This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Thursday, February 6, 2014
"SIDHANI KAMA USHIRIKINA UNAFAIDA KATIKA MUZIKI"...POMMY DIMPOZZ
Leo kupitia Clouds Fm double XXL katika jiwe la wiki rafiki yake wa karibu 'Ommy Dimpoz' aliweza kusema kwa upande wake hadhani kama vitu vya ushirikina vinaleta faida katika upande wa muziki na wala hajawahi kujihusisha navyo maishani mwake.
Swali:Mara ya mwisho baada ya kukutana na Diamond Platinum hamjawahi kuzungumzia mambo ya ushirikina"Kusema kweli mara mwisho nakumbuka nilikutana naye na tukazungumzia kuhusu show yangu lakini mambo mengi hatujazungumza.Ommy Dimpoz alisema
HIVI NDIVYO MATUMAINI ALIVYOPOKELEWA JIJINI DAR
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.
Mshuhudie Shilole akiwa ndani ya vazi la Kanga moja kitandani….
Domo langu limefanikiwa kuzinasa nakala adimu za picha hizo kama zinavyoonekana hapo chini
Wafahamu vijana 10 wa kitanzania wenye mvuto zaidi hapa nchini
Diamond Platnumz
Jina lake halisi ni Naseeb Abdul,so far ni msanii anayelipwa zaidi kuliko msanii yeyote wa bongo fleva hapa Tzee,na kuongoza kulipwa zaidi katika show zake za nje na ndani ya nchi.ukimuongelea Diamond platnumz hivi sasa Africa lazima utakuta idadi flani hivi ya watu wanamfahamu msanii huyu na hiyo ni mbali na huko ulaya na kwingineko duniani,ameweza kufanya kazi zake za muziki na wasanii wakubwa duniani na kuweza ku-share stage moja na wasanii akiwemo rick ross,Ludacriss ,Psquare na wengine wengi,mbali na muziki pia ni ambassador wa cocacola zero,goodwill ambasador wa malaria na ni moja ya wasanii wanaosaidia na kujitolea katika shughuli mbalimbali za kusaidia jamii.
Flavian Matata
Kutoka mshindi wa kwanza wa miss universe Tanzania mwaka 2007 na kwenda kuiwakilisha tanzania mwaka huo huo,Flaviana aliweza kuingia kwenye top 15 , kuingia nusu fainali na baadae kushika nafasi ya Sita na ndiye aliyekuwa mtanzania wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya miss universe huku akiwa amenyoa nywele zake tofauti na washiriki wenzake,it was a game changer kwa jina la Tanzania kujulikana kuwa kuna vipaji vingi vilivyofichika. Matata ameshiriki katika matangazo mengi sana akiwa kama model,mwaka 2011 aliweza kushinda tuzo ya model of the year award ya Arise magazine ya huko nchini Lagos Nigeria,ametokea katika magazine mbalimbali duniani yakiwemo Dazed & Confused, Glass Magazine, L’Officiel and i-D Magazine. mbali na advertisement amefanya modeling ya mavazi ya brand za wanamitindo maarufu duniani kama Mustafa Hassanali, Vivienne Westwood, Tory Burch, Suno, na Louise Gray,pia kushirikishwa katika picha za kutangaza collection ya mwanamitindo maarufu duniani , Alexander McQueen katika Topshop Spring 2011 ad campaign.Flaviana matata baada ya kuchukua tuzo ya “Face of Africa” aliweza kuwasaidia wanawake wenzake na anaendelea na kampeni yake katika kusaidia wasichana waweze kwenda shule kupitia foundation yake, Flaviana foundation.amekuwa ni kioo cha wanawake na vijana wengi sana hapa Tzee.
