This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Friday, March 29, 2013
MUUAJI WA PADRE MUSHI - ZANZIBAR AMEKAMATWA LEO
HUYU NDO BINTI ALIYECHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA MPENZI WAKE BAADA YA KUBUSU KIFUA CHA DIAMOND JANA
Binti uzalendo ulimshinda, akaenda kumnyonya matiti Diamond
Binti huyo akilia baada ya kuvutwa na kuchezea kichapo kutoka kwa bwana wake
Binti alipokua kwenye show ya Diamond, uzalendo ulimshinda, akaenda kunyonya chuchu za diamond kama inavyoonekana pichani Kitendo hicho kilimuudhi bwana wake, ambapo alimvuta binti huyo na kumchapa makofi. Katika picha ya pili, binti huyo anaonekana akilia baada ya kuchezea kichapo, huku akiwa amewekwa “chemba” na boyfriend wake.
RAIS KIKWETE AWAONGOZA VIONGOZI KUMUAGA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHAMBANI, SALIM HEMED KHAMIS
kuaga mwili wa marehemu, Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa maziko, yatakayofanyika leo.
SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,134
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Daudi alifafanua kuwa Waajiri hao ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizaraya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto,…
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Daudi alifafanua kuwa Waajiri hao ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizaraya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili.
Wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,
Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.
Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino, Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.
Katibu huyo amesema kuwa nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (Nafasi 10), Afisa Vipimo II – Nafasi 6, Mpima Ardhi daraja la II (Nafasi 26), Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9, Afisa Mipango Miji daraja la II– Nafasi 13, Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16), Mhandisi daraja la II - Maji (Nafasi 13), Afisa Misitu daraja la II (Nafasi 7), Afisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3, Mtakwimu Daraja la II – nafasi 8, Mthamini daraja la II – Nafasi 7, Mkadiriaji Ujenzi daraja la II – nafasi 4, Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II – nafasi 1, Mhandisi Daraja la II – Nishati (Nafasi 3), Msanifu Majengo Daraja la II– (nafasi 3) na Mjiolojia Daraja la II – Nafasi 7, Fundi Sanifu daraja la II (Ujenzi) -Nafasi
26, Mvuvi Msaidizi Daraja la II – nafasi 8 na Fundi Sanifu Msaidizi (Maji) -nafasi 19.
Nafasi nyingine zilitotangazwa na Serikali ni Nahodha Daraja la II – Nafasi 6, Fundi Sanifu daraja la II - Haidrolojia -Nafasi 6 ,Fundi Sanifu Daraja la II -Nafasi 6, Msaidizi Misitu Daraja la II – nafasi 7, Fundi Sanifu Daraja II – Ramani – Nafasi 6, Fundi Sanifu Daraja la II –Maendeleo ya Jamii– Nafasi 3, Dereva Mitambo Daraja la II– nafasi 1, Mpiga chapa msaidizi- Nafasi 5, Operata wa kompyuta msaidizi - nafasi 3, Fundi Sanifu Daraja la II - Migodi – nafasi 9, Polisi Msaidizi– Nafasi 5, Mpokezi–Nafasi 1, Katibu Mahsusi daraja la III-nafasi 10, Mlinzi –Nafasi 100, Dereva Daraja la II – nafasi 178, Msaidizi wa Ofisi– Nafasi 30, Afisa Kumbukumbu daraja la II– nafasi 1, Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya – nafasi 5, Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la III– nafasi 10, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II– nafasi 6.
Aidha, kada nyingine ni Afisa Mtendaji wa Kijiji daraja la III) – nafasi 232, Afisa Mtendaji Mtaa daraja la III– nafasi 3, Afisa Lishe daraja la II– nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II - Ufundi na Umeme, Afisa Biashara msaidizi– Nafasi 1, Mchapa Hati daraja la II – Nafasi 1, Mhandisi Daraja la II –Baharini-(nafasi 1), Dereva Mitambo Daraja la II – (nafasi 1), Dereva wa Vivuko daraja la II – Nafasi 3, Mkufunzi Mwandamizi Daraja II - Nafasi 1, Mkufunzi Daraja ii - Nafasi 2, Fundi Sanifu Msaidizi (bomba)–nafasi 3, Fundi Sanifu Msaidizi (Umeme) –Nafasi 4, Mkufunzi Daraja II– nafasi 3, Mkufunzi daraja la II -Jiolojia – nafasi 1, Mkufunzi Msaidizi– Jiolojia – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II -Ubunifu Mipango Miji – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II- Urasimu Ramani – Nafasi 5, Fundi Sanifu daraja II- Uchapaji Ramani –Nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II -Maabara– nafasi 13, Fundi Sanifu Msaidizi (Ujenzi– nafasi 1), Fundi Sanifu daraja la II -Nafasi 4, Wakufunzi wasaidizi – nafasi 54 na Mhasibu Mkuu daraja II.
Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 zilizoko katika tangazo la Kiswahili ni kwa ajili ya Waajiri walioainishwa hapo juu na kwa Tangazo la nafasi wazi 185 zilizoko katika tangazo la lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya Taasisi na Wakala mbalimbali za Serikali.
Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9 Aprili, 2013.
Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Machi, 2013
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz au Simu; 255-687624975
HIVI NDIVYO GHOROFA LILIVYOANGUKA POSTA JIJINI DAR
RECHO: SINA UHAKIKA WA KUOLEWA NA SAGUDA
MSANII wa filamu Bongo, Rachel Haule ‘Recho’ amefunguka kuwa japokuwa wamekaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na mpenzi wake George Saguda bado hana uhakika kama ndiye atakayemuoa.
Akichonga na paparazi wetu, Recho alisema kuwa kutoka moyoni anampenda Saguda na anatamani siku moja awe mume wake ila kufanikiwa wao kuoana anamuachia Mungu kwani ndiye anayepanga kila jambo
“Suala la ndoa namuachia Mungu kwa sababu wapo mastaa wengi waliochumbiwa lakini wameishia kuzalishwa na kuachwa hivyo mimi naamini kama Mungu amenipangia Saguda awe mume wangu atanioa lakini kama…
Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Rachel Haule ‘Recho’ amefunguka kuwa japokuwa wamekaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na mpenzi wake George Saguda bado hana uhakika kama ndiye atakayemuoa.
“Suala la ndoa namuachia Mungu kwa sababu wapo mastaa wengi waliochumbiwa lakini wameishia kuzalishwa na kuachwa hivyo mimi naamini kama Mungu amenipangia Saguda awe mume wangu atanioa lakini kama siyo basi siwezi kulazimisha,” alisema Recho.
MSANII MAARUFU AMFUMANIA,ANYWA SUMU
MCHEKESHAJI wa Kundi la Mizegwe, Rashid Coster ‘Maringo Saba,’ anadaiwa kumfumania mkewe anayefahamika kwa jina la mama Zai kisha kuamua kunywa sumu ikisemekana kuwa alitaka kujiua kwa hasira.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina kimenyetisha kuwa, Maringo Saba aliandaa mtego wa fumanizi baada ya kuhisi mkewe anamsaliti kwa rafiki yake anayefahamika kwa jina moja la Sam.
Chanzo hicho kilizidi kushuka na mistari kwamba, baada ya staa huyo kuandaa mtego, ulizaa matunda Jumatano ya Machi 20, mwaka huu ambapo alimfumania mkewe akijivinjari na jamaa.
Sosi huyo alizidi kubainisha kuwa, mke wa Maringo Saba alipoona mumewe amemjazia umati kwa fumanizi hilo, alitimua mbio kwa vile ilidaiwa Maringo Saba alitishia kumfanyia kitu mbaya.
“Ilikuwa vurumai,…
MCHEKESHAJI wa Kundi la Mizegwe, Rashid Coster ‘Maringo Saba,’ anadaiwa kumfumania mkewe anayefahamika kwa jina la mama Zai kisha kuamua kunywa sumu ikisemekana kuwa alitaka kujiua kwa hasira.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina kimenyetisha kuwa, Maringo Saba aliandaa mtego wa fumanizi baada ya kuhisi mkewe anamsaliti kwa rafiki yake anayefahamika kwa jina moja la Sam.
Chanzo hicho kilizidi kushuka na mistari kwamba, baada ya staa huyo kuandaa mtego, ulizaa matunda Jumatano ya Machi 20, mwaka huu ambapo alimfumania mkewe akijivinjari na jamaa.
Sosi huyo alizidi kubainisha kuwa, mke wa Maringo Saba alipoona mumewe amemjazia umati kwa fumanizi hilo, alitimua mbio kwa vile ilidaiwa Maringo Saba alitishia kumfanyia kitu mbaya.
“Ilikuwa vurumai, watu waliokusanyika kufanya fumanizi walimtembezea kichapo Sam kabla hajafanikiwa kuchoropoka kwenye himaya ya chumba hicho na kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mwananyamala CCM,” kilisema chanzo.
Chanzo kingine kilicho karibu na mchekeshaji huyo (jina lipo) kilidai kuwa, baada ya tukio hilo, Maringo Saba alikutwa chumbani kwake amezidiwa ndipo ndugu zake walipomkimbiza kwenye Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za madaktari, imedaiwa kuwa staa huyo alikutwa na kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambayo haikujulikana mara moja ni ya aina gani.
Mara baada ya taarifa hizo kutua kwenye dawati la Amani, waandishi wetu walifika Hospitali ya Mwananyamala na kumkuta mchekeshaji huyo akiwa amewekewa dripu za dawa huku ndugu zake wakisema jamaa alichanganya pombe na dawa na siyo sumu kama ilivyodaiwa.
“Ndugu yetu hakunywa sumu, alichanganya dozi ya malaria na pombe ndiyo maana alizidiwa ghafla,” alisema mmoja wa ndugu hao aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Khalfan.
Hata hivyo, maelezo ya Rashid yalipingana na ya baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo ambao kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini walikiri msanii huyo kukutwa na sumu mwilini.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwinjuma, Allen Mwakitalima alikiri kuwepo kwa fumanizi, lakini kuhusu kunywa sumu alisema alisikia kwa watu mtaani ingawa kwake hajafikishiwa taarifa rasmi.
“Habari za fumanizi kwa Maringo Saba lilifika kwangu kiofisi, hata polisi walishakuja kuniulizia, ila kuhusu kunywa sumu nilisikia kwa watu mtaani, lakini sijapata taarifa rasmi kutoka kwa mjumbe wake, kwa hiyo likinifikia nitalishughulikia kiofisi,” alisema mwenyekiti huyo.