This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, April 30, 2013

BAJETI KIPORO WIZARA YA MAJI YATINGA TENA BUNGENI LEO




Mkutano wa 11 unaendeleo leo mjini Dodoma, ambapo Bajeti ya Wizara ya Maji iliyokwama kupitishwa baada ya wabunge kuigomea, inatarajiwa kuwasilishwa, ikiwa na  maboresho, hususani eneo la nyongeza ya fedha katika miradi ya maji.

Bajeti hiyo ilitarajiwa kupitishwa tangu Alhamisi wiki  iliyopita, lakini kutokana na ufinyu wa fedha zilizotengwa, takribani wabunge wote waliochangia mjadala wake, wakiwemo wa CCM, waligoma kuiunga mkono.
 
Kutokana na hali hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema suala la maji haliwezi kufanyiwa utani na kuitaka Wizara ya Maji, Kamati ya Bajeti na Wizara ya Fedha, kufanyia kazi suala hilo na walete majibu ya uhakika.
 
Leo wabunge hao wanatarajia upande wa Serikali kuwasilisha bajeti hiyo, ikiwa na maboresho mapya ya nyongeza ya fedha za miradi inayotarajiwa kufikia zaidi ya Sh milioni 185, ambazo wabunge hao walipendekeza ili kutekeleza miradi ya maji na kupunguza tatizo la maji katika maeneo yao.
 
Wakati akiiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo wiki iliyopita bungeni, Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, alibainisha kuwa Wizara hiyo imetengewa Sh bilioni 398, fedha ambazo wabunge hao walibainisha kuwa hazitoshi, ikilinganishwa na mahitaji makubwa ya maji nchini.
 
Wakati akiahirisha mjadala huo wa Bajeti ya Maji, Spika alisema: “Naona sasa mahitaji ya wabunge wote na wananchi kwa ujumla ni bajeti hii, kwa kweli iboreshwe ili kufikia malengo stahiki katika maeneo yetu.”

Viongozi wa Wizara ya Fedha, Kamati ya Bajeti na Wizara ya Maji, kwa takribani siku tatu, walikutana na kujadili suala hilo na namna ya kupata fedha za kuongezea kwenye bajeti hiyo, huku wabunge wa CCM nao wakikutana ili kuwekana sawa, kutokana na kilichotokea bungeni kuhusu bajeti hiyo.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, alipongeza hatua za wabunge hasa wa CCM, kuweka itikadi zao pembeni na kuungana pamoja kuikataa bajeti hiyo, ambayo haikuwa na mfumo mzuri wa kumaliza tatizo la maji nchini.
Hata hivyo, alipendekeza leo Serikali ije na maboresho yatakayoainisha namna ya kutekeleza Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo, uliozinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, ambao katika eneo la maji utahitaji Sh bilioni 500.

Pamoja na mjadala wa Bajeti ya Maji kuendelea leo, pia Wizara ya Maliasili na Utalii, inatarajiwa kuwasilisha bajeti yake ya mwaka 2013/2014, itakayojadiliwa kwa siku mbili, ambapo wabunge wengi wanatarajia kuzungumzia suala la mgogoro wa ardhi Loliondo.

Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria nayo inatarajiwa kuwasilishwa kesho huku suala la Mabaraza ya Katiba likiwa ajenda kuu, iliyopaniwa kujadiliwa hasa na wapinzani, ambao wamekuwa wakilalamikia mchakato wake wa uchaguzi, kwamba umekuwa ukitawaliwa zaidi na masuala ya siasa.

Katika wiki hii, bajeti nyingine itakayojadiliwa ni ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambayo itajadiliwa kwa siku moja.

MVUA YASABABISHA MAFURIKO JIJINI DAR LEO

Hapa ni barabara iliyo jirani na jengo la Tume ya Sayansi na Teknolojia Kijitonyama.
Pikipiki hizi zipo karibu na stendi ya basi Mwenge jijini Dar ambazo zimezungukwa na maji na mafundi kukimbia eneo hilo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha. Wenye pikipiki hizi wangejua kuwa mali zao zimemezwa na maji, wangelia!…
Hapa ni barabara iliyo jirani na jengo la Tume ya Sayansi na Teknolojia Kijitonyama.

"LAZIMA TUZIKAGUE KUCHA ZA LEMA..... TUPO TAYARI KUFA....."HAYA NI BAADHI YA MABANGO YA WAANDAMANAJI HUKO ARUSHA


Asubuhi ya leo, kama ilivyotarajiwa na wengi baada kufuatia taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alifikishwa mahakamani baada ya kukaa rumande tangu alipokamatwa usiku wa kumkia siku ya Jumamosi, Aprili 27, 2013.

