Mwili wa Jambazi sugu  Emanuel Blasius Mdendemi ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani akiangalia mwili jambazi lililouwawa na kikosi cha polisi Mbeya
Baadhi ya polisi na waandishi wa habari wakiwa nje yajengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda
 wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio
 hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake 
ambapo alisema tukio hilo lilitokea  jana majira ya Saa 10(kumi) 
Alfajiri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesha baadhi ya siraha alizokutwanazo jamabazi huyo aliyeuwawa
Kamanda
 wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesaha hirizi iliyofungwa 
katika bunduki aliyokuwa anatumia jambazi huyo kama kinga katika matukio
 yake 
Hii
 ndiyo hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jamabazi 
huyo jamani waganga wakienyeji acheni hizo kuwadanganya watu matokeo 
yake ni kuongeza uhalifu nchini hakika nao tutawashughulikia kwani 
wamekuwa chanzo cha uhalifu nchini hayo yamesemwa na kamanda Diwani
Kamanda Diwani akiongea na waandishi wa habari     
MTU
 mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na 
Askari wa Jeshi la Polisi akiwa kwenye harakati za kuteka magari katika 
Eneo la Mlima Nyoka Jijini Mbeya baada ya kutokea kwa majibizano ya 
kurushiana risasi. 
  
Jambazi
 huyo ni miongoni mwa watu waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Polisi 
Mkoani hapa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Askari Polisi mwenye namba
 G 68 PC Jafari yaliyotokea  Februari 6, Mwaka huu  katika eneo la 
Matundasi Wilayani Chunya.
  
Kamanda
 wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio
 hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake 
ambapo alisema tukio hilo lilitokea  jana majira ya Saa 10(kumi) 
Alfajiri .
  
Kamanda
 Diwani alisema kabla ya tukio majambazi wapatao wanne  tayari walikuwa 
wameweka mawe barabarani kwa nia ya kuteka magari ili wafanye uporaji 
katika eneo hilo la Mlima Nyoka ambalo limekuwa na matukio kadhaa ya 
watu kuporwa mali zao.
  
Alisema
 Jeshi la polisi baada ya kupata habari za kutegwa mawe, askari walifika
 kwa wakati kwa kuwa polisi walikuwa jirani na eneo hilo na kuweka mtego
 kwa kuwa majambazi hawakuwa wameonekana kwa wakati ule.
  
Aliongeza
 kuwa baada ya muda majambazi walipoona taa za gari walijitokeza tayari 
kushambulia lakini kabla ya hapo polisi walitoa amri ya kujisalimisha 
kinyume chake wakaanza kupiga risasi ovyo ndipo mashambulizi ya polisi 
yakafanywa.
  
Diwani
 alisema katika mapambano hayo alijeruhiwa jambazi mmoja kwa risasi 
kiunoni na ubavuni kulia na wengine watatu walifanikiwa kutoroka ambapo 
Marehemu alipowahishwa hospitali kwa matibabu daktari alibaini kuwa 
amekwisha fariki.
  
Alisema 
 jambazi huyo alikutwa na silaha moja SMG yenye namba  AB huku namba 
 nyingine zikiwa zimefutwa na magazine yake ikiwa na risasi ishirini na 
mbili (22) pamoja na mapanga mawili([2).
  
Aliongeza
 kuwa baada ya  Marehemu kufanyiwa upekuzi maungoni mwake jambazi huyo 
alikutwa na kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la
 Emanuel Blasius Mdendemi aliyezaliwa mwaka 1984 eneo la Matamba 
wilayani Makete Mkoa wa Iringa makazi yake ni Uwemba Mkoani Njombe.
  
“Jambazi
 huyu amebainika kuwa ni miongoni mwa majambazi waliokuwa kwenye mtandao
 wa majambazi uliokamatwa hivi karibuni kuhusiana na matukio waliyofanya
 Mikoa mbalimbali ikiwemo Mbeya,Njombe na Iringa.aidha amebainika 
kushiriki katika tukio la mauaji ya askari polisi PC Jafari wa kituo cha
 Mkwajuni – Chunya tarehe 06.02.2013.” Alisema Kamanda Diwani.
  
Aliongeza
 kuwa  ufuatiliaji wa majambazi waliotoroka unaendelea kufanywa ambapo 
pia  anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao azitoe bila 
kuchelewa kwa jeshi la polisi ili zifanyiwe kazi.
Pia
  amewatahadhalisha majambazi na wahalifu wa makosa yeyote kuachana na 
uhalifu kwa kuwa ni biashara isiyo na faida badala yake wafanye shughuli
 halali kupata maendeleo ambazo fursa zake ni nyingi.