kuhusika na dawa za kulevya:
ROSE NDAUKA ANASWA AKIPAPASWA NDANI YA GARI KABLA YA KUPELEKWA HOTELINI
![](http://3.bp.blogspot.com/-33aOBEcq2nA/UfjCAfjvpXI/AAAAAAAAj2Q/0eipLhJpSDM/s1600/1.png)
Rose Ndauka au Aisha anaweza kuwa ameitia najisi funga yake baada ya kunaswa akiingia hotel moja iliyoko kinondoni jijini Dar kwa kile kilichoelezwa ni kwenda kuivunja amri ya sita na mwanamziki wa bongo fleva Nassoro Ayoub "Nasry" au Tajiri Boy
![](http://2.bp.blogspot.com/-bBa2963Cmfw/Ufi_2bhukfI/AAAAAAAAj1w/fE-fkqCNczk/s1600/2.gif)
Rose ambaye alisilimu mwaka jana na kupewa jina la Aisha baada ya kuchumbiwa na mwanamziki mwasisi wa kundi wa TNG Squad, Malik Bandawe, alifumwa na kamera za wakazi wa jirani na hoteli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.....
Shuhuda wa tukio hilo amedai kwamba majira ya mchana kweupe gari aina ya Toyota Mark X lenye rangi nyeusi liliwasili kwenye viunga vya hoteli hiyo na kusimama kwa takribani dakika 10 kisha likaondoka na kwenda kupaki sehemu nyingine ambapo ni umbali mfupi toka hotelini hapo...
Kitendo hicho kiliibua mashaka miongoni mwa watu hasa kutokana na vioo vya gari hilo kuwa tinted hivyo kutowaonesha waliokuwemo ndani...
"Walipoondoka na kupaki palipojificha tuliamua kuwasogelea ili tujue ni akina nani
"Baada ya muda, kioo cha dereva kilishushwa kidogo, tukamuona dogo anayefanana na Diamond akiwa anampapasa demu aliyekuwa pembeni yake...
"Tulipoona hivyo, tulidhana mnyamwezi ameamua kumaliza mambo yake ndani ya gari, hivyo tukaziweka simu zetu standby kwa ajili ya kushuhudia" alisema shuhuda huyo
Baada ya muda, mlango wa kulia ulifunguliwa kisha wakamuona dogo aliyetambuliwa kwa jina la Nasry
"Kumbe hakuwa Diamond,alikuwa ni dogo Nasry.Tulipotupa jicho ndani, tulihamaki kumuona Rose Ndauka akibadili nguo na kujitanda baibui.
"Nadhani alifanya hivyo ili watu wasimjue pindi atakaposhuka kwenye gari maana aliposhuka tu, waliongozana na dogo Nasry kwa mwendo wa kasi hadi ndani...
"Toka walipoingia ndani hadi walipotoka iliwachukua kama masaa matatu hivi.Wakati wa kutoka, Nasry alilifuata gari hadi mlangoni na kisha Rose akaingia na kutokomea"...Kilimalizia kusimulia chanzo hicho
SHEIKH PONDA ISSA PONDA APENDEKEZWA KUGOMBEA URAIS MWAKA 2015
Ikiwa imebakia miaka miwili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge hapa nchini,baadhi ya waumini wa kiislamu wameanza kupendekeza wagombea wa urais wanaoona kuwa wanafaa ambapo jina la Sheikh Ponda Issa Ponda limeongoza....
Mapendekezo hayo yamedhihirika katika mihadhara kadhaa anayoifanya Ponda katika mikoa mbalimbali nchini,ambako amekuwa akipendekezwa na kushauriwa na waumini agombee nafasi hiyo.....
Walianza waumini wa msikiti mkuu wa Ijumaa wa Arusha alipokuwa kwenye ziara mkoani humo ambapo muumini mmoja alisimama na kusema kwamba kwa mawazo yake anaona Ponda anafaa kugombea nafasi ya urais kwa vile anaamini kuwa uwezo wa kuongoza anao..
Alisema mbali na uwezo pia yuko makini katika kusimamia jambo lolote lenya maslahi kwa waislam na kwamba mtu wa namna hiyo atafanya vyema zaidi akipewa dhamana ya kuongoza nchi....
Inaelezwa kuwa Ponda alipotembelea Zanzibar alipata wakati mgumu wa kuwakataa waislam waliojitokeza kumlaki katika misikiti ya Mpendae na Mbuyuni ambako alifanya mihadhara na kupendekezwa kugombea urais kwa kura nyingi na waumini ....
Kufuatia kusikika kwa mapendekezo hayo,Kisiwa lilimtafuta Ponda ili kusikia maoni yake juu ya maombi ya waislam kumtaka agombee urais.
"Sikuwa na fikra hiyo hata mara moja,lakini maadam limeletwa nami ni kiongozi wa taasisi ninawashukuru waliofikiria hivyo...
"Kwa sasa siwezi kuzungumza lolote kuhusu hilo, ntalifikisha katika taasisi na maulana ndio watakaolitazama na kutoa uamuzi." Alisema Sheikh Ponda
Ponda alisema kuwa inawezekana waumini wakawa na mtazamo huo lakini viongozi wakawa na mtazamo tofauti kabisa,hivyo akawataka waumini kuwa na subira katika hilo.
-KISIWA.
AGNESS MASOGANGE AMPONZA MADEE NA KUSABABSHA AVULIWE NGUO AIRPORT
Kwenye Exclusive interview na millardayo , Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana (Akina Masogange ) waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.
Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.