This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, June 1, 2013

REDD'S MISS TABATA 2013 APATIKANA

Miss Tabata Dolizi Moleo (Katikati) Upendo Lemana mshindi wa tatu Rechoul Musa.

Mwenyekiti wa kamati ya  Miss Tanzania Prashent Pater (Kushoto) akiongea na Hoice Temu ambae alishawahi kuwa Miss Tanzania.…
 Miss Tabata Dolizi Moleo (Katikati) Upendo Lemana mshindi wa tatu Rechoul Musa.
 Mwenyekiti wa kamati ya  Miss Tanzania Prashent Pater (Kushoto) akiongea na Hoice Temu ambae alishawahi kuwa Miss Tanzania.
Wanamuziki  twanga pepeta Dogo Rama  (Kushoto) na  Ruiza Mbutu wakiimba.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kushuudia kinyanganyiro hicho.
Mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albart Makoe akiwatambulisha wageni wenzake.
Baadhi ya washiriki wakipita na vazi la ufukweni..
Washiriki wote wakiwa katika picha ya pamoja.
Washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora wakipozi ili kupigwa picha.
Majaji wakiwa katika kazi kubwa ya kumpata mshindi.
Jana usiku katika ukumbi wa Da’ west  uliopo Tabata jijini Dar es salaam kinyanganyilo cha kumtafuta Mrembo wa kitongoji hicho kilifanyika na mshiriki Dolizi Moleo aliibuka kidedea kwakuwapiku washiriki wenzake 16 kwa kuwa Redds Miss Tabata 2013,
Katika kunogesha burudani Bendi ya muziki wa dansi ya African Star Twanga Pepeta ilitumbuiza kabla  na baada ya shindano hilo kumalizika.
PICHA:  ISSA MNALLY
 

KIGORI YAZINDULIWA SUNSIRO

Wanenguaji wa kike wa Bendi ya Extra Bongo wakifanya yao jukwaani kusindikiza uzinduzi huo.
 Wanenguaji wa kiume wa Extra Bongo wakionesha mautundu yao.
Msanii mahiri wa ngoma za asili na sanaa za maonesho, One Star…
 Wanenguaji wa kike wa Bendi ya Extra Bongo wakifanya yao jukwaani kusindikiza uzinduzi huo.
Wanenguaji wa kiume wa Extra Bongo wakionesha mautundu yao.
Msanii mahiri wa ngoma za asili na sanaa za maonesho, One Star akionesha utundu wa kucheza na nyoka stejini.
Mmoja kati ya vigori watatu waliojitokeza ukumbini humo akionesha umahiri wa kulisakata sebene.
Majaji wa shindano hilo, John Kitime, Maimatha Jesse na Mussa Husein wakifuatilia shoo ya baadhi ya washiriki (hawapo pichani).
Kigori huyu aligeuka kivutio kikubwa ukumbini humo kwa jinsi ‘alivyochetuka’ na kuonesha manjonjo ya kufa mtu jukwaani.
Mshiriki mwingine wa Kigori 2013 akionesha vitu vyake jukwaani.
SHINDANO la kumtafuta Kigori wa Tanzania 2013 limezinduliwa rasmi jana katika Ukumbi wa SunSiro, Ubungo, jijini Dar ambapo ndani ya ukumbi huo walipatikana warembo watatu ukumbini humo.
Warembo hao wanatarajia kuungana na wenzao ambao wanatarajiwa kufanyiwa usahili hivi karibuni katika mikoa ya Tanga na Morogoro.

BENDI YA AKUDO IMPACT YAFANYA MAKAMUZI KATIKA UKUMBI WA MANGO GARDEN KINONDONI

Kaimu Prezidaa wa Akudo, Tarcis Masela (katikati) akikamua.
Makamuzi yakiendelea.
Mfanyabiashara Pius Ruta ‘Mzee wa Pamba’ (kushoto) na mwanamuziki wa African Stars ‘Twanga Pepeta’ Hamis Amigo ‘Amigoras’ wakiwa kwenye…
Kaimu Prezidaa wa Akudo, Tarcis Masela (katikati) akikamua.
Makamuzi yakiendelea.
Mfanyabiashara Pius Ruta ‘Mzee wa Pamba’ (kushoto) na mwanamuziki wa African Stars ‘Twanga Pepeta’ Hamis Amigo ‘Amigoras’ wakiwa kwenye onesho hilo.
Mzee wa Pamba ‘akimtakasa’ Allain Kabasele ‘Mtoto wa Pepe Kalle’ kwa noti.
Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ usiku wa kuamkia leo imeendeleza makamuzi kwenye Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar na kuendelea kukonga nyoyo za mashabiki wake.
PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL

DIAMOND MUSICA YAFANYA KWELI

Posted by GLOBAL on June 1, 2013 at 3:38pm 1 Comment
Prezidaa wa bendi hiyo, Liver Hassan ‘Sultan’ (katikati) akiongoza kufanya makamuzi.
Mmoja wa wanenguaji wa Diamond Musica akicheza staili ya mutwash ambayo hutumiwa na bendi hiyo.
Bendi ya muziki wa dansi ya Diamond Musica usiku wa kuamkia leo imefanya makamuzi ya nguvu kwenye Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

KIFO CHA MANGWEA NI SUMU!

Stori:Sifael Paul

KIFO cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika, Risasi Jumamosi linafungua kila kitu.
Hospitali aliyopelekwa
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo) alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph ambako mwili wa marehemu…
Stori:Sifael Paul
KIFO cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika, Risasi Jumamosi linafungua kila kitu.
Hospitali aliyopelekwa
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo) alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa kwenye Mochwari ya Hillbrow.
M2 The P akiwa amelazwa Hospitali
Mbongo huyo alisema alifanikiwa kuutazama mwili wa marehemu Ngwea ambapo ulionesha kuwa wakati wa kukata roho damu nyingi zilimtoka kupitia puani na mdomoni kiasi cha kuwashangaza wauguzi.
Mwili wa Marehemu
NI SUMU
Alisema muuguzi mmoja aliyekuwa akimtibu mshirika wa marehemu, Mgaza Pembe a.k.a M2 The P aliyenusurika, alimwambia wawili hao walionekana kuingiwa na kitu cha hatari na kibaya sana mwilini jambo lililowashtua hata madaktari wenyewe.
Mama mzazi wa mangwea akiwa kwenye huzuni
Alisema muuguzi huyo alimweleza kuwa kitu walichokula au kulishwa kiliwadhuru sana ndani ya miili yao na kusababisha mishipa ya damu kwa Mangwea kupasuka hovyo kwa kuwa moyo ulizidiwa na presha ya msukumo wa damu.
Mtanzania huyo alidai kuwa hata kama kweli wawili hao walichanganya vileo kama watu wanavyodai, basi ule mchanganyiko ndiyo uliotengeneza sumu mwilini akisisitiza kuwa hilo halina shaka kwa mujibu wa muuguzi huyo.
Eneo atakalozikwa
“Unajua kuna watu wanapenda kuchanganya pombe kali kwa hiyo kuna wanaodai wawili hao walichanganya ‘unga’, bangi na pombe kali. Mchanganyiko huo tu wenyewe ni sumu tosha mwilini kwa binadamu yeyote yule.
“Wataalam wanajua, ukichanganya pombe kali unapata upungufu wa oksijeni katika damu hivyo unaupa moyo kazi ya ziada ya ‘kupampu’ damu kwa kuwa presha inakuwa kubwa. Kwa hiyo kinachotokea ni kupasuka kwa mishipa mikubwa ya damu, ndiyo maana damu zilitoka puani na kinywani kwa wingi.
“Kwa kuchanganya vileo hivyo unatengeneza sumu ambayo husababisha shambulio kubwa la damu na mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi.
“Sasa usipowahishwa hospitali ili kuchomwa sindano ya limao, kifo kinakuwa njenje.
“Kwa vyovyote walikula au walilishwa sumu, daktari anasema mwili wa Ngwea umeharibika sana kwa ndani.
 “Kile siyo kipigo, hakuna jeraha lolote la kupigwa, ile ni sumu,” kilidai chanzo hicho cha kuaminika.

SAA CHACHE KABLA YA KIFO
Habari za kina kutoka kwa mmoja wa watu waliokuwa nao kabla ya kukutwa na tukio hilo zilieleza kwamba kabla ya kwenda kulala, Ngwea na mwenzake, walikutana na baadhi ya Watanzania waishio Sauzi na kupiga stori kwenye baa moja huku wakitaja majina ya wasanii wa Bongo Fleva waliotangulia mbele ya haki.
Ilidaiwa kuwa kila jina la msanii marehemu lilipotajwa Ngwea alikuwa akitamka ‘OMG’ (Ooh! My God) yaani Ooh! Mungu Wangu, bila kujua kitakachomkuta baadaye.

MADAI MENGINE, MAISHA YA SAUZI
Kuna madai mengine kwamba baadhi ya Wabongo waishio Sauzi huwa wana maisha ya kutegana hasa wakijua Mtanzania mwenzao kaenda kule akiwa na ‘mkwanja’ mrefu.
“Tatizo lingine ni kwamba kama walifanyiziwa na mtu huo uwezekano ni mkubwa sana kwani huku jamaa wakikushtukia tu kuwa una mkwanja, kwanza wanakuwa karibu sana na wewe ‘then’ ukikaa vibaya lazima wakutoe uhai.
“Inawezekana akina Ngwea walifanyiziwa kwa kulishwa sumu kwa sababu walikuwa wameshapiga mkwanja tayari kwa kurejea Bongo,” alisema Mbongo huyo.

