This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, February 28, 2013

MTOTO WA MWENYEKITI WA KIJIJI TANANGOZI IRINGA AJINYONGA KATIKA OFISI YA KIJIJI

Katika hali ya kusikitisha  mtoto wa  mwenyekiti wa serikali ya  kijiji cha Tanangozi katika wilaya ya  Iringa vijijini  Doto Kikoti ameamua kujinyonga katika ofisi ya kijiji  hicho inayoongozwa na babake mzazi kama njia ya kupinga kuwekwa kizuizini katika ofisi hiyo.

Tukio hilo  limetokea  usiku  wa kuamkia leo  baada ya kijana  huyo kutuhumiwa  kufanya  vurugu kubwa  katika kijiji  hicho na mzazi  wake  kuamua kumkamata na kumfungia katika  ofisi hiyo ya  kijiji kwa usalama  wake.

Wakizungumza na mtandao huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com mashuhuda wa  tukio  hilo  wamesema kuwa kijana  huyo alijinyonga kwa kutumia suluali  yake  akiwa ndani ya ofisi  hiyo baada ya mwenyekiti  wa kijiji  hicho ambae ni babake mzazi  Bw Narbeti Kikoti kumfungia katika ofisi hiyo.

Mwili  wa  kijana huyo umetolewa eneo la  ofisi hiyo majira ya saa 5 asubuhi  leo na kupelekwa nyumbani kwa  wazazi kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

HEADLINES ZA HABARI ZA MICHEZO DUNIANI.

RAFAEL BENITEZ VS JOHN TERRY

 Nahodha wa Chelsea John Terry na kocha wa muda wa club hiyo Rafael Benitez wameripotiwa kuwa kwenye mzozo mkubwa kufuatia ugomvi ulioibuka kwenye kiwanja cha mazoezi cha club hiyo Cobham London.Wawili hao walionekana kugombana baada ya Benitez kuitisha mkutano mdogo kabla ya mazoezi ya asubuhi ambao alizungumzia mechi yao ya jumapili waliyochapwa 2-0 na Man City.

LUIS NANI – Mchezaji winga wa Manchester United Luis Nani amepewa nafasi ya mwisho kusaini mkataba mpya na club yake wa mshahara wa pound elfu 90 ama ajiandae kuuzwa. 

DAVID VILLA - Mshambuliaji wa Hispania na club ya Barcelona David Villa ambae amekuwa kwenye orodha ya wanaowaniwa na club ya Arsenal, ameambiwa na club yake kwamba hatolazimishwa kubakia Barca endapo hatokua tayari kuendelea kubaki kwenye club hiyo.
Viongozi wa Barca wamesema wangependa kuona mchezaji huyo anabakia kwenye club yao lakini hawamlazimishi kufanya hivyo endapo atakua na malengo ya kuhamia kwengine.

MESSI NA FABREGAS: – Kiungo wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas ambae sasa yuko Barcelona amesema mshambuliaji wa timu hiyo Lionel Messi bado ana uwezo mkubwa wa kuibeba club yake.
Fabregas amemtetea Messi ikiwa ni kauli ya kumjibu kiungo wa Madrid Jose Callejon ambae anasema alimshuhudia Messi akimdhihaki kwa maneno machafu kocha msaidizi wa Real Madrid Aitor Karanka.