This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, September 24, 2013

TIMU YA NETIBOLI YA UTUMISHI YAICHARAZA UJENZI MABAO 48-5


Timu ya Netiboli ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kabla ya kukaguliwa kwa ajili ya mechi kati yake na timu ya netiboli ya Wizara ya Ujenzi katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma leo.
Timu ya Netiboli ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kabla ya kuanza mechi kati yake na Wizara ya Ujenzi katika Viwanja vya Chuo Kikuu Dodomaleo.
Timu ya Netiboli ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kukaguliwa kwa ajili ya mechi kati yake na timu ya netiboli ya Utumishi katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma leo.

Timu ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikisalimiana na timu ya Wizara ya Ujenzi kabla ya mechi leo.
Mchezaji wa Timu ya Netiboli ya Utumishi Fatma Ahmed (GS) akidaka mpira hewani  wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini  Dodoma leo.
Mchezaji wa timu ya Netiboli ya Utumishi Anna Msulwa (GA)(kulia) akifunga bao wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya Netiboli ya Wizara ya Ujenzi Anjela Mvungi (GK) akidaka mpira wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya Utumishi Joyce Mwakifamba (GD) akitoa pasi wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya Ujenzi Bertha Wilson (GD) akitoa pasi wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Na Happiness Shayo – Utumishi
Timu ya Netiboli ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeendelea kufanya vizuri katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa kuifunga timu ya netiboli ya Wizara ya Ujenzi mabao 48-5 katika mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma leo mchana.
Katika mechi hiyo,timu ya Utumishi ilionekana kuumiliki mchezo kwa kiasi kikubwa kitendo kilichopelekea wachezaji wa timu ya Wizara ya Ujenzi kutokujiamini na hatimaye kupoteza mabao yao kwa wingi katika dakika ishirini za mwanzo ambapo Utumishi ilifunga mabao 12 kupitia mchezaji wake Fatma Ahmed (GS) na mengine 11 kupitia mchezaji wake Anna Msulwa (GA).
Timu ya Wizara ya Ujenzi ilitumia mbinu mbalimbali kurudisha mabao lakini ilifanikiwa kufunga bao 1 kupitia mchezaji wake Kaundime Kizaba (GA).
Kipindi cha pili cha mchezo huo Utumishi iliendelea kwa kasi ileile na kufanikiwa kuifunga timu ya Wizara ya Ujenzi mabao 25 huku Ujenzi ikifunga mabao 4.
Akiongea mara baada ya mchezo huo Kocha wa timu ya Wizara ya Ujenzi Bw.Abilai Ally alisema kuwa timu yake imejitahidi sana katika kiwango chake kwa kuwa ni timu changa.
“Mchezo ni mzuri lakini timu yetu bado ni changa kimashindano na ni mara ya kwanza kushiriki mashindano haya” alisema Bw.Ally.
Aidha,alifafanua kuwa timu hiyo ina upungufu wa wachezaji kitendo kilichopelekea kuelemewa na mchezo na kufungwa mabao mengi.
Naye mchezaji wa timu ya Utumishi Bi.Amina Ahmed (GD) alisema kuwa mchezo umeonekana mzuri kwa upande wa timu ya Utumishi kwa sababu kila mchezaji ametumia nafasi yake vizuri kwa kucheza inavyotakiwa.
Timu ya Utumishi yenye lengo la kunyakua ubingwa katika mechi zijazo imeendelea kujinoa zaidi ili kufikia lengo huku ikihakikisha haipotezi mchezo wowote katika michezo ya SHIMIWI inayoendelea mjini Dodoma.

