Dawa za kulevya.
Kuhusu uvumi, vitu viwili vinavyotajwa sana ni ama kifo chake
kilisababishwa na kuchanganya madawa ya kulevya pamoja na vilevi
vingine, hivyo kutengeneza sumu iliyomuua au alibeba mzigo wa unga
tumboni ambao ulimchachia na kumtanguliza mbele ya haki.
Huku
tukisubiri ripoti hiyo kuwekwa wazi, Uwazi lipo kwenye wakati mzuri
kueleza kinagaubaga jinsi wasanii wa Kitanzania walivyogeuzwa makuli wa
kubeba mizigo ya madawa ya kulevya tumboni na kusafirisha kwenda nchi
mbalimbali.
Habari zinaeleza kuwa wasanii mbalimbali nchini,
wameingia kwenye mkumbo wa kusafirisha unga tumboni kutokana tamaa ya
utajiri na wakati mwingine ni baada ya kuona maisha yao ya kimuziki
hayawaendei vizuri.
Kutokana na kuingia kwenye biashara hiyo,
wasanii hao hususan wanamuziki, hutambuliwa zaidi kwa jina maarufu la
punda, kwa tafsiri kwamba wao ni sawa na mnyama huyo ambaye kazi yake
kubwa ni kubeba mizigo ya binadamu.
Hoja kuhusu jina hilo ni kwamba
wanaobeba madawa ya kulevya tumboni, wanajishusha thamani sawa na punda,
kwani binadamu ni wale matajiri wanaowabebesha mizigo hiyo.
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
USHUHUDA WA SUGU
Ukweli wa jinsi matajiri wauza unga
wanavyowatumia wanamuziki wa Kitanzania kama punda, unapewa nguvu na
ushuhuda aliowahi kuutoa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’.
Mbunge huyo ambaye anapewa heshima kwamba ni mmoja
wa waasisi wa Bongo Fleva, alimweleza mwandishi wetu kuwa kabla hajawa
memba wa jumba hilo la kutunga sheria, aliwahi kufuatwa na wauza unga
kumshawishi awe anabeba mzigo kwenda nao nje ya nchi.
“Jamaa
waliniambia kwa sababu mimi nasafirisafiri sana, passport (hati ya
kusafiria) yangu itakuwa imeshagongwagongwa sana, kwa hiyo ni rahisi
kwenda nchi tofautitofauti kwa urahisi, kwa hiyo wakataka niwe nabeba
unga.
“Kigezo cha pili waliona kwa sababu mimi ni mwanamuziki, kwa
hiyo ni rahisi watu kuamini ziara zangu ni za kimuziki. Nilikataa,
niliwaambia siwezi kufanya biashara hiyo kabisa,” alisema Sugu.
Mwaka 2011, mbunge huyo aliwahi kugusia hilo, wakati akitoa hoja
kuchangia bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa
serikali ni lazima iwasaidie wanamuziki wa Kitanzania kwa sababu
wanaibiwa sana, hivyo kuwafanya vijana kuona kimbilio rahisi la
kutajirika ni kuuza madawa ya kulevya.
“Mheshimiwa spika, serikali
isifanye ili kijana wa Kitanzania afanikiwe lazima auze unga, madawa ya
kulevya,” alisema Sugu na kueleza mfano huo wa jinsi alivyofuatwa
kushawishiwa na matajiri wa unga ili naye awe punda.
Jack Patrick.
PUNDA HULIPWA DOLA 3000 MPAKA 5000
Kwa mujibu wa mwanamuziki
maarufu wa dansi nchini (jina tunalo), kwa wastani punda hulipwa fedha
kulingana na umaarufu wake, kwa kuangalia kiwango cha mzigo anaobeba,
vilevile nchi anayopeleka.
“Mara nyingi watu wanalipwa dola 3000
(shilingi 4,800,000) mpaka dola 5000 (shilingi 8,000,000). Binafsi
nilishabeba madawa kutoka hapa Tanzania kwenda China, Botswana na Afrika
Kusini, kila nilipofikisha mzigo nililipwa dola 5000,” alisema
mwanamuziki huyo na kuongeza:
“Kuna kipindi nilinogewa, nikawa
sijishughulishi sana na muziki, kila mara nipo safarini nakwenda
kupeleka mzigo, nikirudi nipo vizuri na dola 5000 zangu. Hivi sasa
nimeacha baada ya watu wangu wa karibu kunishauri na kunieleza kwa
mapana hatari inayoweza kunipata.”
MTINDO WA SASA
Utafiti wa siku za hivi karibuni, umepata jawabu
kwamba wauza unga wengi, wanawatumia wanamuziki na wasanii mbalimbali
kusafirisha mizigo kwa sababu kwao ni rahisi kugongewa visa katika
balozi za nchi wanazokusudia kwenda.
“Kule inaweza kuandaliwa shoo
ya uongo na kweli, wewe unasafiri kwamba unakwenda kwenye hiyo shoo
lakini kumbe ni utapeli mtupu. Kule hauendi kama mwanamuziki, isipokuwa
ni punda tu,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
“Fikiria mtu
unakwenda kwenye shoo halafu ukumbini wanaingia watu 40, halafu huyo
mwandaaji anakulipa fedha zako vizuri, unalala hoteli nzuri, ukumbi
analipa, kodi anatoa. Hii biashara ya madawa ya kulevya ina siri kubwa.
Khaleed Mohamed ‘TID’.
“Kinachosikitisha kwa wanamuziki wenzetu ni kwamba hawajitambui. Watu
wanakufa jamani, kukubali kusafirisha madawa tumboni ni sawa kujiweka
katikati ya uhai na kifo. Zile dawa zikipata joto tumboni huponi.
Ukijisahau na kunywa kitu cha moto ni kifo.”
Mtoa habari huyo
aliendelea kubainisha kuwa wanamuziki wa Kitanzania wengi wanakuwa
nchini bila kazi mpaka wanakumbwa na hali ngumu ya uchumi kutokana na
kutopata shoo za kutosha, hivyo kuwawia rahisi kukubali ofa ya kubeba
madawa ya kulevya tumboni kwenda nchi mbalimbali.
“Hivi sasa kuna
wimbi kubwa. Watakwenda hivyo ila baadaye madawa hufeli tu. Naamini
itafika wakati tutashuhudia vifo vingi vya wanamuziki wetu. Mungu
akiniweka hai nitasema, kwani nawajua wanamuziki wengi punda,” alisema.
Aidha, mtoa habari huyo aliwataja wanamuziki sita nchini ambao
aliwataja moja kwa moja kuwa wanajishughulisha na usafirishaji wa madawa
ya kulevya lakini majina yao tunayahifadhi kwa sasa.
Ambwene Yesayah ‘AY’.
MWANAMUZIKI ALIVYOMSHAWISHI MFANYABIASHARA
Kuna mwanamuziki (jina
kapuni) ambaye hivi karibuni alirejea nchini baada ya kupata matatizo
akiwa nje ya nchi, aliwahi kumshawishi mfanyabiashara mmoja aingie
kwenye biashara ya madawa ya kulevya halafu yeye atakuwa anabeba.
Mfanyabiashara huyo (naye jina kapuni), alisema: “Nilishangaa yule dogo
ananiambia yeye yupo tayari kubeba mzigo kusafirisha kwenda Afrika
Kusini na nchi nyingine za Kusini ya Afrika.
“Aliniambia yeye
ameshaweza kubeba madawa ya wafanyabiashara wengine na wakapata faida
kubwa. Aliniambia faida ni mara mbili kwa asilimia 100. Nilimjibu siwezi
kufanya hiyo biashara, baadaye akiwa huko alipata matatizo na hivi sasa
yupo hapa nchini.”
MAMA WA MWANAMUZIKI NI TISHIO KWA KUUZA UNGA
Mama wa mwanamuziki mmoja wa Bongo Fleva (jina tunalo), mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam, ni tishio kwa biashara ya kuuza unga.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mama huyo amekuwa akiwatumia mabinti
mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam, kuwabebesha mizigo tumboni na
kuwasafirisha kwenda China na nchi za Kiarabu ambako ndiko lilipo soko
lake.
“Wapo watangazaji wameshabebeshwa mizigo na yule mama. Yeye
hasafiri na mzigo na ana watoto lakini hawabebeshi mizigo watoto wake,
ila anawatumia watoto wa wenzake,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
“Kama ingekuwa ni biashara nzuri kwa nini yeye habebi wala watoto wake?
Hawa dada zetu ambao wanapenda sana maisha ya haraka, inabidi wawe
macho, vinginevyo watakwenda na maji.”
Sandra Khan 'Binti Kiziwi'.
UPO MFANO WA BINTI KIZIWI
Mrembo Sandra Khan, aliyepata jina la
Binti Kiziwi baada ya kushiriki video ya wimbo wa Binti Kiziwi ambao ni
mali ya mwanamuziki Ally Mohamed Ahmad ‘Z-Anto’, alikamatwa Februari,
mwaka huu China na kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni.
Zipo tuhuma kwamba Binti Kiziwi, alikuwa kwenye safari moja na
mwanamitindo Jacqueline Patrick ambaye aliingia mitini baada ya kumwona
mrembo huyo ambaye ni mtalaka wa Z-Anto, akikamatwa na polisi wa China.
Madai yanasema kuwa Binti Kiziwi aliishiwa nguvu na kupata maumivu
makali ya tumbo baada ya kuwasili China, hivyo polisi walimchukua kwa
lengo la kumpa huduma ya kwanza ndipo wakabaini kwamba alikuwa amebeba
madawa ya kulevya tumboni.
Jack Patrick anakiri kwamba alishuhudia
Binti Kiziwi akikamatwa, ila aliona soo kujitokeza kusema anamjua, kwani
naye angewekwa ndani kama mtuhumiwa.
