This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, March 20, 2013

HATIMAYE SERIKALI NA TFF ZAFIKIA MUAFAKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU

Serikali imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Amesema baada ya maafikiano hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo ndilo lililosimamisha mchakato huo ili litume ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.
Rais Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.
“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. FIFA wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.
Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya maana hata kidogo.
Hivyo amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani FIFA watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.
Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.  
Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.
Rais Tenga amewahadharisha watu wanaopitapita mikoani kuomba saini za wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA. Jambo hilo kikatiba ni kosa.

HUU NDIO UNDANI YA MARIDHIANO YA TFF NA SERIKALI KUHUSU UCHAGUZI WA TFF

HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, zimekubaliana ujumbe kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kufika nchini muda wowote kuanzia sasa na kufanya mapitio upya (review) kwa wagombea walioenguliwa katika mbio za uchaguzi wa TFF.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga, leo hii amesema kimsingi wamekubaliana na wizara baada ya kikao cha jana kilichowaushisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fennela Mukangara, naibu wake, Amos Makalla, Tenga na viongozi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), kwamba Fifa waje kufanya review halafu uchaguzi uendelee.
“Tumeangalia mambo mengi ya msingi kwa mustakabali wa mpira wa miguu Tanzania, tuna  heshima kubwa ya uongozi bora katika soka duniani. Hivyo tusingependa sifa hii ipotee kienyeji, ndiyo maana TFF, wizara na BMT tulikutana na kukubaliana kwamba, Fifa waje kufanya review ya kile kilichotokea halafu majibu yakipatikana tuendelee na uchaguzi,” amesema Tenga.
 Tenga amesema, wamefikia uamuzi kwa kuwafikiria pia Watanzania wapenda michezo na hata wagombea ambao wana haki ya kupigiwa kura huku wakiwa hawahusiki na hiki kinachoendelea sasa.
“Kuna watu hawahusiki na jambo hili kwa namna yoyote ile, sasa hawa tumewafikirai sana na tumeamua tuwape haki yao haraka iwezekanavyo. Nina imani nchi itabaki kuwa salama katika soka na upepo huu utapita,” amesema Tenga.
Awali Tenga alikuwa ameridhia kufanyika kwa review za mapingamizi ya wagombea mbalimbali wa TFF, lakini ushauri wake huo ulitupwa mbali na Kamati Huru ya Uchaguzi ya TFF na ile ya Rufaa. Baada ya hapo, ndipo serikali ikaiagiza TFF kufuata katiba ya mwaka 2008 baada ya kupokea malalamiko ya baadhi ya wagombea walioenguliwa.
Baadhi ya wagombea waliochinjwa katika uchaguzi huo ni Jamal Malinzi anayewania nafasi ya rais, Michael Wambura anayewania nafasi ya makamu wa rais ma wengineo.

TENGA AKATAA KUZUNGUMZIA KATIBA

Katika hali ya kushangaza, Tenga alikataa kujibu maswali ya waandishi wa habari yaliyokuwa yakihoji kuhusu katiba itakayotumika katika uchaguzi huo baada ya awali serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kuigiza TFF kutumia katiba ya mwaka 2008 na kuiacha ile ya 2012 inayoelezwa kupitishwa isivyo halali.
“Jamani swali kuhusu katiba sitalijibu hapa, hapa tunazungumzia uchaguzi na mambo mengine yahusuyo,” amesema Tenga na hata aliposisitizwa kuhusu umuhimu wa swali hilo, alijibu: “Hapa si mahala pake jamani.”

SERIKALI YAZIDI KUIKOMALIA TFF

Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi alisisitiza kwamba, Fifa watafika nchini na kufanya review yao kisha wao kama wasimamizi wa serikali wataipitia ripoti ya kazi hiyo kisha kuitolea maamuzi zaidi.
“Tumekubaliana hapa kwamba Fifa waje kufanya review, hawa mabwana wakimaliza kazi yao sisi tutaiangalia na kutazama kama haki imetendeka halafu ndipo tutaruhusu taratibu za uchaguzi kuendelea,” amesema Malinzi.
Malinzi alisema, kimsingi kikao chao na wizara na TFF kilikuwa cha amani na ana uhakika mambo yataenda vizuri na kila mmoja atapata haki yake ipasavyo.
FIFA WANAKUJA, UCHAGUZI SI ZAIDI YA MEI 25

Tenga baada ya maafikiano hayo, TFF itaiandikia Fifa ambao ndiyo wanaosimamisha mchakato huo ili watume wajumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.
Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.
“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. Fifa wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema Tenga.
Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na Fifa baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya maana hata kidogo.

