HATIMAYE
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
zimekubaliana ujumbe kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa)
kufika nchini muda wowote kuanzia sasa na kufanya mapitio upya (review)
kwa wagombea walioenguliwa katika mbio za uchaguzi wa TFF.
TENGA AKATAA KUZUNGUMZIA KATIBA
Katika hali ya kushangaza, Tenga alikataa kujibu maswali ya waandishi wa habari yaliyokuwa yakihoji kuhusu katiba itakayotumika katika uchaguzi huo baada ya awali serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kuigiza TFF kutumia katiba ya mwaka 2008 na kuiacha ile ya 2012 inayoelezwa kupitishwa isivyo halali.
SERIKALI YAZIDI KUIKOMALIA TFF
Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi alisisitiza kwamba, Fifa watafika nchini na kufanya review yao kisha wao kama wasimamizi wa serikali wataipitia ripoti ya kazi hiyo kisha kuitolea maamuzi zaidi.
Tenga baada ya maafikiano hayo, TFF itaiandikia Fifa ambao ndiyo wanaosimamisha mchakato huo ili watume wajumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.
WAGOMBEA KUHOJIWA NA FIFA NA KAMATI YA RUFAA
Tenga amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani Fifa watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga, leo hii amesema kimsingi wamekubaliana na
wizara baada ya kikao cha jana kilichowaushisha Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fennela Mukangara, naibu wake, Amos
Makalla, Tenga na viongozi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), kwamba
Fifa waje kufanya review halafu uchaguzi uendelee.
“Tumeangalia
mambo mengi ya msingi kwa mustakabali wa mpira wa miguu Tanzania, tuna
heshima kubwa ya uongozi bora katika soka duniani. Hivyo tusingependa
sifa hii ipotee kienyeji, ndiyo maana TFF, wizara na BMT tulikutana na
kukubaliana kwamba, Fifa waje kufanya review ya kile kilichotokea halafu
majibu yakipatikana tuendelee na uchaguzi,” amesema Tenga.
Tenga
amesema, wamefikia uamuzi kwa kuwafikiria pia Watanzania wapenda
michezo na hata wagombea ambao wana haki ya kupigiwa kura huku wakiwa
hawahusiki na hiki kinachoendelea sasa.
“Kuna
watu hawahusiki na jambo hili kwa namna yoyote ile, sasa hawa
tumewafikirai sana na tumeamua tuwape haki yao haraka iwezekanavyo. Nina
imani nchi itabaki kuwa salama katika soka na upepo huu utapita,”
amesema Tenga.
Awali
Tenga alikuwa ameridhia kufanyika kwa review za mapingamizi ya wagombea
mbalimbali wa TFF, lakini ushauri wake huo ulitupwa mbali na Kamati
Huru ya Uchaguzi ya TFF na ile ya Rufaa. Baada ya hapo, ndipo serikali
ikaiagiza TFF kufuata katiba ya mwaka 2008 baada ya kupokea malalamiko
ya baadhi ya wagombea walioenguliwa.
Baadhi
ya wagombea waliochinjwa katika uchaguzi huo ni Jamal Malinzi
anayewania nafasi ya rais, Michael Wambura anayewania nafasi ya makamu
wa rais ma wengineo.
TENGA AKATAA KUZUNGUMZIA KATIBA
Katika hali ya kushangaza, Tenga alikataa kujibu maswali ya waandishi wa habari yaliyokuwa yakihoji kuhusu katiba itakayotumika katika uchaguzi huo baada ya awali serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kuigiza TFF kutumia katiba ya mwaka 2008 na kuiacha ile ya 2012 inayoelezwa kupitishwa isivyo halali.
“Jamani
swali kuhusu katiba sitalijibu hapa, hapa tunazungumzia uchaguzi na
mambo mengine yahusuyo,” amesema Tenga na hata aliposisitizwa kuhusu
umuhimu wa swali hilo, alijibu: “Hapa si mahala pake jamani.”
SERIKALI YAZIDI KUIKOMALIA TFF
Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi alisisitiza kwamba, Fifa watafika nchini na kufanya review yao kisha wao kama wasimamizi wa serikali wataipitia ripoti ya kazi hiyo kisha kuitolea maamuzi zaidi.
“Tumekubaliana
hapa kwamba Fifa waje kufanya review, hawa mabwana wakimaliza kazi yao
sisi tutaiangalia na kutazama kama haki imetendeka halafu ndipo
tutaruhusu taratibu za uchaguzi kuendelea,” amesema Malinzi.
Malinzi
alisema, kimsingi kikao chao na wizara na TFF kilikuwa cha amani na ana
uhakika mambo yataenda vizuri na kila mmoja atapata haki yake ipasavyo.
FIFA WANAKUJA, UCHAGUZI SI ZAIDI YA MEI 25
Tenga baada ya maafikiano hayo, TFF itaiandikia Fifa ambao ndiyo wanaosimamisha mchakato huo ili watume wajumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.
Tenga
ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia
ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama
walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali
ionekane imetendeka.
“Serikali
imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko
ni mbali. Fifa wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari.
Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano
tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze
kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema Tenga.
Amesisitiza
kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na Fifa
baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF
hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya
maana hata kidogo.
WAGOMBEA KUHOJIWA NA FIFA NA KAMATI YA RUFAA
Tenga amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani Fifa watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.
Pia
amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini
vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA
ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.
Amewakumbusha
wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina
katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna Fifa.
0 comments:
Post a Comment