This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, February 28, 2013

MTOTO WA MWENYEKITI WA KIJIJI TANANGOZI IRINGA AJINYONGA KATIKA OFISI YA KIJIJI

 

Katika hali ya kusikitisha  mtoto wa  mwenyekiti wa serikali ya  kijiji cha Tanangozi katika wilaya ya  Iringa vijijini  Doto Kikoti ameamua kujinyonga katika ofisi ya kijiji  hicho inayoongozwa na babake mzazi kama njia ya kupinga kuwekwa kizuizini katika ofisi hiyo.

Tukio hilo  limetokea  usiku  wa kuamkia leo  baada ya kijana  huyo kutuhumiwa  kufanya  vurugu kubwa  katika kijiji  hicho na mzazi  wake  kuamua kumkamata na kumfungia katika  ofisi hiyo ya  kijiji kwa usalama  wake.

Wakizungumza na mtandao huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com mashuhuda wa  tukio  hilo  wamesema kuwa kijana  huyo alijinyonga kwa kutumia suluali  yake  akiwa ndani ya ofisi  hiyo baada ya mwenyekiti  wa kijiji  hicho ambae ni babake mzazi  Bw Narbeti Kikoti kumfungia katika ofisi hiyo.

Mwili  wa  kijana huyo umetolewa eneo la  ofisi hiyo majira ya saa 5 asubuhi  leo na kupelekwa nyumbani kwa  wazazi kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

HEADLINES ZA HABARI ZA MICHEZO DUNIANI.

RAFAEL BENITEZ VS JOHN TERRY

 Nahodha wa Chelsea John Terry na kocha wa muda wa club hiyo Rafael Benitez wameripotiwa kuwa kwenye mzozo mkubwa kufuatia ugomvi ulioibuka kwenye kiwanja cha mazoezi cha club hiyo Cobham London.Wawili hao walionekana kugombana baada ya Benitez kuitisha mkutano mdogo kabla ya mazoezi ya asubuhi ambao alizungumzia mechi yao ya jumapili waliyochapwa 2-0 na Man City.


LUIS NANI – Mchezaji winga wa Manchester United Luis Nani amepewa nafasi ya mwisho kusaini mkataba mpya na club yake wa mshahara wa pound elfu 90 ama ajiandae kuuzwa. 

DAVID VILLA - Mshambuliaji wa Hispania na club ya Barcelona David Villa ambae amekuwa kwenye orodha ya wanaowaniwa na club ya Arsenal, ameambiwa na club yake kwamba hatolazimishwa kubakia Barca endapo hatokua tayari kuendelea kubaki kwenye club hiyo.
Viongozi wa Barca wamesema wangependa kuona mchezaji huyo anabakia kwenye club yao lakini hawamlazimishi kufanya hivyo endapo atakua na malengo ya kuhamia kwengine.

MESSI NA FABREGAS: – Kiungo wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas ambae sasa yuko Barcelona amesema mshambuliaji wa timu hiyo Lionel Messi bado ana uwezo mkubwa wa kuibeba club yake.
Fabregas amemtetea Messi ikiwa ni kauli ya kumjibu kiungo wa Madrid Jose Callejon ambae anasema alimshuhudia Messi akimdhihaki kwa maneno machafu kocha msaidizi wa Real Madrid Aitor Karanka.
 

Wednesday, February 27, 2013

KOCHA WA AZAM FC APIGWA ADHABU

Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall (pichani) amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

  Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.
Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.
Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.
Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.
Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.
Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.
Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.
Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.
Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.
Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.
Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

WAFANYA BIASHARA WAVUNA MAHELA VODACOM


 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingw(kulia) akiongea na Mshindi kwenye simu ya mezani wakati wa Droo  ya  kuwapata washindi wa shilingi Milioni 5 na Milioni moja  katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.wanaoshuhudia kushoto kulia ni Matina Nkurlu Meneja Uhusiano,Benjamin Michael Maneja wa Huduma za Ziada na Afisa Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Salehe,Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.



