![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixn_2H5S0KFjPQrvXrC0vbd1J9f-ovfrFKMRzqcDpXxOyf6dJcA-aq4zIyU_9q110F8zs9-QWHTz2KIDOFUlT4JbHeOkt40510lbVJWdnlOgVlnQQLdexHfrMlcxfyA5ugXr6cN0acGp-a/s640/Chinua-Achebe-.jpg)
Mwandishi
Maarufu wa vitabu duniani Chinua Achebe amefariki dunia akiwa na umri
wa miaka 82. Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda
ameiambia BBC kuwa wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la
Nigeria na Afrika kwa ujumla.Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka
30 kabla ya Nigeria kupata uhuru. Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya
familia yake, imemwelezea Chinua Achebe kuwa
mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu vya fasihi katika kipindi chake,
ambaye busara yake ilikuwa kichocheo cha kumwiga kwa wale wote
waliomfahamu. Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe
ataishi daima katika mioyo ya akili za watu wa kizazi kiliochopo na
vijavyo. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na utunzi wa kitabu chake cha
kwanza cha fasihi kitwaacho 'Things Fall Apart', ambacho alikitunga
mwaka 1958 kikizungumzia athari za ukoloni barani Afrika.
Kitabu hiki kiliuza zaidi ya nakala milioni 10. Things Fall Apart kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 na kuelekeza mtazamo wake katika jamii ya Wa-Igbo na mgongano wa kimaadili kati ya nchi za mgaharibi na kijadi.
Alipata ngazi ya uprofesa kutoka chuo kikuu cha Boston nchini Marekani mwaka 1970 ambapo katika siku za hivi karibuni alikuwa akikosoa baadhi ya mienendo mibaya ya serikali ya Nigeria.
Amekuwa akiishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 kufuatia kujeruhiwa katika ajali ya gari.
Ameandika kazi za kitaaluma zaidi ya 20, baadhi zikikosoa vikali wanasiasa na uongozi mbaya nchini Nigeria.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima katika mioyo na akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.
0 comments:
Post a Comment