This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Monday, March 4, 2013
AZAM YAPONGEZWA KUITOA TANZANIA KIMASOMASO MICHUANO YA AFRIKA
Shirikisho
 la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa timu ya Azam ya 
Tanzania Bara kwa kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la 
Shirikisho iliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Ushindi
 wa jumla ya mabao 8-1 ambao Azam imeupata dhidi ya Al Nasir Juba ya 
Sudan Kusini si fahari kwa timu hiyo tu, bali Tanzania kwa ujumla, na 
unaonyesha jinsi klabu hiyo ilivyojipanga kiushindani katika michuano 
hiyo ya Afrika.
Hata
 hivyo, ni vizuri Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, benchi la ufundi na
 wachezaji wa timu hiyo wakautazama ushindi huo kama changamoto kwao 
kuhakikisha wanajipanga vizuri zaidi kwa raundi inayofuata.
Timu
 ya Azam inayofundishwa na Mwingereza John Stewart Hall ilishinda 
nyumbani mechi ya kwanza mabao 3-1, na jana kuibuka na ushindi wa mabao 
5-0 ugenini jijini Juba.
Kwa
 kufanikiwa kuing’oa Al Nasir Juba, Azam sasa watacheza raundi ya kwanza
 (raundi ya 16 bora) ya michuano dhidi ya Barrack Y.C.II ya Liberia 
ambayo katika raundi ya awali iliitoa Johansens ya Sierra Leone. Barrack
 ilishinda bao 1-0 nyumbani katika mechi ya kwanza na kulazimisha suluhu
 katika mechi ya marudiano jijini Freetown.
Azam
 itaanzia mechi hiyo ugenini kati ya Machi 15,16 na 17 mwaka huu wakati 
mechi ya marudiano itachezwa Tanzania kati ya Aprili 5,6 na 7 mwaka huu.
 
PICHA ZA PAMBANO NGUMI LA JAPHET KASEBA DHIDI YA MANENI OSWARD 'MTAMBO WA GONGO'
Bondia Japhert Kaseba akinyooshwa mkono juu na refarii Antoni Ruta baada ya kuibuka mshindi kwa kumgalagaza Maneno Osward picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com