This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, February 11, 2014

ujenzi wa jengo linalochungulia Ikulu

IGOGO wa Wakala wa Majengo (TBA), Makumba Kimweri na Richard Maliyaga walioruhusu ujenzi wa jengo linalochungulia Ikulu wamehukumiwa kwenda jela miaka 9 kila mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni 15 kila mmoja na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar!
Maofisa hao wa serikali kwa sasa wapo mahabusu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo ndugu na jamaa wanaangaika kutafuta fedha za kuwalipia dhamana.
VIGOGOVigogo wa TBA, Makumba Kimweri (kulia) na Richard Maliyaga (kushoto) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar! (Picha na Maktaba).

CHADEMA ni Mzigo kwa Taifa….NAPE

nape
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika kata 27, ambapo CCM imeshinda kata 23.
Kimesema siri ya kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.

Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema hayo na kuongeza kuwa matokeo hayo ni ushahidi kwamba CCM inakubalika zaidi na Watanzania walio wengi.

Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.

Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.

NAPE NAUYE

“CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini,” alisema.

Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na  Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo na Santillya (Mbeya).

Zingine ni Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro), Mrijo (Dodoma).

MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA WATU 9 TARIME AFARIKI DUNIA

Mtuhumiwa wa mauaji na unyang’anyi wilayani Tarime mkoani Mara, aliyekuwa akitumia majina matatu ya Charles  Range Kichune, Josephat Chacha, Charles Joseph Msongo (38) aliyekuwa akihojiwa na Polisi, amefariki katika Hospitali ya wilaya wakati akipatiwa matibabu.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Tarime/ Rorya
JAMBAZI

Justus Kamugisha, alisema mtuhumiwa huyo alifariki usiku wa kuamkia jana wakati akitibiwa ugonjwa wa pumu na kwamba baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa huo, alipelekwa hospitalini. Kamanda Kamugisha alisema mwili umehifadhiwa  kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Alisema kabla ya kufariki, mtuhumiwa  alikiri kuhusika katika mauaji ya watu tisa katika kata za Binagi, Turwa na Kitare katika Vijiji vya Mogabiri, Kenyamanyori, Nkende na Rebu.

 Kamanda huyo alisema Range Kichune alikamatwa Februari 6, mwaka huu  mkoani Tanga baada ya Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema kufuatilia mtandao wake na kuwa ilidaiwa baada ya mauaji ya hao alikodi pikipiki kutoka kijijini kwake Kenyamanyori  hadi Musoma na kuhifadhi bunduki SMG na risasi kadhaa kwa mshirika wake mkuu.

Alipokamatwa alimtaja Marwa Keryoba kuwa mshirika wake na kuwa alihifadhi silaha hiyo kwake na Marwa aliuawa Februa 7, mwaka huu Musoma wakati akirushiana risasi na polisi alipotakiwa kujisalimisha.