MCHUNGAJI ALIKIONA KIFO CHAKE MAPEMA!
Mwezi Machi mwaka huu, kupitia gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa la Machi 22-28, 2013 liliandika ukurasa wa mbele habari yenye kichwa; ‘MASTAA WAWILI KUFA MWAKA HUU’ ambapo mchungaji maarufu jijini Dar alisema mwaka 2013  ameona katika maono yake vifo vya wasanii wawili wa Bongo.
Katika habari hiyo, mchungaji huyo alitahadharisha mapema kuwa wasanii wamrudie Mungu kwani upepo siyo mzuri kwao.
Mchungaji huyo alieleza: “Mwaka huu ulipoanza, Januari 2, Sajuki (Juma Kilowoko) aliaga dunia katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa lakini nimepewa maono na Mungu kwamba wasanii wengine wawili watakufa mwaka huu.
“Katika hayo maono niliona wasanii wenyewe, mmoja wa kike, mwingine wa kiume. Wa kike ni msanii wa filamu, wa kiume anaimba hizi nyimbo za kisasa za Bongo Fleva.
“Huyo wa Bongo Fleva siyo mkongwe sana kama wale waanzilishi wa fani hiyo lakini anajulikana sana na mashabiki wengi. Nyimbo zake zinajulikana pia.
“Huyu wa kike yeye ni mkongwe kidogo, halafu ni mweusi, zamani aliwahi kuwika sana lakini kwa siku za hivi karibuni amepoapoa.”

MANENO YAKE YALIJAA UTABIRI
Watu wa karibu waliokuwa wakichati na Ngwea kupitia mitandao ya kijamii walisema siku za mwisho wa uhai wake, marehemu alipenda kutumia maneno yenye kumtaja Mungu, Yesu au viashiria vingine vinavyofanana  na hivyo.

TURUDI KWENYE TUKIO
Habari zilieleza kuwa baada ya majibu ya kilichomuua Ngwea kujulikana, mwili wa staa huyo utaagwa kesho jijini Dar ambapo msiba upo kwa kaka yake Mbezi Beach na baadaye mwili utasafirishwa kwenda mkoani Morogoro eneo la Kihonda, nyumbani kwao.

NGWEA HAPA, BABA’AKE PALE
Habari kutoka msibani Morogoro zimeeleza kwamba marahemu Ngwea atazikwa jirani kabisa na kaburi alilozikwa marehemu baba yake, mzee Kenneth Mangwea. Huo ni ushauri wa familia yake.

HALI YA M2 THE P
Kwa upande wake, M2 The P, hadi gazeti linakwenda mitamboni alikuwa akiendelea na matibabu huko Sauzi huku hali yake ikisemekana inaendelea kuimarika.
Ngwea alizaliwa Novemba 16, 1982 huko mkoani Mbeya (asili yake ni Mkoa wa Ruvuma) akiwa mtoto wa mwisho katika familia yao. Hajaacha mke wala mtoto.

WANYARWANDA WANASWA LIVE WAKIJIUZA JIJINI DAR


POLISI Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam imeendesha oparesheni maalum ya kuwanasa machangudoa wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo lao na kufanikiwa kuwaweka ‘mtu kati’ makahaba kibao, wakiwemo raia wa Rwanda na Burundi...
Kamatakamata hiyo ilichukua nafasi usiku mnene wa Alhamisi ya Mei 23, mwaka huu kwenye danguro kubwa la makahaba lililopo Kariakoo, jijini Dar ambalo machangu hao hutegea mingo zao kwa ajili ya kuwanasa wateja.

Katika hali iliyowashangaza polisi, midume iliyokutwa na makahaba hao ilitimua mbio ili kujiokoa na mtego huo wa polisi uliodhamiria kusafisha eneo la Kariakoo kwa ukahaba uliopitiliza.
Baadhi ya wanaume wakati wakitimua mbio walisikika wakisema kuwa wakukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola ni wanawake hao kwa vile wanavaa kimitego huku wakijua binadamu anapitiwa na shetani wakati wowote.
“Sisi kosa letu nini? Wakamateni haohao machangudoa, watavaaje kimitego mbele yetu sisi wanaume? Shetani naye atakuwa wapi wakati huo?” alisikika akisema mmoja wa wanaume hao huku akichanganya miguu kupita kawaida.
 
Awali kabla ya zoezi la kuwanasa makahaba hao halijaanza, afande mmoja alipowauliza wanachofanya hapo, kahaba mmoja aliuliza: Una maswali mengi kwani we ni polisi?

Mei 24, mwaka huu, makahaba hao walipandishwa kwenye Mahakama ya Jiji na kusomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka, John Kijumbe mbele ya Hakimu Timoth Lyoni.
Waliosomewa mashitaka ni Natasha Bahati, 30 (Mrundi), Asma Athuman, 23 (Mrundi), Niyonkuru  Evelinde, 29 (Mnyarwanda), Zaimana Hawa, 20 (Mrundi) na Wabongo 35.
 
Wote walikana mashitaka lakini walipelekwa Gereza la Segerea, jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

KIJANA ANUSURIKA KUFA BAADA YA VIBAKA KUMCHOMA MOTO HUKO MKOANI LINDI


Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ismai Mayoba(31) anayefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Manispaa ya Lindi amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto. 

Kwa sasa kijana huyo amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.

Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mtu  mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.


Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndugu Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie Moto huku akijua ni kosa kisheria.

Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo