P Funk majani nae amezungumza lakini alishindwa kutokana na uchungu aliokuwa nao juu ya msiba kwani bado haamni kama Ngwea hayupo tena. |
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Wednesday, May 29, 2013
PICHA ZA BAADHI YA WASANII WALIOHUDHULIA KIKAO CHA MSIBA WA MSANII "ALBERT MANGWEA" PALE LEADERS CLUB.
KIFO CHA NGWEA: LADY JAYDEE NAYE ASITISHA SHOW YAKE
Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
"SITAKI KUSIKIA NYIMBO ZA NGWEA ZIKIPIGWA CLOUDS FM..WAO NDO WALIOMFANYA AANZE KUVUTA BANGI ILI KUONDOA MAWAZO"...P FUNK
Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.
HIVI NDIVYO MAMA DUDE ALIVYOZIKWA
HEE NESII!
MUUGUZI wa kike, Violet Shoo, mkazi wa jijini Dar ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni, Ilala baada ya kunaswa katika jaribio la kutaka kumchoropoa ujauzito msichana mmoja aliyepandikizwa kama mwanafunzi kwa mtego makini ulioratibiwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’.
ILIKUWAJE?
Muuguzi huyo alikutwa ndani ya zahanati hiyo akiwa na zana mbalimbali zinazodaiwa ni za kutolea mimba huku msichana huyo akiwa juu ya kitanda, tayari kwa kufanyiwa zoezi hilo haramu.
Awali, Ijumaa ya Mei 23, mwaka huu baadhi ya wakazi wa eneo hilo walilitumia ujumbe gazeti hili wakimlalamikia muuguzi huyo kwamba amekubuhu katika matukio ya utoaji mimba hivyo wakaomba ikiwezekana OFM imuandalie mtego wa kumnasa ili kukomesha kitendo hicho.
“…huyu nesi amekuwa akiwatoa watoto wetu mimba, kwa siku anaweza kutoa hadi nne, sisi wazazi tumechoshwa, tunaomba mje. Anaitwa Violet…” ilisomeka sehemu ya meseji hiyo huku ikielekeza zahanati anapopatikana.
OFM YAJIPANGA, YAENDA KUCHUNGUZA
Baada ya malalamiko hayo, kikosi cha upelelezi cha OFM chenye wasichana wawili kilikwenda kwenye zahanati hiyo na kukutana uso kwa uso na muuguzi huyo ambapo msichana mmoja aliomba kutolewa mimba na nesi huyo ambapo aliambiwa ni shilingi 50,000.
Kikosi kiliondoka kwa kumwambia muuguzi huyo kwamba wanafuata fedha mahali na wangerejea jioni wakiwa na ‘keshi’ mkononi.
POLISI WASHIRIKISHWA
Timu ya waandishi wa habari wa gazeti hili pamoja na Jeshi la Polisi waliweka mtego baada ya wakazi wa maeneo iliyopo zahanati hiyo kulalamika juu ya kukithiri vitendo vya utoaji mimba vinavyofanywa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.
Wakazi wa maeneo hayo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, walidai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupiga simu katika chumba cha habari kuwa idadi kubwa ya wanawake wanatolewa mimba kwa siku katika zahanati hiyo bubu ambayo haina jina wala hadhi ya kutoa huduma.
Baada ya hapo, waandishi hao wa kike walirejea ofisini na kutoa taarifa kwa mabosi wao ambapo timu kamili ilipangwa.
Mkuu wa timu hiyo alianzia Kituo cha Polisi Buguruni ambapo alitoa taarifa kuhusu malalamiko ya wakazi wa eneo hilo na jinsi muuguzi huyo alivyofikia hatua ya kutaka alipwe elfu hamsini ili kukamilisha zoezi.
Afande mkuu akatoa maagizo kwa watu wa chini yake watatu, akiwemo askari wa kike mmoja kwa ajili ya kwenda kumnasa nesi huyo.
NESI AENDA KUSUKA KWANZA
Msichana aliyepandikizwa kutolewa mimba akiwa na mwenzake walitangulia kufika kwenye zahanati hiyo lakini hawakumkuta muuguzi huyo.
Mfanyakazi mmoja wa zahanati hiyo alimweleza ‘mtolewa mimba’ kwamba nesi huyo alikwenda kusuka na tayari ameshawasiliana naye hivyo wasubiri.
SAA 10:30 alasiri, NESI ATOKEA
Saa kumi na nusu, muuguzi huyo aliwasili kwa ajili ya kazi hiyo huku mawasiliano yakifanyika kati ya mtolewa mimba na waandishi waliokuwa jirani na eneo la tukio.
Ndani ya dakika kumi, waandishi na polisi waliitwa eneo la tukio wakijulishwa kwamba ‘mjamzito’ huyo ameshavua nguo tayari kwa kazi ya kuchoropolewa mimba.
USO KWA USO
Kikosi kazi kilivamia zahanati hiyo ambapo walikuta zoezi linaendelea. Polisi wenye ujuzi wa kazi za kunasa matukio walimtia mbaroni muuguzi huyo akiwa na zana za shughuli huku wakimwambia kosa lake.
Wakati huo, mjamzito alikuwa yupo kitandani katika maandalizi ya kutolewa mimba.
MAJIRANI MENO NJE
Wananchi waliokuwepo eneo la tukio wakati mtanange ukiendelea, walionekana kufurahishwa na kitendo cha kukamatwa kwa muuguzi huyo huku wakidai walikuwa wamechoka naye kutokana na vitendo vyake vya kutoa mimba hadi kwa wanafunzi.
“Tumekuwa tukijitahidi kutoa taarifa katika vyombo vya dola ikiwemo ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu lakini hakuna hatua zozote zilizokuwa zikichukuliwa, ndiyo maana tukaamua kuwasiliana na nyie waandishi wa habari ili mtusaidie,’’ alisema mkazi mmoja bila kutaja jina lake.
SWALI KWA MUUGUZI
Muuguzi huyo alipoulizwa kwa nini amekuwa akijihusisha na vitendo hivyo, alikaa kimya.
MJUMBE ASHUHUDIA
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina Namba 26, Tawi la Mandela, Rogasian Chadima alikuwepo katika eneo la tukio baada ya kufuatwa na polisi, naye aliahidi kufuatilia suala hilo akisema kwanza hakujua kama kuna zahanati katika eneo lake.
SAFARI YA KWENDA POLISI
Safari ya kwenda polisi kwa mahojiano ilianza hapo huku muuguzi huyo akiwa na ‘ushahidi’ wake mkononi. Muda mwingi alionekana asiyeamini macho yake kwa kile kilichomtokea.
Imeandikwa na Makongoro Oging’, Mwaija Salum, Musa Mateja na Joan Lema.