This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, March 2, 2013

ziara ya mwenyekiti wa uvccm taifa morogoro

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Hamis Sadifa
Vijana machacahari Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walioihama Chadema hivi karibubi, wakiserebuka nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro, baada ya msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa,  Sadifa Hamis Juma kuwasili kwenye ofisi hiyo, Februari 28, 2013 kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.

  Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Morogoro Herieth Sutta akimkaribisha Sadifa kuzungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Sixtrus Mapunda
NAFURAHI KUWA NA WEWE! Sadifa akimwambia Sixtus Mapunda kabla ya kuanza hotuba yake ya mkutano huo wa ndani uliofanyika Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro
  Sadifa akitoka na wenyeji wake ukumbini

TCU INAHUSIKA JE NA UBOVU WA MATOKEO YA KIDATU CHA NNE




Hoyce Temu akifundisha katika moja ya shule huko Iringa hivi karibuni alipokuwa huko kuandaa vipindi vya mimi na Tanzania

Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) inatakiwa isibakie tu kuthibitisha kuwepo kwa vyuo vikuu
hapa nchini, bali pia iwe ndiyo tume pekee inayosimamia na kuiandaa mitaala ya vyuo vikuu
vyote hapa nchini. TCU inatakiwa iwe sehemu ambayo kutakuwepo na jopo la maprofesa wa
kila fani ambao watatayarisha mitaala ya kila somo na kila chuo kuufuata mtaala huo.

