Stori:Sifael PaulKIFO
cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea
kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini
‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika,
Risasi Jumamosi linafungua kila kitu.
Hospitali aliyopelekwa
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia
ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo)
alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph
ambako mwili wa marehemu…
Stori:Sifael PaulKIFO
cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea
kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini
‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika,
Risasi Jumamosi linafungua kila kitu.
Hospitali aliyopelekwa
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia
ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo)
alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph
ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa kwenye Mochwari ya
Hillbrow.
M2 The P akiwa amelazwa Hospitali
Mbongo huyo alisema alifanikiwa kuutazama mwili wa marehemu Ngwea
ambapo ulionesha kuwa wakati wa kukata roho damu nyingi zilimtoka
kupitia puani na mdomoni kiasi cha kuwashangaza wauguzi.
Mwili wa Marehemu
NI SUMUAlisema muuguzi mmoja aliyekuwa akimtibu
mshirika wa marehemu, Mgaza Pembe a.k.a M2 The P aliyenusurika,
alimwambia wawili hao walionekana kuingiwa na kitu cha hatari na kibaya
sana mwilini jambo lililowashtua hata madaktari wenyewe.
Mama mzazi wa mangwea akiwa kwenye huzuni
Alisema muuguzi huyo alimweleza kuwa kitu walichokula au kulishwa
kiliwadhuru sana ndani ya miili yao na kusababisha mishipa ya damu kwa
Mangwea kupasuka hovyo kwa kuwa moyo ulizidiwa na presha ya msukumo wa
damu.
Mtanzania huyo alidai kuwa hata kama kweli wawili hao
walichanganya vileo kama watu wanavyodai, basi ule mchanganyiko ndiyo
uliotengeneza sumu mwilini akisisitiza kuwa hilo halina shaka kwa mujibu
wa muuguzi huyo.
Eneo atakalozikwa
“Unajua kuna watu wanapenda kuchanganya pombe kali kwa hiyo kuna
wanaodai wawili hao walichanganya ‘unga’, bangi na pombe kali.
Mchanganyiko huo tu wenyewe ni sumu tosha mwilini kwa binadamu yeyote
yule.
“Wataalam wanajua, ukichanganya pombe kali unapata upungufu wa
oksijeni katika damu hivyo unaupa moyo kazi ya ziada ya ‘kupampu’ damu
kwa kuwa presha inakuwa kubwa. Kwa hiyo kinachotokea ni kupasuka kwa
mishipa mikubwa ya damu, ndiyo maana damu zilitoka puani na kinywani kwa
wingi.
“Kwa kuchanganya vileo hivyo unatengeneza sumu ambayo
husababisha shambulio kubwa la damu na mfumo wa upumuaji kushindwa
kufanya kazi.
“Sasa usipowahishwa hospitali ili kuchomwa sindano ya limao, kifo kinakuwa njenje.
“Kwa vyovyote walikula au walilishwa sumu, daktari anasema mwili wa Ngwea umeharibika sana kwa ndani.
“Kile siyo kipigo, hakuna jeraha lolote la kupigwa, ile ni sumu,” kilidai chanzo hicho cha kuaminika.
SAA CHACHE KABLA YA KIFOHabari
za kina kutoka kwa mmoja wa watu waliokuwa nao kabla ya kukutwa na
tukio hilo zilieleza kwamba kabla ya kwenda kulala, Ngwea na mwenzake,
walikutana na baadhi ya Watanzania waishio Sauzi na kupiga stori kwenye
baa moja huku wakitaja majina ya wasanii wa Bongo Fleva waliotangulia
mbele ya haki.
Ilidaiwa kuwa kila jina la msanii marehemu lilipotajwa
Ngwea alikuwa akitamka ‘OMG’ (Ooh! My God) yaani Ooh! Mungu Wangu, bila
kujua kitakachomkuta baadaye.
MADAI MENGINE, MAISHA YA SAUZI Kuna
madai mengine kwamba baadhi ya Wabongo waishio Sauzi huwa wana maisha
ya kutegana hasa wakijua Mtanzania mwenzao kaenda kule akiwa na
‘mkwanja’ mrefu.
“Tatizo lingine ni kwamba kama walifanyiziwa na mtu
huo uwezekano ni mkubwa sana kwani huku jamaa wakikushtukia tu kuwa una
mkwanja, kwanza wanakuwa karibu sana na wewe ‘then’ ukikaa vibaya lazima
wakutoe uhai.
“Inawezekana akina Ngwea walifanyiziwa kwa kulishwa
sumu kwa sababu walikuwa wameshapiga mkwanja tayari kwa kurejea Bongo,”
alisema Mbongo huyo.
MCHUNGAJI ALIKIONA KIFO CHAKE MAPEMA!Mwezi
Machi mwaka huu, kupitia gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa la Machi
22-28, 2013 liliandika ukurasa wa mbele habari yenye kichwa; ‘MASTAA
WAWILI KUFA MWAKA HUU’ ambapo mchungaji maarufu jijini Dar alisema mwaka
2013 ameona katika maono yake vifo vya wasanii wawili wa Bongo.
Katika habari hiyo, mchungaji huyo alitahadharisha mapema kuwa wasanii wamrudie Mungu kwani upepo siyo mzuri kwao.
Mchungaji
huyo alieleza: “Mwaka huu ulipoanza, Januari 2, Sajuki (Juma Kilowoko)
aliaga dunia katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa lakini nimepewa
maono na Mungu kwamba wasanii wengine wawili watakufa mwaka huu.
“Katika
hayo maono niliona wasanii wenyewe, mmoja wa kike, mwingine wa kiume.
Wa kike ni msanii wa filamu, wa kiume anaimba hizi nyimbo za kisasa za
Bongo Fleva.
“Huyo wa Bongo Fleva siyo mkongwe sana kama wale
waanzilishi wa fani hiyo lakini anajulikana sana na mashabiki wengi.
Nyimbo zake zinajulikana pia.
“Huyu wa kike yeye ni mkongwe kidogo, halafu ni mweusi, zamani aliwahi kuwika sana lakini kwa siku za hivi karibuni amepoapoa.”
MANENO YAKE YALIJAA UTABIRIWatu
wa karibu waliokuwa wakichati na Ngwea kupitia mitandao ya kijamii
walisema siku za mwisho wa uhai wake, marehemu alipenda kutumia maneno
yenye kumtaja Mungu, Yesu au viashiria vingine vinavyofanana na hivyo.
TURUDI KWENYE TUKIOHabari
zilieleza kuwa baada ya majibu ya kilichomuua Ngwea kujulikana, mwili
wa staa huyo utaagwa kesho jijini Dar ambapo msiba upo kwa kaka yake
Mbezi Beach na baadaye mwili utasafirishwa kwenda mkoani Morogoro eneo
la Kihonda, nyumbani kwao.
NGWEA HAPA, BABA’AKE PALEHabari
kutoka msibani Morogoro zimeeleza kwamba marahemu Ngwea atazikwa jirani
kabisa na kaburi alilozikwa marehemu baba yake, mzee Kenneth Mangwea.
Huo ni ushauri wa familia yake.
HALI YA M2 THE PKwa
upande wake, M2 The P, hadi gazeti linakwenda mitamboni alikuwa
akiendelea na matibabu huko Sauzi huku hali yake ikisemekana inaendelea
kuimarika.
Ngwea alizaliwa Novemba 16, 1982 huko mkoani Mbeya (asili
yake ni Mkoa wa Ruvuma) akiwa mtoto wa mwisho katika familia yao.
Hajaacha mke wala mtoto.