This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, May 25, 2013

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA AU JIJINI ADDIS ABABA LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia, mbele) akiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.

AYERN MUNICH BINGWA UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2013

European champions: Philipp Lahm lifts the Champions League trophy for Bayern Munich
Wachezaji wa Buyern Munich wakishangilia na kombe lao.
Winning kick: Arjen Robben pokes Bayern Munich ahead in the 89th minute
Wachezaji wa Buyern Munich wakishangilia bao lao la pili na la ushindi lililofungwa na Arjen Roben dakika ya 89 ya mchezo.
Mario Mandzukic (9) wa Buyern Munich akiifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya…
European champions: Philipp Lahm lifts the Champions League trophy for Bayern Munich
Wachezaji wa Buyern Munich wakishangilia na kombe lao.
Winning kick: Arjen Robben pokes Bayern Munich ahead in the 89th minute
Wachezaji wa Buyern Munich wakishangilia bao lao la pili na la ushindi lililofungwa na Arjen Roben dakika ya 89 ya mchezo.
Mario Mandzukic (9) wa Buyern Munich akiifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 60.
Spot on: Ilkay Gundogan equalises with a penalty for Borussia Dortmund
Ilkay Gundogan wa Borussia Dortmund akiifungia timu yake bao la kusawazisha kwa penalti dakika ya 67 ya mchezo.
(PICHA: AP NA REUTERS)

USIKU WA HIP HOP & THE VODACOM MIC KING KURINDIMA DAR LIVE BAADAYE

Joh Makini.
Fid Q.…


.
Kala Jeremiah.
Stamina.
Nay wa Mitego.
Wasanii wanaotamba kwenye gemu la Hip Hop, Fid Q, Nay wa Mitego, Joh Makini, Kala Jeremiah na Stamina wataongoza safu ya burudani leo ndani ya Ukumbi wa Dar live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar katika Usiku wa Hip Hop (2013) na Fainali za Shindano la The Vodacom Mic King. Usikose!

ABIRIA WAJIPATIA BURUDANI WAKATI WAKISUBIRI PANTONI

Hapa anaonesha ufundi wake kwa kuweka mguu mgongoni
Hapa analamba mguu
Anajikuna pua kwa kutumia mguu
Msanii mmoja…
Hapa anaonesha ufundi wake kwa kuweka mguu mgongoni
Hapa analamba mguu
Anajikuna pua kwa kutumia mguu
Msanii mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, asubuhi ya leo ameonekana kwenye stendi ya kivuko (Ferry) akitoa shoo mbalimbali za mazingaombwe na mazoezi ya viungo wakati wakazi mbalimbali wa jiji wakisubiri kivuko cha pantoni ya kuelekea Kigamboni jiji Dar ambapo alionekana kama kilema kwa kufanya maajabu tofauti.
Kijana huyo anaonekana ana kipaji kwani ana uwezo wa kuwakusanya watu kwa kufanya mikogo mbalimbali, ukimkuta katoa pozi la kilema kama una huruma harakaharaka utaingia mkenge na kumpa pesa kumbe ni mazoezi tu na anafanya ili kujipatia chochote.
(HBR PICHA NA HAMIDA HASSAN GPL)

MWANAMKE MCHAWI ADONDOKA KANISANI AKIWA UCHI WA MNYAMA JIJINI DAR


Wakati Mtwara kukilipuka kwa vurugu za gesi na kusababisha maafa, jijini Dar kumeibuka taharuki ya aina yake baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Anna kudaiwa kuwa ni mchawi na kudondokea kanisani.

Tukio hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
 
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.

Ilidaiwa kuwa muda mfupi baada ya maombi kuanza, katika hali isiyo ya kawaida, mwanamke huyo aliruka kupitia dirishani akapotea na kuacha waumini vinywa wazi.

 
Habari zilidai kuwa kuna baadhi ya watu walimuona kwenye paa ya nyumba ya watu waliojenga karibu na kanisa hilo, hali iliyozidi kusababisha mkusanyiko mkubwa wa watu wakiwemo askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) waliokuwa wakimshangaa.
 
Wakati taharuki hiyo ikiendelea, mwanahabari wetu alitonywa kuwepo kwa tukio hilo ambapo aliwasha ‘tukutuku’ yake na kuwahi eneo la tukio.
Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa viongozi wa kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina la Octavian Mahembe alikuwa na haya ya kusema: 
 
“Nakumbuka kulikuwa na waumini wengi kanisani, walikuja kwa ajili ya maombi, huyo mwanamke naye alikuja hapa kama waumini.

“Ilipofika saa 5:00: asubuhi watu wakawa wanasubiri maombi, baadaye nabii naye akawa amefika na kuanza kutoa maombi. Baada ya maombi kuanza, yule mwanamke alianza kuhangaika, akawa anahamahama, hatulii sehemu moja.