WAGOMBEA KUHOJIWA NA FIFA NA KAMATI YA RUFAA

Tenga amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani Fifa watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.
Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani. 
Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna Fifa.

MJADALA: ZIDANE, INIESTA NANI ZAIDI?

MJADALA: ZIDANE, INIESTA NANI ZAIDI?


ZINEDINE Zidane ni mmoja wa wachezaji wenye kipaji cha aina yake waliowahi kucheza soka akiwa na Ronaldo De Lima.

Akiwa na umri mdogo, Zidane alikuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza mashambulizi kupitia katikati ya uwanja huku akitumia uwezo binafsi na nguvu ipasavyo.

Wakati huo alikuwa akichezea klabu ya Bordeux ya Ufaransa kabla hajasajiliwa na Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho ya thamani ya pauni milioni tatu ambazo ni zaidi ya Sh. 7.5 Bilioni.

Akiwa na Juventus, Zidane hakuanza maisha vyema na kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa na walakini na uwezo wake.

Kadri msimu wa mwaka 1996/97 ulivyozidi kwenda, Zidane taratibu alianza kuonekana muhimu na alikuwa na mchango mkubwa kwa kikosi kilichofika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambacho kwa bahati mbaya kilifungwa na Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Kipigo hicho kilipokewa kwa mshangao na wengi hasa baada ya Zidane maarufu kama Zizzou kukabwa ‘man to man’ kwenye mchezo huo na kiungo wa Dortmund, Paul Lambert ambaye hii leo ni kocha wa Aston Villa.

                
Msimu uliofuata, Juventus ilifungwa katika fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid kwa bao la Predrag Mijatovic. Kikosi hiki cha Juventus kilichokuwa na Didier Deschamps, Edgar Davids, Alesandro Del Piero na Zizzou kilikuwa kinaonekana kama kitatawala soka la Ulaya kwa muda mrefu ujao.


Kwenye fainali za Kombe la Dunia 1998, Zidane alilazimika kungoja hadi mchezo wa fainali kisha kufunga mabao yake ya kwanza ya michuano hiyo. Mabao hayo ndiyo yaliyoipa Ufaransa ubingwa wa Dunia kwa mara ya kwanza, na hapa hakukuwa na ubishi kuwa, Zidane alikuwa mchezaji bora mbele ya kizazi cha dhahabu cha wachezaji wa Les Bleus.


Miaka miwili baadaye, Ufaransa ilitwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya licha ya Zidane kutofunga bao hata moja. Hakuna ubishi kuhusu mchango alioutoa katika mafanikio hayo ya Ufaransa mwaka 2000.



MCHEZAJI GHALI KULIKO WOTE DUNIANI

 

Mwaka 2001 Zidane aliuzwa kwenda klabu ya Real Madrid kwa dau lililoweka rekodi ya Dunia kwa wakati huo la pauni milioni 42 ambazo ni zaidi ya Sh. 105 Bilioni.

Msimu wake wa kwanza akiwa na Real Madrid, ulikuwa mgumu na kulikuwa na taarifa kuwa, presha ya matarajio makubwa yaliyokuwepo mabegani mwake kutokana na fedha nyingi zilizotumika kumsajili ilikuwa kubwa kwake.

Hata hivyo, Real Madrid ilifika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2002 na kwenye fainali yake ya tatu, Zidane alifanikiwa kutimiza ndoto zake.


Kwenye fainali hiyo, Zidane alifunga bao ambalo linaweza kuwa bora kwa miaka yote ya michuano hiyo.

Zidane alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Dunia mwaka 2003, ikiwa mara yake ya tatu kupewa tuzo hiyo. Kabla ya hapo aliwahi kutwaa tuzo hiyo kwenye miaka ya 1998 na 2000.


Uwezo wake wa kubadili matokeo ya mechi ngumu uwanjani, ulimfanya adhihirishe ubora wake mbele ya kila mtu. Kwenye klabu yake, kulikuwa na ‘issue’ za mradi wa Galactico ambazo ziliathiri mafanikio ya klabu.

