Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama
Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha
maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,kwa
msaada wa Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kisima hicho kimegharimu
shilingi milioni sabini. wa pili kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Ndugu Paschal Mabiti na kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya
Serengeti Jaji Mark Bomani na wamwisho kulia ni Mkurugenzi wa
Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela. Uzinduzi huo
ulifanyika tarehe 7.3.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua koki ya maji wakati wa kuzindua
rasmi kisima cha maji katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure .
Mwenyekiti
wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikewte akiwahutubia mamia ya
wafanyakazi na wananchi wa jiji la Mwanza baada ya kuzindua rasmi kisima
cha maji katika hospitali ya Sekou Toure tarehe 7.3.2013.
0 comments:
Post a Comment