Johannesburg, Afrika Kusini
MADAKTARI wanaomtibu Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela,
wanakubali kuwa kiongozi huyo basi tena kwani hali yake ni tata na sasa
wanasubiri kiungo kimojawapo cha mwili wake kishindwe kufanya kazi ndipo
wazime mashine inayomsaidia kupumua.
Nelson Mandela.
Kutokana na subira hiyo madaktari hao sasa wamebadili msimamo wao wa awali wa kuiondoa mashine hiyo inayomsaidia kupumua.
“Madaktari hao, wameishauri familia yake kuachana na ushauri wa awali
wa kuiondoa mashine hiyo hadi tu pale moja ya kiungo chake muhimu cha
mwili…

mwili kitakaposhindwa kufanya kazi,” alisema rafiki wa Mandela, Denis
Goldberg ambaye alikuwa mpigania uhuru aliyewahi kufungwa pamoja na
Mandela.
Amesema madaktari hao waligusia kuhusu suala la kuondoa
mashine lakini baadaye walikataa kwa kuwa kiongozi huyo aliweza kusogeza
baadhi ya viungo na kutambua sauti.
“Ni kweli kuwa hali ya Mandela
ni mbaya lakini si kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa
vikiandika,” alisema Goldberg.
Juzi vyombo vya habari vya hapa
nchini vilitoa hati ya kiapo ya mahakama, ikionyesha kuwa madaktari hao
waliishauri familia ya Mandela kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua
kwani asingeweza kuendelea kuishi.
Hata hivyo, msemaji wa Rais Jacob
Zuma,Mac Maharaj alikataa kuzungumzia kuhusu hati ya mahakama ambayo
ilieleza kuwa Mandela mwenye miaka 94 yupo mahututi.