Mwili wa Chavez ukipitishwa katika barabara za mji mkuu Caracas
Mwili wa
Chavez umelazwa katika kituo cha mafunzo ya kijeshi mjini Caracas na
marais wa nchi jirani walifika kutoa heshima zao za mwisho akiwemo Rais
wa Bolivia Evo Morales na mwenzake wa Argentina Cristina Fernandez de
Kirchner.Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa
heshma zao .
Kifo chake kilitangazwa na serikali ya Venezuela Jumanne wiki hii
Mwaka
uliofuata Chavez alichaguliwa na wananchi kuongoza kwa muhula wwingine
wa miaka sita kuiongoza Venezuela .Watu wengi waliangua kilio huku
wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .
Mwaka 2011 Chavez alisema kuwa anapokea matibabu ya Saratani nchini Cuba
Chavez alionekana kama mpigania haki za watu maskini kwa kusisitiza sera zake za kisosholisti na kuzichanganya na demokrasia.
Mwili wa
Chavez ulipitishwa katikati ya mji mkuu Caracas na kusindikizwa na
maelfu ya watu waliomuunga mkono,Watu wengi waliangua kilio huku
wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .
Chavez
alikuwa na maadui wengi pamoja na wale waliomuona kama mwokozi wao kwa
sababu ya sera zake za kisosholisti.Watu wengi waliangua kilio huku
wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .
Hugo
Chavez hakupendwa na kila mtu Venezuela wakati wa utawala wake.Wapinzani
wa Hugo Chavez wakisherehekea katika moja ya kumbi za maburudiko baada
ya kupokea habari za kifo chake mjini Florida, Marekani. Picha Kwa
Hisani ya Reuters na AFP
……………………………………………………..
Mwili wa
mareheu rais Hugo Chavez wa Venezuela, umelazwa katika kituo cha mafunzo
ya jeshi katika mji mkuu Caracas Mapema leo mwili wa marehemu Chavez
ulipitishwa kwenye umati mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu
Caracas. Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi
wao aliyefariki dunia.Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya
jeneza kutoa heshma zao .
Makamu wa
rais Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo. Mwili wa rais Chavez
umepelekwa katika chuo cha kitaifa cha mafunzo ya kijeshi ambapo
utazikwa kesho Ijumaa. Bwana Chavez alifariki akiwa umri wa miaka 58
baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili. Maelfu ya watu awali
walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima zao za mwisho kwa
Chavez wakifuatana na gari lililokuwa limebeba jeneza lake kuelekea
katika chuo cha mafuzno ya jeshi.
Mazishi ya
kitaifa ya Chavez yatafanyika Ijumaa. Mkuu wa ulinzi wa Rais
alinukuliwa akisema kuwa alikuwa na bwana Chavez alipofariki. Generali
Jose Ornella, alisema kuwa Chavez alifariki kutokana na mshtuko wa moyo
na katika siku zake za mwisho kabla ya kifo cha ealisema angependa
kuendelea kuishi. Jeneza lake lililokuwa limefunikwa bendera ya nchi
hiyo uliwekwa katika ukumbi ambao ni kumbukumbu ya waliopigania uhuru wa
watu wa Amerika ya Kusini
Maelfu ya
watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Chavez,
wakiwemo maafisa wa serikali na viongozi wa Amerika ya Kusini,kama Rais
wa Bolivia Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez de
Kirchner.
Source: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment