This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, August 29, 2013

TRAFIKI FEKI MAZITO TENA!





MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko  Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani, Amani lina mpya hiyo.
Trafiki feki James Hussein akiwa kwenye gari baada ya kunaswa.
Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.
JINA HALISI

Mtoa habari wetu alisema kuwa,…
Na Mwandishi Wetu
MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko  Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani, Amani lina mpya hiyo.
Trafiki feki James Hussein akiwa kwenye gari baada ya kunaswa.
Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.
JINA HALISI
Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.
...Mtuhumiwa huyo akiwa na watuhumiwa wenzake.
“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.
YADAIWA ALIKUWA ASKARI MAGEREZA
Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.

...Akiwa mikononi mwa polisi.
ADAIWA KUNASWA UJAMBAZI, ATUPWA JELA MIAKA 30
Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.
 “Mwaka 2002 mpaka 2003, Kinanda alipata kesi ya ujambazi akiwa na wenzake, sikumbuki idadi yao. Kesi iliisha kwa hukumu ya miaka 30 jela kwenye Gereza la Isanga hapa Dodoma,” alisema mnyetishaji huyo.
“Akiwa gerezani, Kinanda alionekana mtiifu kiasi kwamba alipewa cheo cha kusimamia wenzake, yaani mnyapara wakiamini anaendelea vizuri na kifungo chake hicho.
Trafiki feki katika pozi baada ya kudakwa.
“Hakuna aliyejua kama jamaa anaweza kutoroka. Ama kweli moyo wa mtu anaujua mwenyewe. Hivi hapa (Gereza la Isanga) wafungwa wenzake wameshangaa kusikia jamaa amekuwa trafiki huko Dar es Salaam,” kilidai chanzo.
ADAIWA KUTOROKA JELA
Habari zaidi ziliendelea kudai kwamba, Desemba 10, 2012 akiwa gerezani, mfungwa huyo alitoroka katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya uangalizi wa askari magereza aliyejulikana kwa jina moja la Shaibu.
Ilidaiwa kuwa, baada ya picha yake kuonekana kwenye gazeti, askari magereza wa Isanga waliutaarifu uongozi mara moja ambapo nao ulituma wachunguzi  jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumtia mikononi mfungwa huyo ili akamalizie kifungo chake cha miaka thelathini jela.
Inadaiwa kuwa, wachunguzi hao ambao ni askari magereza  wapo Dar wakisubiri siku ya kesi ya kujifanya trafiki itakapopelekwa kusikilizwa kwa hakimu.

HABARI MPYA, ADAIWA KUFARIKI DUNIA SEGEREA, DAR
Wakati mnyetishaji wetu kutoka gerezani Isanga Dodoma akianika madai ya siri hiyo nzito, Agosti 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mwandishi Wetu, Makongoro Oging’  alipata taarifa kuwa, mtuhumiwa huyo wa kutenda kosa la kujifanya trafiki amefariki dunia ghafla akiwa gerezani Segerea.
Ilibidi mwandishi wetu amtafute Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Mtiga Omar na kumuuliza kuhusu madai hayo ya kifo ambapo alisema:
“Si kweli kwamba amekufa, bali ana tuhuma nyingine ya kutoroka gerezani ambapo tutamfungulia mashitaka mengine  ya kutoroka akiwa gerezani anatumikia kifungo chake.”
Juhudi za kumpata Mkuu wa Gereza la Isanga, Dodoma zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
James Hussein kama ndiye Ali Kinanda yupo Gereza la Segerea, hadi Septemba 5, 2013 kesi yake itakaporudi tena mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde kwa ajili ya kusikilizwa.

MTOTO MIAKA 7 ALEA FAMILIA

Na Imelda Mtema

WAZAZI ambao hawajajulikana walikotokomea wamewatelekeza watoto wao wanne wanaoishi Kata ya Bangulo, Pugu, Ilala, jijini Dar es Salaam, Amani lina mkasa wote.

Mazigira ya nyumba ya watoto hao ni ya kutoa machozi hata kwa mtu mwenye roho ngumu kama jiwe. Nyumba iko hivyo, pa kulala ni chini, wadudu kibao huku wakiwa hawajui hatima yao.

Majirani ndiyo waliowaibua watoto hao baada ya kubaini kuwa baba yao hajaonekana kwa miezi kadhaa nyumbani hapo hali iliyosababisha wengine kulia.

Akizungumza na paparazi wetu juzikati,  Sarah Shija (7) ambaye ndiye anayelea familia hiyo kwa sasa, aliwataja wenzake, Kevin Shija (8), Babu Shija (5) na Brighton Shija (6).

Alisema  mama yao mzazi aliondoka nyumbani hapo miaka miwili iliyopita baada ya kutokea mzozo kati yake na…
Na Imelda Mtema
WAZAZI ambao hawajajulikana walikotokomea wamewatelekeza watoto wao wanne wanaoishi Kata ya Bangulo, Pugu, Ilala, jijini Dar es Salaam, Amani lina mkasa wote.
Mazigira ya nyumba ya watoto hao ni ya kutoa machozi hata kwa mtu mwenye roho ngumu kama jiwe. Nyumba iko hivyo, pa kulala ni chini, wadudu kibao huku wakiwa hawajui hatima yao.
Majirani ndiyo waliowaibua watoto hao baada ya kubaini kuwa baba yao hajaonekana kwa miezi kadhaa nyumbani hapo hali iliyosababisha wengine kulia.
Akizungumza na paparazi wetu juzikati,  Sarah Shija (7) ambaye ndiye anayelea familia hiyo kwa sasa, aliwataja wenzake, Kevin Shija (8), Babu Shija (5) na Brighton Shija (6).
Alisema  mama yao mzazi aliondoka nyumbani hapo miaka miwili iliyopita baada ya kutokea mzozo kati yake na baba yao na kwenda kusikojulikana licha ya kwamba siku hiyo walimsihi sana mama huyo asiondoke.
Sarah aliendelea kuweka wazi kuwa, baada ya mama yao kuingia mitini, baba yao ndiyo akawa kila kitu lakini kumbe  na yeye alikuwa na lake moyoni.
Alisema miezi minne iliyopita, asubuhi baba yao aliamka asubuhi na kuwaachia shilingi 5,000 na kiasi kidogo cha unga kwenye kiroba na kuondoka akisema angerudi jioni.
“Mara ya mwisho baba alipoondoka alituambia angerudi jioni, akatuachia shilingi elfu tano kwa ajili ya kununua mboga na vitu vingine,” alisema Sarah.
Sarah alisema tangu siku hiyo baba yao  hakurudi tena huku wao wakiwa wamebaki wenyewe na elfu tano aliyowaachia ikiwa imeisha.
Alisema hali hiyo iliwalazimisha kusimama masomo kutokana na ugumu wa maisha kwa sababu mara nyingi wanaamka asubuhi wakiwa na njaa hivyo kushindwa kuelewa kinachofundishwa na walimu.
“Tunalala na njaa, tunaamka na njaa, tunashinda na njaa sasa tusingeweza kwenda shule kwa sababu tunakuwa tunatetemeka mwili. Hatujui baba atarudi lini,” alisema Sarah na kuangua kilio.
Alisema imefika hatua nduguze wakishikwa na kiu anawapeleka kunywa maji machafu ya kwenye madimbwi ambayo pia yana chumvi kupita kiasi kwa sababu hawana  fedha (shilingi mia nne) ya kununua maji salama.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Sarah alimuomba baba yao  popote alipo kurudi nyumbani na kuendelea na maisha. Pia walimtaka mama yao akisoma habari hii akawachukue kwani maisha yao ni magumu sana na yeye analazimika kufanya shughuli nyingi za nyumbani ili kuhakikisha uhai wao haukatishwi na njaa.
Ili kujua maisha yao zaidi ya kusikitisha usikose kuangalia Kipindi cha Wanawake Live cha Mtangazaji Joyce Kiria ambacho kitaonesha ‘live’ maisha magumu ya watoto hao.

Monday, August 12, 2013

Kaze, Tambwe wazuiwa Burundi

  Beki wa Simba Kaze Gilbert.
Na Khatimu Naheka
NYOTA wapya wawili wa Klabu ya Simba, straika Khamis Tambwe na beki Kaze Gilbert, watachelewa kujiunga na timu hiyo baada ya klabu yao ya Vital’O ya Burundi kuwazuia kwa muda.
Nyota hao tangu waliposaini mikataba Msimbazi na kurejea kwao hawajarudi na juzi hawakuonekana katika Tamasha la Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, licha ya Simba kuwa na utaratibu wa kulitumia kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wake wote kabla ya msimu kuanza.
Awali, wachezaji hao…
Beki wa Simba Kaze Gilbert.
Na Khatimu Naheka
NYOTA wapya wawili wa Klabu ya Simba, straika Khamis Tambwe na beki Kaze Gilbert, watachelewa kujiunga na timu hiyo baada ya klabu yao ya Vital’O ya Burundi kuwazuia kwa muda.
Nyota hao tangu waliposaini mikataba Msimbazi na kurejea kwao hawajarudi na juzi hawakuonekana katika Tamasha la Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, licha ya Simba kuwa na utaratibu wa kulitumia kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wake wote kabla ya msimu kuanza.
Awali, wachezaji hao walitarajiwa kutua nchini mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini haikuwa hivyo, hali iliyowalazimu Simba kuanza kuwafuatilia kwa haraka.
Joseph Itang’are, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Simba, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, nyota hao wameshindwa kuwasili kwa wakati, baada ya klabu yao kuwazuia kwa muda, ikitaka wamalizie michezo iliyobaki ya Ligi Kuu ya Burundi kabla haijaachana nao rasmi.
Itang’are, maarufu kama Mzee Kinesi, alisema vital’O ilikuwa imebakiza michezo miwili, mmoja ukichezwa juzi.
Mzee Kinesi alisema Vital’O imepanga kuwapa baraka za kuja Tanzania katikati ya wiki hii, tayari kwa kuanza maisha mapya na Wekundu hao.
“Tulilazimika kuwasiliana nao haraka baada ya kuona kimya, lakini hata klabu yao nayo imeonyesha uungwana wa kutupigia na kutueleza kuwa wachezaji hao ni muhimu sana kwao wakati huu ligi yao ikielekea ukingoni,” alisema Mzee Kinesi.
“Kwa shingo upande ilibidi tuwakubalie kwa kuwa sisi bado hatujaanza ligi ya huku kwetu, ingawa tunajua kuchelewa kwao kunaweza kumchelewesha kocha wetu kutengeneza kikosi chake, tunaamini mpaka kufikia katikati ya wiki ijayo (wiki hii), watakuwa wameshafika nchini.”
Nyota hao wanatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi cha Simba. Tambwe alikuwa mfungaji bora kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni nchini Sudan, wakati Kaze alikuwa mhimili mkubwa katika kikosi chao cha Vital’O kilichotwaa ubingwa wa michuano hiyo.

MASTAA BONGO MVUTO WAO SIYO WA KUMULIKA NA TOCHI!

