This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, April 13, 2013

MLELA ADAIWA KUMTUNDIKA DENTI MIMBA

STAA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kumtundika mimba mwanafunzi aliyefahamika kwa jina moja la Salha, mkazi wa Zanzibar ambaye anasoma katika chuo cha ITF, Tandika, jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilichopo chuoni hapo, Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na denti huyo kwa muda mrefu ambapo mashosti wote wa Salha, walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa kibendi.

 “Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema hahitaji mtoto, atoe mimba.

MBWA AKUTWA NA MGUU WA BINTI WA DARASA LA 7

IMANI za kishirikina zimezidi kukitisa Kijiji cha Isange, Kata ya Isange, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya baada ya matukio ya kupotea na kuuawa kwa watoto kutokea mara kwa mara ambapo safari hii binti mmoja wa darasa la saba ameuawa na mguu wake kukutwa ukiliwa na mbwa.

Binti huyo aliyeuawa amegundulika kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba  aliyejulikana kwa jina la Lista Sebule aliyekuwa akisoma katika Shule ya Msingi Mpombo iliyopo Isange na alipotea katika mazingira ya kutatanisha na maiti yake kukutwa kando ya mto siku tisa baadaye. Katika tukio la awali, mtoto mmoja alikatwa kichwa na watu wasiojulikana kisha kutoweka nacho.

Mama mzazi wa marehemu, Christina Sakalile alisema binti yake (Lista) alipotea saa tisa jioni ya Machi 31, mwaka huu baada ya kutumwa kupeleka simu kibandani ili…
IMANI za kishirikina zimezidi kukitisa Kijiji cha Isange, Kata ya Isange, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya baada ya matukio ya kupotea na kuuawa kwa watoto kutokea mara kwa mara ambapo safari hii binti mmoja wa darasa la saba ameuawa na mguu wake kukutwa ukiliwa na mbwa.
Binti huyo aliyeuawa amegundulika kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba  aliyejulikana kwa jina la Lista Sebule aliyekuwa akisoma katika Shule ya Msingi Mpombo iliyopo Isange na alipotea katika mazingira ya kutatanisha na maiti yake kukutwa kando ya mto siku tisa baadaye. Katika tukio la awali, mtoto mmoja alikatwa kichwa na watu wasiojulikana kisha kutoweka nacho.
Mama mzazi wa marehemu, Christina Sakalile alisema binti yake (Lista) alipotea saa tisa jioni ya Machi 31, mwaka huu baada ya kutumwa kupeleka simu kibandani ili ‘ikachajiwe’ lakini hakurudi hadi giza lilipoingia, hali iliyozua wasiwasi na wakaanza kumtafuta bila mafanikio.
“Baada ya tukio hilo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isange, Daudi Nsyani aliitisha mkutano wa wananchi wote ili mtoto atafutwe. Juhudi hizo zilizaa matunda Aprili nane, mwaka huu lakini alipatikana akiwa amekufa huku akiwa hana baadhi ya viungo mwilini,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.
  Mashuhuda wa tukio hilo walisema mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa kando ya Mto Nkalisi uliopo kijijini hapo ukiwa umekatwa kichwa na miguu ambapo mguu mmoja ulipatikana baada ya mbwa kukutwa akiwa anaula na alipoona watu akawa anakimbia nao.
Hali hiyo iliwafanya watu kumfuatilia mbwa huyo ambaye aliongoza hadi kwenye mwili wa marehemu na kuwakuta mbwa wengine wawili wakiwa kando yake ambapo uongozi wa kijiji uliliarifu jeshi la polisi.
“Polisi walipofika walifanya uchunguzi na wananchi wakapiga kura ya siri ambapo watu wawili walikamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio hili. Mwili ulikabidhiwa kwa ndugu na wakauzika siku hiyohiyo na mazishi yake yaliweka historia kwa kuhudhuriwa na watu wengi,” alisema shuhuda huyo.
Diwani wa Kata ya Isange, Elias Mwandele amethibitisha kutokea tukio hilo na aliwataka wazazi kutowapeleka watoto kwenye shughuli za kuchunga mifugo kwa sasa.

Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo…
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 na kuonyesha kuwa kuna skandali kubwa
sana katika akaunti ya Deni la Taifa. Nanukuu

‘Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30
Juni, 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho ya deni ya shilingi
619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha.’
(Taarifa ya CAG, Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 uk 158).
Mwisho wa Kunukuu



Katika Taarifa yake hiyo CAG anaendelea kuonyesha
kuwa Deni la Taifa linazidi kukua na mwaka unaoishia mwezi Juni 2012 deni
lilikuwa kwa asilimia 17 kutoka mwaka unaoishia mwezi Juni 2011.