  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu (kulia)akionesha moja ya namba ya simu ya mshindi wa Promosheni ya"MAHELA"aliejishindia kitita cha shilingi Milioni 5 ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 kila mmoja katika promosheni hiyo inayoendelea kuchezeshwa na Vodacom Tanzania,katikati ni Maneja wa Huduma za ziada wa Vodacom Bw.Benjamin Michael,anaefatia ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bi.Chiku Salehe. Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.

msd yawalipua wanaolinda wabadhirifu

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi.
Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la
kujadili tafiti z\ilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha
zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri

BODI YA UTALII YASAINI MKATABA NA WAANDAAJI WA ONESHO LA UTALII LA INDABA AFRIKA KUSINI, KUANZISHA ONESHO LA SWAHILI TOURISM FAIR NCHINI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga katikati wa tatu kutoka kulia, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki kushoto na Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd wakisaini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha onesha la Utalii litakalojulikana kwa jina la Swahili Tourism Fair kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika nchini Tanzania kwenye ukumbi huohuo wa Mlimani City Dar es salaam kuanzia Oktoba 2-5 mwaka huu, Wanaoshuhudia tendo hilo la kusainiwa kwa mkataba huo nyuma ni Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na kulia ni Ian Kaduma Mwanasheria wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Kampuni ya Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd Pia ndiyo inayoandaa maonyesho makubwa ya utalii nchini Afrika Kusini yanayojulikana kama Indaba 
 Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd akisaini mkataba huo huku Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akishuhudia tukio hilo kushoto ni Ian Kaduma Mwanasheria wa TTB

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea leo February 27, 2013.

Monday, February 25, 2013

MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR

Maalim Seif apinga mauaji ya Padri asema si ya kigaidi

 

 

 

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amepinga kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi kuwa mauaji ya viongozi wa dini Zanzibar ni ugaidi na kusema kuwa wanaofanya hivyo ni watu wenye nia ya kuvunja umoja wa Wazanzibari.
Baada ya mauaji ya Padre Evarist Mushi, akizungumza na wandishi wa habari,Nchimbi alielezea kusikitishwa na mauaji hayo akisema kuwa ni ya kigaidi na yana lengo la kuingiza nchi katika machafuko. Amesema kuwa tukio hilo si tukio la ujambazi bali tukio la kigaidi kwani limelenga zaidi katika kuwashambulia viongozi kidini.


Padre Evaristus Mushi aliuawa Februari 17, mwaka huu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliokuwa katika pikipiki aina ya Vespa wakati akienda kuongoza misa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Beit el Rass.

“Watu hawa wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini ili kuvunja umoja wa Wazanzibari, lakini nasema hakuna ugaidi Zanzibar,” alisema Maalim Seif juzi usiku alipohutubia kwenye hafla ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) mjini Kiuyu, Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba.

Alisema hivi sasa Wazanzibari ni wamoja na watu hao wenye nia mbaya wanayachukulia matukio hayo kwa kutaka kuwagawa na kuwaletea mtafaruku kwa kuonyesha kuwa kuna tofauti za kidini Zanzibar wakati siyo kweli.

Alisema inasikitisha kuona wapo baadhi ya viongozi wenye nia chafu dhidi ya Zanzibar wenye tabia ya kutoa kauli za kujenga chuki na fitina miongoni mwa Wazanzibari chini ya kivuli cha matukio hayo.

Makamu huyo wa Kwanza wa Rais alisema, kinachoonekana kuna ajenda imetayarishwa ya kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, licha ya kuwapo kwa historia ya miaka mingi ya watu kuvumiliana na kuishi kwa pamoja na kuwapo watu wa imani tafauti.

Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar hivi sasa kuwa macho na ajenda zinazolengwa kuwavuruga na waendelee kuishi kwa mshikamano na umoja kama ambavyo wamekuwa wakiishi.

Maalim Seif alisema vitendo vya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini Zanzibar ni mambo mageni na kwa miaka mingi Zanzibar imekuwa ni mfano bora wa uvumilivu wa kiitikadi za kidini, licha ya kuwa asilimia 98 ya wananchi wake ni Waislamu.

Alisema Katiba ya Zanzibar imeweka wazi haki ya mtu kuabudu kwa mujibu wa imani yake na uhuru wa mtu kuabudu umelindwa.

