This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, July 14, 2013

WANAJESHI 7 WA TANZANIA WAMEUAWA HUKO DARFUL- SUDAN

Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa. Taarifa zilizotufikia jana  zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali. Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao...

STARS KIMENUKA, YALALA 1-0 TAIFA

 Stars wakiwa vichwa chini baada ya matokeo ya leo. MATUMAINI ya timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kushiriki fainali za CHAN nchini Afrika Kusini imefifia baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes'. Taifa Stars imelala katika mechi ya kwanza iliyopigwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo, Stars inasubiri mechi ya pili… ...

WALIOMRUHUSU MASOGANGE APITE NA 'UNGA' AIRPORT NI HAWA!

HAKUNA sababu ya kumkamata ‘mchawi’  kwenye skendo ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kukamatwa na madawa ya  kulevya nchini Afrika Kusini wakati ukweli upo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.  Watu mbalimbali ambao wamesoma sakata hili kwenye vyombo vya habari, walitoa maoni yao wakisema kuwa watu wanaotakiwa kuwajibishwa ni waliokuwa uwanjani...

MWANAFUNZI WA IFM AFARIKI DUNIA AKIOGELEA KATIKA UFUKWE WA BAHARI YA HINDI

Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi wa Kompyuta wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Wendy Habakuki Lwendo amefariki dunia katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni akiogelea na wenzake watatu jana jioni.Taarifa kutoka kwa  kaka wa Marehemu, Sammy Lwendo amesema mdogo wao alipatwa na masaibu hayo akiwa na rafiki zake hao watatu wakiogelea baharini na wakati wanaogelea walikuwa katika eneo la kina kifupi cha...

MKUU WA MKOA MOROGORO AFUNIKA KWA KUCHEZA KWAITO UKUMBINI

Stori:Dustan Shekidele,MorogoroMKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera juzikati alionyesha wananchi wake umahiri mkubwa wa kuucheza muziki mtindo wa Kwaito huku akiwafunika vibaya vigogo wa Benki ya NMB Mkoa wa Morogoro waliokuwa wakicheza naye. Hapa Akikonga kwaito na wazee wenzake Bendera alionyesha umahiri huo ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Morogoro kwenye sherehe kabambe ya kumuaga aliyekuwa Meneja wa Benki ya  NMB Tawi...

RAY C AFUTUKA

Stori: Mwandishi  WetuMwanamuziki staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka. Hivi karibuni, Ray C ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na mashabiki wake.Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko...

SHEIKH MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AMWAGIWA TINDIKALI NA KUUMIZWA VIBAYA

Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea...