This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, June 11, 2013

ILIVYOKUWA HARUSI YA H.BABA NA FLORA MVUNGI


H Baba na mkewe Flora Mvungi katika pozi la siku ya sendoff ambayo ilifuatiwa na harusi ya kupendeza..

 Flora Mvungi akimlisha epo H Baba kiashiria kuwa kamtambua ndani ya mamia ya wageni walioalikwa kwenye sendoff paty.



Flora akimnywesha mumewe kinywaji cha kwanza mara baada ya ndoa kufungwa.
H Baba akisaini kitabu cha ndoa.
Flora naye akisaini kitabu cha ndoa.
Baada ya kuvuka mito,milima na mabonde hatimaye wasanii wa filamu na muziki Bongo Hamis Ramadhan Baba jina la jukwaa akifahamika kama  ‘H. Baba‘ na bi mdada kutoka Bongo Movie Flora Mvungi  weekend hii waliamua wakate vilimi vya watu wanaongea mjini na kufanikiwa kutimiza ahadi yao ya kufunga ndoa .

AIRTEL YAKUTANA NA WAHARIRI WA HABARI ZA MICHEZO KUJADILI NAMANA YA KUBORESHA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS‏


Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na wahariri wa habari za Michezo wakati wa hafla iliyoandaliwa na Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam ili kubadilishana mawazo juu ya namna nzuri ya kuboresha michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Raising Stars.   

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sunday Kayuni akizungumza na wahariri wa habari za michezo (Hawapo…
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na wahariri wa habari za Michezo wakati wa hafla iliyoandaliwa na Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam ili kubadilishana mawazo juu ya namna nzuri ya kuboresha michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Raising Stars.   Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sunday Kayuni akizungumza na wahariri wa habari za michezo (Hawapo pichani) wakati wa hafla iliyoandaliwa na Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam ili kubadilishana mawazo juu ya namna nzuri ya kuboresha michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Raising Stars.   
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano akizungumza na wahariri wa  habari za michezo (Hawapo pichani) wakati wa hafla iliyoandaliwa na Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam ili kubadilishana mawazo juu ya namna nzuri ya kuboresha michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Raising Stars.  
Baadhi ya wahariri  wa habari za michezo wakisikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Mawasiliano wa  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Beatrice Singano wakati wa hafla iliyoandaliwa na Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam ili kubadilishana mawazo juu ya namna nzuri ya kuboresha michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Raising Stars.   
Wahariri  wa vyombo vya habari za michezo wakishiriki hafla iliyoandaliwa na Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam ili kubadilishana mawazo juu ya namna nzuri ya kuboresha michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Raising Stars.

MREMBO ACHINJWA

Issa Mnally na Makongoro Oging'

MREMBO aliyejulikana kwa jina la Pepetua Maina au maarufu kama Lucy, Mkikuyu wa Kenya anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na mwili wake kutupwa katika shimo la taka.
Mwili wa Pepetua Maina ukiwa katika shimo la taka.
Mwili wa huo ulikutwa na polisi Juni 8, mwaka huu  Mikocheni B, jirani kabisa na makazi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.