Mbele ya hakimu Joyce Msofe na mawakili Kimomogoro na Humphrey Mtui wanaomtetea, Lema amesomewa shitaka la kosa la uchochezi linalomkabili kwamba aliwachochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha kumzomea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuwaambia wanafunzi kuwa Mkuu huyo wa Mkoa, “hajui chuo cha uhasibu kilipo, amekuja akiwa amechelewa na anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.”
 
Mtuhumiwa Lema amekana kosa hilo.Mwendesha mashitaka alisema dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa endapo atatimiza masharti ya dhamana.

Mtuhumiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwepo kwa mtu mmoja mwenye kitambulisho kinachokubalika kisheria na kuweka rehani kiasi cha shilingi milioni moja.

Baada ya kutoka mahakamani hapo, Lema alielekea kwenye maeneo ya Ofisi za chama, CHADEMA. kwa maandamano  makubwa

Picture

Picture

Picture
Picture

MZEE WA KANISA ALIVYOZIKWA HAI

Na Mwandishi Wetu, Chunya

NI zaidi ya ukatili! Katika hali isiyowahi kufikiriwa na binadamu aliyeumbwa na Mungu, baadhi ya vijana wa  Kijiji cha Mkwajuni Wilaya ya Chunya, Mbeya wamemzika akiwa hai aliyekuwa msaidizi wa padri, Katekista Flavian Mwamosi Mwachirui (68) wakimtuhumu kusababisha kifo cha Peter Robert (28) mkazi wa kijijini hapo.
Jeneza la marehemu Peter Robert baada ya kufukuliwa.
Tukio hilo lililoshtua wengi katika eneo hilo lilitokea saa nane mchana wa Ijumaa…
Na Mwandishi Wetu, Chunya
NI zaidi ya ukatili! Katika hali isiyowahi kufikiriwa na binadamu aliyeumbwa na Mungu, baadhi ya vijana wa  Kijiji cha Mkwajuni Wilaya ya Chunya, Mbeya wamemzika akiwa hai aliyekuwa msaidizi wa padri, Katekista Flavian Mwamosi Mwachirui (68) wakimtuhumu kusababisha kifo cha Peter Robert (28) mkazi wa kijijini hapo.
Jeneza la marehemu Peter Robert baada ya kufukuliwa.
Tukio hilo lililoshtua wengi katika eneo hilo lilitokea saa nane mchana wa Ijumaa iliyopita kwenye Makaburi ya Maweni kufuatia kijana Peter kufariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mwili wa marehemu Mwamosi Mwachirui baada ya kufukuliwa.
DHAMBI ILIPOANZIA
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni ndugu wa mzee huyo (jina tunalo) aliweka wazi kwamba, dhambi ya ukatili huo wa kutisha ilianza pale marehemu Peter alipokumbwa na mauti akiwa anatibiwa kwa mganga wa kienyeji ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Simulizi hii ya kweli inaendelea kuwa, wakati ndugu na jamaa wakilia na kuomboleza na ratiba ya maziko ikitangazwa, ndipo baadhi ya ndugu hao wa marehemu waliibuka na kudai eti kifo cha Peter si cha Mungu, kwa sababu kilikuwa na mkono wa binadamu!
Dada wa marehemu Peter wakilia kwa uchungu.
NDUGU WAMWANIKA ‘MUUAJI’ WAO
Ndugu hao walipoona watu hawawaelewi waliposema marehemu kafa kwa kurogwa, wakaenda mbele zaidi, wakamtaja mzee Flavian Mwamosi Mwachirui ambaye ni katekista mstaafu aliyekuwa akihudumu katika Kigango cha Mkwajuni hadi 2007.

