![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgK81JAMfXq0XUcNeTjBHlkIka6Npn4Ly1RzbVnb3gSaoY0rHMPN4CE8iU4qDxWjiuWYI4FzkQItAqqcJW8tojdbhO-qXG6Bdt8Uc_qWm4i0pARNQC88n2Kn8No81-kP-P9BnUYWFCssAQ5/s640/tbl+mwanza.jpg) |
Meneja
wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia alitumia fursa hiyo
kukabidhi jezi kwa washiriki, kulia ni captein wa timu ya SAUT Jimmy
Nikitas, inayotetea taji la ubingwa wa pool kwa vyuo nchini. |
Mashindano
ya Safari Lager Higher Leaning Pool kwa mkoa wa Mwanza yanataraji
kuanza kutimua vumbi kuanzia kesho katika ukumbi wa Villa Park jijini
Humo.
Kwa mujibu wa Meneja wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza
Bernad Nahum amesema kuwa Mashindano ya Higher Leaning Pool kwa mkoa wa
mwanza yatashirikisha vyuo vinne ambavyo ni CBE Mwanza, Chuo cha Bugando, SAUT na TIA
ambapo vyuo hivyo vitashindana kupata mwakilishi mmoja atakaye shiriki
mashindano ya Pool Taifa kwa mikoa mingine hapa nchini kama Mbeya, Dar
es salaam, Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro na Arusha
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhp2DndNH0ZoHy1ovNgq6U_xtpy9Ruo7NGQBjNKqm7L8mpkTbRgnZ6eOFIrP388wdwwxSHktuhM60SPSvt33uZE_MgFi4W7-13Lm8hpIr_hZKVbF99fWr74_cNj3OU99H_g2l2krzgYYx6G/s640/tbl+mwanza+2.jpg) |
Kushoto aliyesimama ni Afisa habari wa michuano ya Safari
Lager Higher Leaning Pool Machel akitoa ufafanuzi juu ya mafanikio
yaliyopatikana hadi sasa kwa vyuo shiriki kupitia michuano hiyo. |
Zawadi kwa washindi Timu za Pool
Mshindi wa kwanza mkoa ni shilingi laki 5
Mshindi wa pili shilingi laki 3
Mshindi wa tatu shilingi laki 2
Na mshindi wa nne shilingi laki 1
Washindi Single wanaume
Mshindi wa kwanza shilingi laki 1.5
Mshindi wa pili shilingi laki 1
Washindi Single wanaume
Mshindi wa kwanza shilingi laki 1
Mshindi wa pili shilingi elfu 50.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzFI43oBF4wWG5Zx9FQ4_9g6IRGW1e_jRzQcPGHjT1CxQwVIRWXugQioI6z6fvqUdGJOvUd94oGT9rS1zhHp9bR9vG-HzeYi3BbipPiFzRyztiIYJT6220__F4cfESBIHsZbIiwhLlz44g/s640/tbl+mwanza+3.jpg) |
Timu
captein wa timu bingwa Chuo cha SAUT Jimmy Nikitas (kulia) akizungumza
na waandishi wa habari kuelezea jinsi timu yake ilivyojiandaa kwa
michuano ya Safari Lager Higher Leaning Pool 2013. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbVhM6tXECPgX4QY2EyaRpNtYmdF06Tsvmsl3-jOhBdlc03jN3y9Xg2loau5I944Pxhn4uxQZobMvEhz_K87EJK6TjgQCOspVizMrtAeIoCqJBbDf-tF9HP2Gadyc7jKFCGRsOc9JDyMxP/s640/tbl+mwanza+4.jpg) |
Meneja
wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto)
akimkabidhi jezi timu captein wa Chuo cha SAUT Jimmy Nikitas kwaajili ya
michuano hiyo inayotaraji kuanza rasmi kesho Villa Park Resort Mwanza. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj96BlU3NG-K0bSZwh54AiG-yKloaX8vubaPMdk9wJwh4ndNdyy5T7oKL130WgKsV2LF94b7AGQxHuFLaxPeSTjntst6WubEqc6ANDFkNzLTBVPmZ4vCRFgBWk61VgWv9eXoa5EoCgxFAbu/s640/tbl+mwanza+5.jpg) |
Meneja
wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto)
akimkabidhi jezi timu captein wa Chuo cha Bugando Bernad Okamo, kwaajili
ya michuano hiyo inayotaraji kuanza kutimua vumbi rasmi kesho katika
Viunga vya burudani vya Villa Park Resort Mwanza. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh49-fuEuB234ZY_2dfBVnUr4tKqs5tJ0w4myEHp7nE2fZ3zh-XSo3LpAlDM3Tz7qGzUF8m2Vf91HvaBf4L_eUTgQQWuAVwxyuoRLZD40YLLXk1Dhi2ePP-MniVDdjyW3nnmejxggtkr__j/s640/tbl+mwanza+6.jpg) |
Meneja
wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto)
akimkabidhi jezi timu captein wa Chuo cha CBE Mwanza George Izengo,
kwaajili ya michuano ya Safari Lager Higher Leaning Pool inayotaraji
kuanza rasmi kesho Villa Park Resort Mwanza. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3Ss5-7waXibzgXpoVxe5RSTD9V-wnLB0rvzQt8P3T5V_lkuVHVp1uARAkZ6oA9HkL1D9AwMB-OlPyn2BqMpErcFqMZ-aIsAY6805x52eJXJqPxF2u3CgnMvDP_679vAxAoka-smBJtJTa/s640/tbl+mwanza+7.jpg) |
Meneja
wa Matukio wa bia ya Safari mkoa wa Mwanza Bernad Nahum (kushoto)
akimkabidhi jezi timu captein wa Chuo cha TIA Beatrice Benignus,
kwaajili ya michuano ya Safari Lager Higher Leaning Pool inayotaraji
kuanza rasmi kesho viunga vya burudani Villa Park Resort Mwanza. |