This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, April 3, 2013

WATUHUMIWA 11 WA GHOROFA LILILOANGUKA DAR WAFIKISHWA MAHAKAMANI...

HABARI  2  MUHIMU:
  • Hakimu aagiza mtuhumiwa wa wa mauaji ya padre Evaristus Mushi
Hakimu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Isaac Sepetu, ameagiza mtuhumiwa Omar Yusuf Makame wa mauaji ya Padre Evaristus Mushi afikishwe mahakamani mara moja siku ya Jumatatu wiki ijayo, ikiwa ni pamoja na nyaraka zinazoeleza ni kwa nini hakupandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka ndani ya saa 24 kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 390 cha mwenendo wa makosa ya jinai, sura na. 7 ya mwaka 2004. Maombi ya kufikishwa mahaknani yametoka kwenye jopo la mawakili watetezi wa mtuhumiwa.
  • Watuhumiwa wa jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Gandhi, Dar, wafikishwa mahakamani


Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (aliyevaa kanzu nyeupe) na watuhumiwa wenzake 10, wamepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Picture
Raza Hussein Ladha (kulia) na watuhumiwa wenzake kumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picture
Watuhukiwa wakiondoka mahakamani baada ya kusomewa mashitaka

11 KORTINI KWA MAUAJI YA KUANGUKA KWA GHOROFA

Imeandikwa na  Happiness Katabazi via blog


HATIMAYE mfanyabiashara Razah Hussein Ladha na wenzake 10 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam tarehe 3 Aprili 2013, wakikabiliwa na jumla ya makosa 24 ya kuua bila kukusudia.


Mbali na Razah washitakiwa wengine ni Godluck Mbaga, Wilbroad Mugabisyo, Ibrahim Kisoki, Mohamed Abdubakari, Charles Salu, Zonazea Anage,Vedasto Ferand, Michael Hemed  Hemed, Albert  Jones na Joseph  Ringo ambao waliletwa jana saa  nane mchana chini ya ulinzi mkali wa wanausalama ambao walikuwa wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Ilala (RCO), Duwani Nyanda.


Mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka mawakili waandamizi wa serikali waliokuwa wakiongozwa na Bernad Kongora, Tumaini Kweka, Lasdlaus Komanya, Peter  Mahugo, Kinyeshi waliwasomea mashitaka hayo kwa kupokezana.


Wakili Kongora alidai mashitaka yote hayo 24 yanayowakabili washitakiwa wote yanafanana na kwamba wanakabiliwa na makosa ya kuua bila kukusudia kinyume na kifungu cha 195 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kuwa   mnano Machi 29 mwaka huu huko katika eneo la Mtaa wa Indira Gandhi waliwaua watu 24 bila kukusudia.


Hata hivyo wakili Kongora aliwataka washitakiwa hao wajibu chochote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ni Mahakama Kuu na kwamba upepelezi bado haujakamilika na kwamba wanaomba mahakama isiwapatie dhamana kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuwapatia dhamana.


Hata hivyo mawakili wa utetezi zaidi ya saba ambao Jerome Msemwa, Adronicus Byamungu ,John Mhozya waliomba mahakama hiyo iwapatie dhamana na washitakiwa wanao wadhamini wakuaminika kwasababu tayari kuna maamuzi mbalimbali yalishatolewa na mahakama ya Rufaa na mahakama Kuu katika kesi za makosa ya kujaribu kuua. Mahakama hizo zilisema mahakama za chini zina mamlaka ya kutoa dhamana kwa kesi ambazo zinafunguliwa kwanza mahakama ya chini na kisha zinakuja kuamishiwa mahakama kuu kwaajili ya usikilizwaji.


Hata hivyo mawakili wa Serikali walipinga maombi hayo kwa maelezo kuwa maamuzi hayo ya mahakama rufaa yalitolewa kwenye kesi ya kujaribu kuua wakati kesi inayowakabili washitakiwa hao ni kuua bila kukusudia na kusisitiza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na hivyo haina mamlaka ya kuwapatia dhamana.


“Mheshimiwa hakimu  sisi upande wa Jamhuri tunawasii mawakili wa washitakiwa wawe watulivu na wavumilivu kwani kesi hii ndiyo kwanza imefunguliwa leo, na upelelezi bado haujakamilika na sheria zilizotungwa na bunge zipo wazi kabisa zinasema ni Mahakama Kuu peke yake ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hii na si mahakama hii hivyo tunasisitiza kuwa mahakama hii haina mamlaka ya kutoa dhamana,” alidai wakili Kongora.


Itakumbukwa kuwa Machi 29 mwaka huu, ghorofa mmoja lililokuwa linajengwa katika mtaa wa Indira Gandhi lilianguka na kusababisha watu  idadi hiyo ya watu 36 kupoteza maisha.


PICHA ZA MATUKIO YA VURUGU HUKO TUNDUMA......DIWANI ( CHADEMA ) NA MCHUNGAJI KKKT WANASAKWA NA POLISI

 

Hii ndiyo hali halisi ya Mji mdogo wa Tunduma leo kuanzia asubuhi

Matairi yanachomwa katikati ya barabara

Mambo hayo 



Mwandishi wetu pamoja na waandishi wenzake walipata shida sana kufika mji wa Tunduma walikutana na vikwazo vingi sana lakini wananchi walikuwa waelewa waliwasaidia kutoa magogo na matairi ili wapite wakapate habari












Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiongea na waandishi wa habari
Wanafunzi wakisindikizwa na jeshi la polisi kurudi majumbani mwao
Polisi wakiendelea na kazi yao katika mitaa ya Tunduma
Baadhi ya magari ya IT yaendayo nchini Zambia yakiwa yamepakiwa nnje kidogo ya mji wa Tunduma kuogopa kuharibiwa kwa magari hayo

----------------
Diwani wa kata ya Tunduma Ndugu Frank Mwaijoka (Chadema) pamoja na mchungaji wa kanisa la KKT katika eneo hilo la Tunduma wilayani momba Mkoani mbeya wametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya kuhusika na uchochezi wa kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa vurugu  katika eneo hilo.

Vurugu hizo zimeanza majira ya saa 4 asubuhi katika eneo hilo la tunduma mara baada ya kundi la watu wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo wakidai waruhusiwe kuchinja mifugo na kuuza katika mabucha yao hali iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.

Akizungumza kuhusiana na tukio hilko Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi ya 40 tayari wamekwisha kamatwa .

Amesema mpaka sasa taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa miongoni mwa watu walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya Tunduma Ndugu John Mwaijoka pamoja na Mchungaji wa kanisa la kkt ndugu Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja wametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Amesema suala hilo limegubikwa  na siasa kwani tayari viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa huo Ndugu Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi Apri 02 mwaka huu wakiwepo pia viongozi wa dini .
Amesema kwa asilimia kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo ya kisiasa kwani hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika juu ya kutokea kwa vurugu hizo.

Amesema shughuli za kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika eneo hilo hivyo kufanya wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya Zambia ambao kwa asilimia kubwa wanategema kupata mahitaji kutoka mpakani mwa Tanzania.

Hata hivyo Diwani amesema kuwa katika vurugu hizo askari mmoja  pamoja na mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe ambapo tayari wamekwisha fikishwa kituo cha polisi.

Kufuatia hali hiyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kwa sasa hali imelejea katika hali yake ya kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu wakati jeshi hilo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta wahalifu wengine.

HII NDO KAULI YA UCHUNGU ALIYOTOA ABSALOM KIBANDA BAADA YA KUTEKWA NA KUTOBOLEWA JICHO



 

 Kauli  hii  ameitoa  kupitia  ukurasa  wake  wa  facebook:

Si jambo rahisi kibinadamu ingawa kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Japo miye ndiye mwenye maumivu makali na machungu mwilini yanayotokana na majeraha na ulemavu niliotiwa, mke wangu kipenzi al maarufu Mama Joshua alikuwa pembeni mwangu wakati wote nikiwa kitandani hospitalini Dar es Salaam hadi Milipark Afrika Kusini. Pole sana Angela. 

Matendo yanasema zaidi kuliko maneno...umepita nyakati nyingi sana ngumu juu yangu tangu mwaka 2000 tulipokutana na kuwa marafiki na hatimaye mwili mmoja. 

Ni Mungu tu atakayekulipa kile kinachostahili na si mwanadam

KAJALA MASANJA AJICHORA TATTOO YA WEMA SEPETU MGONGONI KAMA ISHARA YA KUMSHUKURU KWA ZILE MILIONI 13



Kajala ameamua kuchora Tattoo yenye jina la WEMA mgongoni mwake  baada ya kutolewa faini ya Shilingi Milioni 13 na msanii mwenzake Wema Sepetu,
 
hii ikiwa kama ishara ya shukrani kwa rafiki yake kipenzi Wema Sepetu.

Kupitia ukurusa wake wa instagram Wema nae ameandika hivi:

BEN POL NA LADY JAYDEE WAZINGUANA....JIDE ANADAI WAMEMTAPELI


So much is happening on Twitter these days. Wengi mnafahamu anachokiandika Lady Jaydee siku za hivi karibuni na sasa kibao kimemuendea Linah na Ben Pol.
 


Lady Jaydee anadai wasanii wa THT wamemsaliti kwa kile anachodai walikatazwa kwenda kuperform Nyumbani Lounge licha ya kuwalipa advance.

“Linah na Ben Pol mnabisha hamkukatazwa? Nisalitini ila hamtapata faida mtatoka kapa pia,” ametweet Jide.

Shutuma hizo zimepolekewa kwa hasira na Ben Pol aliyemjibu Jaydee:

“Hiyo show kulikuwa na wengine pia wakuperform je wali perform? kama nililipwa nanikashindwa ku show up, mbona sidaiwi?? Tafakari.”

Aliongeza, “Ben Pol hana muda wa maneno na majungu. Ombi langu ni mmoja kwako. Put me out of your business. PERIOD.”

“Don’t talk about things you don’t know about. DON’T.”

“Ukiwaza kutumia akili kamwe huwezi kukosea, ila utakapotumia hisia lazima ujikanyage somewhere. Nimekua vya kutosha #Trustme,” alimalizia Ben.

Unazungumziaje hiki kinachooendelea sasa na athari yake kwenye muziki wa Tanzania. Maoni yako tafadhari.

PICHA 5 ZA LAANA YA "KANGA MOJA" KATIKA SHOW YA MSANII DIAMOND- BUKOBA

Mambo yanayofanywa na kundi la kanga moja ni ya aibu sana  kwa  sababu  ni  uchafu  unaotendeka  mbele  ya  watoto......

Mwanamke  hujifunga  kanga  moja  tu  bila  chupi  wala  chochote  ndani.Baada  ya  hapo  humwagiwa  maji  kitu ambacho  huanika  kila  kitu  hadharani......

Kama haitoshi, akimwagiwa  maji, wenzie  huanza  kumtia  chupa  matakoni  hali  inayoashiria  VITENDO  VYA  ULAWITI......

Tunawafundisha  nini  watoto???..Tunaifundisha  nini  jamii  na  kizazi  cha  kesho????



PICHA: WEMA SEPETU AAMUA KUMUENZI MCHINA WAKE KWA KUJITANDIKA TATTOO ZA KICHINA SHINGONI NA MGONGONI


3b7e57489bae11e2807c22000a9e06c7_7 
Baada  ya  Kajala  masanja  kujichora  tattoo  zenye  jina  la  Wema  kama  ishara  ya  kumshukuru  kwa  msaada  wake, Wema  naye  ameamua  kujitandika  tattoo  ya  kichina  yenye  maana  ya  "Potential"  kama  ishara  ya  kumuenzi  mchina  wake