Upande mwingine, mume wa Jack
Patrick, Abdulatif Fundikira, hana muda mrefu tangu aachiwe kwa dhamana,
akikabiliwa na kesi ya usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.
WANAMUZIKI WANAVYOONGEA
Mwana-Hip Hop, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’,
alisema kuwa yeye hajawahi kusafirisha madawa ya kulevya tumboni, kwani
anafahamu kuwa kufanya hivyo ni tatizo, alifafanua:
“Ndiyo maana
mimi nafanya muziki kuelimisha jamii, kwa hiyo siwezi kufanya biashara
ya madawa ya kulevya. Watu wanaingia kwenye hiyo biashara ili watajirike
mapema, hicho ni kitu kibaya sana. Nawaomba wale wanaouza madawa ya
kulevya wabadilike, jamii inawategemea.”
Mkali wa Bongo Fleva,
Ambwene Yesayah ‘AY’ alisema: “Mimi sijawahi kuthibitisha kama kweli
wanamuziki wenzetu wanafanya hivyo, ila kama kweli wanafanya basi
wanahatarisha maisha yao. Kila anayefanya hivyo ajue kwamba akikamatwa
ndiyo mwisho wake. Nashauri wanamuziki tusipende maisha ya mkato.”
Seif Shaaban ‘Matonya’, alisema: “Mimi nimeshawahi kusingiziwa kwamba
nilikamatwa nje ya nchi kitu ambacho siyo kweli. Kwa watu ambao
wanafanya hiyo biashara, nawashauri waache, kwani madawa ya kulevya
yanatuharibia ndugu zetu.”
Mwanamuziki wa mduara, Zuwena Yusuf
Mohamed ‘Shilole’ alisema: “Mimi sijawahi kuona, ila kama ni hivyo
waachane na hiyo biashara kabisa.”
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s38ROvmsbKjqofagRDNIOU3DspHPOS3pp0akcxd9Vpukbj1voARu20QUd44rVwEvVYo9rPeiPVpW-6GQQDjwxvMBeG96YJ-pAGgnijwqQkNRNcq5njfuZFYHsmIYca9tIVuqeDtVPHVvBemhg5c_yrujGFVzOgbl0ouiXZZJ-UV90hdS0I4ZyUJ_i7lcmJBLPae0LOGi7KrS5w5ZaoUw74F47foqMYdw2vZepVnMWHR0T5DXSXVPk9LaNZKEtm=s0-d)
ATHARI ZA MADAWA KULEVYA
Wapo wanamuziki mbalimbali ambao wameshatajwa kwamba wanajihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, wimbi limekuwa kubwa mno.
Mwana-Hip Hop, Kulwa Maujanja wa Kundi la Mapacha, aliwahi kutoa
ushuhuda wake kwa mwandishi wetu kwamba aligongea sigara kwa wanamuziki
wenzake wawili (majina tunayo) na alipovuta, alikuta imewekewa madawa ya
kulevya.
“Kichwa kiliamka nikawa kama nimedata. Kesho yake
nilishinda kichwa kinauma sana. Kumbe wale ndugu zetu wanatumia madawa
ya kulevya, wanachanganya kwenye sigara,” alisema Kulwa.
Rashid
Makwilo ‘Chid Beenz’, aliwahi kukaririwa kwamba ameacha madawa ya
kulevya kama ilivyo kwa mwana Hip Hop mwenzake, Langa Kileo, ingawa yapo
madai kuwa wawili hao bado hawajaacha.
Wanamuziki wengine, Khaleed
Mohamed ‘TID’, Msafiri Saidi ‘Diouf’, Aisha Mbegu ‘Madinda’ na wengine
kibao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na utumiaji wa mihadarati.
Kuhusu athari zake, inashauriwa kitaalamu kwamba ni vema kuacha kutumia
madawa, kwani huharibu ubongo kwa sababu huua mishipa ya fahamu,
huathiri mfumo wa damu, husababisha mhemko na juu ya yote ni huchochea
shambulio la moyo (cardiac arrest) na vifo vya ghafla.
Albert Mangweha.
NGWAIR NA M2 THE P
Kuhusu Ngwair, alikuwa na rafiki yake Mugaza
Pembe ‘M2 The P’, wote walizidiwa pamoja lakini yeye alifariki dunia na
kumwacha mwenzake akiwa mahututi kwenye Hospitali ya Mtakatifu Helen
Joseph, Johannesburg, Afrika Kusini.
Yapo mambo matatu ambayo yanadaiwa lakini ripoti ya daktari au kauli ya M2 The P, ndivyo vinavyoweza kumaliza utata.
Mambo hayo matatu ni kwamba walizidisha kiasi cha unga, madai mengine
ni kwamba walitumia madawa yaliyoisha muda wake, hivyo kuwa sumu, tatu
ni kuwa walikuwa na mzigo tumboni ambao ulifumuka.