This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, April 20, 2013

WAREMBO WAGOMBEA KUMPA NAMBA MZUNGU...

 

  Otilia Boniface kulia na Janeth Tingisha Wanenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Otilia Boniface na Janeth Tingisha mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa kali ya mwaka baada ya kutaka kutwangana makonde wakigombea kutoa namba zao za simu kwa buzi la Kizungu. Tukio hilo lilitokea ndani ya Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza jijini Dar ambapo awali Mzungu huyo alivutiwa na wadada hao hivyo kuwafuata na kuomba namba ya simu ya mmoja wao. Kufuatia ombi la Mtasha huyo, kila mmoja alitaka apate nafasi hiyo ndipo wanenguaji hao waliposukumana na kufikia hatua ya Janeth kuchukua simu ya Otilia na kuipiga chini ila kwa busara za Mzungu huyo alichukua namba za wote.

SPIKA WA BUNGE AWAKAANGA TENA WALE WABUNGE WALIOTIMULIWA BUNGENI.....




Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika.
 Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu jambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.

Kwa uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo.


Uamuzi wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu na wengine  watano na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge umebarikiwa na Mheshimiwa Spika..
 Hivyo Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo Na adhabu iliyotolewa.
Photo
Taswira ya vurugu zilizotokea bungeni dodoma juzi

MWANAMZIKI ARUHUSU MASHABIKI WAMSHIKE NYETI ZAKE AKIWA JUKWAANI


DARASA LA SABA SASA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI

Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.


Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.


Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.


Sifa zinazotakiwa

Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.


Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:


“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”


Vigezo

Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.


“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.


chanzo:gazeti la mwananchi

Airtel Money Yaendeleza udhamini wake katika semina ya wapiga picha wa vyombo 15 vya habari nchini

Meneja wa Airtel Money Asupya Nalingigwa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wapiga katika semina ya upigaji picha iliyofanyika jijini Dar Es Salaam, akifuatiwa ni Afisa uhusisano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki na Muhadhiri wa Chuo Kikuu Richard Ndunguru.

Waandishi wa habari waliohudhuria semina ya ya upigaji picha iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel jijini Dar Es Salaam.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia huduma…
Waandishi wa habari waliohudhuria semina ya ya upigaji picha iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel jijini Dar Es Salaam.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya kibebki ya Airtel Money kwa mara ya pili imedhamini semina ya wapiga picha wanahabari inayofanyika kwa muda wa siku mbili hapa jijini Da r Es Salaam kuanzia leo 18 hadi 19 Apili 2012.

Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money imedhamini kampuni ya jijini Dar es salaam ijulikanayo kama MP5 2011 entertainment kuandaa semina maalum itakayowakutanisha wataalam na wapiga picha za habari wa muda mrefu kukutana na wanahabari wapiga picha ili kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji kazi zao.
Akiongea kwa niaba ya waandishi wapiga picha waliohudhuria semina hiyo Bw, Selemani Mpochi mpiga picha wa muda mrefu nchini alisema “hii ni sehemu muhimu sana kwetu wanahabari kujitengenezea utaratibu wakukaa pamoja na kutafakari mambo muhimu ili kuendelea kufanya kazi zetu kwa ufanisi,Kwa niaba ya wenzangu wote tunawashukuru sana Airtel kupitia huduma yao ya Airtel Money kwa kutudhamini katika semina hii kwa mara ya pili sasa, tunashukuru sana kwa ushirikiano wao wa kuwa tayari kutusaidia kuendeleza taaluma yetu na kuonyesha kuwa wanatambua umuhimu wa wanahabari nchini
Airtel inaendelea kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamenufaika kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hivyo semina hii ni njia nyingine itakayoweza kuinua kiwango cha mapato na uelewa wa Airtel Money kwa waandishi wa habari nchini
Zaidi ya wapiga picha za habari wapatao 15 toka vyombo vya habari nchini wanatarajiwa kuhudhuria semina hiyo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa msimbazi center

FID Q; AFUNGUKIA ALIVYOFANYA KAZI NA BI. KIDUDE

Stori:Chande Abdallah na IssaKwisa Mponi

WIKI iliyopita kwenye safu hii ya Funguka na Risasi tulikuwa naye mwigizaji Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’ ambaye alifungukia ndoa yake na kashfa yake ya kujiuza.
Fid Q akiwa na Bi kidude enzi za uhai wake

ROSE NDAUKA AWATEGA MADENTI


STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye ‘industry’ ya filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni alitinga kivazi kifupi ambacho kiliwachengua madenti wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ambao walibaki kumkodolea macho mwanzo mwisho.
Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.

Kutokana na kivazi hicho alichokivaa na mvuto alionao staa huyo, baadhi ya madenti wakware walionekana wakipoteza usikivu wa hotuba ya mgeni rasmi na kubaki…
Stori:Denis Mtima
STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye ‘industry’ ya filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni alitinga kivazi kifupi ambacho kiliwachengua madenti wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ambao walibaki kumkodolea macho mwanzo mwisho.
Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.
Kutokana na kivazi hicho alichokivaa na mvuto alionao staa huyo, baadhi ya madenti wakware walionekana wakipoteza usikivu wa hotuba ya mgeni rasmi na kubaki kumtazama.
“Mh! Rose ni mzuri jamani uongo dhambi, nilikuwa nikimuona katika runinga leo nimemuona live daaah!” alisikika denti mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.