Kwa mujibu wa mtoa habari, mwili wa msichana…
Issa Mnally na Makongoro Oging'
MREMBO aliyejulikana kwa jina la Pepetua Maina au maarufu kama Lucy, Mkikuyu wa Kenya anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na mwili wake kutupwa katika shimo la taka.
Mwili wa Pepetua Maina ukiwa katika shimo la taka.
Mwili wa huo ulikutwa na polisi Juni 8, mwaka huu  Mikocheni B, jirani kabisa na makazi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Kwa mujibu wa mtoa habari, mwili wa msichana huyo ulionekana na mfanyakazi mmoja wa ndani wakati akienda kutupa takataka eneo hilo ambapo alipouona alipiga kelele zilizowafanya majirani kukimbilia eneo la tukio na kujionea wenyewe.
...Mwili wa Pepetua baada ya kufunikwa.
Taarifa za kipolisi zilidai kuwa mrembo huyo kabla ya kuchinjwa alipigwa kwani mkono mmoja wa kushoto ulivunjika na kukutwa na jeraha kubwa katika paji la uso.
Wakizungumza na Uwazi kwa tahadhari kubwa kuogopa ushahidi, baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema hawakusikia vurugu zozote usiku kwa hiyo huenda wauaji walimchinja mbali na kwenda kuutupa mwili wake eneo hilo.
Mwili wa Pepetua ukitolewa shimoni na polisi.
Juni 9, mwaka huu, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura kuhusu kifo cha msichana huyo ambapo alikiri kutokea.
Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.
Mwili wa Pepetua baada ya kutolewa shimoni.
“Jeshi la polisi tulipokea habari za kuwepo kwa mwili huo jana (Jumamosi) saa sita na nusu, tukaenda na kuukuta ukiwa kwenye shimo la taka umechinjwa shingoni na kiganja cha kushoto kilikatwa na kitu chenye ncha kali na kwenye paji la uso alipasuliwa.
...Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari.
“Tuliuchukua na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Mwananyamala. Vijana wawili wanaoishi kwa Jaji Kileo ndiyo waliofika hospitali na kumtambua marehemu. Jaji mwenyewe alikuwa safarini nje ya nchi, amerejea leo (juzi Jumapili).
“Mpaka sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho, siwezi kuzungumza kwa undani zaidi,” alisema Afande Wambura.

BALAA ZITO!

Dawa za kulevya.
Kuhusu uvumi, vitu viwili vinavyotajwa sana ni ama kifo chake kilisababishwa na kuchanganya madawa ya kulevya pamoja na vilevi vingine, hivyo kutengeneza sumu iliyomuua au alibeba mzigo wa unga tumboni ambao ulimchachia na kumtanguliza mbele ya haki.
Huku tukisubiri ripoti hiyo kuwekwa wazi, Uwazi lipo kwenye wakati mzuri kueleza kinagaubaga jinsi wasanii wa Kitanzania walivyogeuzwa makuli wa kubeba mizigo ya madawa ya kulevya tumboni na kusafirisha kwenda nchi mbalimbali.
Habari zinaeleza kuwa wasanii mbalimbali nchini, wameingia kwenye mkumbo wa kusafirisha unga tumboni kutokana tamaa ya utajiri na wakati mwingine ni baada ya kuona maisha yao ya kimuziki hayawaendei vizuri.
Kutokana na kuingia kwenye biashara hiyo, wasanii hao hususan wanamuziki, hutambuliwa zaidi kwa jina maarufu la punda, kwa tafsiri kwamba wao ni sawa na mnyama huyo ambaye kazi yake kubwa ni kubeba mizigo ya binadamu.
Hoja kuhusu jina hilo ni kwamba wanaobeba madawa ya kulevya tumboni, wanajishusha thamani sawa na punda, kwani binadamu ni wale matajiri wanaowabebesha mizigo hiyo.
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
USHUHUDA WA SUGU
Ukweli wa jinsi matajiri wauza unga wanavyowatumia wanamuziki wa Kitanzania kama punda, unapewa nguvu na ushuhuda aliowahi kuutoa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Mbunge huyo ambaye anapewa heshima kwamba ni mmoja wa waasisi wa Bongo Fleva, alimweleza mwandishi wetu kuwa kabla hajawa memba wa jumba hilo la kutunga sheria, aliwahi kufuatwa na wauza unga kumshawishi awe anabeba mzigo kwenda nao nje ya nchi.
“Jamaa waliniambia kwa sababu mimi nasafirisafiri sana, passport (hati ya kusafiria) yangu itakuwa imeshagongwagongwa sana, kwa hiyo ni rahisi kwenda nchi tofautitofauti kwa urahisi, kwa hiyo wakataka niwe nabeba unga.
“Kigezo cha pili waliona kwa sababu mimi ni mwanamuziki, kwa hiyo ni rahisi watu kuamini ziara zangu ni za kimuziki. Nilikataa, niliwaambia siwezi kufanya biashara hiyo kabisa,” alisema Sugu.
Mwaka 2011, mbunge huyo aliwahi kugusia hilo, wakati akitoa hoja kuchangia bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa serikali ni lazima iwasaidie wanamuziki wa Kitanzania kwa sababu wanaibiwa sana, hivyo kuwafanya vijana kuona kimbilio rahisi la kutajirika ni kuuza madawa ya kulevya.
“Mheshimiwa spika, serikali isifanye ili kijana wa Kitanzania afanikiwe lazima auze unga, madawa ya kulevya,” alisema Sugu na kueleza mfano huo wa jinsi alivyofuatwa kushawishiwa na matajiri wa unga ili naye awe punda.
Jack Patrick.
PUNDA HULIPWA DOLA 3000 MPAKA 5000
Kwa mujibu wa mwanamuziki maarufu wa dansi nchini (jina tunalo), kwa wastani punda hulipwa fedha kulingana na umaarufu wake, kwa kuangalia kiwango cha mzigo anaobeba, vilevile nchi anayopeleka.
“Mara nyingi watu wanalipwa dola 3000 (shilingi 4,800,000) mpaka dola 5000 (shilingi 8,000,000). Binafsi nilishabeba madawa kutoka hapa Tanzania kwenda China, Botswana na Afrika Kusini, kila nilipofikisha mzigo nililipwa dola 5000,” alisema mwanamuziki huyo na kuongeza:
“Kuna kipindi nilinogewa, nikawa sijishughulishi sana na muziki, kila mara nipo safarini nakwenda kupeleka mzigo, nikirudi nipo vizuri na dola 5000 zangu. Hivi sasa nimeacha baada ya watu wangu wa karibu kunishauri na kunieleza kwa mapana hatari inayoweza kunipata.”
MTINDO WA SASA
Utafiti wa siku za hivi karibuni, umepata jawabu kwamba wauza unga wengi, wanawatumia wanamuziki na wasanii mbalimbali kusafirisha mizigo kwa sababu kwao ni rahisi kugongewa visa katika balozi za nchi wanazokusudia kwenda.
“Kule inaweza kuandaliwa shoo ya uongo na kweli, wewe unasafiri kwamba unakwenda kwenye hiyo shoo lakini kumbe ni utapeli mtupu. Kule hauendi kama mwanamuziki, isipokuwa ni punda tu,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
“Fikiria mtu unakwenda kwenye shoo halafu ukumbini wanaingia watu 40, halafu huyo mwandaaji anakulipa fedha zako vizuri, unalala hoteli nzuri, ukumbi analipa, kodi anatoa. Hii biashara ya madawa ya kulevya ina siri kubwa.
Khaleed Mohamed ‘TID’.
“Kinachosikitisha kwa wanamuziki wenzetu ni kwamba hawajitambui. Watu wanakufa jamani, kukubali kusafirisha madawa tumboni ni sawa kujiweka katikati ya uhai na kifo. Zile dawa zikipata joto tumboni huponi. Ukijisahau na kunywa kitu cha moto ni kifo.”
Mtoa habari huyo aliendelea kubainisha kuwa wanamuziki wa Kitanzania wengi wanakuwa nchini bila kazi mpaka wanakumbwa na hali ngumu ya uchumi kutokana na kutopata shoo za kutosha, hivyo kuwawia rahisi kukubali ofa ya kubeba madawa ya kulevya tumboni kwenda nchi mbalimbali.
“Hivi sasa kuna wimbi kubwa. Watakwenda hivyo ila baadaye madawa hufeli tu. Naamini itafika wakati tutashuhudia vifo vingi vya wanamuziki wetu. Mungu akiniweka hai nitasema, kwani nawajua wanamuziki wengi punda,” alisema.
Aidha, mtoa habari huyo aliwataja wanamuziki sita nchini ambao aliwataja moja kwa moja kuwa wanajishughulisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya lakini majina yao tunayahifadhi kwa sasa.
Ambwene Yesayah ‘AY’.
MWANAMUZIKI ALIVYOMSHAWISHI MFANYABIASHARA
Kuna mwanamuziki (jina kapuni) ambaye hivi karibuni alirejea nchini baada ya kupata matatizo akiwa nje ya nchi, aliwahi kumshawishi mfanyabiashara mmoja aingie kwenye biashara ya madawa ya kulevya halafu yeye atakuwa anabeba.
Mfanyabiashara huyo (naye jina kapuni), alisema: “Nilishangaa yule dogo ananiambia yeye yupo tayari kubeba mzigo kusafirisha kwenda Afrika Kusini na nchi nyingine za Kusini ya Afrika.
“Aliniambia yeye ameshaweza kubeba madawa ya wafanyabiashara wengine na wakapata faida kubwa. Aliniambia faida ni mara mbili kwa asilimia 100. Nilimjibu siwezi kufanya hiyo biashara, baadaye akiwa huko alipata matatizo na hivi sasa yupo hapa nchini.”
MAMA WA MWANAMUZIKI NI TISHIO KWA KUUZA UNGA
Mama wa mwanamuziki mmoja wa Bongo Fleva (jina tunalo), mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam, ni tishio kwa biashara ya kuuza unga.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mama huyo amekuwa akiwatumia mabinti mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam, kuwabebesha mizigo tumboni na kuwasafirisha kwenda China na nchi za Kiarabu ambako ndiko lilipo soko lake.
“Wapo watangazaji wameshabebeshwa mizigo na yule mama. Yeye hasafiri na mzigo na ana watoto lakini hawabebeshi mizigo watoto wake, ila anawatumia watoto wa wenzake,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
“Kama ingekuwa ni biashara nzuri kwa nini yeye habebi wala watoto wake? Hawa dada zetu ambao wanapenda sana maisha ya haraka, inabidi wawe macho, vinginevyo watakwenda na maji.”
Sandra Khan 'Binti Kiziwi'.
UPO MFANO WA BINTI KIZIWI
Mrembo Sandra Khan, aliyepata jina la Binti Kiziwi baada ya kushiriki video ya wimbo wa Binti Kiziwi ambao ni mali ya mwanamuziki Ally Mohamed Ahmad ‘Z-Anto’, alikamatwa Februari, mwaka huu China na kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni.
Zipo tuhuma kwamba Binti Kiziwi, alikuwa kwenye safari moja na mwanamitindo Jacqueline Patrick ambaye aliingia mitini baada ya kumwona mrembo huyo ambaye ni mtalaka wa Z-Anto, akikamatwa na polisi wa China.
Madai yanasema kuwa Binti Kiziwi aliishiwa nguvu na kupata maumivu makali ya tumbo baada ya kuwasili China, hivyo polisi walimchukua kwa lengo la kumpa huduma ya kwanza ndipo wakabaini kwamba alikuwa amebeba madawa ya kulevya tumboni.
Jack Patrick anakiri kwamba alishuhudia Binti Kiziwi akikamatwa, ila aliona soo kujitokeza kusema anamjua, kwani naye angewekwa ndani kama mtuhumiwa.
Upande mwingine, mume wa Jack Patrick, Abdulatif Fundikira, hana muda mrefu tangu aachiwe kwa dhamana, akikabiliwa na kesi ya usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.
WANAMUZIKI WANAVYOONGEA
