MWANAMKE anayedaiwa kufunga ndoa ya siri na mchekeshaji 
mahiri Bongo, Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto au King Majuto, 
Rahma Abdallah (20), ameibuka na kudai kutelekezwa na mumewe huyo.
 Mzee Majuto akiwa na mkewe Rahma Abdallah siku ya ndoa yao. 
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa kwa siri jijini Dar Julai 28, mwaka huu na
 kudumu siku 44, inaonekana imevunjika rasmi baada ya Mzee Majuto kutoa 
talaka kupitia kwa msanii wa…
                                 
Na Imelda Mtema MWANAMKE
 anayedaiwa kufunga ndoa ya siri na mchekeshaji mahiri Bongo, Amri 
Athuman maarufu kama Mzee Majuto au King Majuto, Rahma Abdallah (20), 
ameibuka na kudai kutelekezwa na mumewe huyo.
Mzee Majuto akiwa na mkewe Rahma Abdallah siku ya ndoa yao.
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa kwa siri jijini Dar Julai 28, mwaka huu na
 kudumu siku 44, inaonekana imevunjika rasmi baada ya Mzee Majuto kutoa 
talaka kupitia kwa msanii wa filamu aitwaye Rehema Omary.
 Akizungumza na gazeti hili katika ofisi zetu, Bamaga-Mwenge, Dar, 
Septemba 9, mwaka huu, Rahma alidai kuwa alikutana na Mzee Majuto jijini
 Tanga na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa miezi sita kabla ya 
kufunga ndoa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliopita.
 “Tulifahamiana 
Tanga, mimi ni mwenyeji wa huko kama ilivyo kwa Mzee Majuto, wakati 
tukiwa kwenye uhusiano, ulipofika Mwezi wa Ramadhani akaona bora tufunge
 ndoa ili tusiendelee kutenda dhambi, akaniambia dhamira yake hiyo nami 
sikukataa,” alisema Rahma.
Rahma Abdallah (20). 
TOFAUTI MIAKA 40
 Mke huyo ambaye ni kibinti cha umri wa miaka 20 aliyepishana na Mzee 
Majuto kwa umri wa miaka 40 alisema kuwa, mwigizaji huyo alifuata 
taratibu zote za kufunga ndoa kwa kupeleka barua ya posa nyumbani kwao.
 “Alitoa mahari ndipo ilipopangwa siku ya ndoa iliyofungwa nyumbani kwa mama yangu, Mbagala-Zakhem, Dar,” alifafanua Rahma.
ULINZI MKALI, BARAFU MPAMBE
 Katika ndoa hiyo iliyofungwa katika Mtaa wa Kibonde-Maji Julai 28, 
mwaka huu na Shehe Abdurahman Kisoma na kufuatiwa na sherehe nyumbani 
kwa bibi harusi, ulinzi mkali uliwekwa ili siri ya Mzee Majuto kuoa 
isivuje.
 Mashahidi wa ndoa hiyo walikuwa ni Suleiman Said ‘Barafu’ 
ambaye ni mwigizaji aliyekuwa mpambe wa bwana harusi pamoja na Mohammed 
Malila.
...Siku ya ndoa yao. 
MAHARI 20,000 Cheti cha ndoa hiyo, kinaonesha kwamba Mzee Majuto alimuoa mwanamke huyo kwa mahari ya shilingi 20,000 aliyolipa yote.
 “Baada ya ndoa, Mzee Majuto aliwaomba wazazi wangu nikae nyumbani hadi 
Mwezi wa Ramadhani utakapoisha ndipo atakapokuja kunichukua, akaniachia 
shilingi elfu sitini tu, mpaka leo hii sijamuona,” alisikitika mke huyo 
ambaye alikuwa akijua kama Mzee Majuto alikuwa na mke mwingine.
KAZI KWA PROFESSA J
 Mke huyo wa Mzee Majuto alisema kuwa kabla ya kufunga ndoa na gwiji 
huyo wa uchekeshaji alikuwa akifanya kazi katika saluni ya mwanamuziki 
Joseph Haule ‘Profesa Jay’ iliyopo Msasani, Dar.
 “Nilikuwa nafanya 
kazi na kupata kipato huku nikiwa nimepanga chumba lakini Majuto 
aliniambia niache kazi na nirudishe chumba, nami nikafanya hivyo nikijua
 naenda kuishi kwa mume wangu, kumbe!...” alijuta Rahma.
MESEJI CHAFU ZA MKE MKUBWA
 Baada ya Majuto kuondoka mke huyo alikuwa akimpigia simu kutaka fedha 
za matumizi lakini alikuwa akiambiwa awasiliane na Bi. Rehema, mwanamke 
ambaye Mzee Majuto huwa anaigiza naye katika filamu zake.
 Rahma alilalamika kutumiwa ujumbe wa matusi kwenye simu yake na mke mkubwa wa Mzee Majuto.
 “Kitendo hicho kinaniuma sana kwani wakati mwingine huwa ananitukana na
 kunitishia maisha, akidai eti atanifanyia kitu kibaya, nikimpigia 
Majuto na kumweleza naye ananijibu mbovu,” aliongeza.
 Mke huyo mdogo
 wa Mzee Majuto alisema kuwa anaumia kutokana na kuharibiwa maisha kwa 
kuolewa na kuachishwa kazi huku akiendelea kutukanwa na mke mkubwa.
MASHITAKA BAKWATA
 Rahma ambaye aliliachia Amani nakala ya cheti cha ndoa alisema msanii 
huyo amemdhalilisha kwani kila akidai talaka yake anamwambia ameshaituma
 kwa Bi. Rehema na kumtaka aende akaichukue kitu ambacho ni kinyume na 
makubaliano yao.
 Rahma alisema kuwa amejipanga kwenda kumshitaki 
Mzee Majuto katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) ili amlipe 
fidia na kumtafutia kazi.
 “Yeye ndiye aliyenioa lakini nikimdai 
talaka ananimbia alimpa Bi.Rehema, wakati mwanamke huyo siye aliyenioa, 
sasa nampeleka Bakwata ili anikabidhi talaka na kunilipa fidia,” alisema
 kwa hasira mke huyo.
MSIKIE MZEE MAJUTO 
 Akijibu tuhuma hizo akiwa jijini Tanga, Mzee Majuto alikiri kufunga 
ndoa na Rahma na kusema kuwa alishamuacha kwa sababu aligundua 
hajatulia.
 “Huyo mwanamke nimeshaachana naye ila kwa sasa anataka 
kunichafua, kama anahisi ana haki kwa nini asiende mahakamani? Nimemtuma
 mshenga ampe talaka hataki kuipokea, anataka nije Dar. Kama huo siyo 
uhuni ni nini? huyo mwanamke hajatulia,” alisema.
TALAKA KULETWA GLOBAL
 Mzee Majuto alidai kwamba, Rahma amekuwa akimpa usumbufu na kufikia 
kumpa masharti ya ajabu na kuahidi kumtuma mtu ailete nakala ya talaka 
hiyo katika ofisi