Je, mvuto, urembo na uzuri ni vitu gani? Ni kweli kwamba uzuri au urembo uko katika mboni ya jicho la mtazamaji au kwenye akili na macho ya binadamu? Ukweli ni kwamba kila mtu ana namna yake ya kutafsiri maneno hayo.
Wema Sepetu.
Staa wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade huwa anamshukuru Mungu kila kukicha kwa kumuumba mzuri na mwenye mvuto. Je, wewe unafanya hivyo?
Katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo kuna mambo mengi ambayo ukurasa huu kama kawaida yake huyatazama na kukuletea wewe msomaji.
Bongo…
Je, mvuto, urembo na uzuri ni vitu gani? Ni kweli kwamba uzuri au urembo uko katika mboni ya jicho la mtazamaji au kwenye akili na macho ya binadamu? Ukweli ni kwamba kila mtu ana namna yake ya kutafsiri maneno hayo.
Wema Sepetu.
Staa wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade huwa anamshukuru Mungu kila kukicha kwa kumuumba mzuri na mwenye mvuto. Je, wewe unafanya hivyo?
Katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo kuna mambo mengi ambayo ukurasa huu kama kawaida yake huyatazama na kukuletea wewe msomaji.
Bongo kuna mastaa wengi wa kike lakini leo tunakudonoleo listi ya warembo kumi ambao mvuto wao si wa kumulika na tochi katika kipindi chote cha umaarufu wao.
http://1.bp.blogspot.com/_uDjCUzboFtk/TL8RBwfIqmI/AAAAAAAADMk/AMZJrYJ0hF0/s1600/n719178379_1193590_9574%5B1%5D.jpg
Nancy Abraham SUMARI
Huyu ni Miss Tanzania na Miss World Africa wa mwaka 2005. Kilichomfanya akatwaa mataji hayo ni mvuto na uzuri alionao ambao hakika Mungu amempendelea. Kwa mwanaume kamili, ukipishana naye huna jinsi ya kukwepesha macho kumtazama. Kuna taarifa kuwa kwa sasa ni mke wa jamaa anayetajwa kwa jina moja la Luca.

Faraja Kota NYALANDU
Ni Miss Tanzania wa mwaka 2004 ambaye alishinda taji hilo kutokana na mvuto aliokuwanao ambao ameendelea ‘kuumeinteini’ hadi leo. Anapaswa kumshukuru Mungu kwa kumuumba ‘kichuna’. Kumbuka kwa sasa ni mke wa ndoa wa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) na Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-LYINN’
Huyu ni Miss Tanzania wa mwaka 2000 na pia mwanamuziki wa Bongo Fleva lakini siku hizi hasikiki. Mvuto na uzuri aliokuwanao bado anao ndiyo uliomfanya kushinda ‘krauni’ hiyo.
Jokate MWEGELO
Ni Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006. Ana ‘taito’ nyingi kama mwigizaji, MC, mtangazaji, mwanamitindo, mwanamuziki na mjasiriamali anayemiliki lebo ya mavazi ya Kidoti. Ni mzuri na ana mvuto wa aina yake unaowanyima wanaume wengi usingizi. Bado hajaolewa.

Hoyce TEMU
Huyu ni Miss Tanzania wa mwaka 1999 ambaye kwa sasa ni Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa kwa hapa Bongo. Ni mwandishi wa Kitabu cha Nayakubali Yote. Anajishughulisha na kusaidia jamii kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kupitia Runinga ya Chanel Ten. Pamoja na kuwa mke wa mtu na mtoto mmoja, bado mvuto wake upo palepale.

Lisa JENSEN
Huyu ni Miss World Tanzania wa mwaka 2012 ambaye pia ni mwigizaji wa filamu za Kibongo. Ukimuona Lisa lazima utakiri kuwa Mungu kamuumba na kweli kaumbika. Bado hajaolewa lakini kwa sasa ana ‘kibendi’.

Wema Isaac SEPETU
Ni Miss Tanzania wa 2006 na mwigizaji wa filamu za Kibongo ambaye anatarajia kuanzisha kipindi chake cha In My Shoes kupitia Clouds TV. Anajiita Beautiful Onyinye akijilinganisha na mrembo anayesifiwa katika wimbo huo ulioimbwa na P-Square kutokana na mvuto wake japo kwa sasa analalamikiwa kujiharibu kwa kujichubua.

Millen MAGESE
Millen au Happiness Magese ni Miss Tanzania wa 2001 ambaye pia ni modo wa kimataifa. Kwa sasa ana makazi nchini Marekani. Bado ukimuona mtoto ‘anaita’ kutokana na mvuto alionao kiasi cha kupamba majarida mbalimbali makubwa nje ya Bongo.

