This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, March 20, 2013

HATIMAYE SERIKALI NA TFF ZAFIKIA MUAFAKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU

Serikali imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF na Baraza...

HUU NDIO UNDANI YA MARIDHIANO YA TFF NA SERIKALI KUHUSU UCHAGUZI WA TFF

HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, zimekubaliana ujumbe kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kufika nchini muda wowote kuanzia sasa na kufanya mapitio upya (review) kwa wagombea walioenguliwa katika mbio za uchaguzi wa TFF. Rais wa TFF, Leodegar Tenga, leo hii amesema kimsingi wamekubaliana na wizara baada ya kikao...

MJADALA: ZIDANE, INIESTA NANI ZAIDI?

MJADALA: ZIDANE, INIESTA NANI ZAIDI? ZINEDINE Zidane ni mmoja wa wachezaji wenye kipaji cha aina yake waliowahi kucheza soka akiwa na Ronaldo De Lima. Akiwa na umri mdogo, Zidane alikuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza mashambulizi kupitia katikati ya uwanja huku akitumia uwezo binafsi na nguvu ipasavyo. Wakati huo alikuwa akichezea klabu ya Bordeux ya Ufaransa kabla hajasajiliwa na Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho ya thamani ya pauni...

SANDRA AITETEA NDOA YAKE

Sandra alifunguka hayo kupitia Stori 3 ambapo alisema taarifa hizo ndizo zilimpa hata mkosi kwani zilipoanza kuvuma ndiyo kipindi ambacho alipata ajali ya gari. “Sijawahi kuachwa, mimi pamoja na familia yangu tunafurahia maisha ya ndoa. Hao walioeneza hizo taarifa, walikuwa na lengo la kuniharibia na hawajaweza,” alisema Sand...

JB ATOA SOMO KWA WATANZANIA

Na Mwandishi Wetu BONGE la Bwana, Jacob Steve ‘JB’ amewataka Watanzania kuwa na wivu wa kimaendeleo ili kuweza kufika mbali kisanaa kwa kuiga mazuri. JB alifunguka hayo muda mfupi baada ya kutua Bongo akitokea nchini Rwanda walipokwenda kushuhudia Tuzo za Filamu zilizokuwa zikigawiwa kwa wasanii wa nchini humo. “Kuhusu zile tuzo inabidi na sisi tujifunze kuthamini vitu vya kwetu, wadau inabidi walitazame...

AIBU ILIYOJE! MKE WA MTU ABAMBWA ‘AKIBANJUKA’ NA SHEMEJI YAKE

Na Dustan Shekidele, Morogoro MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Bahati ambaye ni mke wa Mrisho Juma, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya aina yake baada ya kunaswa laivu ‘akibanjuka’ na shemeji yake. Tukio hilo lililoshuhudiwa na umati wa watu lilijiri Machi 11, mwaka huu mchana kweupee katika eneo la Mafisa kwa Mbambi ndani ya chumba cha Mbaji Hamis ambaye ni mdogo wa Mrisho. Akizungumza...

LULU: KANUMBA ALIKUWA ZAIDI YA MPENZI, MUME

Na Musa MatejaKWA mara ya kwanza tangu atoke mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar kwa dhamana, staa wa filamu na video za wasanii wa Bongo Fleva, Elizabeth Michael ‘Lulu’ au Lizy amefunguka juu ya uhusiano wake na aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba na kusababisha gumzo kubwa mitandaoni. Huku akipiga picha za pozi kwa mara ya kwanza tangu atoke selo, Lulu alifunguka wikiendi iliyopita kupitia ukurasa wake katika mitandao ya Instagram...

DIAMOND: NIMEMTUNDIKA MIMBA PENNY

Diamond akipozi na Penny. Kwa mujibu wa Diamond, ni kweli yeye na Penny ambaye ni presenta wa Kituo cha Runinga ya DTV wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kabla hata ya ndoa waliyopanga siku zijazo. Diamond alifunguka kuwa tayari amempa mrembo huyo gari la kutembelea huku akimwagizia lingine jipya aina ya Hyundai ix35. ...Wawili hao wakiwa katika pozi la kimahaba. “That’s true (ni kweli) nimemtia mimba Penny, unajua sipendi kusema...

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATOA POLE KWA WAFIWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Prince David, mtoto wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, marehemu WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana. Picha na OMR Picha ya Marehemu enzi za uhai wake. ...

MKUTANO WA KUTOA MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA SHERIA NAMBA 5 YA MWAKA1985 YA MAGAZETI WAFANYIKA ZANZIBAR

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo Fakihi Haji Mbarouk akitoa hotuba ya makaribisho kwa waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sheria namba 5 ya mwaka 1985 hapo katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar.  PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR. Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sheria namba 5...

MKUTANO WA SARPCCO WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa SARPCCO IGP Said Mwema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) baada ya kufungua mkutano wao wa siku mbili jijini Dar es Salaam.Mkutano huo utajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kufanya Operesheni za pamoja baina ya Nchi wanachama wa umoja huo.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi) ...

RC KANALI MSTAAFU ISSA MACHIBYA AYATAKA MAKAMPUNI YA SIMU KUDHIBITI VITENDO VYA UHALIFU KUIPITIA SIMU ZA MKONONI

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akifungua mkutano wa wadau wa Mawasiliano ulioandaliwa na TCRA mkoani humo kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazokabili sekta hiyo jana                          Wadau  mbalimbali Mawasiliano wakiwa katika mkutano huo Na Mwandishi wetu,Kigoma Mkuu wa mkoa kigoma...