This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Monday, February 25, 2013

MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR

Maalim Seif apinga mauaji ya Padri asema si ya kigaidi

 

 

 

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amepinga kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi kuwa mauaji ya viongozi wa dini Zanzibar ni ugaidi na kusema kuwa wanaofanya hivyo ni watu wenye nia ya kuvunja umoja wa Wazanzibari.
Baada ya mauaji ya Padre Evarist Mushi, akizungumza na wandishi wa habari,Nchimbi alielezea kusikitishwa na mauaji hayo akisema kuwa ni ya kigaidi na yana lengo la kuingiza nchi katika machafuko. Amesema kuwa tukio hilo si tukio la ujambazi bali tukio la kigaidi kwani limelenga zaidi katika kuwashambulia viongozi kidini.


Padre Evaristus Mushi aliuawa Februari 17, mwaka huu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliokuwa katika pikipiki aina ya Vespa wakati akienda kuongoza misa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Beit el Rass.

“Watu hawa wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini ili kuvunja umoja wa Wazanzibari, lakini nasema hakuna ugaidi Zanzibar,” alisema Maalim Seif juzi usiku alipohutubia kwenye hafla ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) mjini Kiuyu, Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba.

Alisema hivi sasa Wazanzibari ni wamoja na watu hao wenye nia mbaya wanayachukulia matukio hayo kwa kutaka kuwagawa na kuwaletea mtafaruku kwa kuonyesha kuwa kuna tofauti za kidini Zanzibar wakati siyo kweli.

Alisema inasikitisha kuona wapo baadhi ya viongozi wenye nia chafu dhidi ya Zanzibar wenye tabia ya kutoa kauli za kujenga chuki na fitina miongoni mwa Wazanzibari chini ya kivuli cha matukio hayo.

Makamu huyo wa Kwanza wa Rais alisema, kinachoonekana kuna ajenda imetayarishwa ya kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, licha ya kuwapo kwa historia ya miaka mingi ya watu kuvumiliana na kuishi kwa pamoja na kuwapo watu wa imani tafauti.

Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar hivi sasa kuwa macho na ajenda zinazolengwa kuwavuruga na waendelee kuishi kwa mshikamano na umoja kama ambavyo wamekuwa wakiishi.

Maalim Seif alisema vitendo vya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini Zanzibar ni mambo mageni na kwa miaka mingi Zanzibar imekuwa ni mfano bora wa uvumilivu wa kiitikadi za kidini, licha ya kuwa asilimia 98 ya wananchi wake ni Waislamu.

Alisema Katiba ya Zanzibar imeweka wazi haki ya mtu kuabudu kwa mujibu wa imani yake na uhuru wa mtu kuabudu umelindwa.

“Ni Sultani wa Zanzibar ambaye alikuwa Muislamu ndiye aliyetoa ardhi kwa Wakiristo kujenga Kanisa. Juzi nilipokwenda kutoa salamu za rambirambi kwa Baba Askofu Shayo, baada ya kifo cha Padri Mushi, aliweka bayana kuwa lililotokea lisihusishwe na tofauti za kidini,” alisema Maalim Seif.

Hata hivyo, Maalim Seif alisema inasikitisha kuona wakati Rais Jakaya Kikwete katoa maelekezo uchunguzi wa kina ufanyike na Kamishna wa Polisi Zanzibar ameshaweka wazi kuwa uchunguzi unaendelea, baadhi ya viongozi na vyombo vya habari vinachochea chuki za kidini na kusema kuwa Zanzibar kuna ugaidi.

Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar kwa wakati huu kuwa watulivu na wasitawaliwe na jazba na wala wasichokozane, pia wasikubali kuchokozeka.


Akizungumzia matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotolewa hivi karibuni, Makamu wa wa Kwanza wa Rais alisema ni matokeo mabaya na ya kuliza, kwa sababu hayaonyeshi mustakabali mwema kwa watoto wetu na nchi yetu hapo baadaye.


Alisema ni wakati mwafaka Serikali, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, walimu na jamii nzima kujiuliza nini sababu ya matokeo hayo mabaya, na kujiuliza pia nchi inaelekea wapi?

Maalim Seif alisema sasa si wakati tena wa kutupiana lawama, lazima pande zote zikae zijadili wapi pamekosewa, ili ufumbuzi uweze kupatikana na hali kama hiyo isitokee tena siku nyingine.

 

NI WAREMBO MISS UTALII

HAPA NI WAREMBO TU .... LAKELAND AFRICA WADHAMINI UTALII WA NDANI , MISS UTALII TANZANIA 2012/13

 

 

Washiriki wa Miss Utalii tanzania wakiwa katika moja ya Makaburi ya zamani Kaole Bagamoyo.
Mshiriki wa Miss Utalii Tanzania Pamoja na washiriki wengine wakikata utepe kwa ajili ya uzinduzi wa safari ya Kitalii Bagamoyo.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa katika moja ya Kaburi maarufu la Wapendanao.

MIWA YA MTIBWA YAMLEWESHA SIMBA



 Timu ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo jioni katika Uwanja wa Taifa.

Bao la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja.

Bao hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezua mtafaruku mkubwa baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba, walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharula.

Aidha mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha maji ya kuwasha, huku viongozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika uwanjani hapo. 

Hata hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha pili.

 Beki wa Simba, ambaye leo amechezeshwa kama kiungo wa chini, Shaban Kapombe, akimchezea vibaya Rashid Gumbo.

 Beki wa Simba Keita, akimdhibiti mchezaji wa Mtibwa.
Mshambuliaji wa Mtibwa, akiwasakata mabeki wa Simba.



ANGETILE :TUTAKAA KUJADIRI NINI TUFANYE KUZINGATIA FIFA INATAKA NINI ?

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/AngetilewaTFF(2).jpg
Katibu mkuu wa tff angetile osiah amaesema tff itakutana ili kujadiri maamuzi ya serikali kuifuta kwani wao wanaendesha mpira kikatiba kwani wao wanaongoza mpira unaongozwa na fifa, caf ,cecafa,  na sio serikali na katiba tff inasema kuwa inatakiwa kufuata maagizo ya kutoka  fifa amesema wao watakaa chini na kulitazama na nini wataamua  .



NANI ATAKUWA SAHIHI FIFA,TFF,BMT,AU SERIKALI ,NI BAADA SERIKALI KUFUITA KATIBA MPYA YA TFF

 
WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO FENELLA MUKANGARA.

Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Fenella Mukangara amefuta matumizi ya katiba mpya ya TFF ya mwaka 2012 kwa vile imekiuka kanuni na sheria za BMT hivyo TFF wanatakiwa kutukia katiba ya mwaka 2006 ambayo imetumika katika mikoa kufanyia uchaguzi.

Mukangara amesema TFF inatakiwa kufuata kanuni nasheria za BMT ambazo ambazo ndizo zenye maelekezo ya kufanya marekebisho ya katiba .

Hakuna chama chochote hapa nchini kilicho juu ya BMT yaani baraza la michezo nchini ,hivyo TFF wanatakiwa kufanya mkutano mkuu kwa kutumia katiba ya mwaka 2006 na FIFA wanatakiwa kuelezwa mambo yalivyo pindi watakapokuwa hapa.

Pia waziri amesema anamuondoa kazi msajili aliyepitisha katiba ya TFF kwani hajafuata kanunu na sheria na kumuweka mwingi pamoja na kuhamisha ofisi ya msajili
 

Matokeo ya kidato cha Nne: Wakuu wa shule wadai ilitungwa kwa mfumo tofauti


MATOKEO mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yamezidi kuibua mapya, baada ya wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini kusema mitihani ilitungwa kwa mfumo tofauti na uliozoeleka miaka yote, huku tume iliyounndwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ikipondwa na baadhi ya watu.Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema kwamba maswali waliyoulizwa watahiniwa yalikuwa ya kujieleza tofauti na miaka ya nyuma, ambapo
mfumo uliotumika uliwataka watahiniwa kutaja vitu tu bila ya kulazimika kuvielezea kwa undani.
Kauli yake iliungwa mkono na Mkuu wa Taaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian, Florence Mapunda ambaye alisema kuwa mtihani wa mwaka jana ulitaka zaidi watoto kujieleza tofauti na miaka ya nyuma wakati wanafunzi walipokuwa wanakariri.
Hata hivyo, Msemaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), John Nchimbi alisema mfumo wa mtihani haukubadilika kwa namna yoyote na kuwa upo kama ule wa miaka yote.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo, kwa upande wake alisema madai yanayotolewa hayana msingi, huku akihoji kwa nini yasitoke tangu mitihani ilipokuwa ikifanyika na badala yake yanatoka baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Kutokana na matokeo hayo, Waziri Mkuu Pinda, juzi alitangaza kuunda tume ya kuchunguza chanzo cha matokeo hayo kuwa mabaya, hatua ambayo hata hivyo imekosolewa na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Tume hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka Taasisi za Elimu, Chama cha Waalimu, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa) inatarajiwa kuanza kazi wiki hii.
Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kuunda tume ni kupoteza muda kwa sababu matatizo na changamoto zote ndani ya sekta hiyo yanajulikana, huku mwenzake, Profesa Chriss Maina pia wa UDSM akisema kuunda tume hakutaisaidia kwa kuwa Serikali inaidharau sekta ya elimu.
“Tatizo ni kutowekeza kikamilifu katika sekta ya elimu, imekuwa na matumizi makubwa katika mambo yasiyokuwa ya lazima,”alisema Profesa Mpangala.
Alisema matatizo mengine ni mazingira magumu ya kufundisha na uhaba wa walimu. “Kinachotakiwa wajipange kufanyia kazi changamoto hizi zilizopo badala ya kuunda tume, wakati fedha nyingi tunasikia inapotea kwenye ubadhirifu,”alisema Profesa Mpangala.
Naye Profesa Maina alisema: “Hiyo tume ya kazi gani kwa sababu matatizo yanafahamika wazi, umewahi kusikia taifa gani ambalo halina mtalaa wa elimu. Hiyo ndiyo hali halisi kwa nchi yetu. ”