Zamani tulikuwa na chuo kikuu kimoja cha mlimani (UDSM) wanafunzi wote waliohitimu
walikuwa na kiwango kimoja cha uelewa kulingana na fani walizosoma kwa vile wamesoma
chuo kimoja. Sasa hivi tuna vyuo vikuuu vingi sana ikiwa ni pamoja na vile vya serikali na vile
vya binafsi au taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Vyuo hivi kila kimoja kina mtaala wake
wa kila somo kulingana na chuo kilivyotaarisha mtaala huo au mwalimu wa somo hisika. Baadhi
ya vyuo vinatumia mitaala ya vyuo vya huko nje kwa vile vipo hapa nchini kama matawi ya
vyuo hivyo. Pamoja na kwamba vyuo hivyo vimeandikishwa kwenye tume inayodhibiti vyuo
vikuu vya nchi vilipotoka lakini ni vizuri kama TCU ingetayarisha utaratibu unaziunganisha
program zote na kuziweka kwenye kiwango kimoja (synchronize at par) ili kuwe na uhalali wa
kuwa na kiwango kimoja cha elimu inayotolewa hapa nchini.
Ukiwachukuwa wanafunzi 50 waliohitimu toka kwenye vyuo vikuu vya kwetu hapa
nchini ambao wamesoma fani moja (kwa mfano wana shahada ya hesabu kwa shule za
sekondari) ukaanza kuwafanyia utafiti wa kuwauliza maswali mbalimbali yanayohusiana na
fani waliyosomea utakuta wote hamsini wanatofautiana; na wengine utawagundua kabisa
kwamba wametoka nje kabisa ya ule wigo wa uelewa (Ranger Knowledge) wa hesabu
unaokubalika kimataifa! Pamoja na kwamba wanafunzi 50 toka vyuo vikuu 50 shahada zao
zinakubalika na TCU lakini wana viwango tofauti vya uelewa, na hawa hawa ndiyo walimu
wetu tunaowategemea waende wakafundishe shule zetu za sekondari ambazo matokeo yake
tumeyaona. Walimu 50 ambao wote wa shahada moja lakini wana uelewa tofauti, hivyo hata
wanafunzi wao watakaowafundisha watapata elimu tofauti na uelewa tofauti licha ya kwamba
wanatumia mtaala mmoja!
Nikirudi kule nchini Urusi niliposoma mimi wao mitaala ya kila ngazi inafanana nchi nzima
na vitabu wanavyotumia kufundishia pia vinafanana; mwanafunzi akihama shule moja
kwenda shule nyingine hana wasiwasi kwa vile shule zote zinatumia vitabu sawa na walimu
wote wanatumia mfumo mmoja wa kufundishia: yaani ukichukuwa notice za shule moja na
kulinganisha na notice za shule nyingine zinafana utafikiria zimetolewa photo copy licha
ya kwamba ni shule tofauti na walimu tofauti, lakini somo moja. Hii inakuwa rahisi kupima
maendeleo ya wanafunzi na uwajibikaji wa walimu kwa ujumla kwa vile umeweka kiwango
cha elimu (Range of Knowledge) kwa wanafunzi wote kwa nchi nzima. Huu ndiyo utaratibu
ambao wenzetu wa kule Urusi wameweza kuutumia na kufikia malengo mazuri ya kielimu; na
unapokuwa na utaratibu kama huu ni rahisi hata kupanga mipango ya mbalimbali (strategic
Plan) ya maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Nilipokuwa nafundisha kule chuo kikuu Mzumbe niliwahi kutoa mawazo kama haya kwamba
TCU isiishie tu kuthibitisha kwa kuna chuo kikuu kinachoitwa Mzumbe lakini pia kiwe
kinadhibiti kila kinachofundishwa chuoni hapo kama kweli kinakidhi soko la ajira hapa nchini;
mawazo yangu yalitupwa na nikaoneka kama nataka kuleta mambo mapya yasiyokubalika!
Naomba nisieleweke vibaya kwa hilo sina maana mbaya na elimu inayotolewa Mzumbe, hapana,
bali nimetoa mfano tu wa Mzumbe kwa vile niliwahi kufundisha hapo na wazo hilo nililitoa kwa
walimu wenzangu, pamoja na kwamba Mzumbe ni moja kati ya vyuo vizuri Tanzania.
Pia mimi sikubaliani na utaratibu uliopo sasa hivi hapa nchini jinsi vyuo vikuu vyetu vinavyotoa
digirii ya uzamivu (Ph.Ds); utaratibu uliopo hivi sasa unatoa Ph.Ds ambazo hazina viwango
sawa, kama ambavyo wanafunzi wanaopata shahada ya kwanza toka vyuo mbalimbali lakini
wana uelewa tofauti! Mtu aliyehitimu digirii ya uzamivu ni mtu mwenye kiwango kikubwa cha
uelewa na utafiti wa kisayansi kulingana na fani yake, hivyo nchi kama taifa moja ambalo lina
mkakati mmoja wa kitaifa wa kuendeleza sayansi na tekinolojia linatakiwa liwe na utaratibu
mmoja unaoeleweka kitaifa wa kuzitoa hizi digirii za uzamivu (Ph.Ds). TCU iunde tume 2
maalumu za majopo la maprofesa 21 kila tume toka vyuo mbalimbali; tume ya kwanza iwe ni
tume ya masomo ya Arts, na tume ya pili iwe ya masomo ya sayansi. Tume hizi ndizo pekee
zitakazokuwa na mamlaka ya kuisoma ripoti ya mtafiti wa kiwango cha uzamivu (Ph.D) na
kumuhoji maswali mtafiti mbele ya jopo la maprofesa 21 na baada ya kumuhoji maswali
zitapigwa kura na matokeo ya kwamba kazi imekidhi viwango vya kimataifa vya kupewa digirii
ya uzamivu au lah, itategemea na kura za jopo la maprofesa 21, wengi wape. Baada ya hapo
ripoti ya jopo la maprofesa ipelekwe TCU kwa ajili ya kutoa idhini kwa chuo kikuu husika
kumpa mtafiti digirii yake ya uzamivu.
Mwisho kabisa naiomba TCU isiishie tu kuthibitisha kuwepo kwa vyuo hapa nchini bali iwe
mustari wa mbele katika kutengeneza kuandaa na kusimamia mitaala huko vyuoni ili tuweze
kupata wataala wenye kiwango kimoja cha elimu; kwa kufanya hivyo tutakuwa tumejijengea
uwezo wa kuweka mikakati mbalimbali ya maendeleo ya muda mrefu. Unapokuwa una
wataalamu wenye shahada moja lakini uelewa tofauti inakuwa vigumu sana kufikia malengo ya
kimaendeleo hasa kwenye fani ya elimu kwa ujumla, kwa vile elimu ya sekondari ndiyo msingi
wa elimu ya chuo kikuu; na digirii ya uzamivu ndiyo kitovu cha utafiti na jiko la mawazo kwa
taifa, hivyo ukitoa Ph.Ds ambazo hazikidhi kiwango cha kimataifa unaliua taifa.
Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics)
Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU – Dar, Universities.
Currently: Freelance Journalist & Seasonal Economical &
Political Analyst