This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, June 22, 2013

MCHUNGAJI AZAA NA HAUSIGE

Stori:Gladness Mallya na Harun Sanchawa
HAYA ni madai mazito! Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Kijito cha Utakaso au Healing Centre International lililopo Kimara-Mwisho, Dar, Thomas Mariki anadaiwa kuvuliwa kofia ya uchungaji baada ya kutuhumiwa kuzaa na ‘hausigeli’ wake, Sessy Mwambashi.

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa masikitiko, mke wa ndoa wa Mariki, Joyce Thomas Mariki alidai kuwa yeye na mchungaji huyo walioana mwaka 2004 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Lungai Mwika, Moshi.
Alisema walijaliwa kupata watoto watatu lakini mmoja hakuwa bahati.…
Stori:Gladness Mallya na Harun Sanchawa
HAYA ni madai mazito! Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Kijito cha Utakaso au Healing Centre International lililopo Kimara-Mwisho, Dar, Thomas Mariki anadaiwa kuvuliwa kofia ya uchungaji baada ya kutuhumiwa kuzaa na ‘hausigeli’ wake, Sessy Mwambashi.

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa masikitiko, mke wa ndoa wa Mariki, Joyce Thomas Mariki alidai kuwa yeye na mchungaji huyo walioana mwaka 2004 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Lungai Mwika, Moshi.
Alisema walijaliwa kupata watoto watatu lakini mmoja hakuwa bahati.
MATESO YAANZA
Mwanamke huyo alidai amani katika ndoa yake ilipotea baada ya kujifungua mtoto wa pili (marehemu), mumewe alianza kumtuhumu kuwa alitoka nje ya ndoa na huyo mtoto hakuwa wake.
Aliendelea kudai kuwa, mtoto alipofikisha mwaka mmoja na miezi nane, walishauriana watafute hausigeli ili mama huyo afanye biashara ya kuwaongezea kipato.
Mama mchungaji alisema alimpata Sessy akiwa na miaka 15, mkazi wa Mbozi, Mkoa wa Mbeya.
Alisema yeye alianza biashara ya genge maeneo ya Kimara-Mwisho ambapo alikuwa akiwahi sokoni saa 11:00 alfajiri na kumwacha msichana huyo akiendelea na kazi za nyumbani.

VISA VYAANZA
Mama mchungaji aliendelea kudai: Baada ya miezi michache, mchungaji alibadilika tabia, alikuwa mkali, wakati mwingine alinifuata sokoni na kunipiga akinishutumu nina uhusiano na wanaume ndiyo maana nachelewa kurudi nyumbani.

MUMEWE AMFICHULIA SIRI
Akadai: “Siku moja mchungaji alinifichulia siri kuwa hausigeli wetu ni mjamzito na mimba ilikuwa yake hivyo akataka iwe siri kati yetu watatu.”
Mama Mariki alisema alikubaliana na mumewe ambapo alivumilia kwa kipindi kirefu lakini uzalendo ulimshinda baada ya msichana huyo kuwa na tabia ya kuwatesa watoto huku akisema aachwe kwani ni mjamzito.

MKE NAYE AFICHUA SIRI
Alisema kuwa baada ya kuona mumewe anamjali zaidi hausigeli kuliko yeye na watoto aliamua kwenda kutoa siri kwa wasimamizi wa ndoa, wakaitwa na kusuluhishwa ambapo waliamua kuwa msichana huyo arudishwe nyumbani kwao Mbeya jambo ambalo mtumishi huyo wa Mungu alilitekeleza, yeye mwenyewe alimrudisha msichana huyo kwao.