“Watu waliokuwa wanataka kuombewa waliambiwa wapite mbele.


“Yule mwanamke alikurupuka na kurukia ukuta wa futi sita na nusu, akadondoka nje.

“Nabii alisema afuatwe ili aombewe, alidai kwa kuwa si mtu mwema ni hatari na anaweza kuliangamiza kanisa na waumini kwa jumla kwani alikuwa na nguvu za giza.

“Alipochukuliwa akapelekwa kwa Nabii, akaombewa sala ya toba huku akikataa kwa kusema hana dhambi.
 

“Aliendelea kuombewa na baada ya maombi alitoka nje kupitia mlangoni. Akiwa nje alivua nguo na kubaki na ile ya ndani tu, akapanda juu ya paa la nyumba jirani na kanisa, akarukia nyumba nyingine juu kwa juu bila kushuka.
 

“Hakuishia hapo, akawa amerukia mti huku akionekana kama mtu wa ajabu kiasi kwamba hata watu wengine hawawezi kufanya yale aliyokuwa akiyafanya.

“Watu wengi walikusanyika wakiwemo polisi na wanajeshi. Baada ya kupotelea mitini, ghafla kilisikika kishindo kanisani baada kudondoka eneo hilo.

“Baadaye alipelekwa ofisi ya serikali ya mtaa kwa usalama wake kwani watu walitaka kuchukua sheria mikononi wakidai ni mchawi,” alimaliza kusimulia kiongozi huyo wa kanisa.

Hata hivyo, habari nyingine zilidai kwamba kabla ya mwanamke huyo kupelekwa serikali ya mtaa, wakati akiombewa alikuwa akitangaza mambo mengi aliyokuwa akiyafanya yasiyoeleweka kwa watu wasiojua mambo ya kilozi.

Mwandishi wetu hakuishia hapo, alikwenda hadi ofisi za serikali za mtaa kutaka kujua kama mwanamke huyo alifikiswa hapo na sehemu alipo kwa sasa.
 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Salasala, Monica Timba alikiri kutokea kwa tukio hilo akidai kuwa siku hiyo hakuwepo ofisini lakini alipigiwa simu na mkazi wa eneo lake kujulishwa juu ya tukio hilo.
 

“Niliambiwa kuna vurugu kubwa katika mtaa wangu na kwamba kulikuwa na mchawi amedondoka kanisani,” alisema mwenyekiti huyo.
 

Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa  baada ya kupewa taarifa hiyo alimpigia simu mtendaji wake, Ramadhan Juma ili mwanamke huyo aokolewe na walifanya hivyo.

Alisema kuwa baadaye mwanamke huyo alipelekwa kituo kidogo cha polisi kilichopo eneo hilo cha Mtongani. 

BOMU LALIPUKA NA KUWAJERUHI WANAFUNZI 7 WA NABOTI SEKONDARI HUKO IRINGA

 Baadhi ya Maeneo walimo jeruhiwa wanafunzi hao na Mmoja kupatwa na Mshtuko wa Mlipuko wa Mabaki ya Mabomu hayo kutokana na Tatizo lake la Moyo alilonalo na hivyo kupelekea wanafunzi Watano kulazwa Ilembula Hospitali.


 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akiwajulia Hali wanafunzi hao katika Hospitali ya Lutherani ya Ilembula.


 Mwanafunzi Evance Joseph[16]kidato cha Kwanza ambaye alikuwa akifanya Majaribio ya Kuchoma Mabaki hayo ya Bomu huku Mengine akiyahifadhi kwenye Tranka lake la Nguo.


 Wanafunzi wakiwa wanaendelea kufanyiwa Vipimo vya Mionzi ya Jua kutambua ukubwa wa Tatizo  katika Hospitali ya Ilembula Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe.


 DC Njombe na Msafara Wake wakiwatazama Wanafunzi waliojeruhiwa na Mabaki ya Mabomu hayo.


 Hapa Mkuu wa Wilaya na Msafara wake ukiongozwa Na JWTZ Makambako.


 Msafara ukiwasili katika Shule ya Sekondari NABOTI Iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako.



 Wanafunzi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Njombe.


 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari NABOTI Mara baada ya kutoka katika Hospitali ya Ilembula kuwajulia Hali wanafunzi Watano waliolazwa kwa Matibabu.


 Wanafunzi wa NABOTI Sekondari wakimsikiliza DC na Msafara wake.


 
Wanafunzi Wanne wa shule ya sekondari NABOTI iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamejeruhiwa na Mlipuko wa Mabaki ya Bomu huku mmoja akipata Mshtuko wa Moyo kutokana na Mlipuko huo Baada ya Wanafunzi Takribani saba wa Kidato cha Kwanza kwenda kuyaokota Mabaki hayo kwenye Mlima uliopo Jirani na maeneo ya Jeshi.