![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgn4AacsCa95mey0DUDXmo6xh1xJ_lbMK3YY0zZhjJDPqGumdPSw5iDNg6SfzoO9lwap77PMO0oTZ1jVYZjbhNpnQ_HnkG6qAB-SRhAwXyWx4jJDBS4u9kjoxMftPXUm80xRRq7QPOEvz5S/s640/Yanga-Champions-300.jpg?width=450)
Wachezaji wa Yanga SC wakishangilia na kombe lao baada ya mechi dhidi ya Simba SC.
Timu ya Yanga leo imewaadhibu watani wao wa jadi, Simba SC baada ya
kuwalaza kwa bao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa
na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza. Baada a mchezo huo, Yanga SC ambao
ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom mwaka huu, walikabidhiwa kombe lao.
0 comments:
Post a Comment