jk atua uganda kumzika baba yake rais museveni

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake
 Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya  Februari 24, 2013.Picha na IKULU

Man United yaelekea kushinda ligi kuu

Man United yaelekea kushinda ligi kuu

Ryan Giggs
Ligi kuu ya soka nchini England, imeendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbali mbali.
Huko Loftous Road, Manchester United imeebuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya QPR, huku mshambuliaji Ryan Giggs akifunga bao la pili na kufikisha mabao 999 toka aanze kucheza soka la ushindani na kuifanya timu yake ya Manchester United, kuongeza tofauti ya point 15 na mabingwa watetezi Manchester City.
United ilipata bao lake la mapema kupitia kwa Rafael Da Silva ambaye alifunga kwa shuti kali dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinda mlango wa QPR,Julio Cesar kuokoa kiki la Robin Van Persie.
Rafael ambaye mdogo wake,Fabio yupo QPR kwa mkopo,hii leo alionekana kuwa kwenye kiwango kizuri na kuokoa hatari kadhaa langoni mwa United hasa baada ya kuokoa mpira wa kichwa wa Criss Samba ambao ulikuwa uingie nyavuni.
Licha ya Dan Welbeck na Wayne Rooney kuingia wakitokea benchi,hii leo hawakuweza kupata bao katika ushindi huo ambao unawabakisha United kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka nchini England.
Matokeo haya,yanaendelea kuwabakisha QPR kwenye nafasi ya mwisho ya msimamo wa ligi hiyo yenye upinzani mkubwa duniani.

Man City yailemea Chelsea

Wachezaji wa Manchester City
Mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City wameandikisha ushindi mkubwa dhidi ya mabingwa wa ulaya Chelsea na hivyo kufufua matumaini yao ya kuhifadhi kombe hilo kwa mwaka wa pili, licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka wa vinara wa ligi hiyo kwa sasa Manchester United.
Mechi hiyo iliyokuwa na mashambulizi na kila aina ya vivutio baina ya timu hizo zinazomilikiwa na matajiri wawili tofauti,imemalizika kwa ushindi wa Man City wa mabao mawili kwa bila.
Mabao ya kipindi cha pili ya Yaya Toure na Carlos Tevez yalitosha kuizamisha Chelsea, na kufufua matumaini ya Man City, kutetea taji lao ambalo sasa linaonekana kuwa mikononi mwa majirani zao Manchster United wanaoongoza ligi wakiwa na tofauti ya point 12.
Mapema kipindi cha pili, Chelsea, walipata penat baada ya Demba BA, kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Man City, Joe Hart, lakini penat iliyopigwa na nahodha wa Chelsea, Frank Lampard, ilipanguliwa Joe Hart na kuamsha mashambulizi zaidi ya Manchester City.
Yaya Toure kunako dakika ya 63 alipenyeza shuti la wastani pembeni mwa lango la Chelsea na kuwafanya Manchester City, kuongoza kwa bao moja kabla Chelsea, kufanya juhudi za kutaka kusawazisha lakini wakajikuta wanoangezwa bao la pili maraidadi kabisa lililofungwa na Carlos Tevez ambaye aliingia akitokea benchi,huku likiwa bao lake la kwanza baada ya mechi sita alizocheza bila kuifungia timu yake.
Kwingineko,katika mchezo mwingine wa leo, Newcastle wakiwa nyumbani,walitoka nyuma baada ya kufungwa bao la mapema na kuchomoza na ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Southampton.
Mabao wa Newcastle yamefungwa na Musa Sisoko,Papis Demba Cisse,Yohan Cabaye aliyefungwa kwa mkwaju wa penati huku bao la nne watakatifu au Southampton wakijifunga.
Mabao ya Southampton yalifungwa na Morgan Scheneiderlin dakika tatu tu baada ya mchezo kuanza huku bao la pili likifungwa na Rickie Lamber