NDOA YATIBUKA
Mwanamke huyo alidai mumewe huyo aliporudi Dar, alianza visa akisema kuwa hausigeli alikuwa akimpa ‘mambo’ kuliko yeye ambaye amezeeka huku vitisho na vipigo vikiongezeka maradufu!
“Wasimamizi wa ndoa walituita kwa mara nyingine wakatusuluhisha lakini tulipofika nyumbani, mateso yakawa palepale ndipo wasimamizi waliponiambia nirudi kwa wazazi wangu kwani ni aibu kubwa kwa mtumishi wa Mungu kufanya vile,” alisema na kuongeza:
“Kweli nilirudi kwetu Moshi, wazazi wangu walimpigia simu mume wangu kuhusu matatizo yetu, lakini aliwajibu hanitaki na ataniletea talaka nyumbani.”
Alisema miezi mitatu baadaye, wasimamizi wa ndoa walimtaka arudi Dar kwa ajili ya kujua hatima ya ndoa yake.
Aliambatana na kaka yake hadi nyumbani kwa mumewe, cha ajabu walimkuta hausigeli akiwa na mtoto mchanga. Aliwazuia kuingia ndani akidai hawakuwa na mamlaka hayo.
Alisema kaka yake alimtaka hausigeli ampigie simu mchungaji amwambie shemeji yake anamhitaji, alifanya hivyo na mchungaji alifika lakini alipowaona alitoka nduki.

WAZEE WA KANISA WAINGILIA KATI
Aliendelea kudai kuwa ulifika wakati wazee wa kanisa waliingilia kati, wakamuweka mchungaji kikao na kumuuliza kulikoni hawamuoni mke nyumbani badala yake  msichana wa kazi tena akiwa na kichanga.
“Cha kushangaza mchungaji alipandwa na hasira, akawafanyia fujo wazee hao, alimpiga na kiti mzee mmoja ambaye alikuwa msaidizi wake anayeitwa Kisaka na kumjeruhi,” alisema mama mchungaji.
Alisema sakata la kujeruhiwa kwa Kisaka liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Mbezi Kwayusuf na kufunguliwa jalada namba KMR/RB/2125/2013- SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.

AVULIWA UCHUNGAJI
Alisema katika kikao hicho, wazee hao walifikia uamuzi wa kumvua rasmi uchungaji kwa kumwandikia barua na kumkabidhi.
Mchungaji aliipokea barua hiyo lakini hadi sasa anaendelea na huduma kwani wapo waumini wachache walio upande wake huku wengine wakidaiwa kulikimbia kanisa hilo.

BOFYA HAPA UMSIKIE MCHUNGAJI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, Juni 18, mwaka huu, mapaparazi wetu walimtafuta Mchungaji Mariki na kufanikiwa kumkuta nyumbani kwake Kimara-Mwisho ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Siwezi kuzungumzia lolote kuhusu habari alizosema mke wangu kwa sababu suala hili lipo kwenye Baraza la Usuluhishi wa Ndoa na lipo kwa maandishi, naweza kuwaambia kuwa kuna watu wanataka kunipindua, wanapanga hila na njama ili walichukue kanisa na ndiyo wanamtumia mke wangu lakini hawawezi, wameshindwa.
“Kuhusu kuzaa na hausigeli wangu ni kweli na mtoto ana miezi saba sasa, lakini hizo shutuma kwamba alikuwa na miaka 15 siyo kweli, alikuwa na miaka 17 na sasa ana miaka hiyohiyo.”

HAUSIGELI VIPI?
Risasi Jumamosi lilizungumza pia na hausigeli ambaye anaishi na mchungaji huyo kwa sasa kama mke ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Anayesema nilikuwa na miaka 15 ana ushahidi? Wanaoweza kujua umri wangu ni wazazi wangu na ukweli ni kwamba mwezi wa kumi mwaka huu natimiza miaka kumi na nane.
“Kuhusu kwamba nilikuja kufanya nini Dar, nilikuja kwa mume wangu mwenye ushahidi kuwa nilimfukukuza mke wake alipokuja nyumbani aniletee.”
Hata hivyo, Risasi Jumamosi linaendelea kufuatilia sakata hili ili kukujuza nini hatima yake.

SHOW YA MIAKA 13 YA KIKOSI CHA MIZINGA JANA VIWANJA VYA MSASANI CLUB DAR

Mashabiki wakiwa mzukaa mbaya
Chidi Benz akifanaya yake
Ilikuwa aibu Babu…
Mashabiki wakiwa mzukaa mbaya
Chidi Benz akifanaya yake
Ilikuwa aibu Babu
hayaaaa
afande Sele akikinukisha kwa hisia stegini
Mashabiki waki enjoy show ya miaka 13 ya kikosi cha mizinga
Songa akiwa kwa steji akifanya yake
Kalapina akifanya mambo kwenye stegi
Tabla akifanya yake kwa steji            Mashuati kwenye stage wakionyesha ujuzi wa karate raha kwelii                       Haya sasa Man 2 Man Battle nichane nikupasue                             Ohhh usiogope jamaa hapigwiiii ila ni mizuka ya battle man 2 man
Kundi la Kiokosi cha Mizinga limefanya show ya kutimiza miaka 13 tangu lianzishwe
Show hiyo iliyo hudhuliwa na mashabiki kibao wa hip hop wa Jijini Dar es salaam.
Onyesho hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudhuliwa na wasanii wa muda mrefu sana waliopotea katika mziki huo wakiwemo Member wa Kundi la Wateule,Mark 2 Be aka Simba wa kundi la Big Dogg Poz

CHEKA NA KATUNI ZA GPL LEO

CHEKA UONGEZE SIKU
ZAMANI MPAKA SIKU HIZI
CHEKA MPAKA BASI
TEMBWE
MZEE…
CHEKA UONGEZE SIKU
ZAMANI MPAKA SIKU HIZI
CHEKA MPAKA BASI
TEMBWE
MZEE HAMNAZO
KATAFUNUA
CHEKA MPAKA BASI
SKENDO KITAANI

REDD'S MISS KINONDONI 2013 APATIKANA

Redd's Miss Kinondoni 2013, Lucy Tomeka (katikati), akiwa kwenye pozi la pamoja na warembo wenzake walioingia kwenye Tatu Bora.

Lucy akikabidhiwa taji hilo na Miss Kinondoni wa mwaka uliopita.
Warembo walioingia…
Redd's Miss Kinondoni 2013, Lucy Tomeka (katikati), akiwa kwenye pozi la pamoja na warembo wenzake walioingia kwenye Tatu Bora.
Lucy akikabidhiwa taji hilo na Miss Kinondoni wa mwaka uliopita.
Warembo walioingia kwenye Tano Bora wakiwa katika pozi la pamoja muda mfupi baada ya kutajwa kwenye nafasi hiyo.
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchakato mzima ulivyokuwa ukiendelea.
USIKU wa kuamkia leo kulifanyika Shindano la kumsaka mrimbwende wa Kinondoni, ambapo Lucy Tomeka, aliwamwaga warembo 11 na kuibuka kidedea, huku nafasi ya pili ikitua mikononi mwa  Prisca Clement na Philious  Lemi akifunga pazia la Tatu Bora itakayojiunga katika kambi ya Taifa ya kumsaka Miss Tanzania 2013/2014.
Nafasi ya nne katika kinyang’anyilo hicho ilichukuliwa na  Sarah Paul huku Tano Bora ikihitimishwa na Linda Joseph.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

NCHI IMEVAMIWA


Stori:Mwandishi wetu

Taifa linapepesuka, linayumbishwa na adui asiyeonekana, anayesababisha kizaazaa kisha yeye kukaa pembeni akiwaacha Watanzania wao kwa wao wakinyoosheana vidole kutuhumiana kuhusika.

IGP Saidi Mwema
Adui huyo ameivamia Tanzania na ndiye inafaa awe mtuhumiwa nambari moja wa bomu lililolipuliwa Soweto, Arusha, katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani, Jumamosi ya wiki iliyopita.

Jinsi nchi…
Stori:Mwandishi wetu
Taifa linapepesuka, linayumbishwa na adui asiyeonekana, anayesababisha kizaazaa kisha yeye kukaa pembeni akiwaacha Watanzania wao kwa wao wakinyoosheana vidole kutuhumiana kuhusika.

IGP Saidi Mwema
Adui huyo ameivamia Tanzania na ndiye inafaa awe mtuhumiwa nambari moja wa bomu lililolipuliwa Soweto, Arusha, katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani, Jumamosi ya wiki iliyopita.
Jinsi nchi inavyopepesuka kwa sasa, ni ishara ya mafanikio ya adui huyo ambaye lengo la uvamizi wake na harakati zake za kutibua amani ya nchi kuona Watanzania wao kwa wao wanashikana mashati, badala ya kuzingatia masuala muhimu yanayohitaji mshikamano wa kitaifa.
Namna Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chadema, vinavyotuhumiana kuhusika na ulipuaji wa bomu hilo ambalo imeshaelezwa kusababisha vifo vya watu wanne, ni ushindi kwa adui huyo mwenye shabaha ya kutenda tukio kiuchochezi na kuzigeuza fikra za watu kutuhumu wasiohusika.
“Tuache kufikiria haya mambo kisiasa, tuyatafakari katika sura yenye hoja mahususi, utaona kwamba siyo CCM wala Chadema wanaohusika na ulipuaji wa bomu Arusha,” alisema Job Ngarano, mkazi wa Arusha, aliyejitambulisha kuwa msomi wa shahada ya kwanza ya Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa.

NANI KALIPUA BOMU?
Ripoti ya uchunguzi wa gazeti hili, iliyokusanya taarifa za eneo la tukio na mambo mengine ya pembeni kuhusiana na bomu la Arusha, imebaini kuwa siyo Chadema wala CCM, mwenye uhakika na tuhuma dhidi ya mwenzake.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alishatoa kauli yenye kudai kuwa anao mkanda wa video unaoonesha namna tukio lilivyotendeka na akasisitiza kuwa mlipuaji ni askari polisi aliyekuwa amevalia sare za kikosi cha kutuliza ghasia (FFU).
Upande mwingine, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alirusha kombora kwamba Chadema ndiyo wahusika wa bomu hilo.
Tuhuma za Nape, zinaendana na dhana kuwa Chadema walijilipua wenyewe kwa lengo la kutafuta huruma ya wapiga kura ili wakichague chenyewe katika uchaguzi mdogo wa udiwani, uliofanyika Juni 16, mwaka huu.
Uchunguzi unapingana na dhana hiyo kwa hoja kwamba Chadema kilikuwa na nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika uchaguzi huo bila hata kusaka huruma ya wapiga kura, kutokana na jinsi kilivyokuwa kinakubalika.
 Macho yanayoona mbali aliyonayo Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ndiyo yaliyomuongoza pale alipowataka wanasiasa kukaa kimya na kuacha mamlaka zinazohusika kufanya kazi yake.
“Natoa rambirambi zangu na kulaani. Naamini katika mambo haya ni vyema wanasiasa tukafunga midomo yetu hadi ukweli ujulikane,” January, aliandika ujumbe huo kuhusiana na tukio la Arusha, kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Wakati January akiwataka watu kutulia na kuacha kusemasema, Noel Kyaro ambaye ni mwongozaji wa watalii (tour guider) Arusha, alisema kuwa kama Chadema na CCM, watakaa pamoja na kuacha kutuhumiana, wanaweza kumpata kwa urahisi mhusika wa mabomu.
“Kuna changamoto nzito hapa, inabidi pia tuangalie uhusiano wa nchi yetu na mataifa mengine. Tanzania inaonewa wivu sana kutokana na uimara wake wa vivutio vya utalii,” alisema Kyaro na kuongeza:
“Hivi karibuni Rais wa Rwanda, Paul Kagame, alitoa kauli chafu sana dhidi ya Rais Jakaya Kikwete. Sasa haishindikani Rwanda kufanya huo ugaidi kwa sababu wameonesha waziwazi kupitia kwa rais wao kuwa hawatupendi.”
Rwanda inapotajwa, moja kwa moja kikundi cha waasi cha chini DRC cha M23, kinaingizwa katika skendo hiyo kwa sababu haijapita muda mrefu tangu nacho kiutangazie ulimwengu kuwa kitapambana na Tanzania.
Mei 5, mwaka huu (Jumapili), saa 4:30 asubuhi, bomu lilirushwa kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi zaidi ya 40.
Siku moja kabla, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alitoa tamko la serikali kuwa Tanzania lazima ipeleke majeshi DRC kupigania amani na haitishwi na vitisho vya waasi wa M23.
Kauli ya Membe, ilifuatia waraka wa M23 ambao waliutuma nchini, wakieleza kuwa ni ujumbe kutoka kwa Mungu, wakiionya Tanzania kutopeleka majeshi DRC, vinginevyo itakiona cha moto.
Baada ya kauli hiyo ya Membe, M23 walihamishia mashambulizi yao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, wakiitishia Tanzania.
Baadhi ya ‘twiti’ za M23, siku moja kabla ya bomu la kanisani Arusha, mojawapo ilisema: “Membe usiwadanganye watu, mnakuja DRC kuweka petroli kwenye moto, hamji kutafuta amani.”
Twiti nyingine inasomeka: “Hatutishwi na scout (askari chipukizi), Tanzania leteni majeshi yenu halafu mtaona.”
Hatari kubwa zaidi ni kwamba M23, walitishia kuingia nchini na kufanya mashambulizi, wakitamba wana uwezo mkubwa sana wa kufanya hivyo.
Kutokana na hatari hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ‘alitwiti’, akionya kwamba M23 walikuwa ‘wanatwiti’ wakiwa Dar es Salaam, hivyo ni dhahiri kuwa kundi hilo lilikuwa limeshaingia nchini.
Kauli hiyo ya Zitto, ilikuwa inaweka wazi namna taifa letu lilivyo hatarini, kwani maadui wanaweza kuingia nchini na kupanga mashambulizi dhidi yetu bila sisi wenyewe kujua.
“Kabla ya kurushiana makombora na kutuhumiana bila ushahidi ni bora tukaangalia uhusiano wa nchi yetu na mataifa mengine. Nchi majirani zetu hazitupendi, wanatuonea wivu, hawashindwi kupanga njama za kutuchonganisha sisi kwa sisi,” alisema Matilda Urio wa Kijenge Chini, Arusha na kuongeza:
“Hatutamjua adui, hatutapata ufumbuzi wa haya matatizo mpaka tutakapoacha kutuhumiana sisi kwa sisi. Chadema waache kuwalaumu CCM kuwa wanahusika, vilevile CCM wasiituhumu Chadema. Tuhuma hizo zinapoteza uelekeo wa kumjua adui.”
Mtumiaji wa Twitter mwenye akaunti yenye jina @iAlen, aliandika ujumbe wake kwa Lugha ya Kiingereza; This Chadema CCM blame game isn’t going to help anyone. People have lost their lives here folks (Huu mchezo wa kulaumiana CCM na Chadema hautamsaidia yeyote. Watu wamepoteza maisha).

KWA NINI
NI WATU WA NJE?
Kwa mujibu wa watu waliozungumza na gazeti hili ambao wanalitazama tukio la Arusha kwa jicho la mbali zaidi ni kwamba sura ya nchi kiutalii ndiyo inayosababisha jiji hilo likumbwe na misukosuko ya milipuko ya mabomu.
“Unalengwa utalii wetu, majirani wanataka Tanzania ionekane ina machafuko ili watalii wawe wanaenda kwenye nchi zao,” alisema Rachel Komba ambaye ni Meneja Uhusiano wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya OTSG.
Rachel alisema: “Jinsi tunavyogombana ni sawa na mgonjwa wa kifafa halafu arogwe ugonjwa wa malaria ya kichwa, akianguka, kila mtu atajua kifafa ndicho kimemfanya aanguke.
“Tanzania kuna udini, kuna mvutano mkubwa wa kisiasa kati ya CCM na Chadema. Bomu likitupwa kanisani, haraka sana Wakristo wanawatuhumu Waislamu, vilevile bomu likitupwa kwenye mkutano wa Chadema, wafuasi wa Chadema watawatuhumu CCM.
“Tuliona jinsi bomu la kanisani Arusha lilivyoleta sintofahamu, vilevile hili la mkutano wa Chadema, linavyowagombanisha CCM na Chadema. Kuna adui wa nje anayewachonganisha Watanzania.
“Anafanya makusudi kwa kutumia udhaifu wetu. Anajua tuna udini, anapiga upande mmoja halafu Waislamu na Wakristo wanakamatana, amepiga mkutano wa Chadema, tunaona hali ilivyo.”
Rachel aliongeza: “Inakuwa vigumu kuwajua hawa maadui kwa sababu wanatupiga kwa kutuchonganisha. Kama wangelipua reli au bandari, moja kwa moja tungejua ni wavamizi kutoka nje. Tatizo wanapiga makanisa, misikiti na mikutano ya vyama vya siasa ndiyo maana inatuchukua wepesi kutuhumiana sisi kwa sisi.”
Elibariki Munishi wa Unga Limited, Arusha, alikumbusha tukio la bomu ambalo alipigwa Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Arusha, Sheikh Abdulkarim Jonjo, akiwa nyumbani kwake na kumjeruhi vibaya.
“Inawezekana kabisa, watu waliomrushia bomu Sheikh Abdulkarim ndiyo haohao waliolishambulia kanisa na ni haohao waliorusha kwenye mkutano wa Chadema. Inabidi tuwe makini sana.
“Tukidanganyika, tunaweza kupigana sisi kwa sisi. Hakuna Muislamu Mtanzania anayeweza kumdhuru Mkristo, vilevile Mkristo hawezi kumdhuru Muislamu kutokana na asili yetu na tunavyojijua,” Elibariki.

LENGO LA NINI?
John Sebless wa Ngarenaro, alisema kuwa lengo la adui ni kuvuruga sura ya utalii wa nchi, hivyo kuyafaidisha mataifa ya kigeni.
“Haya machafuko malengo ya wachafuaji ni kuifanya nchi yetu ionekane siyo salama kwa kupokea watalii. Halafu jiulize kwa nini Arusha ambayo ndiyo mji ambao unaoongoza kwa utalii nchini?
“Tunatakiwa kuacha kulumbana na kusimamia utaifa wetu. Adui kutoka nje anatugawa, tuache kuzingatia mambo ya msingi na matokeo yake tubaki tunalumbana wenyewe. CCM hakiwezi kulipua bomu Chadema kwa sababu viongozi wake wana akili na wanajua kufanya hivyo, wao watakuwa watuhumiwa nambari moja.
“Vilevile haiingii akilini Chadema kujilipua wenyewe. Tuache kulumbana, Wakristo kwa Waislamu, Chadema, CCM na vyama vingine vyote, tunatakiwa tutambue kwamba tumevamiwa kisha tuanze kupambana na adui huyo wa nje anayetaka kuvuruga sifa njema ya nchi yetu kiutalii,” alisema Sebless.
Hata Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, mapema wiki hii, alithubutu kulinyooshea kidole jeshi la polisi, akalitaka kuacha kutumia mabomu kutuliza machafuko, akafafanua kwamba kufanya hivyo kunazidi kuuweka utalii wa nchi katika hali mbaya.

KUTOKA KWA MHARIRI
Tunapaswa kulinda amani yetu ambayo inavutia watalii na wawekezaji wengi kuja nchini. Tuamke sasa na kupambana na adui anayetaka kuivuruga nchi yetu. Bila umoja na mshikamano hatutashinda. Tusikubali kuchochewa kupigana sisi kwa sisi. MHARIRI.

WEMA SEPETU APOTEZA MVUTO....MIKOROGO YAMUATHIRI....MICHIRIZI YAANZA KUPANDA USONI

Matumizi mabaya ya vipodozi yameanza kumuathiri  wema  Sepetu  ambaye  ni  miss Tanzania  2006..
Wema  ambaye umri wake bado  haujamtupa  , hivi  sasa  anakabiriwa na tatizo la  ngozi  kutokana  na michirizi  kusambaa  mwili mzima  hasa  mapajani....
 Kamera  zetu  si  mara  ya  kwanza  kumshuhudia  Mrembo  huyu  akizingirwa  na  uzee  kwani  miezi  kadhaa  nyuma  tuliwahi andika  habari  inayofanana  na  hii  lakini  ikielezea  zaidi  michirizi  ya  mapajani....
Tofauti  na  hivyo, hivi  sasa  michirizi  hiyo   imekimbilia  kifuani  na  mabegani  hali  inayoashiria  kwamba  siku  si  nyingi  itahamia  usoni...
"Ukweli  Wema  Sepetu  sasa  amebaki sura  tu,mwili  umemtupa  kabisa .Nadhani  hii  yote  inatokana  na  matumizi  mabaya  ya  mikorogo"...alisema  shuhuda  mmoja  akimtazama  Wema sepetu  aliyekuwa  jaji  katika  shindano  moja  la  umiss  jijini  Dar

Baada  ya  kumsikia  shuhuda  huyo  akimtoa  kasoro  mrembo  huyo, mwandishi  wetu  alitinga  nyumbani  kwa  Wema  Sepetu  kufanya  naye  mahojiano  juu  ya jambo  hili
Alipofika  nyumbani  hapo, mwandishi  wetu  aligonga  geti  na  kufunguliwa  na  dada  mmoja  ambaye  alidai  kuwa  maadam Wema  alikuwa  amelala  na  kwamba  hawezi  kuamshwa mpaka  aamke  mwenyewe..