January Makamba
Hashim Thabeet
Lady Jay Dee
Ni moja kati ya wanawake wenye majina makubwa sana hapa mjini,ikiwa ni msanii mkubwa sana wa kike anayeheshimika kutokana na kazi zake nzuri za kimuziki, anamiliki biashara mbalimbali hiyo ni mbali kabisa na muziki unaosemekana unamuingizia hela nyingi sana,mbali na muziki pia ni mjasiliamari mkubwa sana,akiwa ni CEO wa Nyumbani Lounge ,Studios na biashara nyingine nyingi,she is a hustler.ukimuongelea lady jay dee ni msanii wa kike mwenye umaarufu na utajiri mkubwa, anapendwa na kila mtu na kukubalika sana kimuziki na nje ya mziki huu wa Bongo fleva.
Jerry slaa,
Osse Greca Sinare
Talking about photographers maarufu sana hapa Tanzania na nje ya Tanzania,Osse is the name to be mentioned, Jina lake na kazi yake imeweza kutambulika na mataifa mbali mbali hata nje ya Tanzania,na kuweza kuongelewa na baadhi ya majarida na mitandao mikubwa sana ikiwemo Africa-vogue,fashion Ghana.com ,FAS mgazine na Msongo,si tu hapo pia ameweza kufanya interview nyingi sana na media kubwa africca ikiwa inaongelea kazi zake kwa kutambua uwezo wa kazi zake,mwaka 2012 aliweza kupikea tuzo kutoka Swahili Fashion Week tuzo ya Best Fashion Photographer,pia hujishughulisha na kazi za kusaidia jamii katika kuleta mabadiliko katika maisha ya jamii zetu za hapa Tanzania.
Zitto Kabwe
Jina lake halisi anaitwa Kabwe Zuberi Zitto ila maarufu anajulikana tu kama Zitto Kabwe,huyu ni mmoja wa wanaharakati wanaojitahidi kutetea haki za wananchi bila kuficha lolote lile kwa hadhira,ni moja ya tunda litokalo kwenye chama cha demokrasia,pia ni mheshimiwa mbunge wa jimbo la huko kigoma,ni moja kati ya vijana wenye umri mdogo na kuweza kutikisa sana nchi haswa kwa hoja zake,umahiri wake kisiasa ndio moja ya vitu vinavyopelekea kuzidi kupendwa sana na wananchi na hasa katika swala zima la kutetea haki za wananchi,ni kijana hodari sana inapokuja kwenye swala zima la siasa.
Patrick Ngowi
Tupe Maoni yako hapo chini
Mbunge Chadema Kortini vurugu za Udiwani Kahama
Kasulumbayi na wenzake 15, ambao wanaaminika kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama saa 8.00 mchana jana na kusomewa mashtaka sita kila mmoja.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Gadiel Mariki, Mwendesha Mashtaka Shukrani Madulu alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitenda makosa hayo Februari 4, mwaka huu.
Madulu aliiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao wakiongozwa na mbunge huyo walitenda kosa hilo la kuwashambulia kwa mapanga wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za kuwania udiwani wa Kata ya Ubagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka yote na kuomba mahakama iwape dhamana ili waendelee na kampeni za kumnadi mgombea wao wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo ya Ubagwe.
Maombi hayo yalipingwa na Mwendesha Mashtaka, akiiomba mahakama isitoe dhamana kwa kuwa hali za majeruhi watatu ni mbaya kwa kuwa tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Rufaa na Bugando mkoani Mwanza, baada ya matibabu yao kushindikana wilayani Kahama.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mariki alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo kesi hiyo itasikilizwa.
Watuhumiwa wote walipelekwa mahabusu baada ya dhamana hiyo kuzuiliwa.
