Mkuu
 wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati (kushoto) 
akiwaelezea waandishi wa habari jinsi ya kutoa fedha  kwenye mashine za 
kutolea fedha za DTB kupitia huduma ya Vodacom M PESA ambapo sasa wateja
 wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote 
walipo nchini.  Huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia
 ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.… 
Mkuu
 wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati (kushoto) 
akiwaelezea waandishi wa habari jinsi ya kutoa fedha  kwenye mashine za 
kutolea fedha za DTB kupitia huduma ya Vodacom M PESA ambapo sasa wateja
 wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote 
walipo nchini.  Huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia
 ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim. 
Meneja 
 Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akitoa fedha kwa 
mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya kutoa fedha kupitia 
mashine za kutoa fedha za DTB kupitia huduma ya M PESA. Anayeshuhudia ni
 Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati. 
Salum
 Mwalim na Sylvester Bahati wakifurahi baada ya kutoa fedha kwa mara ya 
kwanza kupitia mashine za kutoa fedha za DTB kwa huduma ya M PESA. 
Dar es Salaam, 26th Machi, 2013 ...Ukuaji wa teknolojia ya huduma 
maarufu ya kutuma, kupokea fedha pamoja na kufanya malipo ya huduma 
mbalimbali kwa njia ya simu za mkononi ya kampuni ya Vodacom ya M-pesa 
inazidi kupanuka na hivyo kuongeza kiwango cha matumizi ya huduma hiyo 
kuzidi kuboresha maisha na kuyafanya kuwa rahisi zaidi. 
 Katika 
kufikia mafanikio hayo Benki ya Diamond Trust (DTB) leo imetangaza ubia 
wa kibiashara na kampuni ya Vodacom Tanzania ubia ambao unawawezesha 
wateja wa M-pesa kuwa na uwezo wa kutoa fedha kutoka katika akuanti za 
M-pesa kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM) za benki ya Diamond 
Trust. 
 Wakitangaza na kuzindua huduma hiyo jijini Dar es salaam
 Mkuu wa Kitengo za Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati,  
amesema hayo ni mafanikio mengine ya kibishara kwa benki hiyo ya DTB 
katika kupanua wigo wa huduma na namna benki hiyo inavyoweza kuunganisha
 teknolojia ili kuleta urahisi kwa watanzania. 
 “DTB inayo 
Furaha kubwa kuwa sehemu ya mapinduzi ya kiteknolojia hapa nchini. Hii 
ni huduma ya kwanza na ya aina yake ambayo hakuna shaka kwamba 
inaashiria uwezo wa DTB katika kuleta ufumbuzi wa namna bora ya kutumia 
teknolojia kurahisisha maisha.”Amesema Bahati 
 “Tukishirikiana 
na Vodacom tunawawezesha wateja wa M-pesa walio karibu na benki zetu na 
hususan mtandao wa ATM kuwa na uhakika wa kutoa fedha kutoka akaunti zao
 za M-pesa saa ishirini na nne katika siku zote saba za wiki.” 
 
Bahati amesema jambo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha 
upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na 
uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini.  
 Hata hivyo hii 
ni frusa ya kipekee kwa wateja wa benki ya DTB ambao wamejiandikisha kwa
 ajili ya huduma ya M-Pesa hawana haja tena ya kutembelea matawi ya 
benki hiyo ili kuweza kuweka amana zao au kuhamisha fedha kwa biashara, 
marafiki na familia zao. Pia uzinduzi wa huduma hiyo utawezesha kujenga 
urahisi wa kuruhusu wasiotumia huduma ya benki kupata huduma za kifedha 
karibu nao.  
 Azma ya DTB ni kuzidi kuongeza kasi na maboresho 
ya utoaji wa huduma kwa wateja wake na washirika wake wengine kwa 
kuhakikisha inaendelea kupanua wigo wa huduma zake ikiwemo kuongeza 
ATMs, matawi na huduma nyinginezo kwa lengo la kusogeza karibu huduma za
 kibenki nchi nzima.  
 Kwa upande wake Afisa Mkuu wa M- Biashara
 wa Vodacom Jacques Voogt, amesema, "Hii ni hatua nyingine ambayo 
tunaifikia leo. Kampuni ya Vodacom inaendelea kupanua mtandao wake wa 
huduma ya M-Pesa.”
 Voogtz ameongeza kuwa ubia huo ni mwendelezo wa 
azma ya kampuni ya Vodacom kutumia fursa za teknolojia ya M-pesa kuzidi 
kuleta amsiha ya watu mikononi mwao kutumia simu za kiganjani. 
 
“Wateja wa Vodacom M-pesa wanayo sababu nyingine ya kujivunia kuwa 
sehemu ya mtandao mpana wa huduma hii salama, rahisi na yenye kuaminika 
zaidi nchini wakiunganishwa na makampuni na hata tasisi zaidi ya 200 
kufanya malipo ya huduma na manunuzi kwa urahisi na wepesi zaidi kupitia
 simu za viganjani.”Aliongeza Voogtz  
 Kuhusu DTB…..
 Kuhusu Vodacom Tanzania: 
 Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya 
kushirikiana na jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake 
ya Vodacom Foundation. Vodacom Foundation ina nguzo kuu tatu: Afya, 
Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo imechangia zaidi ya 
miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo mbalimbali za 
kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa 
Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and 
Inclusion Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone. 
 
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza 
Tanzania inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Vodacom 
Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca,
 ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) 
Limited inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35 
zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.