This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, June 23, 2013

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUGONGA NYUMBA AKIJIFUNZA KUENDESHA GARI MORO



Gari hilo baada ya kugonga nyumba na kuingia mpaka chumbani.
Chumba ambapo gari hilo liliingia.…
Gari hilo baada ya kugonga nyumba na kuingia mpaka chumbani.
Chumba ambapo gari hilo liliingia.
Baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la ajali.
Wananchi wakilifunga gari hilo tayari kuondolewa na winchi.
Likinyanyuliwa na winchi.
Likitolewa eneo la ajali.
NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja jana usiku alinusurika kifo baada ya kugonga nyumba wakati akijifunza kuendesha gari aina ya Prado lenye namba za usajili T 952 BTJ.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu usiku maeneo ya uwanja wa ndege jirani na Chuo cha Ujenzi njia panda ya kuelekea gereji ya Msuya.
Mbali na mwanamke huyo kunusurika kifo, pia familia iliyokuwa ikiishi kwenye nyumba iliyogongwa nayo ilinusurika baada ya gari hilo kuvunja ukuta wa nyumba na kuingia mpaka chumbani ambako familia ilikuwa inajianda kulala.
Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na mtandao huu walidai kwamba mwanamke huyo ambaye bado hajaiva kwenye udereva alikata kona iliyo eneo hilo kwa mwendo kasi.
"Huyu mama anajifunza kama unavyoona kibao cha 'L' kwenye gari yake, uzembe alioufanya alikata kona hii kwa mwendo wa kasi na kwamba badala ya kukanyaga breki alikanyaga moto na kuzidisha kasi ndipo alipogonga nyumba hii." Alisema shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jumanne Athuman.

TASWIRA ZA KILI MUSIC TOUR NDANI YA DODOMA


Hatimaye ile ziara ya Muziki Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imeanza rasmi leo kwa show baab kubwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Katika onyesho hilo lililohusisha wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012 kwa utangulizi wa waendeshaji wake Dulla na Zembwela kutoka East Africa TV kugawa zawadi kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwa kuendesha mashindano mbali mbali.
Hakuna ubishi kuwa Ben Pol ndiye mfalme wa R&B na alilithibitisha hilo alipoponda jukwaani na kuwaimbisha…
Hatimaye ile ziara ya Muziki Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imeanza rasmi leo kwa show baab kubwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Katika onyesho hilo lililohusisha wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012 kwa utangulizi wa waendeshaji wake Dulla na Zembwela kutoka East Africa TV kugawa zawadi kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwa kuendesha mashindano mbali mbali.
Hakuna ubishi kuwa Ben Pol ndiye mfalme wa R&B na alilithibitisha hilo alipoponda jukwaani na kuwaimbisha mashabiki wake mwanzo hadi mwisho kwa nyimbo zake kali Pete, Jikubali, Samboira huku kivutio kikiwa pale uwanja mzima ulipoimba pamoja nae wimbo wa Nikikupata.
Malkia wa Bongo Flava, Lady Jaydee ambaye ni mwanamke pekee katika wasanii waliokuja Dodoma alithibitisha kwamba habahatishi baada ya kulishambulia jukwaa kwa nyimbo zake zote zililizompa umaarufu. Jide nae kama wasanii wengine alianza kwa kumkumbuka marehemu Albert Mangwea kwa kuimba chorus ya wimbo wa "Sikiliza" ambao ni ushirikiano wake, MwanaFalsafa na Mangwair kisha kuanza kuimba nyimbo zake kali na kumalizia na Joto Hasira alioshirikiana na Profesa Jay aliepanda jukwaani kuungana nae.
Profesa Jay anapenda kuitwa The Heavy Weight MC na alililithibitisha hilo wakati alipokabidhiwa jukumu la kufunga show, kwa zaidi ya nusu "Jay wa Mitulinga" kama anavyojulikana aliwaimbisha mashabiki nyimbo zake kali toka Bongo Dar es Salaam, Chemsha Bongo, Piga Makofi nk. Kivutio kilikuwa pale alipoimba wimbo wake wa zari la mentali na kumpandisha jukwaani moja ya mashabiki kuimba mistari ya "Zubeda" huku akishangiliwa na wengi kabla ya kuendelea kuchana nyimbo zake nyingine zilizompatia umaarufu.
Alipotajwa kuwa zamu yake imefika ulitokea mtafaruku wa mashabiki kusukumana kila mmoja akitaka kuwa mbele ili amuone vizuri, lakini huyu ndiye Mfalme wa Hip Hop kwa mwaka 2012, Kala Jeremiah ambaye alilishambulia jukwaa kwa zaidi ya nusu saa huku akwadatisha maelfu waliojitokeza huku kama kawaida wimbo wake wa Dear God ukionekana kumgusa kila mtu.
Wa kwanza kupanda kwenye steji alikuwa Linex "Mjeda" alieimba nyimbo zake zilizotamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni. Wimbo ulioonekana kuwakonga wengi ulikuwa "Aifola".
Wa pili jukwaani alikuwa ni Ommy Dimpoz aliepanda jukwaani na madansa wake wanaosifika kwa uhodari wao wa kumiliki jukwaa na kuimba nyimbo zake mbili za Baadae na Me and You kabla ya kushuka na kumpisha Ben Pol.
Roma! Roma! Roma! ndio kelele zilizopigwa na mashabiki wakati akipanda jukwaani na kama ilivyo kawaida ilikuwa ni michano mwanzo hadi mwisho. Roma ambaye mwaka jana alishinda tuzo mbili alizidi kuonyesha ubora wake pale alipoimba nyimbo zake kama "Pastor", "Tanzania", "Kidole cha mwisho juu" na "2030" huku akitumia dakika kadhaa kumkumbuka marehemu Albert Mangwair.

