This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, April 21, 2013

"SPIKA WA BUNGE ANALIONGOZA BUNGE KWA " REMOTE CONTROL" TOKA NJE.....HII NI KAULI YA DR. SLAA


Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amesema Spika wa Bunge Anne Makinda amekinajisi kiti cha spika.

Dr Slaa ambaye ni gwiji wa siasa za Tanzania amemshutumu vikali Spika na Naibu wake kwa kuharibu kabisa bunge la Tanzania na kupoteza kabisa heshima yake ndani na nje ya nchi.


Dr Slaa amefichua kwamba maamuzi yote yanayofanywa na Anne Makinda si kwa utashi wake bali ni kutokana na maelekezo maalum anayoelekezwa kutoka nje ya bunge.


Kutokana na vitendo vinavyofanywa na kiti cha Spika imefika mahali Spika na Naibu wake wanadharauliwa hata na watoto wadogo.


Spika Anne Makinda kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri kuu ya CCM.

WABUNGE WACHACHAMAA JUMBA LA MCHUNGAJI LWAKATARE LIVUNJWE


'Hekalu' linalomilikiwa na Mchungaji Getrude Lwakatare.

Wabunge wamemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Terezya Huvisa kuzivunja nyumba mbili zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam zilizojengwa katika fukwe ya bahari ya Hindi ikiwemo ya mbunge licha ya kwamba kuna zuio la mahakama.

Bila kutaja majina ya wamiliki hao, wabunge hao walitaka hatua hizo zichukuliwe kwa haraka kwa nyumba hizo zilizojengwa kwenye fukwe kinyume cha sheria zivunjwe kwa maelezo kuwa hazina ofa wala hati.
 
Sambamba na hilo wametaka watendaji wa serikali waliohusika kutoa vibali kuruhusu ujenzi huo kwa maelezo kuwa walichukua rushwa wachukuliwe hatua.
 
 Mbunge wa kwanza kuanza kuzungumzia hilo ni wa viti maalum, Esther Bulaya (CCM) aliyetaja viwanja viwili vyenye namba 2019 na 2020 kikiwemo cha mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani waliojenga  nyumba zivunjwe licha ya kuwepo zuio la mahakama.
 
 “Mwaka jana waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka alivunja nyumba za kawaida licha ya zuio la mahakama, lakini nyumba zilizo kwenye viwanja namba 2019 na 2020 hazikuvunjwa kwa sababu ya zuio la mahakama hii ni double standard hatuwezi kuvumilia. 
“Wengine wenye nyumba ni viongozi tupo nao humu tena wa kiimani, lakini kwa nini viongozi tunafaya hivi wakati tunatakiwa tuwe wa mfano na tunawafanya viongozi wenzetu washindwe kufanya kazi zao?…hakuna haja ya kuogopa waziri Huvisa (Mazingira) vunja nyumba, haiwezekani kuwa na nguvu ya fedha.
 
 “Wabunge wenzangu tuazimie Manispaa ya Kinondoni na NEMC (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira), wakavunje nyumba hizo ndani ya wiki moja , naomba kutoa hoja,” alisema.
 
 Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimweleza; “Haiwezekani kutoa hoja kwa kuingilia vyombo vingine”.
 
 Mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani mwenye nyumba katika  eneo hilo la Mbezi Beach aliyejenga katika fukwe ya bahari kwa kuondoa mikoko na kuweka kifusi na kujenga nyumba ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Dk. Getrude Lwakatare (CCM).
Naye Mbunge wa viti maalumu, Grace Kiwelu (Chadema) akichangia bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, alisema kamati yake ya Ardhi na Mazingira ilitembelea eneo hilo la Mbezi Beach na kukuta aliyejenga katika kiwanja 2019 hakuwa na ofa wala hati.
 
 “Ametumia pesa kuwarubuni watendaji akaondoa mikoko, akaweka kifusi na akajenga nyumba naomba wizara ya Ardhi na ya mazingira wawachukulie hatua watendaiji hao,” alisema. 

Akijibu hoja ya Bulaya, kuwa kwanini nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuvunjwa wakati nyingine zilivunjwa, mwanasheria mkuu wa Serikali, Frederick Werema alisema: 
 
“Sisi ni wajibu wetu twende mahakamani kusema watu hao wamevunja sheria kujenga hapo. Wao wanaruhusiwa na Katiba na mahakama itafuata sheria.

“Nashauri Bulaya usitoe shilingi kuzuia Bajeti ya Waziri, uje tuone huyo kigogo itakuwaje.” 
Hata hivyo, Huvisa alisema: “Nyumba tulizovunja hazikuwa na kesi na hii tuliyoiacha ilikuwa na kesi.”
Jumba la kifahari linalodaiwa kuwa la Mchungaji Lwakatare ambalo lilizinduliwa mwaka jana, limekuwa klikitajwa kuwa lina thamani ya takribani sh bilioni 1.5.
zero99

JUMA NATURE ATIMULIWA EATV BAADA YA KUINGIA AKIWA AMEVAA KANDAMBILI.....

Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kitendo  cha  kutimuliwa  jana usiku katika kipindi cha burudani cha televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview. 
Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo  mtangazaji alisema watarejea baada ya mapumziko mafupi  na ndipo Nature hakuonekana tena.
  Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfuata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika yafuatayo  kupitia ukurasa wake wa facebook....

"hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo....

kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview"

Waziri wa Mawasiliano Prof: Makame Mbarawa akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akimkaribisha ofisini kwake jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza ambapo baadae viongozi hao walifanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.…
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akimkaribisha ofisini kwake jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza ambapo baadae viongozi hao walifanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Masuala ya Sheria wa Vodacom Tanzania Bw.Walarick Nittu wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania(katikati)akiwa na ujumbe wake walipomtembelea Waziri Prof:Mbarawa na kuwa na mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Mitandao wa Vodacom Tanzania Bw.Alec Mulugo wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania(kulia)akiwa na ujumbe wake walipomtembelea Waziri  wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof: Mbarawa na kuwa na mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo

CHEKA NA KATUNI ZA GPL LEO

visa vya chakunogela
Tembwe
mzee hamnazo…
visa vya chakunogela
Tembwe
mzee hamnazo
skendo kitaani