Mhe. rais wa zanzibar Dr Shein na 
viongozi wengine wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya marehemu Bi 
Kidue kabla ya kuhifadhiwa kwenye jeneza.
Makamu
 wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika dua ya 
pamoja kumuombea Gwiji la sanaa Zanzibar Bi. Fatma Binti Baraka (Bi. 
Kidude) nyumbani kwake Rahaelo nyuma ya Studio ya ZBC Redio.
Makamu
 wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na baadhi
 ya Familia ya Bi. Kidude wakati alipofika kutoa mkono wa pole kwa ndugu
 na jamaa wa msanii huyo. Kushoto kwa Balozi  ni Ndg. Haji Ramadhani 
Suwed na kulia ni Bw. Abdullrahman Saleh.
Umati
 mkubwa wa Wananchi walioshiriki mazishi ya Msanii Gwiji wa sanaa kanda 
ya Afrika Mashariki na Mipaka yake  Bi. Fatma Binti Baraka (Bi Kidude) 
nyumbani kwake Rahaleo nyuma ya Studio ya ZBC Redio.
 Baadhi
 ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakiendelea na dua ya kumuombea msanii 
Gwiji wa Taarab Bi. Fatma Binti Baraka ( Bi Kidude) nyumbani kwake 
Rahaleo.
------------  
Serikali
 ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kugharamia mazishi ya Gwigi la Sanaa 
ndani ya ukanda wa Afrika ya Mashariki na mipaka yake Anti Fatma Binti 
Baraka (Maarufu Bi. Kidule) aliyefariki dunia jana mchana baada ya 
kuugua kwa muda mrefu.
  
 
Hatua
 hiyo imekuja kufuatia  mchango wake katika kuitangaza sanaa ya Zanzibar
 nje ya mipaka ya Tanzania hasa kwenye  fani ya muziki wa Taarabu asilia
 na ile ngoma maarufu ya Unyago inayotumika katika sherehe za harusi.
  
Makamu
 wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo 
wakati akiifariji familia ya Marehemu Bi. Kidude wakati wa matayarisho 
ya mazishi yake eneo la Rahaleo nyuma ya Kituo cha ZBC Redio Rahaleo 
Mjini Zanzibar.
  
Balozi
 Seif akitoa ubani wa shilingi Milioni (2,000,000/- )kwa niaba ya Serikali
 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa familia ya marehemu amesema jamii na 
waswahili wote katika mwambao wa Afrika Mashariki wanafahamu mchango 
mkubwa wa Msanii Bi. Kidude  katika fani ya muziki wa taarabu.
  
 
Amesema
 Zanzibar imepata sifa kubwa katika Nyanja za Kimataifa kutokana na 
mchango wa wasanii kwa kueneza sanaa ya Taarabu iliyotoa  fursa kwa 
baadhi ya watalii na wataalamu kuvitembelea Visiwa vya Zanzibar.
  
Makamu
 wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameitaka Familia ya Msanii Bi. Kidude kuwa 
na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha msiba na kuwaeleza 
kwamba msiba huo sio wao peke yao.
  
Balozi
 Seif amesema kwa kweli sisi sote tulimpenda sana Bi. Fatma Binti Baraka
 (Kidude) lakini tuelewe kwamba Mwenyezi Mungu amempenda zaidi na ndio 
maana akamuhitaji.
  
Naye
 Mmoja wa wana Familia hiyo Bw. Haji Ramadhan Suwed Buda kwa niaba ya 
Familia ya Marehemu Bi. Kidude ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya 
Zanzibar kwa mchango wake wa kuungana nao katika msiba huo.
  
Bw. Haji amesema hatua hiyo ya Serikali imeleta faraja kwao na kupunguza machungu ya msiba huo.
  
Msanii
 Gwiji wa sanaa ya Taarab asilia na ngoma ya Unyago Marehemu Bi. Kidude 
aliyekadiriwa kufikia umri wa zaidi ya miaka 98 hakuwahi kuolewa wala 
kupata Mtoto.
  
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Bi. Kidude mahali pema peponi – Amin.