Ulikuwa wakati mgumu kwa Zidane kwa kuwa hata timu yake ya taifa ilikuwa na matatizo kwenye michuano mikubwa. Majeraha aliyopata mwaka 2002 yalishuhudia timu yake ikitemeshwa ubingwa wa Dunia kwenye hatua ya makundi.Ufaransa ilishindwa kupata hata bao moja.

Timu zote mbili za Zidane, kwa maana ya Ufaransa na Real Madrid zilikosa ‘balance’ na hii ilimnyima mafanikio japo aliyopata kwenye tuzo binafsi mojawapo ikiwa ya kuteuliwa kuwa mmoja wa wachezaji 50 bora wa miaka yote.



Mwaka 2006 ulikuwa wa aina yake kwenye historia ya mchezo wa soka. Mwaka 2003 Barcelona walimnunua Ronaldinho Gaucho wakati Real Madrid walimnunua David Beckham. Wachezaji hawa wawili walikuwa gumzo na walionyesha mwelekeo wa mchezo wa soka kwa kipindi hicho.


Beckham alionekana kuwa mtu aliyejengwa kwenye miaka ya 90 na Gaucho akionekana wa miaka ijayo. Wakati Madrid na mradi wao wa Galactico wakionekana ‘wana-flop’, Barcelona walikuwa wakicheza soka safi na la kuvutia.

Mwaka 2006 walitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiifunga Arsenal mabao 2-1. Mtindo wao wa soka lao la kushambulia kwa pasi nyingi huku ukiongozwa na Samuel Eto’o na Gaucho, ulivutia machoni kwa watazamaji. Haya yalikuwa mapinduzi ya soka.

Mwaka huo pia kulikuwa na Kombe la Dunia huko Ujerumani. Zidane aliamua kurejea kwenye timu ya taifa na kuiongoza Ufaransa kwa mara ya mwisho. Mkataba wake na Real Madrid uliisha msimu wa 2005/06 na katika michuano ya Kombe la Dunia 2006, ndipo alipocheza soka kwa mara ya mwisho.


MCHEZO ULIOLETA MABADILIKO.


Kama ndoto, Zidane aliiifikisha Ufaransa hadi fainali ya Kombe la Dunia 2006. Mechi ambayo itakumbukwa na wengi ilikuwa robo fainali dhidi ya Brazil, ambapo ilikuwa vita yake na Ronaldinho Gaucho.

Ilikuwa inaonekana kama imepangwa kwa Ufaransa na Zidane kutwaa ubingwa wa Dunia na kwenye fainali alifunga bao la mkwaju wa penati ambalo lilimfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanne pekee ambao wamewahi kufunga kwenye fainali mbili tofauti.


Hata mchezo huo ulipomalizika katika muda wa kawaida, ulilazimika kuamuliwa kwa muda wa nyongeza ambako Zidane almanusra afunge bao kwa kichwa lakini mpira aliopiga uligonga mwamba. 


Kwa mshangao wa wengi, Zidane alionyeshwa kadi nyekundu zikiwa zimebaki dakika kumi fainali ifikie hatua ya matuta baada ya kumpiga kichwa beki wa Italia, Marco Materazzi.

Ufaransa iliishia kufungwa kwa mikwaju ya penalti na wengi walifikiri kuwa endapo Zidane asingetolewa, Ufaransa ingekuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa wao wa pili.

Fainali hiyo ilikuwa siku ambayo mabadiliko yalifanyika ambapo ‘master’ wa soka kwa muongo uliopita yaani Zidane, alikuwa anamaliza zama zake na kijana ambaye anakuja kurithi nafasi yake alikuwa anaanza taratibu.


KIUNGO MCHEZESHAJI BORA


Mwaka 2006 kundi la watu liliamua kuanzisha tuzo maalum kwa viungo wachezeshaji, tuzo ambayo ilipewa jina la WORLD PLAYMAKER AWARD yaani kiungo mchezeshaji bora, na tuzo ya kwanza kwa mwaka huo ilikwenda kwa Zidane.

Ilikuwa njia nzuri ya kumuenzi kiungo mchezeshaji bora wa kizazi cha hivi karibuni. Kaka alishinda mwaka uliofuatia na kwa upande wake alikuwa kama Zidane kwa njia nyingi.

Mwaka 2008, kiungo mchezeshaji wa aina mpya aliibuka. Aliwahi kuwepo tangu awali, ila kwa mwaka huo alianza kuchukua nafasi yake kama mtu muhimu kwenye timu alizochezea, alianza kutawala mechi alizocheza katika njia ambayo ilisababisha ushindi kwa timu yake.


