This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, March 22, 2013

NANI ANASTAHILI KUTWAA TUZO YA 'WOMAN OF THE YEAR' ? TUMA JINA LA MWANAMKE UNAYEDHANI ANAFAA

Mtandao wa Global Publishers umeaandaa tuzo kwa mwanamke bora wa mwaka 'WOMAN OF THE YEAR' katika sehemu zifuatazo: Siasa, Biashara, Jamii, Utawala na Haki za Binadamu. Ili kushiriki, tuma jina la mwanamke unayeona anafaa kutwaa tuzo hii katika sehemu ya maoni.

 
NANI MFALME WA TEMEKE, TMK HALISI AU TMK FAMILY?




SHILOLE, BABY MADAHA WAFUATA NYAYO ZA WEMA

 

Na Gladness Mallya

WAREMBO wawili wanaotesa katika soko la muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wameamua kufuata nyayo za Wema Sepetu kwa kunyoa nywele na kuonekana katika muonekano mpya.
Wema.
Akizungumza na paparazi wetu, Shilole ambaye amenyoa nywele staili ya kiduku alisema ameamua kufanya bhiv yo ili kuwa na muonekano wa tofauti kwani watu wameshamzoea kila siku kumuona na mawigi na rasta.…
Kwa upande wa Baby Madaha alisema ameamua kubadilisha mfumo wa maisha kuanzia nywele hadi mavazi kwani huu ni mwaka mpya hivyo kutoka na staili mpya.
Hivi karibuni Wema alikuwa wa kwanza kutangaza kuwa na muonekano tofauti kwa kutupia picha zake mtandaoni zilizomuonesha akiwa amenyoa.
Madaha.

UKATILI 100%

Na Patrick Mabula, Kahama

HUU ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni na mume wake, Amani lina habari ya kusikitisha.
Marehemu Martha Charles (22) baada ya kuchinjwa shingoni na mume wake, Isack Nzwalile. (29).
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki…
Na Patrick Mabula, Kahama
HUU ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni na mume wake, Amani lina habari ya kusikitisha.
Marehemu Martha Charles (22) baada ya kuchinjwa shingoni na mume wake, Isack Nzwalile. (29).
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita ambapo pia alimtaja mume anayedaiwa kutekeleza unyama huo kuwa ni Isack Nzwalile (29), mfanyabiashara wa bucha la nyama ya ng’ombe.
Isack Nzwalile aliyemchinja mkewe, Martha Charles.
Afande Lyanga alisema mtuhumiwa alimchinja  mkewe wakiwa wamelala chumbani kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume huyo na baada ya kufanya ukatili huo alikimbia.
Jessica Elialinga (19) baada ya kuchinjwa na mpenzi wake, Musa Petro (27).
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika familia ya marehemu zilisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia ambapo mtuhumiwa alianza kwa kumlaumu mama yake mzazi kwa kitendo cha kumtafutia kazi mkewe katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati yeye alikuwa hataki mkewe afanye kazi.
Musa Petro aliyemchinja mpenzi wake Jessica Elialinga.
Habari zilizopatikana eneo la tukio kutoka kwa mmoja wa ndugu anayeishi na familia hiyo, Paul Edward alisema mbali na kuchinjwa shingoni pia marehemu alikatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Marehemu Martha Charles (kulia) enzi za uhai wake akiwa na rafiki yake.
Edward alisema usiku wa tukio akiwa amelala katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo, alisikia kelele za ugomvi kutoka kwenye chumba cha wanandoa hao hali iliyomfanya apige kelele zilizowafikia majirani ambao walifika kutoa msaada.
Akasema majirani hao sanjari na yeye walimkuta mtuhumiwa ameshamchinja mkewe kwa kisu na kutoweka kusikojulikana.
Marehemu Martha Charles akiwa na mumewe, Isack Nzwalile wakifurahia maisha enzi za uhai wake.
Nao majirani waliokwenda kutoa msaada ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema walikuta mwili wa Martha ukiwa kitandani huku amekatwa na kitu chenye ncha kali katika eneo lote la shingo, ndipo walipomchukua na kumkimbiza hospitali lakini tayari alikuwa ameshakata roho.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Noel Mkisi alisema baada ya muuaji huyo kutoroka usiku huohuo jitihada za kumsaka zilianza.
Tukio la kuchinjwa kinyama kwa mwanamke huyo limetokea siku chache baada ya hivi karibuni, mchuna ng’ombe Musa Petro (27) naye kumuua kwa kumchinja kwa kisu mpenzi wake, Jessica Elialinga (19).
Jessica Elialinga enzi za uhai wake.
Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Maduka ya Nyama Kahama, Faraji Mohamed akiongea na gazeti hili alisema Petro ni mfanyakazi wa Nzwalile katika duka lake la nyama (bucha) ambapo alishangaa kusikia Nzwalile amemchinja mke wake kama alivyofanya mfanyakazi wake, Petro.
Wakati tunakwenda mitamboni habari zilizopatikana kutoka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kahama na kudhibitishwa na OCD George Simba zilisema mtuhumiwa huyo amekamatwa.
SOMA HABARI INAYOELEKEZEA MAREHEMU JESSICA ALIVYOCHINJWA HAPA

MADENTI WA KIKE CHUO KIKUU UDOM WASEMA: WABUNGE MABUZI YETU

Na Mwandishi Wetu

MITANDAO mingi ya kijamii na kurasa binafsi za mawasiliano zinazopatikana ndani ya simu za viganjani kama Instagram, WhatsApp na BBM (Blackberry Messenger) zinazomilikiwa na baadhi ya wasichana wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) zimejaa mambo ya ngono na kashfa kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Unyemeleaji taarifa uliofanywa na Ijumaa kwa muda mrefu kwenye huduma hizo za mawasiliano ya kisasa  umebaini wanafunzi wa kike wamewabatiza jina la ‘mabuzi yao’ baadhi ya wabunge.

Bila kupepesa mitandao hiyo imekuwa pia ikitumiwa na wasichana hao kuuza miili yao huku ufahari kama si ujanja ukiwa ni mtu kujipatia bwana mwenye cheo cha ubunge ambaye anaaminika waleti yake haikaukiwi fedha kutokana na posho za vikao na utumishi wa…
Na Mwandishi Wetu
MITANDAO mingi ya kijamii na kurasa binafsi za mawasiliano zinazopatikana ndani ya simu za viganjani kama Instagram, WhatsApp na BBM (Blackberry Messenger) zinazomilikiwa na baadhi ya wasichana wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) zimejaa mambo ya ngono na kashfa kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Unyemeleaji taarifa uliofanywa na Ijumaa kwa muda mrefu kwenye huduma hizo za mawasiliano ya kisasa  umebaini wanafunzi wa kike wamewabatiza jina la ‘mabuzi yao’ baadhi ya wabunge.
Bila kupepesa mitandao hiyo imekuwa pia ikitumiwa na wasichana hao kuuza miili yao huku ufahari kama si ujanja ukiwa ni mtu kujipatia bwana mwenye cheo cha ubunge ambaye anaaminika waleti yake haikaukiwi fedha kutokana na posho za vikao na utumishi wa umma.
SIKILIZA TUKUPASHE
“Shoga naona unawapanga tu waheshimiwa,” mchangiaji mmoja kupitia kundi la BBM alichangia kwenye moja ya picha aliyoweka rafiki yake akiwa amepozi na mbunge mmoja kutoka mikoa ya Magharibi  (jina kapuni) ambapo bila haya majibu ya mwenye ukarasa huo yalikuwa: “Maisha bila mabuzi hayaendi bi dada.”
Upekuzi wa kiintelijensia wa Ijumaa ulichungulia dokezo za wachangia mada na kubaini kuwa waheshimiwa wanaoingia mjengoni kama wawakilishi wa wananchi wanachukuliwa kama mabuzi kwa tafsiri ya kuchunwa fedha huku kipindi cha vikao vya bunge vikichukuliwa kama nyakati za migodi kutema dhahabu.
MAMBO YA KUFEDHEHESHA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wasichana hao wa chuo wamekuwa wakihifadhi picha za utupu za wabunge wenye uhusiano nao kwenye simu zao za mikononi walizowapiga walipokuwa wakifanya nao ngono ambapo wakati mwingine huzitundika
mitandaoni kwa kubipu na kuziondoa haraka lengo likiwa ni kuwaonesha ushahidi huo marafiki zao.
Miongoni wa wabunge waliokumbwa na aibu hiyo ambao Ijumaa liliziona picha zake za aibu ni pamoja na mbunge anayetoka kanda ya Kusini, mwingine kanda ya ziwa na mmoja kutoka jijini Dar es Salaam huku waziri mwenye heshima kubwa naye akiingia mkenge kwa kupiga picha na msichana wakiwa kitandani vifua wazi.
WANAFUNZI WA KIUME WANASEMAJE?
Ijumaa lilipowauliza baadhi ya wanafunzi wavulana wanaosoma chuoni hapo juu ya kuwepo kwa tabia za  baadhi ya wabunge kutembea na wanafunzi wa kike walikiri na kuongeza kuwa ukata ndiyo unaosababisha baadhi ya wanachuo wajitongozeshe kwa waheshimiwa.
“Wanachofuata ni fedha siyo mapenzi, wapo wasichana hapa kipindi cha bunge hawaonekani kabisa chuoni, wanakuwa na waheshimiwa wakistarehe, kuna wengine wanasomeshwa, wanahudumiwa,” alisema mwanafunzi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Bonny.
IJUMAA LINASEMAJE?
Dawati la Ijumaa linawatahadharisha waheshimiwa wabunge wenye tabia za ukware kuachana na mambo ya kihuni, badala yake wajiheshimu vinginevyo watajikuta matatizoni na kuambulia aibu kubwa mbele ya jamii kwa kuanikwa kwenye magazeti siku si nyingi pia picha zao za aibu zitafikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.

MASOGANGE AKIMBIA BONGO KISA MAKALIO YAKE!

Na Imelda Mtema
‘VIDEO Queen’ maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye muda mwingi amekuwa akiishi Afrika Kusini ameelezea jinsi maisha ya Bongo yalivyomchosha huku usumbufu anaopata kutokana na makalio yake makubwa ikiwa moja ya sababu.
 
Agnes Gerald ‘Masogange’.
Akipiga stori na Ijumaa juzikati, Masogange alisema umbile lake hilo limekuwa likimfanya akose amani anapokatiza mitaani, tofauti na Sauzi ambako wanawake wengi wamefungashia huku yeye akionekana ‘cha mtoto’.
“Muda mwingi niko Sauzi, Bongo miyeyusho na hili umbo langu nimekuwa nikisumbuliwa sana na wanaume lakini Sauzi hili langu la kawaida, wengi wamefungashia ile mbaya, kwa hiyo muda mwingi nitakuwa huko, huku nitakuwa nakuja na kuondoka,” alisema Masogange.