“Ni Sultani wa Zanzibar ambaye alikuwa Muislamu ndiye aliyetoa ardhi kwa Wakiristo kujenga Kanisa. Juzi nilipokwenda kutoa salamu za rambirambi kwa Baba Askofu Shayo, baada ya kifo cha Padri Mushi, aliweka bayana kuwa lililotokea lisihusishwe na tofauti za kidini,” alisema Maalim Seif.

Hata hivyo, Maalim Seif alisema inasikitisha kuona wakati Rais Jakaya Kikwete katoa maelekezo uchunguzi wa kina ufanyike na Kamishna wa Polisi Zanzibar ameshaweka wazi kuwa uchunguzi unaendelea, baadhi ya viongozi na vyombo vya habari vinachochea chuki za kidini na kusema kuwa Zanzibar kuna ugaidi.

Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar kwa wakati huu kuwa watulivu na wasitawaliwe na jazba na wala wasichokozane, pia wasikubali kuchokozeka.


Akizungumzia matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotolewa hivi karibuni, Makamu wa wa Kwanza wa Rais alisema ni matokeo mabaya na ya kuliza, kwa sababu hayaonyeshi mustakabali mwema kwa watoto wetu na nchi yetu hapo baadaye.


Alisema ni wakati mwafaka Serikali, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, walimu na jamii nzima kujiuliza nini sababu ya matokeo hayo mabaya, na kujiuliza pia nchi inaelekea wapi?

Maalim Seif alisema sasa si wakati tena wa kutupiana lawama, lazima pande zote zikae zijadili wapi pamekosewa, ili ufumbuzi uweze kupatikana na hali kama hiyo isitokee tena siku nyingine.

 

NI WAREMBO MISS UTALII

HAPA NI WAREMBO TU .... LAKELAND AFRICA WADHAMINI UTALII WA NDANI , MISS UTALII TANZANIA 2012/13

 

 

Washiriki wa Miss Utalii tanzania wakiwa katika moja ya Makaburi ya zamani Kaole Bagamoyo.
Mshiriki wa Miss Utalii Tanzania Pamoja na washiriki wengine wakikata utepe kwa ajili ya uzinduzi wa safari ya Kitalii Bagamoyo.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa katika moja ya Kaburi maarufu la Wapendanao.

MIWA YA MTIBWA YAMLEWESHA SIMBA



 Timu ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo jioni katika Uwanja wa Taifa.

Bao la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja.

Bao hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezua mtafaruku mkubwa baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba, walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharula.

Aidha mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha maji ya kuwasha, huku viongozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika uwanjani hapo. 

Hata hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha pili.

 Beki wa Simba, ambaye leo amechezeshwa kama kiungo wa chini, Shaban Kapombe, akimchezea vibaya Rashid Gumbo.

 Beki wa Simba Keita, akimdhibiti mchezaji wa Mtibwa.
Mshambuliaji wa Mtibwa, akiwasakata mabeki wa Simba.



ANGETILE :TUTAKAA KUJADIRI NINI TUFANYE KUZINGATIA FIFA INATAKA NINI ?

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/AngetilewaTFF(2).jpg
Katibu mkuu wa tff angetile osiah amaesema tff itakutana ili kujadiri maamuzi ya serikali kuifuta kwani wao wanaendesha mpira kikatiba kwani wao wanaongoza mpira unaongozwa na fifa, caf ,cecafa,  na sio serikali na katiba tff inasema kuwa inatakiwa kufuata maagizo ya kutoka  fifa amesema wao watakaa chini na kulitazama na nini wataamua  .



NANI ATAKUWA SAHIHI FIFA,TFF,BMT,AU SERIKALI ,NI BAADA SERIKALI KUFUITA KATIBA MPYA YA TFF

 
WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO FENELLA MUKANGARA.

Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Fenella Mukangara amefuta matumizi ya katiba mpya ya TFF ya mwaka 2012 kwa vile imekiuka kanuni na sheria za BMT hivyo TFF wanatakiwa kutukia katiba ya mwaka 2006 ambayo imetumika katika mikoa kufanyia uchaguzi.

Mukangara amesema TFF inatakiwa kufuata kanuni nasheria za BMT ambazo ambazo ndizo zenye maelekezo ya kufanya marekebisho ya katiba .

Hakuna chama chochote hapa nchini kilicho juu ya BMT yaani baraza la michezo nchini ,hivyo TFF wanatakiwa kufanya mkutano mkuu kwa kutumia katiba ya mwaka 2006 na FIFA wanatakiwa kuelezwa mambo yalivyo pindi watakapokuwa hapa.

Pia waziri amesema anamuondoa kazi msajili aliyepitisha katiba ya TFF kwani hajafuata kanunu na sheria na kumuweka mwingi pamoja na kuhamisha ofisi ya msajili
 

Matokeo ya kidato cha Nne: Wakuu wa shule wadai ilitungwa kwa mfumo tofauti


MATOKEO mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yamezidi kuibua mapya, baada ya wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini kusema mitihani ilitungwa kwa mfumo tofauti na uliozoeleka miaka yote, huku tume iliyounndwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ikipondwa na baadhi ya watu.Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema kwamba maswali waliyoulizwa watahiniwa yalikuwa ya kujieleza tofauti na miaka ya nyuma, ambapo
mfumo uliotumika uliwataka watahiniwa kutaja vitu tu bila ya kulazimika kuvielezea kwa undani.
Kauli yake iliungwa mkono na Mkuu wa Taaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian, Florence Mapunda ambaye alisema kuwa mtihani wa mwaka jana ulitaka zaidi watoto kujieleza tofauti na miaka ya nyuma wakati wanafunzi walipokuwa wanakariri.
Hata hivyo, Msemaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), John Nchimbi alisema mfumo wa mtihani haukubadilika kwa namna yoyote na kuwa upo kama ule wa miaka yote.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo, kwa upande wake alisema madai yanayotolewa hayana msingi, huku akihoji kwa nini yasitoke tangu mitihani ilipokuwa ikifanyika na badala yake yanatoka baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Kutokana na matokeo hayo, Waziri Mkuu Pinda, juzi alitangaza kuunda tume ya kuchunguza chanzo cha matokeo hayo kuwa mabaya, hatua ambayo hata hivyo imekosolewa na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Tume hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka Taasisi za Elimu, Chama cha Waalimu, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa) inatarajiwa kuanza kazi wiki hii.
Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kuunda tume ni kupoteza muda kwa sababu matatizo na changamoto zote ndani ya sekta hiyo yanajulikana, huku mwenzake, Profesa Chriss Maina pia wa UDSM akisema kuunda tume hakutaisaidia kwa kuwa Serikali inaidharau sekta ya elimu.
“Tatizo ni kutowekeza kikamilifu katika sekta ya elimu, imekuwa na matumizi makubwa katika mambo yasiyokuwa ya lazima,”alisema Profesa Mpangala.
Alisema matatizo mengine ni mazingira magumu ya kufundisha na uhaba wa walimu. “Kinachotakiwa wajipange kufanyia kazi changamoto hizi zilizopo badala ya kuunda tume, wakati fedha nyingi tunasikia inapotea kwenye ubadhirifu,”alisema Profesa Mpangala.
Naye Profesa Maina alisema: “Hiyo tume ya kazi gani kwa sababu matatizo yanafahamika wazi, umewahi kusikia taifa gani ambalo halina mtalaa wa elimu. Hiyo ndiyo hali halisi kwa nchi yetu. ”

jk atua uganda kumzika baba yake rais museveni

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake
 Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya  Februari 24, 2013.Picha na IKULU

Man United yaelekea kushinda ligi kuu

Man United yaelekea kushinda ligi kuu

Ryan Giggs
Ligi kuu ya soka nchini England, imeendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbali mbali.
Huko Loftous Road, Manchester United imeebuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya QPR, huku mshambuliaji Ryan Giggs akifunga bao la pili na kufikisha mabao 999 toka aanze kucheza soka la ushindani na kuifanya timu yake ya Manchester United, kuongeza tofauti ya point 15 na mabingwa watetezi Manchester City.
United ilipata bao lake la mapema kupitia kwa Rafael Da Silva ambaye alifunga kwa shuti kali dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinda mlango wa QPR,Julio Cesar kuokoa kiki la Robin Van Persie.
Rafael ambaye mdogo wake,Fabio yupo QPR kwa mkopo,hii leo alionekana kuwa kwenye kiwango kizuri na kuokoa hatari kadhaa langoni mwa United hasa baada ya kuokoa mpira wa kichwa wa Criss Samba ambao ulikuwa uingie nyavuni.
Licha ya Dan Welbeck na Wayne Rooney kuingia wakitokea benchi,hii leo hawakuweza kupata bao katika ushindi huo ambao unawabakisha United kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka nchini England.
Matokeo haya,yanaendelea kuwabakisha QPR kwenye nafasi ya mwisho ya msimamo wa ligi hiyo yenye upinzani mkubwa duniani.

Man City yailemea Chelsea

Wachezaji wa Manchester City
Mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City wameandikisha ushindi mkubwa dhidi ya mabingwa wa ulaya Chelsea na hivyo kufufua matumaini yao ya kuhifadhi kombe hilo kwa mwaka wa pili, licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka wa vinara wa ligi hiyo kwa sasa Manchester United.
Mechi hiyo iliyokuwa na mashambulizi na kila aina ya vivutio baina ya timu hizo zinazomilikiwa na matajiri wawili tofauti,imemalizika kwa ushindi wa Man City wa mabao mawili kwa bila.
Mabao ya kipindi cha pili ya Yaya Toure na Carlos Tevez yalitosha kuizamisha Chelsea, na kufufua matumaini ya Man City, kutetea taji lao ambalo sasa linaonekana kuwa mikononi mwa majirani zao Manchster United wanaoongoza ligi wakiwa na tofauti ya point 12.
Mapema kipindi cha pili, Chelsea, walipata penat baada ya Demba BA, kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Man City, Joe Hart, lakini penat iliyopigwa na nahodha wa Chelsea, Frank Lampard, ilipanguliwa Joe Hart na kuamsha mashambulizi zaidi ya Manchester City.
Yaya Toure kunako dakika ya 63 alipenyeza shuti la wastani pembeni mwa lango la Chelsea na kuwafanya Manchester City, kuongoza kwa bao moja kabla Chelsea, kufanya juhudi za kutaka kusawazisha lakini wakajikuta wanoangezwa bao la pili maraidadi kabisa lililofungwa na Carlos Tevez ambaye aliingia akitokea benchi,huku likiwa bao lake la kwanza baada ya mechi sita alizocheza bila kuifungia timu yake.
Kwingineko,katika mchezo mwingine wa leo, Newcastle wakiwa nyumbani,walitoka nyuma baada ya kufungwa bao la mapema na kuchomoza na ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Southampton.
Mabao wa Newcastle yamefungwa na Musa Sisoko,Papis Demba Cisse,Yohan Cabaye aliyefungwa kwa mkwaju wa penati huku bao la nne watakatifu au Southampton wakijifunga.
Mabao ya Southampton yalifungwa na Morgan Scheneiderlin dakika tatu tu baada ya mchezo kuanza huku bao la pili likifungwa na Rickie Lamber

Saturday, February 23, 2013

FIFA WAJA KUFATILIA SOKA

OFISA Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi amewasili leo kwa ajili ya kufuatilia shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu.
 Mamelodi, ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa shughuli za maendeleo nchini Tanzania tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, pia amekuja kumtambulisha msaidizi wake, Patrick Onyango aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni.