Mashabiki walianza kuona kile ambacho anafanya akiwa uwanjani, jinsi alivyokuwa akiwaongoza wenzake uwanjani. Xavi Hernandez ndiye kiungo mchezeshaji anayezungumziwa.

Mwaka 2006 pia ulikuwa mwaka ambao Barcelona walianza kutambulika kama timu ya kuogopwa Ulaya, na mwaka 2008 timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, ilianza rasmi safari yake kuelekea mafanikio ya kiwango cha juu.

Mchezo wa soka ambao ulikuwa ukitegemea zaidi nguvu katika miaka iliyopita ulianza kubadilika. Barcelona na Hispania zikiwa na wachezaji wadogo kimaumbo lakini wenye uwezo mkubwa kimbinu na kiuwezo kama Xavi Hernandez, Andres Iniesta na Lionel Messi zilibadilisha jinsi soka la Ulaya lilivyochezwa na wachezaji hawa wakiibuka kama wachezeshaji wapya kwenye soka.

Xavi Hernandez alishinda tuzo ya kiungo mchezeshaji bora kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2008 mpaka 2011. Alistahili tuzo hiyo na alistahili tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka 2008.


Xavi aliziongoza Barcelona na Hispania kupata mafanikio kwa miaka minne akitwaa mataji karibu yote kwenye soka la klabu na timu ya taifa. Xavi alikuwa kama funguo iliyofanya wenzie wacheze vizuri.
     

 
Mwaka 2012, tuzo ya kiungo mchezeshaji bora ilihamia kwa mwenzie Andres Iniesta. Michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2012 ilimshuhudia Xavi akitwaa tuzo ya mchezaji bora na alimaliza kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Cristiano Ronaldo na Messi kwenye tuzo za Ballon D’or.

Hatimaye Iniesta alitambuliwa kama mmoja wa wachezaji bora. Miaka kumi ikiwa imepita tangu Zidane alipotwaa ubingwa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid pamoja na tuzo ya mchezaji bora wa dunia, kiungo mchezeshaji wa aina mpya alichukua mikoba ya Zidane akiwa anacheza kwa staili tofauti na Zidane lakini kwa ubora, kiwango na matokeo yale yale .



KIUNGO MCHEZESHAJI ALIYEKAMILIKA


Andres Iniesta alianzia soka lake akiwa kwenye Academy ya La Massia inayomilikiwa na Barcelona. Uwezo wake wa kucheza kwenye nafasi tofauti, kujituma, na umuhimu kwenye mchezo, ulimfanya achukua nafasi kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 18 na alianza kucheza mechi mfululizo kwenye msimu wa mwaka 2004/05.

Akiwa kama mchezaji mchanga, Iniesta alianza kufanya mazoezi akiwa na kikosi cha kwanza na Pep Guardiola (kocha wa zamani wa Barcelona wakati akiwa bado mchezaji) alimwambia Xavi kuwa, yeye (Xavi) angemfanya Guardiola astaafu lakini Iniesta atawafanya wote wawili yaani Xavi na Pep wastaafu.


Pep Guardiola na Andres Iniesta

Guardiola aliona mbali na hakukosea kwa kauli aliyoitoa, Iniesta hakuwa bora kwenye pasi pekee bali alikuwa mzuri kwenye ukokotaji wa mpira, alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza maeneo tofauti ya uwanja na alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kutoa pasi muhimu.


Ilikuwa chini ya Guardiola ambapo Iniesta aliuteka ulimwengu. Guardiola alimtengeneza Iniesta na kumfanya kuwa mchezaji muhimu kwa Barcelona na Hispania na kubwa alilofanya Guardiola ni kumfanya Iniesta ambaye kwa kawaida ni mtu mkimya, kuwa kiongozi kwenye timu yake.


Chini ya nahodha huyu wa zamani wa Barcelona, soka la Iniesta lilifikia kiwango cha juu kupita hata Xavi na Guardiola kama ilivyokuwa kauli ya Guardiola. Alikuwa kiungo mchezeshaji aliyekamilika na hadi sasa ameingia kwenye orodha ya wachezaji bora waliowahi kucheza Barcelona.