Mwana-Hip Hop, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, alisema kuwa yeye hajawahi kusafirisha madawa ya kulevya tumboni, kwani anafahamu kuwa kufanya hivyo ni tatizo, alifafanua:
“Ndiyo maana mimi nafanya muziki kuelimisha jamii, kwa hiyo siwezi kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Watu wanaingia kwenye hiyo biashara ili watajirike mapema, hicho ni kitu kibaya sana. Nawaomba wale wanaouza madawa ya kulevya wabadilike, jamii inawategemea.”
Mkali wa Bongo Fleva, Ambwene Yesayah ‘AY’ alisema: “Mimi sijawahi kuthibitisha kama kweli wanamuziki wenzetu wanafanya hivyo, ila kama kweli wanafanya basi wanahatarisha maisha yao. Kila anayefanya hivyo ajue kwamba akikamatwa ndiyo mwisho wake. Nashauri wanamuziki tusipende maisha ya mkato.”
Seif Shaaban ‘Matonya’, alisema: “Mimi nimeshawahi kusingiziwa kwamba nilikamatwa nje ya nchi kitu ambacho siyo kweli. Kwa watu ambao wanafanya hiyo biashara, nawashauri waache, kwani madawa ya kulevya yanatuharibia ndugu zetu.”
Mwanamuziki wa mduara, Zuwena Yusuf Mohamed ‘Shilole’ alisema: “Mimi sijawahi kuona, ila kama ni hivyo waachane na hiyo biashara kabisa.”
ATHARI ZA MADAWA KULEVYA
Wapo wanamuziki mbalimbali ambao wameshatajwa kwamba wanajihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, wimbi limekuwa kubwa mno.
Mwana-Hip Hop, Kulwa Maujanja wa Kundi la Mapacha, aliwahi kutoa ushuhuda wake kwa mwandishi wetu kwamba aligongea sigara kwa wanamuziki wenzake wawili (majina tunayo) na alipovuta, alikuta imewekewa madawa ya kulevya.
“Kichwa kiliamka nikawa kama nimedata. Kesho yake nilishinda kichwa kinauma sana. Kumbe wale ndugu zetu wanatumia madawa ya kulevya, wanachanganya kwenye sigara,” alisema Kulwa.
Rashid Makwilo ‘Chid Beenz’, aliwahi kukaririwa kwamba ameacha madawa ya kulevya kama ilivyo kwa mwana Hip Hop mwenzake, Langa Kileo, ingawa yapo madai kuwa wawili hao bado hawajaacha.
Wanamuziki wengine, Khaleed Mohamed ‘TID’, Msafiri Saidi ‘Diouf’, Aisha Mbegu ‘Madinda’ na wengine kibao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na utumiaji wa mihadarati.
Kuhusu athari zake, inashauriwa kitaalamu kwamba ni vema kuacha kutumia madawa, kwani huharibu ubongo kwa sababu huua mishipa ya fahamu, huathiri mfumo wa damu, husababisha mhemko na juu ya yote ni huchochea shambulio la moyo (cardiac arrest) na vifo vya ghafla.
Albert Mangweha.
NGWAIR NA M2 THE P
Kuhusu Ngwair, alikuwa na rafiki yake Mugaza Pembe ‘M2 The P’, wote walizidiwa pamoja lakini yeye alifariki dunia na kumwacha mwenzake akiwa mahututi kwenye Hospitali ya Mtakatifu Helen Joseph, Johannesburg, Afrika Kusini.
Yapo mambo matatu ambayo yanadaiwa lakini ripoti ya daktari au kauli ya M2 The P, ndivyo vinavyoweza kumaliza utata.
Mambo hayo matatu ni kwamba walizidisha kiasi cha unga, madai mengine ni kwamba walitumia madawa yaliyoisha muda wake, hivyo kuwa sumu, tatu ni kuwa walikuwa na mzigo tumboni ambao ulifumuka.

MSANII MATONYA AFIKISHWA MAHAKAMANI HUKO SONGEA KWA TUHUMA ZA UTAPELI....HUU NDO MKASA WAKE


Msanii Matonya  amekamatwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliopo manispaa ya Songea mkoani ruvuma. 

Taarifa  zinadai  kuwa  Matonya  aliingia ukumbini akiwa amelewa,  hali iliyomfanya  ashindwe  kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi  huo baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo...


Baada  ua  hali  hiyo,  waandaaji wa show hiyo waliamua  show  hiyo  ifanyike kesho yake na kiingilo kiwe ni  kununua bia .

Mbali na sakata hilo, Matonya alitakiwa akafanye show nyingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivyo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurudi Dar es Salaam ....

 Baada ya kuvuja taarifa hizo , waandaji walimfuata hadi alipo kuwa amefikia nakukuta amehamia sehemu nyingine. ...

Walipomkosa, waliamua  kumvizia katika  stendi  ya mabasi ambako  walifanikiwa  kumkamata  akijiandaa  kusepa..!!!


Hadi sasa, msanii huyo  yupo mahakama ya mwanzo ...