Na: Gustav Chahe, Iringa
MTU
mmoja amenusurika katika ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria
kuacha njia na kutumbukia kwenye mtaro wa maji. Ajali hiyo imetokea
majira ya saa 11 alfajiri katika barabara ya Iringa – Dodoma maeneo ya
Sabasaba katika Manispaa ya Iringa ambapo gari lenye namba za usajili T
287 AAG Prado limetumbukia kwenye mtaro kwa kile kilichoelezwa kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni
hitilafu katika maungio ya tairi (boll joint).
Kwa
mujibu wa maelezo yaliyotolewa na kikosi cha uokoaji (K.B. WORKSHOP)
zinasema kuwa baada ya kupata hitilafu katika tairi moja, gari
lilipoteza mwelekeo na kuhama njia kasha kutumbukia kwenye mtaro.
Imeelezwa kuwa katika gari hilo alikuwemo dereva pekee ambapo hata hivyo hakupata majeraha makubwa.
Gari
hilo lilikuwa likitokea mjini Iringa kuelekea Kihesa ambapo mara baada
ya ajali hiyo imeelezwa kuwa dereva alikwenda kupumzika kutokana na
maumivu ya majeraha aliyopata japo kuwa jina lake halikutajwa.
Mtandao huu umeshuhudia gari lenye namba za usajili T 332 AKP mali ya K.B.WORKSHOP wakiokoa gari hilo lililokuwa kwenye mtaro.