hali ni tete drc;un


Na Mwandishi Maalum
Hali katika eneo la Mashariki ya Kongo inaelezwa kwamba ni tete na ya hatari kiasi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuibuka mgogoro mkubwa yoyote.Onyo hilo limetolewa siku ya Ijumaa na Bw. Roger Meece ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa Bw. Roger Meece amelitoa toa onyo hilo, wakati Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki Moon pamoja na baadhi ya viongozi wa Afrika wanatarajiwa Februari 24 jumapili hii, kusaini Jijini Addis Abba Ethiopia, Mpango Mpya wa Amani, Usalama na Ushirikiano nchini DRC.
“Kwa ujumla hali ni tete mkubwa bila ya onyo”. Akaliambia Baraza Kuu na kuongeza . “ Ninatoa wito kwa Baraza hili kutoa kila aina ya msaada na ushirikiano ili Brigedi mpya itakayoogeza  nguvu iweze kupelekwa DRC mapema iwezekanavyo”. Akielezea zaidi kuhusu hali hatari ilivyo nchini humo.
Mkuu huyo wa MONUSCO anasema imefikia katika ukomo wa kutisha. Yakiwamo pia matatizo ya kibinadamu ambapo inakadiriwa zaidi ya watu 316,000 wameyakimbia makazi yao. Vile vile akaongeza kuwa kuzorota kwa hali ya usalama katika jimbo hilo kunachangiwa na kuongezeka kwa shughuli za kundi la wake anayefahamika kama Gedeon, kutoroka anajihusisha na makundi mengine ya wanamgambo likiwamo la Katangais Kata. Akizungumzia kundi la M23 ambalo mwaka jana liliteka Goma ambayo ni mji mkuu wa Jimbo la Kivu kwamba, ingawa kundi hilo linaonyesha kutulia lakini hakuna ushahidi kuwa limerudisha nyuma vikosi vyake au kubadili mkao wa kijeshi.
Bw. Rogers Meece ambaye pia ni Mkuu wa
 uwa, mapigano kati ya wapiganaji wa M23 na Jeshi la Kitaifa la DRC ( FARDC) yamesabisha karibu watu milioni kuyakimbia makazi yao katika eno la Kivu Kaskazini. bila na ya hatari wakati wowote kunaweza kuzuka mgogoro hali katika eneo la Kusini- Mashariki ya Jimbo la Katanga Mayi -Mayi hasa baada ya kiongozi gerezani mwaka 2011 na kwamba MONUSCO, amelieleza Baraza Kuu Amefafanua zaidi kwa kusema ,
likabailiwa na matatizo makubwa ya rasmali vikiwemo vifaa.Kwa sababu hiyo akasema uamuzi wa
zisizoendeshwa na rubani ( unmanned Aerial System) utasaidia sana katika ukusanyaji
wa taaarifa kwa ajili ya matumizi ya UN,
makosa yasitendeke.
Akasema yeye binafsi
kwamba teknolojia hiyo inatakiwa kupelekwa haraka iwezekanavyo.
Bw. Rogers Meece pia amezungumzia uwezekano wa kuongeza nguvu za kijeshi au
Brigedi pamoja na kuongeza mamlaka zaidi zaidi ya utekelezaji na wajibu
amani nje ya utaratribu wa jadi wa kulinda amani wa UN.
Akasema, ni imani yake kwamba uongezaji wa nguvu ya ziada ardhini ni muhimu sana
ili kufikia malengo yanayokusudiwa na amelitaka Baraza Kuu la Usalama kuidhinisha
matumizi ya nguvu.
Jeshi la kutuliza amani lililoko hivi sasa katika DRC
kutumia
teknolojia ya kisasa ya ndege
kuiongezea uwezo MONUSCO na kuzuia
analishukuru
Baraza hilo kwa kuridhia pendekezo hilo na
wa kulinda

ZACO TECHNOLOGY

inatoa offer kwa wateja wake ambao wanataka kufanyiwa kazi za editing  kama vile matangazo ya mabango website movie  photo graphics kua wanatoa offer bomba kabisa kwa wateja wao
tunapunguzo kubwa sana kwa yoyote yule atakaefanya kazi nasi zaidi ya moja

SMART BOY

 zaidi fika mataa Karibu Smart Boy kwa mahitaji yako yote ya nguo za kisasa na zakijanja unakaribishwa kwa mawasilianowa uhuru karibu na daraja la wamasai kuna suti za kila aina mashart vibody vya kina dada watoto wadogo pia tuna punguzo la aslimia 90% kwa yule atakae nunua nguo zaidi ya moja