Waliojeruhiwa kwenye vurugu
Wafuasi watano wa CCM wilayani Kahama akiwamo ofisa mtendaji wa Kata ya Ubagwe walijeruhiwa kwa mapanga kwenye vurugu hizo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Andrew Emmanuel alisema Masunga, Kamaro na Peter walisafirishwa kwenda Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Chanzo cha vurugu
Vurugu hizo zilitokea juzi saa moja usiku katika Kata ya Ubagwe muda mfupi baada ya wafuasi hao kumaliza kampeni zao za kumnadi mgombea wa CCM, Hamis Majogolo anayewania udiwani kwenye kata hiyo.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, wafuasi hao walikumbwa na mkasa huo wakati wakiwa kwenye gari la CCM ambalo pia lilikuwa na watuhumiwa watatu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipelekwa Kituo Kidogo cha Polisi Bulungwa.
Ilidaiwa watuhumiwa hao nao walidaiwa kufanya fujo kwenye mkutano wa Kampeni wa Chama cha Tadea ambacho pia kina mgombea anayewania nafasi hiyo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa wanachama wa Chadema waliweka kizuizi kwa kutumia gari la Kasulumbayi kwenye barabara ya kuelekea kituo kidogo cha polisi.
Peter, ambaye ni dereva wa gari la CCM alisimulia kuwa walipofika kwenye kizuizi hicho walisimama, ndipo wafuasi wa Chadema waliposhuka kwenye gari la Mbunge huyo na kuanza kuwashambulia kwa mapanga wakitaka kuwaokoa wenzao watatu.CHANZO MWANANCHI
Watatu wakamatwa Njombe
Pia Jeshi la Polisi wilayani Njombe linawashikilia watu watatu wanaodaiwa kufanya fujo katika ofisi ya CCM ya tawi la Matalawe, Jumatatu iliyopita.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani alisema kuwa watu hao walikwenda kwa gari kwenye maeneo ya tawi hilo na kuanza kuchana picha za mgombea udiwani wa CCM, Menard Mlyuka.
Aliwataja watu waliokamatwa kuwa ni Award Karonga (40), Ally Mhagama (43) na Robert Mabu (24)
FAMILIA KUMINA TANO HAZINA MAHALA PAKUISHI GEREZA PAWAGA
Nini hatma ya kesi ya Kenyatta ICC?
Pande zinazohusika katika kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC Mjini The Hague zimekuwa na kikao cha kujadili mstakabali wa kesi hiyo.
Kiongozi wa mashtaka wa ICC Fatou Bensouda amekiri kuwa bado hana ushahidi wa kutosha kuwezesha kesi hiyo kuendelea.
Mawakili wanaomwakilisha Rais Kenyatta wanataka kesi hiyo kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007 itupiliwe mbali.
Bensouda amesema kuwa bado kuna maswala yanayozua utata na ambayo yanahitaji uchunguzi wa kina. Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mashahidi wengi wamehongwa au kutishwa kiasi cha kujiondoa katika kesi hiyo.
Viongozi wa mashitaka ICC wanasema kuwa Kenyatta aliongoza ghasia hizo lakini kesi dhidi yake imefanywa dhaifu kutokana na baadhi ya mashahidi kujiondoa katika kesi hiyo.
Wakili wa waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi amesisitizia mahakama kuwa kutupiliwa mbali kwa kesi kutawakosesha waathiriwa haki. Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi katika siku chache zijazo.
Rais Kenyatta alifikishwa ICC kutokana na tuhuma kuwa alikuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007/2008. Anakabiliwa na makosa ya mauaji na uhalifu mwingine dhidi ya binadamu.
Kadhalika Kenyatta alishitakiwa pamoja na makamu wake William Ruto kwa tuhuma sawa. Kesi dhidi ya Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.
Watu 1,200 walipoteza maisha yao katika ghasia za uchaguzi mkuu mwaka 2007/08 huku maelfu wakilazimika kutoroka makwao. Wote wamekanusha mashitaka.
Kesi yenyewe ilitarajiwa kuanza Jumatano, lakini ikaahirishwa kwa mara ya nne mwezi jana wakati ambapo wendesha mashitaka waliposema kuwa shahidi mwingine alijiondoa kwenye kesi huku wakiomba mahakama kuwapa muda zaidi kutafuta ushahidi. CHANZO BBC SWAHILI