This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, April 27, 2013

NU JOINT: JANA NA LEO / YOUNG KILLER FEAT STAMINA NA QUICK RACKA




 Ikiwa bado ngoma yake "Dear Gambe" bado inafanya vizuri kaika chati mbali mbali, leo hii Young Killer, msanii anae wakilisha Mwanza, amedondosha boooonge moja la pini ikiwa ni kolabo na Stamina na Quick Racka akiwa ameshikilia chorus, mkono wa producer D classic na Mona Gangsta.

RAISI KIKWETE ASAMEHE WAFUNGWA 40000



Rais Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya Watanzania katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na baadaye kusamehe wafungwa 4,180.
 
Idadi kubwa ya watanzania walishiriki katika maadhimisho hayo hayo ambayo yalianza saa 2:30 asubuhi na kupambwa na gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama na kupendezeshwa na halaiki ya wanafunzi 2,695 kutoka Tanzania Bara na Visiwani waliofanya maonyesho mbalimbali ya kuashiria maadhimisho ya muungano.
 
Viongozi mbalimbali wakiwamo wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani walishiriki kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni ishara ya kuuenzi na kuulinda muungano huo.
 
Viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd.
 
Wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa na mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
 
Baada ya viongozi kuketi katika nafasi zao, gwaride rasmi lenye gadi kumi lilipita na kutoa heshima zao mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Baada ya hapo vijana wa halaiki walionyesha maumbo mbalimbali kuashiria maendeleo yaliyopatikana nchini kwa muda wa miaka 49 tokea taifa la Tanzania liundwe rasmi kabla ya Wanahalaiki kujipanga na kuonyesha taswira mbalimbali na kuimba wimbo wa kuhamasisha kudumisha muungano.
 
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani hawakuweza kushiriki kwenye maonyesho hayo.
 
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

 Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa shughuli za maadhimisho hayo, mjumbe wa Kamati Kuu Chadema ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu alisema kuwa, Watanzania wanapaswa kujivunia Muungano walionao kwa sababu umedumu kwa miaka 49, akieleza kuwa ni nadra sana kuona nchi za Afrika au Ulaya kuendeleza muungano wenye umri mkubwa kama huu wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo basi wanapaswa kuuenzi na kuulinda kuendeleza amani iliyopo.
 
Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,180 waliokuwa wakitumikia vifungo vyao katika magereza mbalimbali hapa nchini katika kuadhimisha miaka 49 ya muungano.
 
Wafungwa waliosamehewa ni wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano, ambapo mpaka siku ya msamaha yaani April 26, watakuwa wameshatumikia robo ya vifungo vyao, wafungwa wagonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu na kansa ambao wamethibitishwa na jopo la madaktari.
 
Pia wazee wenye umri wa miaka sabini au zaidi, wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya, wakiwamo walemavu.
 
Msamaha wa Rais pia umeenda kwa wafungwa walemavu wa mwili na akili na wafungwa ambao hadi siku ya jana walikuwa wameshakaa gerezani kwa muda wa miaka mitano na wameonyesha kuwa na tabia nzuri.

Chanzo: mwananchi.co.tz

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU 13 WASHIRIKI KWENYE WARSHA YA MAANDALIZI YA AJIRA PINDI WAMALIZAPO MASOMO YAO‏

Rais wa chama cha wanafunzi wa vyuo vikuu(AIESEC)Bw.Frank Mushi,akiongea katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo ya vyuo vikuuwarsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu 13 walioshiriki katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu,warsha hiyo…

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu 13 walioshiriki katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu,warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Ofisa raslimali watu wa Vodacom Tanzania,Bw.Stephen Kisanko,akiongea na waandishi wa habari juu ya udhamini wa warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa chama cha wanafunzi wa vyuo vikuu(AISEC)Bw.Elvis Kashaija,akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi na umuhimu wa vijana kushiriki katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Ofisa raslimali watu wa Vodacom Tanzania,Bw.Stephen Kisanko,akitoa mada kwa wanafunzi  juu ya maandalizi na umuhimu wa vijana kujiandaa katika kuingia kwenye ajira pindi wamalizapo masomo yao ya vyuo vikuu,wakati wa warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania .iliyofanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Ofisa raslimali watu wa Vodacom Tanzania,Bw.Stephen Kisanko,akisikiliza maswali mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu 13 waliohudhuria katika warsha ya  maandalizi na umuhimu wa vijana kujiandaa katika kuingia kwenye ajira pindi wamalizapo masomo yao ya vyuo vikuu, warsha hiyo ya 14 kufanyika hapa nchini ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania,na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu 13 walioshiriki katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu,warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 

HAYA NDO MAKOSA MATATU YALIYOMFANYA GODBLESS LEMA ANYIMWE DHAMANA JANA JIONI


Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jana  jioni ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui

i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi

iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni uchochezi.

Maneno ya hapo juu ndiyo yaliyosababisha jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane ....

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 075296027*  aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye.

REDDS MISS DAR INDIAN OCEAN‏ WATEMBELEA OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS

Washiriki wa Redds Miss Dar Indian Ocean 2013 wakiwa katika picha ya pamoja wapotembelea Ofisi za Global Pulishers zilizopo maeneo ya Bamaba-Mwenge, Dar Jana
Washiliki wakiwa na Mhariri wa Gazeti la Championi Ijumaa, John…

Washiriki wa Redds Miss Dar Indian Ocean 2013 wakiwa katika picha ya pamoja wapotembelea Ofisi za Global Pulishers zilizopo maeneo ya Bamaba-Mwenge, Dar Jana