Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiangalia hali ya uokoaji inavyoendelea.
Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akitoa maelekezo ya jinsi ya kuondoa kifusi eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) akifuatilia shughuli ya uokoaji.
Watu mbalimbali wakiondoa kifusi.
Askari aliyejuu ya farasi akihakikisha usalama eneo hilo.
Baadhi ya watu wakilisukuma gari ambalo pia lilikuwa kwenye ajali hiyo.
Mama Salma Kikwete (kulia) na Rais Kikwete wakiangalia kifusi.
Kijana aliyenusurika katika ajali hiyo akinywa kahawa.
LEO majira ya saa mbili na nusu asubuhi Watanzania wameingia kwenye
vilio baada ya jengo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa
ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar
es Salaam, kuanguka na kuwafunika watu waliokuwa eneo hilo na
kusababisha wengine kupoteza maisha. Mpaka sasa haijajulikana idadi
kamili ya watu waliokuwemo ndani yake, ila watu wawili wamethibitishwa
kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment