This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, May 29, 2013

PICHA ZA BAADHI YA WASANII WALIOHUDHULIA KIKAO CHA MSIBA WA MSANII "ALBERT MANGWEA" PALE LEADERS CLUB.

Kala Jeremiah amemwelezea Ngwea kama msanii wa pekee alikuwa 100% mkali wa Free Style na alimpenda kwa nyimbo kali kama Ghetto langu iliyom inspire kuingia kwenye Game.

Mwana FA amesema ni vitu vingi vya kukumbuka kutoka kwa Ngwea lakini kikubwa ni uwezo wake wa kuandika na mashairi yake kutojirudia hadi akatoa mfano kuwa mara nyingi alikuwa akimwambia Ngwea kwamba ana Range anatembea nalo kichwani lakini Ngwea alimjibu kuwa si Range moja tu bali mawili anamiliki kichwani kwake so tunaweza kuona jinsi gani alikuwa mtu muhimu kwenye game.
P Funk majani nae amezungumza lakini alishindwa kutokana na uchungu aliokuwa nao juu ya msiba kwani bado haamni kama Ngwea hayupo tena.


Noorah, Mez B na Proffesa Jay

KIFO CHA NGWEA: LADY JAYDEE NAYE ASITISHA SHOW YAKE

Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, mwanadada Judith Wambura Maarufu kama Lady Jaydee ametangaza kuahirisha shughuli ya maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge kupisha msiba wa kifo cha msanii Albert Robert Mangweha aliyeripotiwa kufariki nchini Afrika Kusini jana.

Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
  
Jaydee ameeeleza uamuzi wake wa kutitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.
 

Tangu amekaribishwa studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonzi sana kiasi cha kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na kukabwa na kilio.

"SITAKI KUSIKIA NYIMBO ZA NGWEA ZIKIPIGWA CLOUDS FM..WAO NDO WALIOMFANYA AANZE KUVUTA BANGI ILI KUONDOA MAWAZO"...P FUNK




Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.

HIVI NDIVYO MAMA DUDE ALIVYOZIKWA


Jeneza lililobeba mwili wa marehemu.
Mwili ukipelekwa makaburini.…
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu.
Mwili ukipelekwa makaburini.
  Dude (aliyesimama) akiwa katikati ya waombolezaji.
Umati wa wanaume waliohudhuria kwenye msiba huo ukiwa nyumbani kwa mama Dude, Ilala, Dar.
  Wasanii wa filamu, Mzee Chillo na Cloud (waliokaa chini wamevaa baragashia) wakijadiliana jambo.
  Kala Jeremiah naye alikuwepo (aliyevaa kofia nyekundu iliyochanganyika na nyeusi).
Wasanii wa filamu kwa upande wa wanaume.
    Wasanii wa filamu kwa upande wa wanawake.
MAMA wa msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, marehemu Mwadodo Ramadhan ‘Bi. Dodo’ leo amezikwa katika makaburi ya Malapa yaliyopo Buguruni-Malapa jijini Dar ambapo mazishi hayo yamehudhuriwa na watu kibao wakiwemo wasanii wa filamu, vichekesho na wa Bongo Fleva. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen!

HEE NESII!


Na Waandishi Wetu
MUUGUZI wa kike, Violet Shoo, mkazi wa jijini Dar ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni, Ilala baada ya kunaswa katika jaribio la kutaka kumchoropoa ujauzito msichana mmoja aliyepandikizwa kama mwanafunzi kwa mtego makini ulioratibiwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’.
Violet Shoo (kushoto) akidhibitiwa na polisi baada kunaswa katika jaribio la kutaka kumchoropoa ujauzito 'Denti'.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita, saa 11 jioni kwenye zahanati iliyopo Tabata Matumbi, jijini Dar es Salaam.
ILIKUWAJE?
Muuguzi huyo alikutwa ndani ya zahanati hiyo akiwa na zana mbalimbali zinazodaiwa ni za kutolea mimba huku msichana huyo akiwa juu ya kitanda, tayari kwa kufanyiwa zoezi hilo haramu.
...Vitendea kazi anavyotumia Violet Shoo kuchoropoa mimba.
Awali, Ijumaa ya Mei 23, mwaka huu baadhi ya wakazi wa eneo hilo walilitumia ujumbe gazeti hili wakimlalamikia muuguzi huyo kwamba amekubuhu katika matukio ya utoaji mimba hivyo wakaomba ikiwezekana OFM imuandalie mtego wa kumnasa ili kukomesha kitendo hicho.
“…huyu nesi amekuwa akiwatoa watoto wetu mimba, kwa siku anaweza kutoa hadi nne, sisi wazazi tumechoshwa, tunaomba mje. Anaitwa Violet…” ilisomeka sehemu ya meseji hiyo huku ikielekeza zahanati anapopatikana.
...'Denti' akiwa tayari kuchoropolewa mimba.
OFM YAJIPANGA, YAENDA KUCHUNGUZA
Baada ya malalamiko hayo, kikosi cha upelelezi cha OFM chenye wasichana wawili kilikwenda kwenye zahanati hiyo na kukutana uso kwa uso na muuguzi huyo ambapo msichana mmoja aliomba kutolewa mimba na nesi huyo ambapo aliambiwa ni shilingi 50,000.
Zahanati yenyewe hii hapa.
Kikosi kiliondoka kwa kumwambia muuguzi huyo kwamba wanafuata fedha mahali na wangerejea jioni wakiwa na ‘keshi’ mkononi.
Takataka kutoka katika zahanati hiyo.
POLISI WASHIRIKISHWA
Timu ya waandishi wa habari wa gazeti hili pamoja na Jeshi la Polisi waliweka mtego baada ya wakazi wa maeneo iliyopo zahanati hiyo kulalamika juu ya kukithiri vitendo vya utoaji mimba vinavyofanywa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.
Wakazi wa maeneo hayo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, walidai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupiga simu katika chumba cha habari kuwa idadi kubwa ya wanawake wanatolewa mimba kwa siku katika zahanati hiyo bubu ambayo haina jina wala hadhi ya kutoa huduma.
Mtuhumiwa akizidi kutulizwa na polisi.
Baada ya hapo, waandishi hao wa kike walirejea ofisini na kutoa taarifa kwa mabosi wao ambapo timu kamili ilipangwa.
Mkuu wa timu hiyo alianzia Kituo cha Polisi Buguruni ambapo alitoa taarifa kuhusu malalamiko ya wakazi wa eneo hilo na jinsi muuguzi huyo alivyofikia hatua ya kutaka alipwe elfu hamsini ili kukamilisha zoezi.
...akiwa chini ya ulinzi.
Afande mkuu akatoa maagizo kwa watu wa chini yake watatu, akiwemo askari wa kike mmoja kwa ajili ya kwenda kumnasa nesi huyo.
NESI AENDA KUSUKA KWANZA
Msichana aliyepandikizwa kutolewa mimba akiwa na mwenzake walitangulia kufika kwenye zahanati hiyo lakini hawakumkuta muuguzi huyo.
...mikononi mwa polisi.
Mfanyakazi mmoja wa zahanati hiyo alimweleza ‘mtolewa mimba’ kwamba nesi huyo alikwenda kusuka na tayari ameshawasiliana naye hivyo wasubiri.
SAA 10:30 alasiri, NESI ATOKEA
Saa kumi na nusu, muuguzi huyo aliwasili kwa ajili ya kazi hiyo huku mawasiliano yakifanyika kati ya mtolewa mimba na waandishi waliokuwa jirani na eneo la tukio.
Ndani ya dakika kumi, waandishi na polisi waliitwa eneo la tukio wakijulishwa kwamba ‘mjamzito’ huyo ameshavua nguo tayari kwa kazi ya kuchoropolewa mimba.
...tayari kwa safari ya kuelekea polisi.
USO KWA USO
Kikosi kazi kilivamia zahanati hiyo ambapo walikuta zoezi linaendelea. Polisi wenye ujuzi wa kazi za kunasa matukio walimtia mbaroni muuguzi huyo akiwa na zana za shughuli huku wakimwambia kosa lake.
Wakati huo, mjamzito alikuwa yupo kitandani katika maandalizi ya kutolewa mimba.
MAJIRANI MENO NJE
Wananchi waliokuwepo eneo la tukio wakati mtanange ukiendelea, walionekana kufurahishwa na kitendo cha kukamatwa kwa muuguzi huyo huku wakidai walikuwa wamechoka naye kutokana na vitendo vyake vya kutoa mimba hadi kwa wanafunzi.
“Tumekuwa tukijitahidi kutoa taarifa katika vyombo vya dola ikiwemo ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu lakini hakuna hatua zozote zilizokuwa zikichukuliwa, ndiyo maana tukaamua kuwasiliana na nyie waandishi wa habari ili mtusaidie,’’ alisema mkazi mmoja bila kutaja jina lake.
...safari ya kuelekea polisi ikaanza.
SWALI KWA MUUGUZI
Muuguzi huyo alipoulizwa kwa nini amekuwa akijihusisha na vitendo hivyo, alikaa kimya.
MJUMBE ASHUHUDIA
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina Namba 26, Tawi la Mandela, Rogasian Chadima alikuwepo katika eneo la tukio baada ya kufuatwa na polisi, naye aliahidi kufuatilia suala hilo akisema kwanza hakujua kama kuna zahanati katika eneo lake.
SAFARI YA KWENDA POLISI
Safari ya kwenda polisi kwa mahojiano ilianza hapo huku muuguzi huyo akiwa na ‘ushahidi’ wake mkononi. Muda mwingi alionekana asiyeamini macho yake kwa kile kilichomtokea.
Imeandikwa na Makongoro Oging’, Mwaija Salum, Musa Mateja na Joan Lema.