SIKU YA MAZISHI YAFIKA
Madai ya baadhi ya ndugu hao yalinaswa na vijana kadhaa wa kijiji hicho ambao waliapa kwa miungu wao kwamba lazima marehemu wamzike na ‘muuaji’ wake, yaani mzee Mwachirui. Inauma sana!
“Siku ya kumzika Peter, kuna vijana walisikika wakisema marehemu watamzika na mzee Mwachirui tena wakaongeza kuwa  watamzika mzee huyo akiwa hai ili aone maumivu ya kifo utadhani walimuona akimuua huyo Peter,” kilisema chanzo huku kikibubujika machozi.
Chanzo kikaongeza: “Watu wa huku wanaishi kwa kutumia akili za waganga wa kienyeji. Mganga akisema unakosa mazao shamba kwa sababu mama yako anakuroga, basi mama huyo atauawa! Mbeya si sehemu salama tena.”
Mwili wa mzee Mwachirui ukufukuliwa.
‘MUUAJI’ AITWA KUCHUNGULIA KABURI LAKE
Kaburi la kumzikia marehemu Peter lilimalizika kuchimbwa, vijana waliokuwa wakiliandaa waliagiza wazee wa kimila wafike kwa lengo la kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa kaburi lenyewe kama lipo sawa.
Wito huo uliwagusa wazee wanne wa kijiji hicho, (masikini ya Mungu) akiwemo Mzee Mwachirui ambaye vijana hao walimsisitiza yeye asogee jirani kabisa na kaburi.
Bila kujua alibakiza sukunde chache za kuishi duniani, mzee huyo alisogea na kuchungulia kaburi ili atoe utafiti wake kwa vijana hao wenye moyo wa kikatili kuliko wanyama wa porini, akiwemo simba anayekula wenzake.
Kushoto ni mwili wa mzee Mwachirui baada ya kufukuliwa , kulia ni kaburi la Peter.
SAA YA KIFO INAFIKA
Ilikuwa kufumba na kufumbua, kijana mmoja aliyeshika sururu alimpiga nayo kichwani mzee huyo hali iliyomfanya ayumbe.
Kama vile haitoshi, wapo vijana waliomsindikiza kwa kumpiga na marungu hadi akaangukia kaburini.

MAISHA NDANI YA KABURI
Chanzo kikasema: Masikini mzee wa watu, alijaribu kujiokoa kwa kutaka kutoka kaburini lakini wale vijana wakamwamuru akae, alipokataa alizidi kupigwa.
“Ilifika mahali aliishiwa nguvu huku akijiona. Mbaya zaidi vijana waliokuwa wakimfanyia unyama huo anawajua kwa majina na alijaribu kuwaita mmoja mmoja ili wamwachie lakini wapi!”
Kinachoumiza zaidi, mzee huyo aliingia kaburini na nguo zake, suruali iliyofungwa mkanda mweusi, nguo ya ndani, shati jeupe la mikono mirefu lenye mistari ndani akiwa ametinga ‘singlendi’. Miguuni alikuwa pekuwa.

APOTEZA FAHAMU, WAMWEKEA JENEZA JUU YAKE, WATIA UDONGO
‘Wauaji’ hao walipojiridhisha kwamba mzee huyo hakuwa na uwezo wa kutoka kaburini, walichukua fito wakamfunika nazo kisha wakafukia udongo mchache, juu yake wakaliweka jeneza la marehemu Peter, wakafukia udongo kwa majembe na masepetu mpaka kaburi kukamilika. Ni zaidi ya ukatili uliowahi kufanywa mwaka 2013!

KAMA VILE HAITOSHI
Baada ya kukamilika kwa zoezi la mazishi kundi la vijana lilipiga mbio hadi  nyumbani kwa marehemu mzee Mwachirui na kuiteketeza nyumba yake huku wakiapa kuwa, hakuna kutoa siri ya tukio hilo. Walisema walichokifanya ni ‘siri ya jeshi’.

WANAKIJIJI WAKERWA, WAKIMBILIA SERIKALINI
Baada ya tukio hilo, baadhi ya wananchi walikimbia hadi kwa Mwenyekiti wa Kijiji, Credo Kayanza na kumpa ripoti ya unyama huo.
Naye mwenyekiti alipoona ni unyama uliopita kiwango cha ubinadamu alishika njia hadi kwa diwani wa kata hiyo, Chesco Ngairo ambapo wote kwa pamoja walikimbia hadi Kituo cha Polisi Mkwajuni na kusema yote huku wakiomba maafande wenye uwezo wa kivita kufika kijijini hapo kushughulikia hali hiyo.

KABURI LAFUKULIWA
Polisi walifika kijijini hapo kwa spidi ya ndege ya kijeshi na kukuta tukio likiwa bichi, wakawaamuru baadhi ya vijana kulifukua kaburi hilo zoezi ambalo lilifanyika baada ya vijana hao kulipwa fedha!
Baada ya kufukua kaburi,
jeneza la marehemu Peter ndilo lililoanza kutolewa na kuwekwa pembeni, zikafuata fito kisha mwili wa marehmu mzee Mwachirui ambao uliwekwa pembeni pia.
Polisi wakaamuru mwili wa Peter uzikwe, wao wakaondoka na mwili wa mzee Mwachirui hadi Hospitali ya Misheni ya Mkwajuni kwa ajili ya uchunguzi na kujiridhisha juu ya kifo chake.
Madaktari waliokuwa zamu walithibitisha kuwa, mzee huyo alishaaga dunia, hivyo ndugu wakakabidhiwa mwili huo kwa ajili ya
kwenda kuuzika sehemu nyingine lakini katika makaburi alikozikwa Peter.

HUYU HAPA KAMANDA WA POLISI MBEYA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Diwani Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo,  pia ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia  ya kuamini mambo ya ushirikina na uchawi kwa madai kuwa hakuna faida zaidi ya kuchochea migogoro.

MADAI YA NYUMA
Kwa miaka mingi, marehemu mzee Mwachirui na wenzake wawili ambao majina yao hayakutajwa walikuwa wakituhumiwa kwa vitendo vya kishirikina licha ya kwamba hakuna aliyewahi kuona matukio yao laivu au kuwa na ushahidi mkononi.


HAMMER Q AMTOA MANUNDU MKEWE BAADA YA UTAMBULISHO WA TX MOSHI


Baadhi ya picha za mkewe baada ya kipigo








Nguo za Hammer Q zikiwa zimetapakaa damu



Hiki ni kipigo ambacho  Salha  alikipata baada ya kumtambulisha rafiki yake wa kiume ambae ni Tx Moshi kwa mumewe Hammer Q.

Baada  ya  utambulisho  huo....sinema  ya  ngumi  na  mateke  ilianza....
Inavyosemekana alimpiga mateke, mangumi, akampasulia kioo kichwani, kampiga na jiko la mkaa kichwani

Saturday, April 27, 2013

NU JOINT: JANA NA LEO / YOUNG KILLER FEAT STAMINA NA QUICK RACKA




 Ikiwa bado ngoma yake "Dear Gambe" bado inafanya vizuri kaika chati mbali mbali, leo hii Young Killer, msanii anae wakilisha Mwanza, amedondosha boooonge moja la pini ikiwa ni kolabo na Stamina na Quick Racka akiwa ameshikilia chorus, mkono wa producer D classic na Mona Gangsta.

RAISI KIKWETE ASAMEHE WAFUNGWA 40000



Rais Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya Watanzania katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na baadaye kusamehe wafungwa 4,180.
 
Idadi kubwa ya watanzania walishiriki katika maadhimisho hayo hayo ambayo yalianza saa 2:30 asubuhi na kupambwa na gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama na kupendezeshwa na halaiki ya wanafunzi 2,695 kutoka Tanzania Bara na Visiwani waliofanya maonyesho mbalimbali ya kuashiria maadhimisho ya muungano.
 
Viongozi mbalimbali wakiwamo wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani walishiriki kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni ishara ya kuuenzi na kuulinda muungano huo.
 
Viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd.
 
Wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa na mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
 
Baada ya viongozi kuketi katika nafasi zao, gwaride rasmi lenye gadi kumi lilipita na kutoa heshima zao mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Baada ya hapo vijana wa halaiki walionyesha maumbo mbalimbali kuashiria maendeleo yaliyopatikana nchini kwa muda wa miaka 49 tokea taifa la Tanzania liundwe rasmi kabla ya Wanahalaiki kujipanga na kuonyesha taswira mbalimbali na kuimba wimbo wa kuhamasisha kudumisha muungano.
 
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani hawakuweza kushiriki kwenye maonyesho hayo.
 
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

 Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa shughuli za maadhimisho hayo, mjumbe wa Kamati Kuu Chadema ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu alisema kuwa, Watanzania wanapaswa kujivunia Muungano walionao kwa sababu umedumu kwa miaka 49, akieleza kuwa ni nadra sana kuona nchi za Afrika au Ulaya kuendeleza muungano wenye umri mkubwa kama huu wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo basi wanapaswa kuuenzi na kuulinda kuendeleza amani iliyopo.
 
Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,180 waliokuwa wakitumikia vifungo vyao katika magereza mbalimbali hapa nchini katika kuadhimisha miaka 49 ya muungano.
 
Wafungwa waliosamehewa ni wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano, ambapo mpaka siku ya msamaha yaani April 26, watakuwa wameshatumikia robo ya vifungo vyao, wafungwa wagonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu na kansa ambao wamethibitishwa na jopo la madaktari.
 
Pia wazee wenye umri wa miaka sabini au zaidi, wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya, wakiwamo walemavu.
 
Msamaha wa Rais pia umeenda kwa wafungwa walemavu wa mwili na akili na wafungwa ambao hadi siku ya jana walikuwa wameshakaa gerezani kwa muda wa miaka mitano na wameonyesha kuwa na tabia nzuri.

Chanzo: mwananchi.co.tz