Stori:Gladness Mallya na Harun Sanchawa
HAYA
ni madai mazito! Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Kijito cha Utakaso au
Healing Centre International lililopo Kimara-Mwisho, Dar, Thomas Mariki
anadaiwa kuvuliwa kofia ya uchungaji baada ya kutuhumiwa kuzaa na
‘hausigeli’ wake, Sessy Mwambashi.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa masikitiko, mke wa ndoa wa Mariki,
Joyce Thomas Mariki alidai kuwa yeye na mchungaji huyo walioana mwaka
2004 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa
Lungai Mwika, Moshi.
Alisema walijaliwa kupata watoto watatu lakini
mmoja hakuwa bahati.…
Stori:Gladness Mallya na Harun Sanchawa
HAYA
ni madai mazito! Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Kijito cha Utakaso au
Healing Centre International lililopo Kimara-Mwisho, Dar, Thomas Mariki
anadaiwa kuvuliwa kofia ya uchungaji baada ya kutuhumiwa kuzaa na
‘hausigeli’ wake, Sessy Mwambashi.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa masikitiko, mke wa ndoa wa Mariki,
Joyce Thomas Mariki alidai kuwa yeye na mchungaji huyo walioana mwaka
2004 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa
Lungai Mwika, Moshi.
Alisema walijaliwa kupata watoto watatu lakini
mmoja hakuwa bahati.
MATESO YAANZA
Mwanamke huyo alidai
amani katika ndoa yake ilipotea baada ya kujifungua mtoto wa pili
(marehemu), mumewe alianza kumtuhumu kuwa alitoka nje ya ndoa na huyo
mtoto hakuwa wake.
Aliendelea kudai kuwa, mtoto alipofikisha mwaka
mmoja na miezi nane, walishauriana watafute hausigeli ili mama huyo
afanye biashara ya kuwaongezea kipato.
Mama mchungaji alisema
alimpata Sessy akiwa na miaka 15, mkazi wa Mbozi, Mkoa wa Mbeya.
Alisema
yeye alianza biashara ya genge maeneo ya Kimara-Mwisho ambapo alikuwa
akiwahi sokoni saa 11:00 alfajiri na kumwacha msichana huyo akiendelea
na kazi za nyumbani.
VISA VYAANZA
Mama mchungaji aliendelea
kudai: Baada ya miezi michache, mchungaji alibadilika tabia, alikuwa
mkali, wakati mwingine alinifuata sokoni na kunipiga akinishutumu nina
uhusiano na wanaume ndiyo maana nachelewa kurudi nyumbani.
MUMEWE
AMFICHULIA SIRI
Akadai: “Siku moja mchungaji alinifichulia siri kuwa
hausigeli wetu ni mjamzito na mimba ilikuwa yake hivyo akataka iwe siri
kati yetu watatu.”
Mama Mariki alisema alikubaliana na mumewe ambapo
alivumilia kwa kipindi kirefu lakini uzalendo ulimshinda baada ya
msichana huyo kuwa na tabia ya kuwatesa watoto huku akisema aachwe kwani
ni mjamzito.
MKE NAYE AFICHUA SIRI
Alisema kuwa baada ya
kuona mumewe anamjali zaidi hausigeli kuliko yeye na watoto aliamua
kwenda kutoa siri kwa wasimamizi wa ndoa, wakaitwa na kusuluhishwa
ambapo waliamua kuwa msichana huyo arudishwe nyumbani kwao Mbeya jambo
ambalo mtumishi huyo wa Mungu alilitekeleza, yeye mwenyewe alimrudisha
msichana huyo kwao.
NDOA YATIBUKA
Mwanamke huyo alidai mumewe
huyo aliporudi Dar, alianza visa akisema kuwa hausigeli alikuwa akimpa
‘mambo’ kuliko yeye ambaye amezeeka huku vitisho na vipigo vikiongezeka
maradufu!
“Wasimamizi wa ndoa walituita kwa mara nyingine
wakatusuluhisha lakini tulipofika nyumbani, mateso yakawa palepale ndipo
wasimamizi waliponiambia nirudi kwa wazazi wangu kwani ni aibu kubwa
kwa mtumishi wa Mungu kufanya vile,” alisema na kuongeza:
“Kweli
nilirudi kwetu Moshi, wazazi wangu walimpigia simu mume wangu kuhusu
matatizo yetu, lakini aliwajibu hanitaki na ataniletea talaka nyumbani.”
Alisema
miezi mitatu baadaye, wasimamizi wa ndoa walimtaka arudi Dar kwa ajili
ya kujua hatima ya ndoa yake.
Aliambatana na kaka yake hadi nyumbani
kwa mumewe, cha ajabu walimkuta hausigeli akiwa na mtoto mchanga.
Aliwazuia kuingia ndani akidai hawakuwa na mamlaka hayo.
Alisema kaka
yake alimtaka hausigeli ampigie simu mchungaji amwambie shemeji yake
anamhitaji, alifanya hivyo na mchungaji alifika lakini alipowaona
alitoka nduki.
WAZEE WA KANISA WAINGILIA KATI
Aliendelea kudai
kuwa ulifika wakati wazee wa kanisa waliingilia kati, wakamuweka
mchungaji kikao na kumuuliza kulikoni hawamuoni mke nyumbani badala
yake msichana wa kazi tena akiwa na kichanga.
“Cha kushangaza
mchungaji alipandwa na hasira, akawafanyia fujo wazee hao, alimpiga na
kiti mzee mmoja ambaye alikuwa msaidizi wake anayeitwa Kisaka na
kumjeruhi,” alisema mama mchungaji.
Alisema sakata la kujeruhiwa kwa
Kisaka liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Mbezi Kwayusuf na
kufunguliwa jalada namba KMR/RB/2125/2013- SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.
AVULIWA
UCHUNGAJI
Alisema katika kikao hicho, wazee hao walifikia uamuzi wa
kumvua rasmi uchungaji kwa kumwandikia barua na kumkabidhi.
Mchungaji
aliipokea barua hiyo lakini hadi sasa anaendelea na huduma kwani wapo
waumini wachache walio upande wake huku wengine wakidaiwa kulikimbia
kanisa hilo.
BOFYA HAPA UMSIKIE MCHUNGAJI
Baada ya kuzinyaka
habari hizo, Juni 18, mwaka huu, mapaparazi wetu walimtafuta Mchungaji
Mariki na kufanikiwa kumkuta nyumbani kwake Kimara-Mwisho ambapo alikuwa
na haya ya kusema:
“Siwezi kuzungumzia lolote kuhusu habari
alizosema mke wangu kwa sababu suala hili lipo kwenye Baraza la
Usuluhishi wa Ndoa na lipo kwa maandishi, naweza kuwaambia kuwa kuna
watu wanataka kunipindua, wanapanga hila na njama ili walichukue kanisa
na ndiyo wanamtumia mke wangu lakini hawawezi, wameshindwa.
“Kuhusu
kuzaa na hausigeli wangu ni kweli na mtoto ana miezi saba sasa, lakini
hizo shutuma kwamba alikuwa na miaka 15 siyo kweli, alikuwa na miaka 17
na sasa ana miaka hiyohiyo.”
HAUSIGELI VIPI?
Risasi Jumamosi
lilizungumza pia na hausigeli ambaye anaishi na mchungaji huyo kwa sasa
kama mke ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Anayesema nilikuwa na
miaka 15 ana ushahidi? Wanaoweza kujua umri wangu ni wazazi wangu na
ukweli ni kwamba mwezi wa kumi mwaka huu natimiza miaka kumi na nane.
“Kuhusu
kwamba nilikuja kufanya nini Dar, nilikuja kwa mume wangu mwenye
ushahidi kuwa nilimfukukuza mke wake alipokuja nyumbani aniletee.”
Hata
hivyo, Risasi Jumamosi linaendelea kufuatilia sakata hili ili kukujuza
nini hatima yake.
0 comments:
Post a Comment