MBUNGE
wa Jimbo la Rorya Mkoani Mara Lameck Airo (La-Kairo) amesikitishwa na
kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje kumtapeli kiasi
cha fedha shilingi milioni moja alizozitoa ili zikatangazwe kama sehemu
ya mchango kwa lengo la kuchangia harambee aliyoiendesha katika kijiji
cha Buchile Kata ya Mkoma Mjini Shirati Mkoani Mara alikozaliwa Wenje.
Hatua hiyo imekuja mara baada
ya tukio la hivi karibu la Bw. Wenje kutumia jukwaa la harambee hiyo ya
kuchangia elimu katika kijiji cha Buchile kumkashifu kwa maneno
yasiyofaa Mbunge wa jimbo la Rorya na kusema kuwa mbunge huyo hajafanya
maendeleo yoyote kwa watu wa jimbo lake licha ya kusaidiwa kuongea
Bungeni.
Bw. Airo alisema kwamba
kitendo alichokifanya Bw. Wenje cha kushindwa kuwasilisha mchango wa
shilingi milioni moja alioutoa Airo katika harambee hiyo, kumchafua kwa
kutumia lugha chafu pamoja na kushindwa kutambua thamani ya kazi
mbalimbali ambazo amekuwa akizifanya katika kijiji hicho alikozaliwa
Mbunge Wenje ni kitendo kisicho na uungwana na hakipaswi kufanywa na mtu
wa hadhi yake anayetizamwa kama mfano wa kuigwa na jamii.
"Nadhani Bw.Wenje anapaswa kushindana nami kwa kwa vitendo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa majimbo yetu badala ya kuhangaika na maneno jukwaani bila vitendo,
hili haliwasaidii wananchi ila ninaamini mwisho wa siku tutakapokwenda
kwenye tathimini tutaona ni nani aliwatumikia wananchi wake waliomchagua
kikamilifu" "Mimi sitafuti umaarufu kwa wananchi wa Rorya na wao
wanatambua hilo bali ni mimi niko kwaajili ya kutekeleza nilichowaahidi"
alisisitiza Bw.Airo.
![]() |
Mbunge Ezekiel Wenje. |
“Nimeshangazwa kuona hata michango yetu mimi shilingi milioni moja na
Mwenyekiti wangu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Bw.Charles Ochele
aliyetoa laki tano hazikutajwa zaidi ya Bw. Wenje kutoa milioni moja tu
kwenye harambee hiyo fedha aliyodai imetoka mfukoni mwake, hii
inaonyesha kuwa hakuwa na harambee ya kweli bali lengo lilikuwa
kuwachafua na kuwakashifu kwa maneno yasiyofaa viongozi wenzake ili
kujitafutia umaarufu wa kisiasa” alisema Airo.
Bw. Airo amesisitiza kwamba kamwe hatomjibu kwa matusi mbunge Wenje na
badala yake atamjibu kwa vitendo kwenye utekelezaji shughuli za
maendeleo kupitia ilani ya CCM.
Jimboni Rolya ahadi nyingi zilizoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya
CCM ya 2010-2015 hadi sasa miradi mingi inatajwa kukamilika kwa asilimia
90 huku mbunge wa jimbo hilo akiahidi kukamilisha miradi mingine
iliyoainishwa mapema zaidi hata kabla ya kumalizika kwa msimu.
0 comments:
Post a Comment