MFUNGAJI WA MABAO MUHIMU

Iniesta siyo mfungaji wa mabao mengi, lakini ni mfungaji wa mabao mazuri na muhimu kwa timu yake kama Zidane. Iniesta alikuwa akifunga kwenye mechi muhimu na kubwa.

Moja ya mabao ambayo yatakumbukwa na wengi ni bao alilowafunga Chelsea mwaka 2009 kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ulikuwa mpira wa mwisho kwenye mechi hiyo na ulikuwa mpira ambao Iniesta alifunga bao lililoivusha Barcelona hadi fainali.


Kwenye Kombe la Dunia 2010, Iniesta alifunga bao muhimu kwenye historia ya soka la Hispania. Huku ubao wa matokeo ukisomeka 0-0 wakati wa fainali hiyo dhidi ya Uholanzi, mpira ulimfikia Iniesta upande wa kulia wa eneo la 18, halikuwa bao kama la Zidane kwenye fainali ya mwaka 2002 wakati Real Madrid walipocheza na Bayer Leverkusen, lakini umuhimu wake ulikuwa ule ule.

Zidane alitwaa Kombe la Dunia na ubingwa wa Ulaya akiwa na Ufaransa, lakini hakuweza kutwaa mataji matatu mfululizo na hakuna yeyote aliyewahi kufanya hivyo kabla.


Hispania waliweka historia hiyo na Iniesta alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2012. Aliiongoza timu yake akiwa ndani ya uwanja kwa uwezo wake na miaka minne baada ya Xavi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2008, Iniesta alitimiza utabiri wa Guardiola.


 

Kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2011, Kocha wa Manchester United, Sir. Alex Ferguson alisema kuwa, kwake Messi si mchezaji anayemuogopa, anamuogopa zaidi Iniesta kwani ndiye hasa mwenye funguo za Barcelona kwa jinsi anavyotafuta upenyo wa kupitisha mipira kwa wenzake na mabao yake muhimu.


Vicente Del Bosque ambaye aliwahi kufanya kazi na Zidane kwenye klabu ya Real Madrid, alimtaja Iniesta kama mchezaji aliyekamilika kuliko wote aliowahi kuwaona.

Na mchezaji mwingine, Samuel Eto’o alimtaja Iniesta kama mchezaji bora duniani kwani kila awapo uwanjani huwa anatengeneza maajabu.

Hakuna ubishi kuwa Iniesta amekuwa akibadilika kwenye nafasi ya kiungo mchezeshaji bora kuendana na mchezo wa soka kwa zama za sasa.

Akiwa kwenye mfumo wa Barcelona huku akicheza soka kuendana na umbo lake dogo, Iniesta alijifunza kumiliki mpira na kuuelewa mchezo kwa jinsi anavyotengeneza ‘movement’ zake, mbinu na hata maamuzi ambayo anayafanya, kitu kinachofanya soka kuonekana rahisi kwake. 

SANDRA AITETEA NDOA YAKE

Sandra alifunguka hayo kupitia Stori 3 ambapo alisema taarifa hizo ndizo zilimpa hata mkosi kwani zilipoanza kuvuma ndiyo kipindi ambacho alipata ajali ya gari.
“Sijawahi kuachwa, mimi pamoja na familia yangu tunafurahia maisha ya ndoa. Hao walioeneza hizo taarifa, walikuwa na lengo la kuniharibia na hawajaweza,” alisema Sandra.

JB ATOA SOMO KWA WATANZANIA

Na Mwandishi Wetu
BONGE la Bwana, Jacob Steve ‘JB’ amewataka Watanzania kuwa na wivu wa kimaendeleo ili kuweza kufika mbali kisanaa kwa kuiga mazuri.
JB alifunguka hayo muda mfupi baada ya kutua Bongo akitokea nchini Rwanda walipokwenda kushuhudia Tuzo za Filamu zilizokuwa zikigawiwa kwa wasanii wa nchini humo.
“Kuhusu zile tuzo inabidi na sisi tujifunze kuthamini vitu vya kwetu, wadau inabidi walitazame kwani kwa hatua ambayo sisi tumefikia, ilipaswa tuwe na tuzo nyingi kuliko hata Rwanda ambao ndiyo kwanza wanainuka kwenye soko la filamu,” alisema JB.

AIBU ILIYOJE! MKE WA MTU ABAMBWA ‘AKIBANJUKA’ NA SHEMEJI YAKE


Na Dustan Shekidele, Morogoro
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Bahati ambaye ni mke wa Mrisho Juma, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya aina yake baada ya kunaswa laivu ‘akibanjuka’ na shemeji yake.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na umati wa watu lilijiri Machi 11, mwaka huu mchana kweupee katika eneo la Mafisa kwa Mbambi ndani ya chumba cha Mbaji Hamis ambaye ni mdogo wa Mrisho.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Mrisho ambaye anafanya kazi ya kupiga debe katika stendi ya mabasi ya Msamvu alisema, fumanizi hilo halikutokea kwa kuweka mtego bali ni Mungu tu.
Alieleza kuwa alikamatwa Ijumaa na kutupwa mahabusu kwa kosa la kutovaa ‘yunifomu’. Mkewe na mdogo wake wakawa wanampelekea chakula.
“Jumapili jioni walikuja tena kuniletea chakula ila kwa bahati nzuri Jumatatu nikapewa onyo na kuachiwa. Cha ajabu nilipofika nyumbani nilimkuta mtoto wangu wa miaka 2 analelewa na majirani.
“Nilipowauliza mke wangu yuko wapi walidai tangu Jumamosi hajaonekana kwa maelezo kwamba amekwenda kushughulikia dhamana yangu,” alisema Mrisho na kuongeza kuwa aliendelea kumtafuta sehemu mbalimbali hadi alipoamua kwenda nyumbani kwa mdogo wake.
“Nilipofika nilimkuta mke na mdogo wangu wakiwa pamoja kitandani. Baada ya mdogo wangu kuniona alinyanyuka na kuvaa bukta kisha akatoka nduki,” alisema Mrisho.
Ikaelezwa kuwa, baada ya mwanaume huyo kumfumania mkewe huku majirani wakishuhudia, alimshushia kipigo kisha akampa talaka kabla ya kuamua kumrudisha kwao Tabora.
Akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na kufumaniwa huko, Bahati alisema shemeji yake alimlazimisha kulala naye baada ya kutoka polisi kumpelekea chakula mumewe.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Rehema Dimoso alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake.”

LULU: KANUMBA ALIKUWA ZAIDI YA MPENZI, MUME

Na Musa Mateja
KWA mara ya kwanza tangu atoke mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar kwa dhamana, staa wa filamu na video za wasanii wa Bongo Fleva, Elizabeth Michael ‘Lulu’ au Lizy amefunguka juu ya uhusiano wake na aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba na kusababisha gumzo kubwa mitandaoni.
Huku akipiga picha za pozi kwa mara ya kwanza tangu atoke selo, Lulu alifunguka wikiendi iliyopita kupitia ukurasa wake katika mitandao ya Instagram na Twitter kuwa Kanumba alikuwa zaidi ya baba, kaka, mpenzi, mume, ndugu na rafiki hivyo hataacha kumlilia maisha yake yote.
Huku akitanguliza picha ya marehemu Kanumba enzi za uhai wake akipokea moja ya tuzo zake, Lulu aliandika:
“Ulikuwa zaidi ya baba, kaka, mpenzi, mume, ndugu na rafiki…sitaacha kukulilia katika maisha yangu yote!! R.I.P daddy yangu Steven Kanumba.”
Kanumba.
Ndani ya muda mfupi, kauli hiyo ya Lulu ilipata maoni mengi huku baadhi ya watu wakimpa pole kumtia moyo na wengine wakijibizana kwa hasira juu ya ishu hiyo.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia marehemu Kanumba ambayo inatarajiwa kuanza kuunguruma muda wowote.

DIAMOND: NIMEMTUNDIKA MIMBA PENNY






Diamond akipozi na Penny.
Kwa mujibu wa Diamond, ni kweli yeye na Penny ambaye ni presenta wa Kituo cha Runinga ya DTV wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kabla hata ya ndoa waliyopanga siku zijazo.
Diamond alifunguka kuwa tayari amempa mrembo huyo gari la kutembelea huku akimwagizia lingine jipya aina ya Hyundai ix35.
...Wawili hao wakiwa katika pozi la kimahaba.
“That’s true (ni kweli) nimemtia mimba Penny, unajua sipendi kusema mpenzi wangu, sasa hivi ni mama watoto wangu. Ni kweli pia nimempa gari kwa sababu ya mizunguko ya kwenda kliniki na nini, nikaona siyo vizuri kwenda kugombea daladala,” alisema Diamond.
Gari hilo jipya aina ya Hyundai ix35 gharama yake inakadiriwa kufikia Sh. milioni 50. 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATOA POLE KWA WAFIWA

4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Prince David, mtoto wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, marehemu WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana. Picha na OMR
Picha ya Marehemu enzi za uhai wake.
1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana. Picha na OMR

MKUTANO WA KUTOA MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA SHERIA NAMBA 5 YA MWAKA1985 YA MAGAZETI WAFANYIKA ZANZIBAR

DSC07005
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo Fakihi Haji Mbarouk akitoa hotuba ya makaribisho kwa waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sheria namba 5 ya mwaka 1985 hapo katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar.  PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

MKUTANO WA SARPCCO WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

NO 1Mwenyekiti wa SARPCCO IGP Said Mwema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) baada ya kufungua mkutano wao wa siku mbili jijini Dar es Salaam.Mkutano huo utajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kufanya Operesheni za pamoja baina ya Nchi wanachama wa umoja huo.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mwenyekiti wa SARPCCO IGP Said Mwema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na wajumbe wa Kamati tendaji za Mafunzo, Sheria na wanawake  baada ya kufungua mkutano wao wa siku mbili jijini Dar es Salaam.Mkutano huo utajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kufanya Operesheni za pamoja baina ya Nchi wanachama wa umoja huo.(Picha na Frank Geofray-Jeshi laPolisi)

NO 4
Kaimu DCI, Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Mngulu  akiongea katika mkutano wa wakurugenzi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).Mkutano huo wa siku mbili utajadili mambo mbalimbali yanayohusu uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kufanya Operesheni za pamoja baina ya Nchi wanachama wa umoja huo.

RC KANALI MSTAAFU ISSA MACHIBYA AYATAKA MAKAMPUNI YA SIMU KUDHIBITI VITENDO VYA UHALIFU KUIPITIA SIMU ZA MKONONI

kikwete 1316Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akifungua mkutano wa wadau wa Mawasiliano ulioandaliwa na TCRA mkoani humo kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazokabili sekta hiyo jana kikwete 1319
                         Wadau  mbalimbali Mawasiliano wakiwa katika mkutano huo
Na Mwandishi wetu,Kigoma
Mkuu wa mkoa kigoma Issa Machibya amezitaka kampuni za simu za mkononi kuweka udhibiti wa kutosha kwa mitandao yao ya simu ili kuzuia vitendo vya utapeli na uhalifu ambavyo vimechangiwa na simu hizo. Akifungua kikao cha
siku moja cha wadau wa mawasiliano leo kilichoitishwa na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) Machibya alisema kuwa mitandao ya simu imekuwa ikitumika sana kwa sasa katika kufanyia utapeli lakini juhudi za kuwakamata wahusika hazizai matunda.
 Alisema kuwa moja ya sababu za kushindwa kukamatwa kwa wahalifu hao ni pamoja na kusajili kwa kutumia majina bandia jambo ambalo amesema linaviwia vigumu vyombo vya usalama kuwamakata wahusika waliojiandikisha kwa majina bandia.
 Ili kufanikisha kuhakikisha mwenye simu ndiye mwenye jina halisi amezitaka kampuni za simu kuhakikisha kwamba mawakala wao wanaohuza laini za simu wanapata vitambulisho sahihi vya wahusika na kutokubali kusajili namba ya simu kam muhusika hana kitambulisho.
 Akizungumzia kuhusu kuanza kwa matumizi ya teknolojia ya digitali kutoka analojia Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wananchi wanapaswa kukubaliana na mabadiliko ya teknolojia kwani jambo hilo si la Tanzania peke yake bali ni suala la kidunia.
 Alisema kuwa jambo kubwa ambalo linapaswa klufanywa kwa sasa ni kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa mfumo huo na kuona namna gani serikali na wadau mbalimbali wanashirikiana kuhakikisha wananchi wanatumia teknolojia hiyo kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake Meneja mipango na utafiti wa mamlaka ya mwasiliano nchini (TCRA), Ally Simba alisema kuwa moja ya kazi za mamlaka ni kuhakikisha teknolojia mbalimbali zilizochini ya mamlaka hizo zinatumika bila kuleta athari kwa jamii na kwamba kutokana na hilo wanatarajia kukaa tena na wadau mbalimbali katika kuangalia suala la udhibiti wa simu za mkononi zisitumike vibaya.