This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Thursday, March 7, 2013
waziri wa denmark aandaliwa dhima ya kitaifa
MAMA SALMA AZINDUA KISIMA CHA MAJI -MWANZA
mamilioni wamuaga rais wa venezuela
WANAWAKE WASHEREKE SIKU YAO KWA KUPEWA KIPAO MBELE
Ofisa Mawasiliano Mwandamizi, Mradi wa CHAMPION, Muganyizi Mutta akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa royal hotel mafinga wiki hii.
Na Denis Mlowe, Iringa
WANAHABARI nchini wametakiwa kuandika habari zinazolenga kukuza usawa wa jinsia katika vyombo vyao vya kazi.
Ofisa Mawasiliano Mwandamizi, Mradi wa CHAMPION, Muganyizi Mutta alisema hayo wiki hii wakati wa mafunzo ya wanahabari mkoani Iringa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Royal Park mjini Mafinga.Mutta alisema, uwiano wa habari zinazoripotiwa na vyombo vya habari nchini kuhusiana hauko sawa hivyo kushindwa kufikia malengo ya uwiano wa nusu-kwa-nusu ambao unahimizwa kwa sasa kote ulimwenguni.Alisema, vyombo vingi vya habari kuanzia magazeti, televisheni na radio kwa asilimia kubwa vimebeba habari za wanaume kuliko wanawake, jambo ambalo linapaswa kubadilika.
“Vyombo vingi vya habari vimeegemea katika habari ambazo hazina usawa kwa upande wa wanawake kuanzia kwenye habari zenyewe, picha zanazochapishwa na matangazo ambayo yameegemea upande wa jinsia ya kiume,” alisema.
Mutta alisema, tofauti ya uwiano huo inaanzia ngazi za chini katika jamii hadi kwenye sekta nyingine, hivyo kuwataka wanahabari kuondokana na mtazamo huo hasi ambao haulengi kuleta usawa na zaidi humbagua mwanamke.
Aidha, alitoa mfano wa vichwa vya habari vinavyotumika katika vyombo vingi vya habari, hususan magazeti, ambavyo vinamuonyesha mwanamke kama ndiye mwathirika mkubwa katika masuala yote ya ujinsia.
“Kati ya vitu vinavyokuwa na tofauti ni katika kuchagua vichwa vya habari, picha zinazochapishwa katika vyombo vya habari, sentensi zinazotumika na maneno vinaonyesha ni kiasi gani mwanamke anabaguliwa katika vyombo vya habari” alisema Mutta
Naye Paulina Kuye mwandishi wa habari wa radios Nuru Fm alisema kwamba wanawake wengi wanakosa kujiamini katika kufanya kazi za uandishi wa habari na kukata tamaa kutokana na kutokukubali kukosolewa.
“Sisi wanawake pia tunachangia sana kuwa wachache katika tasnia ya habari na kutojiamini kwetu nacho ni chanzo kikubwa sana kufanya fani hii kutawaliwa na wanaume” alisema Kuye.
Ipc yalaani alichofanyiwa kibanda
Na Francis Godwin,Iringa
KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) imeeleza kusikitishwa na wimbo la vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoendelea kujitokeza kwa wanahabari hapa nchini na kulitaka jeshi la polisi kuusaka mtandao huu wa utekaji wa wanahabari nchini.Akizungumza na wanahaari mjini hapa leo , Mwenyekiti wa IPC. Frank Leonard alisema muda umefika kwa wanahabari nchini kote bila kujali tofauti zao kufanya tathimini ya mahusiano na wadau wao ili tahadhari zianze kuchukuliwa.
Akizungumzia tukio la kinyama ambalo amefanyiwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini, Absolom Kibanda ambae pia ni Mhariri wa Kampuni ya New Habari, Leonard alisema nimuhimu kwa wanahabari kukataa kuendelea kushuhudia wenzao wakinyamazishwa kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na kuuawa.
Alisema katika mazingira ya kushangaza, ukuaji wa tasnia ya habari unaolenga kuchochea maendeleo ya nchi, unakwenda sambamba na mfululizo wa matukio yanayolenga kuipunguza kasi hiyo.
Alisema baadhi ya wanahabari wanaofuatilia na kuchapisha au kurusha matukio yanayohusu maslai ya umma wamekuwa wakifukuzwa, wakitukanwa, wakinyang'anywa au kuvunjiwa vifaa vyao vya kazi, wakipigwa na kuuawa jambo linaouwa semokrasia, haki na maendeleo ya nchi.
"Ni wazi usalama wa wanahabari upo mashakani; ni muhumi tukaitathimini hali hiyo na kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kupunguza mahusiano ya kudumu na wadau wasiopenda uwepo wa vyombo hivyo vya habari," alisema.
Alisema wakati matukio ya wanahabari kushambuliwa yakishamiri, kasi ya vyombo vya dola katika kuwasaka na kuwafikisha wahusika katika mikono ya sheria ni ndogo ikilinganishwa na matukio yanayohusu wadau wengine likiwemo jeshi la Polisi.
Leonard alisema wanahabari wanatakiwa kushikamana na kupaza sauti zao juu ili matukio ya aina hiyo yakomeshwe na yanapotokea wahusika wasakwe kwa nguvu zote na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Alisema unyama uliofanywa kwa Kibanda, unakumbusha majonzi kwa watanzania ambao bado hawajasahau jinsi Mwandishi wa Channel Ten na Mwenyekiti wa IPC, Marehemu Daudi Mwangosi alivyouawa kinyama na Polisi wakati akitimiza wajibu wake Septemba 2, mwaka jana katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Pia tukio la kutekwa kwa mtangazaji wa Redio Kwizera-Kibondo Issa Ngumba na kukutwa akiwa ameuwawa kinyama pamoja na matukio mengine ya uvamizi wa wanahabari likiwemo la akina Said Kubenea na Ndimara Tegambwage kumwagiwa tindikali wakiwa ofisini kwao.
"Tunajiona kama watoto tusio na msaada; kilio chetu hakifiki mbali; tuko katika wakati mgumu tunapokuwa katika mazingira ya kutimiza wajibu wetu kwasababu hatujui nani ni adui wa habari na wanahabari," alisema.
Wakati hayo yakitokea kwa wanahabari, Leoanard alikwenda mbali zaidi na kuzungumza uwepo wa baadhi ya wanahabari wanaofurahi wakiona wanahabari wenzao wanaokutwa na matukio ya aina hiyo.
"Wapo, tena wengi tu na wengine wanajulikana; kwa lugha za mtaani wanaitwa risasi kidole, kazi yao ni kuvujisha taarifa ya kazi zinazofanywa na wanahabari wenzao kwa wadau wanaofahamiana nao; lengo lao ni kupata ujira lakini ujira unaouwa haki ya watanzania ya kupata habari zinazohusu maendeleo yao bila kujali kama ni mbaya au nzuri," alisema.
Katika kuchochea maendeleo ya taifa, Leonard alisema habari ni muhimu katika ujenzi wa Taifa; ukimfanyia unyama mwandishi wa habari unaongeza manung'uniko katika jamii na kuzorotesha maendeleo.
Alisema Jeshi la Polisi linapaswa kutumia nguvu zake zote kuwasaka wahusika wa tukio lililomkuta Kibanda na kuwafikisha katika vyombo vya dola ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye hila dhidi ya wanahabari na vyombo vya habari.