TANZANIA MABINGWA WASICHANA MASHINDANO YA KIMATAIFA AIRTEL RISING STARS

Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania na kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika
Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars wakishangilia ushindi
Mwakilishi na kiongozi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi na Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika
Mwakilishi na kiongozi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi wa kikosi cha timu ya wasichana mara baada ya kuibuka washindi katika michuano ya kimataifa ya Airtel Rising stars
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya akimkabithi kombe captain wa timu ya wasichana Tanzania mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika jana jijini Lagos Nigeria
Ni Tanzania
Kikosi cha timu mabigwa ya Airtel Rising stars Afrika cha wasichana cha Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja pichani waliosimama  (wa mwisho kushoto) ni kocha wa timu ya wavulana Abel Mtweve na wa mwisho kulia ni kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage
Tanziania mabingwa wasichana mashindano ya kimataifa Air Rising Stars
Timu ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yaliyokuwa yanafanyika mwaka huu  nchi Nigeria.
Tanzania ilipata ubigwa huo baada ya kuchuana vikali na timu ya Kenya katika mechi ya Fainali  na kuifunga Kenya goli moja bila na kuibuka mabingwa . Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania.
Tanzania ilikua kundi moja na Sierra-Leone , Malawi , na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1 , wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na Malawi 1-1.

Wakashinda 4-2 katika mikwaju ya penati dhidi ya DRC katika robo fainali mechi zilizopigwa katika uwanja wa NIS Sports. Na wakawatoa Uganda kwa mvua ya magoli 8-1.

Mbali na ushindi huo wa wasichana watanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana Shelda Boniface.

Kwa upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa  baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6  katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.

Niger wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi  baada ya kushinda michezo yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita . Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda.

Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo
Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na  Main bowl.
Kulianza na “ gala night” jumapili usiku ikafatia  sherehe za ufunguzi , na mechi za ufunguzi za makudi katika uwanja wa AgegeTownship .

Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili , mashindano haya yamekua bora kwa vijana wadogo na kwakuzingatia jinsia.

ILIVYOKUWA SEMINA YA KAMATA FURSA TWENZETU MKOANI SHINYANGA JUMAPILI.


 
 Mbuge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Wa Nishati na Madini,Mh Steven Masele akizungumza na sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Mh Steven amewataka vijana wa Shinyanga kuwa na moyo wa kujituma na kuzifanyia kazi ipasavyo fursa wanazokumbana nazo bila kukata tamaa,ameeleza kuwa hivu karibuni mkoa huo,unatarajia kufungua viwanda kadhaa,ambapo anaamini kuanzia fursa ya kupata ajira kwa vijana itaongezeka.
 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Maxmalipo,Bernard Munubi akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twendzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.
 sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center. 
 Mkurugezi  wa Vipindi na Uzalishaji Kutoka Clouds Media Groug,Ruge Mutahaba akizungumza sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Ruge pia amefunga semina hiyo ya fursa kwa vijana mapema loe mchana,ambayo imekuwa ikiandaliwa na kampuni ya Clouds Media,Semina hiyo imefanyika  ndani ya mikoa takribani zadi ya kumi  ikiwemo   Kigoma,Singida,Tabora,Mtwara,Morogoro,Dodoma,Mbeya,Iringa,Bukoba na sasa ndani ya mkoa wa Shinyanga.

 sehemu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika kwenye semina ya Kamata ya Fursa Twendzetu kwa vijana,iliofanyika leo kwenye ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.  

 Wengine tena ndio hivyo teena,fursaaa fursaaaaa. 
 Sehemu ya meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.

 Wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini.

 Mtangazaji wa Clouds FM,Shaffih Dauda akitoa mada ya fursa ndani ya michezo na changamoto zake,lakini pia namna ya kukabiliana nazo kiasi hata kupata mafanikio kwa namna moja ama nyingine,
Mwakalilishi kutoka TPSF,Jane Gonsalves akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twendzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali ya ujasiliamali kwa vijana ikiwa ni sehemu pia kujiongezea kipato,semina hiyo imefanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center. 
Baadhi wakazi wa mkoa wa Shinnyanga wakifuatila mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,semina hiyo imefanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Shinyanga Vijana Center.Picha na Michuzijr wa MICHUZI MEDIA GROUP-SHINYANGA.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AWASHANGAA WANAOPINGA PENDEKEZO LA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUITWA SERENGETI



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utalii Jijini Mwanza ambapo yanaanza rasmi leo kwa ufunguzi na kumalizika tarehe 27/09/2013 uwanja wa Nyamagana.