Na Mwandishi WetuMITANDAO
mingi ya kijamii na kurasa binafsi za mawasiliano zinazopatikana ndani
ya simu za viganjani kama Instagram, WhatsApp na BBM (Blackberry
Messenger) zinazomilikiwa na baadhi ya wasichana wanaosoma Chuo Kikuu
cha Dodoma (Udom) zimejaa mambo ya ngono na kashfa kwa baadhi ya wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Unyemeleaji taarifa
uliofanywa na Ijumaa kwa muda mrefu kwenye huduma hizo za mawasiliano
ya kisasa umebaini wanafunzi wa kike wamewabatiza jina la ‘mabuzi yao’
baadhi ya wabunge.
Bila kupepesa mitandao hiyo imekuwa pia
ikitumiwa na wasichana hao kuuza miili yao huku ufahari kama si ujanja
ukiwa ni mtu kujipatia bwana mwenye cheo cha ubunge ambaye anaaminika
waleti yake haikaukiwi fedha kutokana na posho za vikao na utumishi wa…
Na Mwandishi WetuMITANDAO
mingi ya kijamii na kurasa binafsi za mawasiliano zinazopatikana ndani
ya simu za viganjani kama Instagram, WhatsApp na BBM (Blackberry
Messenger) zinazomilikiwa na baadhi ya wasichana wanaosoma Chuo Kikuu
cha Dodoma (Udom) zimejaa mambo ya ngono na kashfa kwa baadhi ya wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Unyemeleaji taarifa
uliofanywa na Ijumaa kwa muda mrefu kwenye huduma hizo za mawasiliano ya
kisasa umebaini wanafunzi wa kike wamewabatiza jina la ‘mabuzi yao’
baadhi ya wabunge.
Bila kupepesa mitandao hiyo imekuwa pia ikitumiwa
na wasichana hao kuuza miili yao huku ufahari kama si ujanja ukiwa ni
mtu kujipatia bwana mwenye cheo cha ubunge ambaye anaaminika waleti yake
haikaukiwi fedha kutokana na posho za vikao na utumishi wa umma.
SIKILIZA TUKUPASHE
“Shoga naona unawapanga tu waheshimiwa,”
mchangiaji mmoja kupitia kundi la BBM alichangia kwenye moja ya picha
aliyoweka rafiki yake akiwa amepozi na mbunge mmoja kutoka mikoa ya
Magharibi (jina kapuni) ambapo bila haya majibu ya mwenye ukarasa huo
yalikuwa: “Maisha bila mabuzi hayaendi bi dada.”
Upekuzi wa
kiintelijensia wa Ijumaa ulichungulia dokezo za wachangia mada na
kubaini kuwa waheshimiwa wanaoingia mjengoni kama wawakilishi wa
wananchi wanachukuliwa kama mabuzi kwa tafsiri ya kuchunwa fedha huku
kipindi cha vikao vya bunge vikichukuliwa kama nyakati za migodi kutema
dhahabu.
MAMBO YA KUFEDHEHESHA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wasichana
hao wa chuo wamekuwa wakihifadhi picha za utupu za wabunge wenye
uhusiano nao kwenye simu zao za mikononi walizowapiga walipokuwa
wakifanya nao ngono ambapo wakati mwingine huzitundika
mitandaoni kwa kubipu na kuziondoa haraka lengo likiwa ni kuwaonesha ushahidi huo marafiki zao.
Miongoni
wa wabunge waliokumbwa na aibu hiyo ambao Ijumaa liliziona picha zake
za aibu ni pamoja na mbunge anayetoka kanda ya Kusini, mwingine kanda ya
ziwa na mmoja kutoka jijini Dar es Salaam huku waziri mwenye heshima
kubwa naye akiingia mkenge kwa kupiga picha na msichana wakiwa kitandani
vifua wazi.
WANAFUNZI WA KIUME WANASEMAJE?
Ijumaa lilipowauliza baadhi ya
wanafunzi wavulana wanaosoma chuoni hapo juu ya kuwepo kwa tabia za
baadhi ya wabunge kutembea na wanafunzi wa kike walikiri na kuongeza
kuwa ukata ndiyo unaosababisha baadhi ya wanachuo wajitongozeshe kwa
waheshimiwa.
“Wanachofuata ni fedha siyo mapenzi, wapo wasichana hapa
kipindi cha bunge hawaonekani kabisa chuoni, wanakuwa na waheshimiwa
wakistarehe, kuna wengine wanasomeshwa, wanahudumiwa,” alisema
mwanafunzi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Bonny.
IJUMAA LINASEMAJE?
Dawati la Ijumaa linawatahadharisha waheshimiwa
wabunge wenye tabia za ukware kuachana na mambo ya kihuni, badala yake
wajiheshimu vinginevyo watajikuta matatizoni na kuambulia aibu kubwa
mbele ya jamii kwa kuanikwa kwenye magazeti siku si nyingi pia picha zao
za aibu zitafikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.