Wachezaji wa Manchester City
Mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City wameandikisha ushindi
mkubwa dhidi ya mabingwa wa ulaya Chelsea na hivyo kufufua matumaini
yao ya kuhifadhi kombe hilo kwa mwaka wa pili, licha ya kukabiliwa na
upinzani mkali kutoka wa vinara wa ligi hiyo kwa sasa Manchester United.
Mechi hiyo iliyokuwa na mashambulizi na kila aina ya vivutio baina ya
timu hizo zinazomilikiwa na matajiri wawili tofauti,imemalizika kwa
ushindi wa Man City wa mabao mawili kwa bila.
Mabao ya kipindi cha pili ya Yaya Toure na Carlos Tevez yalitosha
kuizamisha Chelsea, na kufufua matumaini ya Man City, kutetea taji lao
ambalo sasa linaonekana kuwa mikononi mwa majirani zao Manchster United
wanaoongoza ligi wakiwa na tofauti ya point 12.
Mapema kipindi cha pili, Chelsea, walipata penat baada ya Demba BA,
kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Man City, Joe Hart,
lakini penat iliyopigwa na nahodha wa Chelsea, Frank Lampard,
ilipanguliwa Joe Hart na kuamsha mashambulizi zaidi ya Manchester City.
Yaya Toure kunako dakika ya 63 alipenyeza shuti la wastani pembeni
mwa lango la Chelsea na kuwafanya Manchester City, kuongoza kwa bao moja
kabla Chelsea, kufanya juhudi za kutaka kusawazisha lakini wakajikuta
wanoangezwa bao la pili maraidadi kabisa lililofungwa na Carlos Tevez
ambaye aliingia akitokea benchi,huku likiwa bao lake la kwanza baada ya
mechi sita alizocheza bila kuifungia timu yake.
Kwingineko,katika mchezo mwingine wa leo, Newcastle wakiwa
nyumbani,walitoka nyuma baada ya kufungwa bao la mapema na kuchomoza na
ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Southampton.
Mabao wa Newcastle yamefungwa na Musa Sisoko,Papis Demba Cisse,Yohan
Cabaye aliyefungwa kwa mkwaju wa penati huku bao la nne watakatifu au
Southampton wakijifunga.
Mabao ya Southampton yalifungwa na Morgan Scheneiderlin dakika tatu
tu baada ya mchezo kuanza huku bao la pili likifungwa na Rickie Lamber
0 comments:
Post a Comment