CHEKA NAO YAZIDI KUPOKELEWA VIZURI NA WAKAZI WA MBAGALA‏


Baadhi ya watoto wakiwa tayari kushindana katika mbio za Vodacom Cheka Nao zilizofanyika Dar Live, Mbagala siku ya kifamilia iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kila mmoja kwa mwezi, ili kujiunga na kufaidika na ofa  piga…
Baadhi ya watoto wakiwa tayari kushindana katika mbio za Vodacom Cheka Nao zilizofanyika Dar Live, Mbagala siku ya kifamilia iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kila mmoja kwa mwezi, ili kujiunga na kufaidika na ofa  piga *149*01#.
Ofisa wa Voacom Tanzania Alfani Mdachi (katikati) akimwandikisha Mustafa Mustafa mkazi wa Mbagala ili kumpatia kadi ya simu tayari kwa matumizi halali, zoezi hilo lilifanyika wakati wa kampeni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi, ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#. Anaeshuhudia ni Meneja wa kanda ya Mbagala, Idd Mawe.
Ofisa wa Vodacom Tanzania, Bi. Rehema William (aliyeketi) akimwelezea jambo mkazi wa Mbagala Dar es Salaam, wakati Promosheni ya Cheka Nao iliyofanyika Mbagala hapo jana inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwa mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi, ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#.
Bi.Tumu Said ambaye ni mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam akimsikiliza Ofisa wa Vodacom Tanzania jinsi anavyomfafanulia faida za kujiunga na Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwa mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi, ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa kanda ya Mbagala, Idd Mawe na kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo, Bw. Matina Nkurlu.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bw. Matina Nkurlu (kulia) akimwelezea Bi.Tumu Said ambaye ni mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam manufaa na faida za kujiunga na Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mtandao wowote na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi, ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#.

"TUNAJIANDAA KUIPINDUA NCHI ENDAPO SERIKALI HAITAWASHUGHULIKIA WATU WALIOFICHA MABILIONI USWISWI"...ZITTO KABWE


Zitto  Kabwe  amefunguka  na  kudai  kuwa  kwa  sasa  wanajiandaa  kufanya  mapinduzi  ya  nchi  endapo   watu  walioficha    mabilioni  uswiswi    hawatashughulikiwa  ipasavyo....

Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
  
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
 
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge.

Zitto  Kabwe  anatoa  angalizo  katika  hatua  hiyo  ya jaji Werema   kwa  kusema  kuwa  hatua  hii  isiwe  "zima  moto"   na  daganya  toto  ili  kuwafumba  macho  watanzania...

Ubabaishaji  wowote  kwa  mujibu  wa  Zitto  Kabwe  utasababisha  mapinduzi  ya  nchi.....

Hii  ni  post  yake  aliyoweka  katika  mtandao  wa  twitter

OMMY DIMPOZ APIGWA CHUPA NA MASHABIKI AKIWA JUKWAANI HUKO DODOMA

Kuna tetesi kuwa Ommy dimpoz amepigwa mawe jukwaaani dodoma na kushindwa kufanya show ya kilimanjaro music award dodoma. 
Wadau toka  Dodoma wasema  msanii yoyote atakaye mdiss msanii wa dodoma hawatamruhusu kufanya show Dodoma  na watamshusha jukwaani kama walivyo fanya leo  kwa  Ommy

Tunafuatilia  undani  wa  habari  hii