Kukosekana kwa maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi
ya nusu trilioni za Deni la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka
makubwa, kuchunguzwa na kupata majawabu stahiki. Tafiti mbalimbali duniani
zinaonyesha kuwa kuna mahusiano makubwa sana kati ya Deni la Taifa la
utoroshaji wa fedha kwenda kwenye mabenki ya ‘offshore’. Katika kitabu cha
‘Africa’s Odious Debts: How Foreign Loans and Capital flight bled a continent’
kilichoandikwa mabwana Leonce Ndikumana na James Boyce imeonekana kwamba Deni
la Taifa huchochea utoroshwaji wa Fedha kwenda kuficha nje ya Tanzania.

Mabilioni haya kwenye akaunti ya Deni la Taifa
yanashtusha sana. Kambi ya Upinzani Bungeni kwa miaka miwili mfululizo imekuwa
ikitaka ukaguzi maalumu kwenye akaunti za Deni la Taifa lakini Serikali
imeshindwa kufanya hivyo. Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC pia nimemtaka CAG
afanye ukaguzi huu maalumu.

Kambi ya upinzani Bungeni ilisema hivi katika
Bajeti yake kivuli 2012/13:

DENI LA TAIFA

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inasikitika kwa serikali kuendelea kutengeneza
madeni kwa Taifa kwa kuendelea kukopa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya
serikali. Wakati Serikali inasisitiza kwamba Deni letu linastahmilika, Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anaonyesha mashaka makubwa sana kutokana na kasi ya
kukua kwa Deni la Taifa. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali inaonyesha  kuwa Deni la Taifa
linazidi kuongezeka kwa asilimia 38% kutoka shilingi trillion 10.5 mwaka
2009/2010 hadi shilingi trillion 14.4 mwaka 2010/2011. Kwa mujibu wa Waziri wa
Fedha Deni la Taifa limefikia shilingi trillion 20.3 mpaka ilipofika mwezi
Machi mwaka 2012. Ukisoma taarifa ya Mwezi wa Mei 2012 ya Benki Kuu ya
Tanzania, Deni la Taifa sasa limefikia shilingi trillion 22.



Mheshimiwa Spika, Suala hapa sio ustahmilivu wa
Deni kama inavyodai Serikali bali ni kwamba tunakopa kufanyia nini? Bajeti ya
Mwaka 2012/13 inayopendekezwa inaonyesha kwamba Serikali itakusanya shilingi
trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama
matumizi ya kawaida. Ni dhahiri kwamba sehemu ya mikopo ambayo serikali
inachukua sasa itakwenda kwenye matumizi ya kawaida. Hatutaki mikopo kwa ajili
ya matumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari nk. Tuchukue mikopo kuwekeza
kwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi. Bajeti inaonyesha kwamba
Serikali itakopa shilingi takribani trillion 5 mwaka 2012/13.  Serikali ikubalikutekeleza mapendekezoya
Kambi ya Upinzani ya kuimarisha ukusanyaji
wa kodi na kupanua wigo wa kodi katika maeneo muhimu kama sekta ya
madini na mawasiliano, kuzuia misamaha ya kodi, kutokomeza ukwepaji kodi, na
kuepuka matumizi mabaya ili kuepuka madeni yasiyo ya lazima.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapenda
kusisitiza kwamba Bunge lifanye ukaguzi maalumu kuhusu akaunti ya Deni la Taifa
ili kuweza kubaini ukweli kuhusu ustahmilivu wa Deni na mikopo ambayo Serikali
inachukua kama inakwenda kwenye Maendeleo na miradi ipi na kama miradi hiyo ina
tija. Vilevile tumependekeza kwamba Mikopo yote ambayo Serikali inachukua iwe
inapata idhini ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi au Bunge litunge sharia
ili kiwango cha juu cha kukopa ambacho Serikali haipaswi kuvuka. Kuiacha
Serikali inaendelea kukopa bila mpango ni kuliweka Taifa rehani na kupeleka
mzigo wa kulipa madeni haya kwa kizazi kijacho. Hatuwezi kukubali Wazee wetu waishi maisha yao, waishi maisha yetu na
pia wakope maisha ya watoto wetu.
Mwisho wa
kunukuu.

Kambi ya Upinzani inarejea kutaka
ukaguzi maalumu kuhusu akaunti za Deni la Taifa na maelezo ya kina ya Serikali
kuhusu shilingi 620 bilioni ambazo hazina maelezo kwenye Deni la Taifa.
Hatuwezi kukaa kimya kuona Watanzania wanabebeshwa madeni ambayo kimsingi ni
madeni bandia yanayotajirisha watu wachache wenye uwezo na ujasiri mkubwa wa
kuiba, kupora nakufisidi hazina ya Taifa letu.