Salha ISRAEL
Huyu ni Miss Tanzania wa mwaka 2011 ambaye hivi karibuni alizama kwenye filamu za Kibongo. Mrembo huyu ana mvuto kiasi kwamba akikatiza lazima wanaume wageuke kukamilisha fahari ya macho.

Vanessa MDEE
Van Vee au Van Money ni Mtangazaji wa Radio Choice FM ya jijini Dar. Pia ni mwanamuziki, alisikika vema kwenye ngoma kama Me and You na Closer. Ni balozi wa vijana Tanzania na hajaolewa. Kuhusu mvuto, Vanessa ni ‘chuma’.

GARI NA BAJAJ ZAGONGANA KINONDONI

Bajaj ilivyogongwa.
Inavyoonekana kwa chini.
Dreva wa Bajaj akilia kwa uchungu.…
Bajaj ilivyogongwa.
Inavyoonekana kwa chini.
Dreva wa Bajaj akilia kwa uchungu.
Wananchi wenye hasira wakimsulubu dereva Suzuki kwa kupita eneo lisilo lake.
Askari akimuokoa dereva  kutoka kwenye kipondo.
.Mashuhuda  wamelizingira gari lililosababisha ajali.
Dereva wa Bajaj akisaidiwa na Wasamaria Wema kupelekwa hospitali.
8.Mmoja wa Wasamaria Wema akimweka vizuri dereva wa Bajaj.
...Akiangalia mkono wake jinsi alivyoumia.
Hiki ni kiatu cha abiria wa Bajaj ambaye hakueleweka alipoelekea baada ya ajali hiyo.
GARI aina ya Suzuki namba SM 4726 mali ya Manispaa ya Kinondoni imegongana uso kwa uso jioni hii na Bajaj yenye namba za usajili T 761 CKR kwenye bonde linalounganisha Kinondoni na Magomeni, Jijini Dar es Salaam.

PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY GPL

MWANAUME AFIA GESTI AKIFANYA MAPENZI NA MPENZI WAKE JIJINI DAR



MFANYABIASHARA wa sokoni Kariakoo jijini Dar ambaye pia ni mkazi wa Kigogo Flesh, Hamad Kiponda (46), amefia nyumba ya kulala wageni akiwa na mpenzi wake Latifa Saidi (25).


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika nyumba hiyo iitwayo Sansiro iliyoko Kiwalani kwa Gude.

 
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo, Latifa alitoa taarifa polisi kwamba mpenzi wake aliishiwa na nguvu ghafla na kuanza kutokwa povu mdomoni wakati wakifanya mapenzi.
 
Minangi alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliomba msaada kwa wahudumu wa gesti hiyo, lakini Kiponda alifariki papo hapo kabla ya kupelekwa hospitali.


Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, wakati mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi huku Latifa akishikiliwa kwa kuhojiwa.
 
Wakati huo huo, moto umezuka ghafla katika nyumba ya Matiku Nestori (43) mkazi wa Tuamoyo Kigamboni, yenye vyumba sita na kuteketeza vyumba vinne pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ambazo bado thamani yake haijajulikana.


Kwa mujibu wa Kamanda Minangi tukio hilo lilitokea juzi saa nane mchana na chanzo cha moto huo inasadikiwa ni hitilafu ya umeme iliyosababisha moto kuanzia kwenye nguzo.

SHEIKH PONDA AWEKWA CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI.....JUMUIYA YA KIISLAM YATOA MASHARTI KWA SERIKALI



Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda yupo chini ya ulinzi huku akitibiwa majeraha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 


Sheikh Ponda alisafirishwa usiku wa manane kutoka Morogoro baada ya juzi kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni mtutu wa bomu saa 12:25 jioni alipokuwa akisindikizwa na wafuasi wake kwenda katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano mjini hapo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema, alidai kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi tatu begani.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Ponda zilisema kwamba baada ya kupata taarifa za kupigwa risasi, baadhi ya masheikh walifunga safari kwenda Morogoro na kumrejesha Dar es Salaam usiku huohuo. 



Kabla ya kurudishwa Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Sheikh Ponda alipelekwa katika Zahanati ya Islamic Foundation.
 

Mmoja wa wanafamilia alidokeza kwamba Sheikh Ponda alifichwa na alikuwa chini ya ulinzi mkali wa wafuasi wake na hakuna aliyeruhusiwa kumsogelea.

 

Muhimbili

Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa alifikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 

Sheikh Ponda alifikishwa Muhimbili jana saa 7:18 mchana na alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa wa dharura na baadaye alitolewa na kupelekwa kwenye chumba cha x-ray kwa ajili ya vipimo. Baadaye alipelekwa chumba cha upasuaji.

 

Eneo kubwa la hospitali hiyo lilikuwa na idadi kubwa ya askari na mmoja wa askari waliokuwa doria hospitalini hapo alisema walitawanywa kwenye hospitali mbalimbali za Dar es Salaam baada ya kupata taarifa kuwa angeletwa kwa matibabu.


“Nakuambia tuko hapa tangu saa kumi na moja asubuhi, tumetawanywa hospitali mbalimbali baada ya kupata taarifa kuwa analetwa Dar. Bahati nzuri kaletwa hapa Muhimbili... tunasubiri apate matibabu na tutamtia mbaroni,” alisema askari huyo.
 

Taarifa ya polisi

Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema jana katika taarifa yake kuwa Sheikh Ponda yuko Hospitali ya Muhimbili akitibiwa baada ya kupata majeraha yaliyotokana na purukushani na polisi wakati wafuasi wake walipokuwa wanataka kumtorosha.

“Kutokana na tukio hilo, timu inayoshirikisha wajumbe kutoka Jukwaa la Haki Jinai likiongozwa na Kamishna wa Polisi Isaya Mungulu imeanza uchunguzi wa tukio hilo na Polisi inawataka wananchi kuwa watulivu wakati wanashughulikia suala hilo kisheria.”

 
Polisi Morogoro wapigwa chenga
Wakati akiwa Muhimbili, Polisi mkoani Morogoro, lilisema bado linamtafuta Sheikh Ponda.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alisema jana kuwa kwa taarifa zilizopo, bado Sheikh Ponda amefichwa mkoani Morogoro na kwamba anaendelea kutafutwa.
 
“Tamko la Serikali mpaka sasa hatujathibitisha kwamba Sheikh Ponda amejeruhiwa na risasi na tunamtaka mtu yeyote awe yeye au ndugu yake aje kuthibitisha kwamba amepigwa risasi,” alisema.
 
Alikanusha madai kwamba jeshi hilo limehusika kumpiga risasi akisema hakuna ushahidi kwa kuwa hajaonekana ili kuonyesha kuwa amepata majeraha sehemu yoyote ya mwili wake.

 
“Siku zote risasi haifichiki, kama amepigwa angejitokeza ili kupewa kibali cha matibabu,” alisema Shilogile.
Alisema polisi inawashikilia watu wawili na inawatafuta viongozi watano wa Umoja wa Waadhiri wa Kiislamu Mkoa wa Morogoro walioandaa kongamano hilo.

 
Kamanda Shilogile alisema waandaaji wa kongamano hilo walipewa kibali na polisi kufanya kongamano kwa masharti ya kutokutoa matamshi ya uchochezi ikiwa ni pamoja na Sheikh Ponda kutokuhudhuria.

 
Alisema hata hivyo, katika kongamano hilo lililofanyika eneo la Kiwanja cha Ndege kulikuwapo na wageni zaidi ya watano waliohutubia. 


Kamanda Shilogile alisema ilipofika saa 12.50 jioni ndipo Sheikh Ponda alipofika na baadaye kupewa dakika tano kuzungumza na alieleza kuwa yeye si mzungumzaji kwa siku hiyo na badala yake angezungumza leo katika Viwanja vya Msikiti wa Jabal Hirra.
 
Alisema baada ya hapo mkutano ulifungwa na wafuasi wake wakaanza kusukuma gari alilokuwa amepanda katika Barabara ya Tumbaku karibu na Kituo cha Mafuta cha El Saedy. 



Alisema kuwa, polisi walimfuata kutaka kumtia mbaroni lakini wafuasi wake walianza kurusha mawe na ndipo askari hao walipofyatua juu risasi tatu za baridi ili kuwatawanya.
Hata hivyo, alisema polisi walizidiwa nguvu na wafuasi hao ambao walifanikiwa kumtorosha Sheikh huyo kwa pikipiki.Alisema kuwa baadaye zilizagaa taarifa kuwa amepigwa risasi ya begani na kupelekwa Hospitali ya Mkoa kisha kutoroshwa kusikojulikana.

Wavamia hospitali
Katika hatua nyingine, watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa Sheikh Ponda wamevamia Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na kufanya uharibifu kwa kuvunja vioo katika wodi namba sita ya watoto wakishinikiza kuonyeshwa Sheikh huyo alipo.
Baadhi ya wagonjwa waliolazwa na watoto wao katika wodi hiyo, Kibua Michael na Cecilia Clemence kwa nyakati tofauti walisema kwamba wafuasi hao walikusanyana nje ya hospitali hiyo na kurusha mawe na kusababisha taharuki kwa baadhi ya wagonjwa.
Sheikh Kundecha atoa sharti
Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, imeitaka Serikali kuunda tume huru ya uchunguzi wa tukio la kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda na majibu yake ndiyo yatakayoamua uhusiano baina ya Waislamu nchini na Serikali iliyopo madarakani.

 
Akitoa tamko la Jumuiya hiyo katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni, Dar es Salaam jana, Amiri wa Jumuiya hiyo, Sheikh Yusufu Mussa Kundecha alisema pamoja na mambo mengine, pia wanataka kuona askari polisi aliyemdhuru Sheikh Ponda anachukuliwa hatua za kisheria.
Alisema kitendo alichofanyiwa Sheikh Ponda ni mtiririko wa vitendo vya uonevu na unyanyasaji na aliishangaa Serikali kumtafuta Sheikh huyo kupitia vyombo vya habari wakati inafahamu hatua za kuchukua pale wanapokuwa wanamtafuta mtu.
Alisema hata yeye wakati anatafutwa na polisi alipelekewa barua akitakiwa kuripoti kituoni lakini si kupitia vyombo vya habari na kitendo hicho kinaonyesha wazi kuwa Serikali imeshindwa kuwahakikishia raia usalama wao.

 
“Mbaya zaidi, wao ambao wanataka watu wasichukue sheria mkononi ndiyo hao wa kwanza kufanya hivyo jambo ambalo sidhani kama litatufikisha pazuri,” alisema Kundecha.

 
Aliitaka Serikali kufuata sheria na kufuata taratibu husika katika kushughulikia masuala yanayowahusu makundi mbalimbali katika jamii badala ya inavyofanya sasa akisema hiyo inachangia chuki kati ya Waislamu na Serikali.

 
Profesa Lipumba atoa tamko
Mwenyekiti wa (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati suala la kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda ili nchi isije kuingia kwenye machafuko yenye mrengo wa kidini.

Profesa Lipumba aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake Dar es Salaam kuwa chama hicho kinalaani vikali tukio hilo na kutaka polisi kuwakamata waliompiga risasi.

 
“Nimetoka kumjulia hali muda mfupi uliopita, nimemkuta akiwa katika hali mbaya japo anaweza kuzungumza na kutambua watu wanaokwenda kumwona... kwa kweli tukio la kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda linaweza kusababisha nchi kuingia kwenye machafuko ya kidini kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

 
“Tukio la Sheikh Ponda kupigwa risasi tena na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi, limeleta sura mbaya kwa taifa,” alisema Lipumba.

 
Rufaa ya wafuasi wake leo
Wakati hayo yakitokea, rufaa ya wafuasi 52 wa Sheikh Ponda waliohukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela inatarajiwa kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

 
Wafuasi hao walihukumiwa kifungo hicho, Machi 21, mwaka huu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutiwa hatiani kwa makosa matatu kati ya manne yaliyokuwa yakiwakabili.

 
Walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama, kutenda makosa, kukaidi amri ya polisi kabla na baada ya kufanya maandamano yaliyozuiwa na polisi, kufanya mikusanyiko haramu na kusababisha uvunjifu wa amani na uchochezi.

 
Hata hivyo, kupitia kwa Wakili wao, Mohamed Tibanyendera walikata rufaa wakipinga hukumu na adhabu waliyopewa.


Rufaa hiyo itasikilizwa leo na Jaji Salvatory Bongole.
Kwa mujibu wa hati ya rufani waliyoiwasilisha mahakamani hapo, wafuasi hao, pamoja na mambo mengine, wanadai kuwa hakimu alikosea kisheria katika kuchambua ushahidi wa pande zote uliowasilishwa mahakamani.

 
Pia wanadai kuwa katika hukumu hiyo, hakimu alijikanganya kwa kumwachia huru mmoja wa washtakiwa na kuwatia hatiani washtakiwa wengine.

 
Watu hao walikamatwa na Polisi Machi 15, mwaka huu, wakiandamana kwenda Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa lengo la kumshinikiza kumpa dhamana Sheikh Ponda na mshtakiwa mwenzake Mukadam Swalehe na Machi 18, mwaka huu walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka.

NEY WA MITEGO


 
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego, ameweka wazi kuwa ikitokea amefariki dunia hatohitaji kamati kwa ajili ya kuendesha mipango ya msiba wake, kwa kile anachodai kuwa kamati hizo zipo kwa ajili ya kuvuna pesa.

Hayo aliweka wazi baada kupokea ujumbe mfupi kwenye simu yake wenye vitisho uliotokana na mashairi alioimba kwenye single yake mpya ya 'Salaam zao' .

Ujumbe huo wa vitisho ambao umepokelewa na msanii huyo umekuja mara baada ya msanii huyo kuachia single yake hiyo ambapo moja ya mashahiri ni juu ya hela za rambirambi zilizopatikana katika msiba wa msanii Ngwear pamoja na Kanumba kushindwa kuwafikia walengwa.

Akizungumza na jarida la Maisha, mara baada ya kutuma ujumbe alioupokea wa vitisho kwenye ukurasa wake wa 'Instagram', Ney wa Mitego aliweka wazi kuwa amepokea ujumbe wa vitisho mara baada ya kuachia nyimbo hiyo.

Alisema kuwa amepokea ujumbe mbalimbali ambazo zipo zinazowataja wahusika moja kwa moja wale waliohusika kula rambirambi, huku wengine wakimtumia ujumbe wa kumtisha kwa kile alichokiimba katika nyimbo hiyo.

"Mimi hata ikitokea nakufa leo sihitaji mtu yeyote wa  kuweka  kamati ya mazishi yangu kwani najua kitakachotokea siyo mazishi bali ni kula hela na rambirambi hizo kushindwa kutimiza malengo kama yalivyokusudiwa" alisema Ney wa Mitego.

Aliongezea kuwa hawezi kuacha kuimba ukweli hata kama ataendelea kupokea vitisho.


AGNESS MASOGANGE AMPONZA AY NA MWANA FA HUKO AFRIKA KUSINI....


Msanii Madee alivyokuwa airport huko South Africa alipekuliwa sana kutokana na historia ya kukamatwa kwa watanzania na madawa ya kulevya kwenye viwanja vya ndege vya huko South Africa. 


Tukio hilo limewatokea Mwana F.A akiwa na swahiba wake A.Y baada ya kufika bondeni kwa ajili ya show ambapo  wamepekuliwa  kupita  kiasi


Mwana F.A hali ilimshinda ikabidi aanze ku-share na marafiki zake kwenye twitter kuhusu mambo yaliyowakuta huko bondeni.
 
Hizi ni baadhi ya caption za Mwana F.A na watu wengine baada ya tukio hili kutoke.